Nyumba hii inakalika ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Vingenevyo issues tunazozileta humu zisingekua MTAMBUKA basi Jf isingeleta maana as a society ! .
Same circumstance inayotokea kwangu leo, ndiyo itakayotokea kwako kesho.
Na ndiyo maana likikuchanganya fasta break ya kwanza mkekani.
Jana usiku, kaka yangu mkubwa alinifika nyumbani kwangu. Kunitaka ushauri, kaka yangu huyu ana mke na watoto wa4.
Aidha yeye na familia yake wanaishi nyumba ya kupanga.
Baba mkwe wake ana nyumba zaidi ya 3 kilichotokea Baba mkwe amempa offer akaiishi na familia yake kati ya nyumba hizo.
"mdogo wangu ni vyema nikaishi ukweni ? Sitokuja nyanyasika ?" (namnukuu).
Nimemuomba anipe time hadi sunday nami nifikiri cha kumjibu.
Wadau namie nimepitia kwenu mwanishaurije cha kumjibu ?
 
ukaishi ukweni??????????


nyie kabilagani?????????

sisi wengine ni matusi kuishi ukweni
 
mkuu inategemea na huyo mwanamke ana heshima kiasi kwa kaka yako'ningekuwa mimi hiyo ndo isue ya kwanza kuchungulia'vilevile hao wakwe zake ni watu wa kuheshimu watu?
Kama akiona hawafai hiyo nyumba wapangishe halafu hela ya rent waitumie kupanga mbali na wakwe zao
 
aende akaishi kambi popote duniani hapa
kama wanamuheshimu haina shida sema sio abweteke na kujiachia ndani ya miaka miwili ajiwekee lengo la kuhamia kwake
 
akaishi tu lakini akae akijua huo ndo mwanzo wa heshima yake kushuka na ikifika siku atafukuzwa kama mbwa
 
Sijui ninyi ni kabila gani, lakini kwetu ni matusi kwenda kukaa ukweni. Aangalie na heshima aliyojijengea huko kwa wakwe inaweza kushuka endapo atahamia katika mojawapo ya nyumba zao.
 
Its a taboo
Bora tukapange kwa Mfuga Mbwa
Nyumba ya baba Mkwe? Hell NO

Afadhali hata ingekuwa nyumba ya huyo dada
Atakuwa hana hata sauti kwa shemeji zake
Wakileta maneno maneno inabidi auchune tu
acheni hzo mbona kawaida tu jamani?
 
Heshima hailetwi na unaishi wapi. Mimi wakwe zangu wanaishi katika moja ya nyumba zangu na hawaniheshimu. At the same time binamu yangu ameoa kwa vibopa anaishi ktk nyumba aliyojengewa na mkwewe na wanampenda na kumuheshimu utafikiri wamezaliwa wote. Yeye na baba mkwe wake wanapiga masanga pamoja kila jioni na wanapeana 5 kama long time friends. Kwa kuwa sisi hatujui hiyo familia ya mkewe ni watu wa namna gani ni vyema akaliamua hilo mwenyewe
 
kama ana malengo mazuri ya maisha ya baadae huu ni wakati mzuri wa kuishi kwa wakwe. Unatunza akiba ya fedha ambayo angelipia pango then unanunua kiwanja....na wazazi wa mkeo watafarijika sana.
Ukiamua kutanua eti kwasababu hudaiwi kodi ya nyumba,fedhea itakuelemea hata kama wakwe hawatasema lolote...na hasa hilo ndio linamfanya akuombe ushauri. Vinginevyo wakwe zake wana nia njema tu tatizo ni jinsi ya kutumia nafasi hiyo kwa busara.
 
kwani kaka yako alipomuoa huyo aliendelea kukaa kwa baba yenu si aliondoka sasa kitu gani kimfanye aende kuishi ukweni?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom