nyumba chungu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
MUME wa Grace amemtaka mke wake huyo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kama hajafanikiwa kushika mimba basi atalazimika aione nyumba chungu kwa kuwa hataweza kuvumilia kuendelea kuishi nae kama mke na mume.

Grace alitamkiwa hayo juzi usiku wakati wakila walipokuwa wakipata chakula cha usiku wakiwa pamoja.

Grace alidai kuwa, wakati wakiwa mezani wakiongea mawili matatu huku wakiwa wanakula chakula cha usiku, ndipo mume wake alimtamkia hivyo na kumwambia azingatie hayo kwani alikuwa hayupo kaitka mzaha.

Grace alipomuuliza ni kwanini aliamua maamuzi hayo mumewe huyo alidai hana mjadala juu ya hilo kwani alishamueleza.

Hata hivyo Grace alimtaka mume wake huyo waende kituo cha afya wakaangalie huenda mmoja wao alikuwa na matatizo lakini mume wake alimjibu yeye ana uhakika hana matatizo anayoyafikiria wka asilimia zote na atamthibitishia hilo.

Alisema mwishoni mwa juma hili ataenda kuripoti tukio hilo kwa wazazi wake .
 
hii ni tamthilia au ni habari kutoka kwenye gazeti la uwazi......
 
Kuna jirani yangu nae alimfukuza mke wake kisa eti hashiki ujauzito, wameishi miaka mitano bila kitu. Yule mke akachukuliwa na jirani yake nyumba ya pili, baada ya miezi miwili mke akashika mimba, jamaa hivi sasa kwa aibu hashindi nyumbani, anatoka alfajiri sana na kurudi usiku sana kwa kuona aibu.
Huyo mume wa Grace aende hospital wakapime!!
 
dah
mume mnyanyasaji jaman
kuna mwanamke asiyependa kushika mimba jaman?tena ushaolewwa?ahh mbona anamowngozea donda kwenye kidonda?
ilibd mume wake awe anamfariji sasa si maneno shombo km ayo

jamaa anajifanya yupo fit kwa uhakika gan?usikute ana mtoto nje tayar?
dah pole
 
Huyo hana lolote,anajua tatizo lake ndiyo mana hataki kwenda kupima,anaamua kujikinga kwa kumfukuza mwanamke.
 
dah
mume mnyanyasaji jaman
kuna mwanamke asiyependa kushika mimba jaman?tena ushaolewwa?ahh mbona anamowngozea donda kwenye kidonda?
ilibd mume wake awe anamfariji sasa si maneno shombo km ayo

jamaa anajifanya yupo fit kwa uhakika gan?usikute ana mtoto nje tayar?
dah pole

Rose, kama kuna mtoto wa nje anaweza kuwa sio wake vile vile. Ni vizuri wakaenda wote Hospitali
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom