Nyumba Imara ni ile yenye msingi imara; Je, Nyerere hakuweza kujenga msingi Imara wa viongozi?

Taifa halijengwi na mtu mmoja hujengwa na watu wengi kwa pamoja; Nyerere alikuwa muasisi tu na ilitakiwa waliomfuata nao waendeleze jitihada ili kuimarisha ujenzi wa taifa imara. Unfortunately hatukuwa na akina Nyerere wengi.

Nyerere alitekeleza jukumu la kwake, waliomfuata hawakutekeleza ya kwao; wakajiswagia kiholela bila hata vision.

Exactly, kwa vile alikua muasisi basi alipaswa aweke mambo sawa ili watakaomfuata baada yake waendeleze yale aliyoyaasisi!
 
Lakini alituachia misingi. Azimio la Arusha lilikuwa ni msingi kama vile declaration of independence na bill of rights ulivyokuwa msingi wa Wamarekani.
Akaenda mbali zaidi akatuwekea leadership code. Mfanyibiashara asiwe kiongozi wa wakulima na wafanyikazi. Huo ulikuwa ni msingi. Sasa wewe ulitaka afanye nini? Baada ya kuondoka mamlakani hakuwa na mamlaka tena. Angeamua kukaa kimya, lakini kwa kadri alivyokuwa anaona mambo yanakwenda mrama hakusita kupaaza sauti yake kuwatahadharisha viongozi na watawaliwqa. How much more could he have done?

Aisee washabiki wa nyerere bana!

Azimio la Arusha lilikuwa na codes za kinafiki na kibaguzi hakuna binadamu mwenye akili timamu atafuata ule upuuzi ulioko kwenye azimio la arusha trust me... ndio maana ilibidi ibadilishwe haraka sana..moja ya kasoro zake kubwa ni

a. Ubaguzi..huwezi kusema wafanyabiashara wasiwe viongozi kwasababu kufanya biashara si dhambi wala si uwizi na si kila mfanyabiashara ni mwizi na si kila mfanyakazi na mkulima ni mtu mwema..watu wenye akili wakaenda zanzibar wakaondoa hiyo dhana potofu

b. Azimio lililkuwa linawafanya wafanyakazi wa serikali wasimiliki hata nyumba (upuuzi) sasa wewe unalipwa mshahara unywe pombe tu usijenge nyumba wala kufanya biashara halali ndio maana watu wenye akili waliondoa hiyo codes za kijinga na wengi nafikiri walikubali jambo hili kwa kuogopa nyerere kwasababu wapinzani wake aliwauumiza..kulikuwa na nidhamu ya uwogo...baada ya kuondoka wakaondoa huo uchafu..
 
K

Kurekebish siyo kufuta. Huwezi kuwa kiongozi na mfanya biashara, na wala huo siyo ubaguzi. Hata Marekani kwa wakongwe wa ubepari hawachanganyi biashara na siasa. Unaruhusiwa kufanya biashara au kufanya siasa. Iwapo wewe ni mfanya biashara halafu ukaamua kuingia kwenye siasa, basi wana utaratibu mzuri sana wa kukubana ili usichanganye siasa na biashara. Ndiyo maana wafanya biashara wakubwa hawaingii kwenye siasa.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Aisee washabiki wa nyerere bana!

Azimio la Arusha lilikuwa na codes za kinafiki na kibaguzi hakuna binadamu mwenye akili timamu atafuata ule upuuzi ulioko kwenye azimio la arusha trust me... ndio maana ilibidi ibadilishwe haraka sana..moja ya kasoro zake kubwa ni

a. Ubaguzi..huwezi kusema wafanyabiashara wasiwe viongozi kwasababu kufanya biashara si dhambi wala si uwizi na si kila mfanyabiashara ni mwizi na si kila mfanyakazi na mkulima ni mtu mwema..watu wenye akili wakaenda zanzibar wakaondoa hiyo dhana potofu

b. Azimio lililkuwa linawafanya wafanyakazi wa serikali wasimiliki hata nyumba (upuuzi) sasa wewe unalipwa mshahara unywe pombe tu usijenge nyumba wala kufanya biashara halali ndio maana watu wenye akili waliondoa hiyo codes za kijinga na wengi nafikiri walikubali jambo hili kwa kuogopa nyerere kwasababu wapinzani wake aliwauumiza..kulikuwa na nidhamu ya uwogo...baada ya kuondoka wakaondoa huo uchafu..
b. Ni uongo kusema kuwa azimio lilikataza wafanyikazi serikalini kumiliki nyumba. Azimio lilisema kiongozi hapaswi kujenga nyumba za kupangisha lakini halikukataza mfanyikazi wa serikali kujijengea nyumba.
Sasa hivi tunaongozwa na wafanyibiashara, tumeona yaliyotokea kwa kuwapa uongozi akina Karamagi, wanajifagilia kampuni zao, akina Ngeleja, wanatekeleza maslahi ya waajiri wao wa zamani katika madini. Nchi inazidi kufilisika wakati tuna madini. Hata Marekani ambayo ni nchi ya kibepari wafanyibiashara wamewekewa masharti magumu sana kama wanataka kugombea ubunge na uongozi wa nchi. Sisi leo mfanyibiashara anaingia serikalini na kutumia cheo chake kuendeleza maslahi yake kibiashara. Na hao watu wenye akili ndio waliotuwekea msingi huu wa ufisadi uliokithiri. Kweli ni watu wenye akili...
 
He did that, but the followers decided to take another route.
He didn't do it better that is why his followers decided to take another route as they couldn't understand (failure to understand is credited to Mwalimu's failure to make them understand) the need for them to take Mwalimu's route!!
 
a. Ubaguzi..huwezi kusema wafanyabiashara wasiwe viongozi kwasababu kufanya biashara si dhambi wala si uwizi na si kila mfanyabiashara ni mwizi na si kila mfanyakazi na mkulima ni mtu mwema..watu wenye akili wakaenda zanzibar wakaondoa hiyo dhana potofu b. Azimio lililkuwa linawafanya wafanyakazi wa serikali wasimiliki hata nyumba (upuuzi) sasa wewe unalipwa mshahara unywe pombe tu usijenge nyumba wala kufanya biashara halali ndio maana watu wenye akili waliondoa hiyo codes za kijinga na wengi nafikiri walikubali jambo hili kwa kuogopa nyerere kwasababu wapinzani wake aliwauumiza..kulikuwa na nidhamu ya uwogo...baada ya kuondoka wakaondoa huo uchafu..
On this Mwalimu was very right...tatizo hao wanafunzi wake hawakumuelewa Mwalimu..na hili ndio tatizo la watu aina ya Mwalimu. Namna wanavyowaelewesha na kuwaelimisha wanafunzi wao kwa kutumia falsafa za hali ya juu inakua vigumu kwa wanafunzi hao kuelewa. Ndio maana genge lilimfuata Mwalimu likaona izo codes hazina maana. Waswahili usema, "mshika mbili, moja umponyoka"..so huwezi kuwa mfanyabiashara at the same time ukawa mwanasiasa; kimoja kitakuponyoka na ufanisi/utendaji wa kazi unakua hovyo.
 
Dhulma ni mbaya tena sana na hata vitabu vyote vya dini vimenena hivyo.

Je kudhulumu watu katika So called Azimio la Arusha unafikiri atasalimika na dua za wenye kudhulumiwa?

We unafikir kuwahadaa wananchi wake kuwa Tv ni anasa wakti yeye ana Tv kuuuubwa pale kwake msasani mnafikiri atasalimika?
 
Dhulma ni mbaya tena sana na hata vitabu vyote vya dini vimenena hivyo.

Je kudhulumu watu katika So called Azimio la Arusha unafikiri atasalimika na dua za wenye kudhulumiwa?

We unafikir kuwahadaa wananchi wake kuwa Tv ni anasa wakti yeye ana Tv kuuuubwa pale kwake msasani mnafikiri
atasalimika?
Muone muongo mwingine huyu hapa.
Nani alidhulumiwa katika azimio la Arusha? Wanyonyaji? Mwalimu hakuwa na tv kubwa Msasani. Huo ni uongo mwingine naona unaendelea kuusambaza hapa JF. Mwaka 1977 alipokuja state visit hapa Marekani balozi Bomani alimnunulia video player ili aweze kuangalia footages za safari yake. Na akanunua pia TV ya Sony ambayo alitumia kuangalia hizo video. Na kwa sababu tv ilikuwa NTSC usingeweza kuona chochote bali video za VHS ambazo ubalozi ulimpelekea. Sasa unasema alikuwa na TV kuuubwa Msasani uliiona? Acheni kutumia uongo kama propaganda.
 
He didn't do it better that is why his followers decided to take another route as they couldn't understand (failure to understand is credited to Mwalimu's failure to make them understand) the need for them to take Mwalimu's route!!
Ok nimekuuliza swali huko nyuma. Ungekuwa katika viatu vya Mwalimu wewe ungefanya nini ili kuhakikisha unaacha misingi imara?
 
Ok nimekuuliza swali huko nyuma. Ungekuwa katika viatu vya Mwalimu wewe ungefanya nini ili kuhakikisha unaacha misingi imara?

Ningehakikisha ninaowafundisha na kuwaandaa kuongoza nchi wanaelewa maana ya misingi ninayowajengea na kuwaachia kwa kutumia njia rahisi kwa wao kunielewa....ningeepuka kutumia falsafa sana. Mfano, unajua mengi aliyokua akifundisha Mwalimu na watu kucheka pale anapochekesha, watu wengi walicheka kutokana na vichekesho vyake; lakini hawakuelewa yaliyomo ndani ya vichekesho hivyo. Mwalimu alipaswa atumie lugha nyepesi kwa watu waliokua wanamwangalia yeye kama Mwalimu. Hapo ndipo ninasema misingi yake haikua imara!
 
Mwalimu alikua na udhaifu mkubwa katika uteuzi wa viongozi. Alitumia zaidi hisia zake binafsi na sio sifa zilozowazi katika uteuzi. Alijizungusha na vilaza wasio mpa changamoto ila wanaujua kusema ndio kwa kila kitu. There must be a clear criteria for ascendence to leadership position not huu ujinga wa " fikra sahihi" za mtu mwenyecheo cha mwenyekiti. Udhaifu huo katika uteuzi umeendelea hadi Leo.

Unaposema alijizungushia vilaza unataka kusema nini? Unataka kusema vilaza ndio walimwambia Mwalimu asianze kuchimba madini asubiri mpaka nchi itakapopata wataalamu ndio waanze kuchimba? Unataka kusema kuzungukwa na vilaza ndio kidogo kilichopatikana kakjenga miundo mbinu za shule, afya, umeme, maji, nyumba, viwanda na kadhalika? Nafikiri unatakiwa kuwa makini unaposema aliteua vilaza wakati baadhi ya watendaji walifanya vizuri na sifa zao zikawa mfano wa kuigwa.

Ulafi na ombwe na uongozi wa sasa hivi sio wa kumsakizia Mwalimu. Wa kujilaumu ni sisi wenyewe amabao ambao tunawapa uongozi kwa kuangalia maslahi binafsi bila kutanguliza uzalendo wa nchi hii. Mwenyezi Mungu ametupa uwezo hatutaki kuutumia.Tutumie haki ya kupiga kura, kulinda kura na kuwawajibisha viongozi na maadili yatarudi. Lakini tukiendelea kunyoshea vodole waliokufa hatufiki mbali. Ulafi, kutokujiheshimu, ubadhirifu nk havina shule na jinsi mtu anavyojiheshimu. Kama vingekuwa na shule basi vibaka wanaopigwa na kuchoma moto lingekuwa fundisho kwa wengine ili wasiibe lakini kila ucaho ni wizi
 
Ndio wa kulaumiwa ni baba yangu!! Hakunilea vizuri. Angenilea vizuri mkuu nisingiweza kuwa jambazi; mimi nimejifunzia wapi ujambazi wakati nimezaliwa sijui ujambazi?!?

Watoto wasiokuwa na akili nzuri huacha kabisa maadili ya wazazi wao na kujifunza kutoka mitaani kwa marafiki zao. Ufisadi wa akina Mkapa na Kikwete siyo kosa la Nyerere.

Kosa pekee la Nyerere ni lile la kuamini na kuhubiri kuwa kiongozi mzuri lazima atoke CCM, na hivyo kufanya mafisadi wote waone kuwa uanachama na ungozi ndnai ya CCM ni utakaso. Baada ya Nyerere kutoka madarakani na utaratibu wa vyama vingi kuanza kutumika nchini, yeye alitakiwa awe kweli baba wa Taifa kwa kuwa Neutral na kuacha kuishabikia CCM au chama chochote tena.
 
Hilo ni kosa mkuu! Mzazi anaefahamu namna ya kumlea na kumfunda mtoto katika misingi bora na imara hawezi kuvumilia mwanae ajifunze kutoka mitaani!! Ikiwa hivyo, nini maana ya kuwa mzazi? Mzazi alikua wapi mpaka mtoto akifunze mambo ya hovyo kwa watu wa mtaani?! Mkuu kama unaelewa kuhusu malezi nadhani itakua rahisi kunielewa ninachokimaanisha. Kwaiyo misingi mibovu ya Mkapa et al huwezi kuiepusha katika kuihusisha na Mwalimu!

Ingekua ngumu wa Mwalimu kuwa neutral wakati huo huo ni mwanachama wa CCM!! Pia Mwalimu alihubiri hivyo kwa kuamini kwamba mafundisho ya kiuongozi aliyoyatoa kwa makada wa CCM yalitosha kuwafanya kuwa wazuri. Hapa tunarudi mwanzo tena; Mwalimu kutokana alishindwa kugundua kwamba mafundisho yake hayakueleweka bali hao aliowafundisha walikua wanafiki katika kumridhisha ya kwamba wameelewa kumbe hawajaelewa!!
 
Tatizo lako unafikiri mwanadamu ni kama kitanda kwamba ukishakifikisha chumbani hakiwezi kujipeleka sebuleni, unasemaje kwa watoto mapacha lakini wakawa na tabia mbili tofauti, mmoja tabia nzuri na mwingine tabia mbaya?
 
Back
Top Bottom