Nyumba kubwa inauzwa bei karibu na bure

Akiri

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,445
212
nyumba 01.JPG Nyumba ni kubwa ina vyumba 4 vya kulala na uwani ina vyumba 3 jumla ina vyumba 7. pia ina choo ( public toilet) uwani, mbele ina vyumba 2 vya biashara ambavyo vimeunganishwa na nyumba. imeezekwa bati. ina umeme, na kisima cha maji , imewekwa milango na madirisha na tayari kuna wapangaji wanaishi. picha za vyumba vya ndani ya nyumba inakuwa vigumu kupata sababu nyumba tayari inakariwa na imewekwa dhamani mbali mbali. na mmiliki wa nyumba ndiyo ameamua kuiuza. nyaraka zote muhimu zipo. Ipo wilaya ya Temeke, mbagala chamanzi ( nyumba inauzwa kama ilivyo. haina gati la kuingiza gari ndani japo gari inafika mpaka hapo mlangoni labla mnunuzi afanye marekebisho. bei ni Tsh. 37,000,000.00 tuwasiliane 0755 099 291, 0686 200 117, 0657 14 5555.
 
Jamani kwa asiye na nyumba lakini angalau mfuko unamruhusu wahi chukua nyumba hii, unaweza ifanyia marekebisho kama kutoa sehemu ya flem nk
 
Bei nzuri lakini isijekuwa nyumba ya urithi zina matatizo sana.
 
Mbagala chukua 20,000,000/=
Acha dharau kwa nini unasema mbagala kwani mbagala kuna nini, kuna watu wanishi mbagala na wanamaisha mazuri sana. hiyo pesa ni ndogo ungeza japo 8 then tuwasiliane.
 
Bei nzuri lakini isijekuwa nyumba ya urithi zina matatizo sana.

Hapana sio ya urithi , ukiangalia vizuri utangundua haina muda mrefu sana tangu kujengwa kwake, ina mwaka mmoja , hili eneo lina nyumba nyingi zinauzwa zikiwa bado hazijakamililka vyema. nimegundua wengi walipata pesa ya mara moja na wakaidumbukiza kwenye nyumba . sasa pesa imekwisha nyumba haijakamilika na maisha yanaendelea. wengi huamua kuuza ili wapate mtaji wa kuendeleza biashara
 
Nyumba kama hii unaweza kuijenga kwa 15M na zikabaki ukiongeza na gharama ya kiwanja 3M jumla 18M kwa hiyo ukipata 20M zinakutosha sana
 
Nyumba kama hii unaweza kuijenga kwa 15M na zikabaki ukiongeza na gharama ya kiwanja 3M jumla 18M kwa hiyo ukipata 20M zinakutosha sana
we unajuaje kama zinanitosha , sina hakina na utimamu wa akiri yako .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom