Nyumba ya Dr. Dau yavamiwa; vitu vyaibwa, vingine vyarudishwa kiana

Huyu Bwana sio siri ana agenda ya Uislamu.
Nimecheck hayo ni matamshi aliyoyatoa ,na nimenukuu kutoka source hii:www.igs.net/~kassim/an-nuur2/201/201-12.htm





Wacha udini wewe na mawazo yako finyu, Kama alikua anawashauri waislam ulitaka aongee dance? ulokole? Nchi haina dini lakini viongozi wanadini zao na wengi wanatekeleza majukumu wa dini yao. Pinda anapokutana na nyie walokole anaongea kuwa encourage walokole wenzake, Hakuna tafauti na Dr. Dau. Wewe ni udini ndio unaokusumbua
 
Kama top kama huyo anavamiwa,je mlalahoi wa Manzese afanyeje?
Au hawa majambazi ni Mafia waliotumwa kuchukua documents za siri zinazohusika na utendaji wake wa NSSF?
hii ni bongo yetu
MlALAHOI WA MANZESE ANA WASIWASI KWANI? WA KUMVAMIA ATAKUWA KIBAKA TU AMBAYE HATA UKIMTISHIA SHIIII KAMA KUKU ATAKIMBIA.
 
[SIZE=+2]Oneni fahari kuwa Waislamu-Dk. Dau[/SIZE]

[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]VIJANA wa Kiislamu wametakiwa kujifakhalisha na Uislamu wao ili kuweza kuwavutia hata walio nje ya Uislamu.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Wito huo umetolewa na mgeni rasmi Dk. Ramadhani Dau katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kiislamu wa kidato cha sita iliyoandaliwa na Jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu mkoa wa Dar es Salaam ambayo ilifanyika katika shule ya sekondari ya Tambaza siku ya Jumapili Mei 5, mwaka huu.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Akitoa nasaha zake katika mahafali hayo, Dk. Dau alisema moja ya sababu zinazofanya Uislamu kuwa nyuma ni kuwa Waislamu wenyewe wanaona aibu kutekeleza Uislamu mbele ya wasiokuwa Waislamu.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]"Imefikia wakati mtu anaona aibu kuwa na jina la Kiislamu au anaona aibu kutekeleza Uislamu wake. Muislamu anatoka ofisini kuelekea Msikitini lakini anaogopa kuvaa kofia yake barabarani. Ataivaa Msikitini na akimaliza anaivua kabla ya kutoka", alisema Dk. Dau kwa masikitiko.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Dk. Dau alitoa mfano wa Mayahudi na kusema kuwa ingawa Mayahudi ni wachache hapa duniani lakini wao ndio wanaotawala dunia nzima.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]"Idadi ya Mayahudi haizidi milioni tatu duniani hivi sasa, lakini wao ndio waamuzi wa kila kitu, hata Rais wa Marekani hawezi kuchaguliwa bila ya Support yao", alisema na kutaja moja ya sababu za Mayahudi kufanikiwa kiasi hicho ni kuwa na fakhari na imani yao licha ya uchache walionao.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kivutio kikubwa katika mahafali hayo kilikuwa ni onyesho la video la mikanda ya Mwembechai na hotuba ya Sheikh Ponda aliyoitoa Mtambani siku ya Eid el Hajj.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Aidha, akitoa nasaha zake katika mahafali hayo, Mhadhiri maarufu Ustadh Shaabani Omar aliwataka Waislamu hususan vijana kuwa tayari kubadili tabia zao kuelekea katika tabia halisi za Kiislamu ili kupata radhi za Allah (s.w.).[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Katika risala yao, wanafunzi wa kidato cha sita walimueleza mgeni rasmi kuwa miongoni mwa matatizo yanyowakabili ni ukosefu wa nafasi za masomo ya juu kutokana na uhaba wa vyuo hapa nchini na dhuluma iliyopo dhidi ya Waislamu.[/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Walimuomba mgeni rasmi kuangalia uwezekano wa kuwatafutia nafasi za masomo nje ya nchi ili kuweza kuutumikia Uislamu hapo baadaye.[/SIZE][/FONT]

[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1] [/SIZE][/FONT]
[FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Bonyeza hapa[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji[/SIZE][/FONT]


Sioni Ubaya wowote Dr Dau kuwataka wanafunzi hao waone fahari na dini yao.Wakubali kuanzia majina yao hadi utamaduni mwingine utakaowatambulisha kuwa wao ni waumini wa imani hiyo. Ila nimeshindwa kuoanisha Video ya mwembechai na mahafali!
Wajuzi hebu nifafanulieni jinsi gani mwembechai incidence itachochea taaluma.Hapo nimetoka kapa.
 
Sioni Ubaya wowote Dr Dau kuwataka wanafunzi hao waone fahari na dini yao.Wakubali kuanzia majina yao hadi utamaduni mwingine utakaowatambulisha kuwa wao ni waumini wa imani hiyo. Ila nimeshindwa kuoanisha Video ya mwembechai na mahafali!
Wajuzi hebu nifafanulieni jinsi gani mwembechai incidence itachochoea taaluma.Hapo nimetoka kapa.

Ungekuwa muislam ungeelewa haraka! Hujambo lakini?
 
..Ulieleta Hotuba ya Dr.Dau hapa jamvini naona unataka ku-divert mjadala...!!! your motives behind is known...!!! Ukiwa Mgeni rasmi huwezi kuwachagulia waliokualika wafanye nini...!!! Kuhusu Mkanda wa Mwembechai na Hotuba za Ustadh Ponda ni ktk program za Waandaaji kuwakumbusha vijana walipotoka na wanapokwenda.

Hijab NSSF??....duh hii mpya...ama kweli wenzetu chuki zenu zimezidi mipaka !!!! Labda mdau atupe hesabu za wanaovaa Hijabu pale NSSF na wasiovaa...!!! so mnataka wote muwaone Mapaja sio...!!!

Back to Ujambazi...Tunatoa pole kwa familia na wale marafiki wa karibu ambao kwa namna moja au ingine wameathiriwa na Ujambazi Huu...!!! MwenyeziMungu Awasaidie kuwapata wahusika na kuchukuliwa hatua madhubuti....Hakuna Nafsi inayojua nini kitatokea kesho...wala hakuna Nafsi inayojua itakufa Mji/mahala gani...!!!

Kwa wale ambao washawahi kuibiwa nafikiri wanajua nature ya wezi wetu ikoje na pains wanazozipata.
 
Ndio maana naomba kuelimishwa maana kuuliza ndio mwanzo wa kujua.
Mi mzima sana..sijui wewe
Huyu Mchangiaji alieleta hii hotuba ni ya mwaka before 2000...hii 2010...lkn hata kama ingekuwa ya hivi karibuni bado ingekuwa inalipa tu..!! ila Lengo lake ni ku-divert ajenda ya mjadala wa ujambazi ili uwe wa udini wa Dr.Dau....may be ana-justify ujambazi alofanyiwa Dr.Dau.
 
Huyu Mchangiaji alieleta hii hotuba ni ya mwaka before 2000...hii 2010...lkn hata kama ingekuwa ya hivi karibuni bado ingekuwa inalipa tu..!! ila Lengo lake ni ku-divert ajenda ya mjadala wa ujambazi ili uwe wa udini wa Dr.Dau....may be ana-justify ujambazi alofanyiwa Dr.Dau.

You are more than right!!! kavamiwa na kuibiwa Mh. Joel Bendera...mbona tulimuonea huruma kama binadamu, mzazi na mwananchi. Unajua haya mambo ya kutazamana kwa dini zetu iko siku PATACHIMBIKA hapa TZ.
 
KIASI kikubwa cha fedha ambacho idadi yake haijajulikana pamoja na nyaraka mbalimbali zimeibwa kutoka kwenye nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau. Akithibitisha kutokea kwa wizi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Elias Kalinga, aliliambia Tanzania Daima Jumapili kwamba tukio hilo limetokea majira ya saa tisa usiku wa kuamkia jana.
Kamanda huyo alisema nyumba iliyovunjwa ni mali ya Dau, iliyoko jirani na viwanja vya Leaders Kinondoni, ambayo hata hivyo hakuna anayeishi humo baada ya mmiliki wake kuhamia sehemu nyingine.
"Mwenye mali yake amesema hawezi kwa haraka haraka kukumbuka ni kiasi gani cha fedha ingawa anasema kulikua na pesa nyingi pamoja na nyaraka zake mbalimbali. Hakuna mali zaidi zilizoibwa.
"Hiyo nyumba iko jirani na viwanja vya Leaders pale Kinondoni… awali Dau alikuwa akiishi humo, lakini mpaka wizi unatokea yeye na familia yake walikuwa wanaishi kwenye nyumba nyingine,"
alisema.
Akielezea namna wizi huo ulivyofanyika, kamanda Kalinga, alisema ukuta mkubwa unaozunguka nyumba hiyo ulitobolewa kwa kitu kizito ambacho kilitoa sauti na kwamba wahalifu hao waliingia na kuwafunga kamba walinzi.
Alisema jeshi la polisi linawashikilia walinzi hao ambao ni wafanyakazi wa NSSF kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio hilo na kuwataja kuwa ni Deus Mtatiro (52) mkazi wa Kinondoni na Yusuf Bakari (56), mkazi wa Ubungo.
"Tunawahusisha hawa walinzi na wizi huo… ni vigumu mwizi kuvunja ukuta na kuingia ndani bila walinzi kushtuka na kutumia silaha zao mpaka wanafungwa kamba hakuna juhudi zozote za kuzuia wizi huo walizofanya.
"…Ndiyo maana tunawahoji ili kujua kama walihusika ama laa tukimaliza tutawapeleka mahakamani lakini juhudi za kuwapata wengine zinaendelea," alisema kamanda Kalinga.

maswali ambayo yanakosa majibu
1. Inakuwaje CEO mzima ambaye amesoma anaweka pesa nyingi nyumbani na sio bank, nini anaogopa?
2. CEO mzima ambaye anasadikiwa kuwa na hakili sana hajui kiasi gani cha fedha kilikuwa kwenye safe? this raise more queations than answers. Ningemuona anakili kama angetaja kiasi kidogo cha hela ndio kimeibiwa.
3 Je anayo risiti au anaweza kuthibitisha kwa bank statement hizo hela ni legal?
4. kama hawezi kuthibitisha upatikanaji wa hela nyingi huyu jamaa si anaweza akashitakiwa kwa corruption na money laundering
5. Je kuweka pesa nyingi nyumba ambayo haukai sio kuficha hela kwa ajili unaogopa kuweka bank?
6. Inakuwaje walinzi wa NSSF wanalinda nyumba ambayo mfanyakazi wa NSSF hakai, yani inamaanisha ana set mbili ya walinzi nyumbani anakokaa na asikokaa. Je huu sio ubadhirifu wa mali ya umma

kama hawezi kuthibitisha upatikanaji wa hizo hela ni dhairi hizo hela zimepatikana kwa dili, kwa hiyo ni haki kwa walinzi kucheza dili na kuzichukua.
 
Vladmir Semilong,

Ni bahati mbaya nyumba yake kuvamiwa na maisha yake kuwa hatarini. Lakini kuna haya ya msingi ya kujiuliza.

Huyu ni mtu ambaye tuliambiwa alipaswa kuwa Gavana wa Benki Kuu na anaweka fedha nyingi sana nyumbani!

Je hizi fedha nyingi ni kiasi gani? au tafsiri ya fedha nyingi ni nini?

Kwa nini aweke fedha nyingi nyumbani? Ningeelewa japo angekuwa na shilingi Milioni moja na kusema hizi ni kipu chenji za dharura pale nyumbani, lakini akisema kaibiwa milioni kumi nyumbani tumhoji milioni kumi zinafanya nini nyumbani?

Yeye kama mchumi na mtaalamu wa masuala ya fedha aliyebobea, anausaidiaje uchumi wa Tanzania kudhibiti thamani na mzunguko wa shilingi ya Tanzania ikiwa anahifadhi fedha nyingi nyumbani na si Benki?

Hata kama angedai ilikuwa ni kuwalipa vibarua, je vibarua ujira wao ni kiasi gani mpaka awe na "fedha nyingi" nyumbani? Je nyaraka hizi ni zake binafsi na mali zake binafsi au kuna nyaraka za shirika?

Inasikitisha sana unapoona Wasomi wanashindwa kuwa mstari wa mbele kufundisha umma wa Tanzania mambo endelevu. Kila siku tunapiga kelele Ujima wa Tanzania na Watanzania kuficha fedha kwenye godoro na nyaraka uvunguni badala ya kupeleka Benki hata kuweka kwenye sefu la vitu ambavyo ni fedha.

Wenzetu huweka nyaraka na vitu vya muhimu mahali pa salama panapolindwa na nyaraka na vitu hivi vya thamani huwekewa bima, kwa kuwa vyote vina thamani.

Sijui ni lini tutaanza kuyaleta Tanzania yafanyike kwa kweli na si kuendelea kuhubiri "wenzetu ulaya wameendelea" huku wewe ndio wa kwanza kuweka fedha kwenye chungu ukakichimbia kwenye udongo wenye mchwa!
 
"Idadi ya Mayahudi haizidi milioni tatu duniani hivi sasa, lakini wao ndio waamuzi wa kila kitu, hata Rais wa Marekani hawezi kuchaguliwa bila ya Support yao", alisema na kutaja moja ya sababu za Mayahudi kufanikiwa kiasi hicho ni kuwa na fakhari na imani yao licha ya uchache walionao"

Bwana Dau ukimnukuu naona ni mawazo ya Islamists kama akina Osama & Co.Naona hata matatizo ya Uislamu Bongo,ni Mayahudi .Udini upo sasa Tanzania,ukiwa political Correct huwezi kuona haya.At least Mchungaji Mtikila ameamua kuchukua hatua binafsi.

Of course mtu wa kawaida akivamiwa ntakuwa sorry,lakini tunaambiwa alikuwa na kiasi kikubwa home kwake,it will be interesting kuona shilingi ngapi jamaa walichukua.
Mkapa,Cheyo,Lowassa,Rostam wakifanyiwa hivi ,wala sitasikitika
 
ukitaka kujua kama nchi ya Tanzania haina watu waliolemika ndo utajua hapa!...

"It is not the education which works but rather the effect of the education!"...

How can you justify ujambazi? unless you are a criminal minded person. So how many are criminal minded to that extent kujustify ujambazi? Halafu cha kushangaza mtu kaingiliwa na majambazi, watu mnaanza kuquestion pesa kiasi gani? what docs?
 
Dini forum dini forum, kila kitu lazima kigeuzwe kuwa na harufu ya udini.

Muna ushahidi gani kwamba amefanya overinvoicing? Na hiyo hotuba yake tuna uhakika gani kwamba haikuwa "edited to suit the circumstance?" Au ina kosa gani kubwa ambalo wenzake wakristo hawazungumzi wakialikwa kwenye hafla za kidini huko makanisani?

Kama munazungumza kuhusu kuibiwa kwake basi endeleeni na hiyo, lakini musihusishe na dini yake na ufisadi ambao hamuna uhakika nao
 
Mkurugenzi huyu ni Daktari wa Elimu,Mwenye pHD kitendo alichokifanya kuhusu Pesa nyingi kuibiwa ni kitendo cha Mtu wa Darasa la nne la leo sio la zamani, Nafikiri kwa wingi wa hizo Pesa ndio maana amebaki kusema Pesanyingi! pesanyingi! Na kweli mkubwa huyu Pesa anayo maana hata nyumba yake iliyojengwa Dodoma na wachina (CRJE) Si ya pesa kidogo. Lakini kwa usomi wake atushawishi tusiwe na mashaka kumhusu!! Vinginevyo tutamuingiza kwenye kundi la ..........di
 
Mimi sikujua kuwa Tambaza ni shule ya Kiislamu. Nilisoma pale enzi hizo ikiitwa Aga Khan. Sikujua imebadilishwa kuwa shule ya Kiislamu.
 
Hiyo ni fedha chafu ndio maana hakuweka kule anakokaa,sielewi nyumba haishi mtu hhela lakini mifezwa imeachwa humo,sijui Dr anafanya biashara haramu kiasi cha kulifanya hame lake bank,na ndio maana hasemi ni kiasi gani cha nijifweza anaona soo kwani nina hakika hiyo fweza si halali na Dr sio msafi kwani tumesahau yeye na profesa Kapuya na Manji walivyotoa bwelele magodown pale Ubungo kwa Manji halafu wakaja nunua tena kwa bei zaidi ya ile waliyompa Manji,
 
...................Katika risala yao, wanafunzi wa kidato cha sita walimueleza mgeni rasmi kuwa miongoni mwa matatizo yanyowakabili ni ukosefu wa nafasi za masomo ya juu kutokana na uhaba wa vyuo hapa nchini na dhuluma iliyopo dhidi ya Waislamu...................

mmhh!!

maswali ambayo yanakosa majibu
1. Inakuwaje CEO mzima ambaye amesoma anaweka pesa nyingi nyumbani na sio bank, nini anaogopa?
2. CEO mzima ambaye anasadikiwa kuwa na hakili sana hajui kiasi gani cha fedha kilikuwa kwenye safe? this raise more queations than answers. Ningemuona anakili kama angetaja kiasi kidogo cha hela ndio kimeibiwa.
3 Je anayo risiti au anaweza kuthibitisha kwa bank statement hizo hela ni legal?
4. kama hawezi kuthibitisha upatikanaji wa hela nyingi huyu jamaa si anaweza akashitakiwa kwa corruption na money laundering
5. Je kuweka pesa nyingi nyumba ambayo haukai sio kuficha hela kwa ajili unaogopa kuweka bank?
6. Inakuwaje walinzi wa NSSF wanalinda nyumba ambayo mfanyakazi wa NSSF hakai, yani inamaanisha ana set mbili ya walinzi nyumbani anakokaa na asikokaa. Je huu sio ubadhirifu wa mali ya umma

kama hawezi kuthibitisha upatikanaji wa hizo hela ni dhairi hizo hela zimepatikana kwa dili, kwa hiyo ni haki kwa walinzi kucheza dili na kuzichukua.

..........Maswali ya msingi sana hayo juu.............

No doubt kitendo kilichofanyika ni Ujambazi....................Pili, kuhusu neno "pesa nyingi" ni very subjective..............in this case.........tuta-assume/value kutokana na aliyesema zilikuwepo "pesa nyingi"..............i.e. Dr. Dau............the valid question is why keep "pesa nyingi" nyumbani?
 
Kwanini atunze kiasi kikubwa cha hela nyumbani? Yeye hana akaunti bank?
 
Back
Top Bottom