Nyumba isiyo na mwenyewe ipo hapa

Obe

JF-Expert Member
Dec 31, 2007
9,982
34,476
Kwa jinsi hali inavyoendelea hapa Tz, nashindwa kutoifananisha nchi yangu na gesti bubu ambapo kila mwenye uwezo wa kulipia chumba anaweza kufanya anavyotaka chumbani hata kama kalipia 'show time'. Angalia suala la umeme, moja, sasa hii imekuwa si habari tena kwani kwa wiki sasa hatujasikia mgao wa umeme, mbili, funga kazi, wauzaji wa mafuta wamefungia bidhaa yao na wanaitaka serikali iwapigie magoti.
Usemi wa Kafulila alionukuu kitabu chwa Mwl Nyerere kuwa 'serikali legelege' ndiyo tunayoiona leo, serikali iliyopo madarakani imekuwa ni mateka wa wafanyabiashara na haina ubavu wa kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtz yanapatikana,
Fikiria nyumba ambayo haina mzazi................... nakulilia mwananchi mwenzangu wa TZ
 
1995 to 2005
alikuwa busy anajinga kushinda uchaguzi na si kuongoza nchi, Tanzania baada ya uchaguzi 2005:
Hili halikuwemo ktka ajenda yake, hapa ndipo tulipokwamia sbb hakuwa akijua na mpaka leo hii hajui ni vp anatakiwa km rais aiongoze nchi yake katika kujiletea maendeleo na kwamba maendeleo ya nchi hayaji kwa kuzurura zurura kwenye nchi za wengine na kuombaomba misaada.
 
  • Thanks
Reactions: Obe

Similar Discussions

Back
Top Bottom