Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
- Thread starter
- #21
Sasa huo walakini alaumiwe mzazi wako? Leo wewe ukiamua kuwa jambazi licha ya kwamba baba yako kakusomesha na kukuwezesha utasema baba yako ndio wa kulaumu? When do we take our own responsibilities?
Ikiwa hivyo mkuu, basi elewa kwamba mzazi wangu hakunipa malezi na mwongozo ulio bora. Mtoto akizaliwa anakua na almost zero memory (kichwa chake kinakua hakina aina yoyote ya jambo jema au baya). Sasa huo ujumbazi kajifunzia wapi? Inaweza ikawa hajajifunza kutoka kwa mzazi; akawa amejifunza kutoka pengine kwa ndugu, jamaa au marafiki. Hapo napo kuna swali,kwanini huyu mtoto apate nafasi ya kujifunza mambo mabaya kutoka kwa watu wengine? Mzazi wake alikua anafanya nini mpaka iwe hivyo? Kwanini mzazi hakufahamu mapema kwamba mwanae anajifunza mambo mabaya?! Kwa nini mzazi kama aligundua mwanae anaelekea kuwa jambazi, kwanini hakumwelekeza na kumfundisha ubaya wa ujambazi?!?
Hapo ndio linakuja pungufu jingine la Mwalimu; aliwaadhibu na kuwaogopesha sana viongozi wa wakati wake, lakini hakuwaelekeza na kuwafundisha kwanini aliwaadhibu; yaani makosa waliyofanya hao viongozi wake, Mwalimu hakuwafundisha namna ya kuyaepuka na kwanini yalikua ni makosa.