Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #61
Boss.. safi umekumbushia hilo.. tunajua kilichotokea kwa yule mlinzi wa Balozi Daraja?
Hapa huyu Dau either hajaeleza vizuri au kuna kitu anaficha, majambazi hawaibi vyeti na pasi za kusafiria bwana.
you seem to know a lot kuhusu majambazi na ujambazi!..
Hoja murua kabisa hii. Inatakiwa Napster, WomanofSubtance na Chuma waje waitolee maelezo. Angeyasema hayo Kinondoni Moslem hakuna ambaye angeshtuka lakini Tambaza!1???:frown:Mimi sikujua kuwa Tambaza ni shule ya Kiislamu. Nilisoma pale enzi hizo ikiitwa Aga Khan. Sikujua imebadilishwa kuwa shule ya Kiislamu.
Polisi tunafanya msako mkali msione vitu vinarudi tu, ni matokeo ya msako wetu na tunawaambia majambazi hao warudishe kila kitu walichochukua kabla hatujawakamata na vielelezo hivyo, alitoa amri.
Jambazi gani anaiba vyeti vya shule na hati za kuasafiria? Mheshimiwa anatuambia jambazi katafuta kitu cha kuchukua akaona hati za kusafiria na vyeti ?
Kuna kitu hakielezwi vizuri hapa.
Bahati mbaya kwamba imeshakuwa issue ya dini tayari mimi hilo silipendi sana kulijadili kwa sababu kwenye masuala ya imani watu wengi busara na hekima huwaacha na kwenda na jazba zinazoshabihiana na imani zao.
Nikirudi kwenye mada nashindwa kuamini na hata kuelewa ilikuwaje nyumba isiyo na mkaazi au wakaazi ikawa na pesa ndani au ulikuwa ni mpango wa kuanzisha benki? Vinginevyo huyu ni mtumishi wa umma halafu pia ni msomi hivyo kuhusika kwake na matukio kama haya unatia shaka, kwa sababu 1.yeye akiwa kama mtunza mafao yetu halafu hazingatii taratibu za utunzaji fedha usalama wa pesa zetu ni mashaka matupu huko NSSF. 2.kama tungekuwa na vyombo na uongozi makini hili sio suala dogo la kufumbia macho na mwisho wa siku kuchukuliwa kama udaku. Ina paswa kuchunguzwa na kujiridhisha source ya pesa hizi ila kwa maoni yangu bila kujali pesa ni za nani huyu bwana anapaswa kuwajibishwa kama kiongozi kwa kutozingatia taratibu za utunzaji wa pesa.
Mwisho: mazingira ya pesa kupatikana katika nyumba wasioishi watu ni lazima zitakuwa na walakini hivyo kuna kazi makini inatakiwa ifanyike hapa.
Mara ya kwanza alipotoa taarifa ya kuibiwa alisema kuwa kiasi kikubwa cha fedha kiliibiwa!! Sasa watu wanapohoji uhalali wa pesa nyingi kuwekwa nyumbani badala ya kuziweka benki kama ni pesa halali na CEO wa NSSF na pia msomi; jamaa ndio anakuja na hadithi kuwa zilikuwa milioni nne tu!! Huyu jamaa anaficha kitu, ni fisadi anayetumia dini yake kupata watu wa kumlinda dhidi ya madhambi yake!!
Suffice it to say I have my ear to the ground, I know everything that goes around.
Wabongo inabidi tujue jinsi ya ku communicate.Huyu Dau alikuwa hahitaji hata kudiscloe publicly amount iliyochukuliwa, na polisi wasingeweza ku disclose hiyo info, sasa kashawatangazia wazee wa kazi kwamba anaweka milioni tano nyumbani, next thing you know watam time kwenye gari.
If at all huu ni ujambazi, maana ina sound kama kuna deals gone awry na espionage/ revenge zaidi ya ujambazi.Jambazi gani anakuja kukurudishia bunduki, lakini anakimbia na vyeti?
Brilliant! excellent! did find out this by yourself? case closed! super detective!... I wonder why they dont hire you to do the job. Come you should work for interpol or something!
unajua tatizo letu watanzania? kila mtu anajua kila tu! "Everybody is everything"
Mimi sikujua kuwa Tambaza ni shule ya Kiislamu. Nilisoma pale enzi hizo ikiitwa Aga Khan. Sikujua imebadilishwa kuwa shule ya Kiislamu.
Nafikiri jamaa waliona kukamatwa na silaha ya wizi tena ya kibosile ingekuwa soo, wakaamua kuirudisha.....
....Nafikiri nyinyi ni miongoni mwa wale wanaofeli mitihani ya "UFAHAMU" ...!!!..Sijui ni nani amewaroga!!!Hoja murua kabisa hii. Inatakiwa Napster, WomanofSubtance na Chuma waje waitolee maelezo. Angeyasema hayo Kinondoni Moslem hakuna ambaye angeshtuka lakini Tambaza!1???:frown:
...So Bulesi wewe ni Yule unaechukizwa na DINI yake ndio maana unamtuhumu...!!! Do you think Uislam unaficha mafisadi?...waulize wanaoukataa uislam ni kwaajili gani? wanaogopa sheria zake zilivyo straight!!!Mara ya kwanza alipotoa taarifa ya kuibiwa alisema kuwa kiasi kikubwa cha fedha kiliibiwa!! Sasa watu wanapohoji uhalali wa pesa nyingi kuwekwa nyumbani badala ya kuziweka benki kama ni pesa halali na CEO wa NSSF na pia msomi; jamaa ndio anakuja na hadithi kuwa zilikuwa milioni nne tu!! Huyu jamaa anaficha kitu, ni fisadi anayetumia dini yake kupata watu wa kumlinda dhidi ya madhambi yake!!