TUTUO
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 3,253
- 2,023
Huku mabondeni tu viwanja bei mbaya achilia mbali nyumba sasa iweje kati ya zilizouzwa ziko prime areas zikauzwa bei sio ya soko?Mkuu J.Kuu, watu wanacho sahau ni kwamba kinacho fanyika ni kwamba unangalia nyumba ulijengwa kwa gharama gani, je tangu wakazi/tenants waanze kulipa kodi, je, sum total ya kodi over the years ilishavuka return of investment na kuhanza kuvuna faida au la?
Tukiweka maanani kwamba nyumba hizo zilijengwa zamani sana ni dhahili ziliisha jilipa na faida juu, hivyo Serikali ikiwahuzia wapangaji kwa bei ya kawaida haitapata hasara after all lengo la Serikali lilikuwa ni kuwawezesha wapangaji kumudu kununua nyumba hizo kwa bei ndogo siyo Serikali kupata faida ya ziada.
Zamani hata National Housing Corp iliwahi kuwauzia tenants nyumba, hata Ulaya specifically Uingereza huwauzia wapangaji Council flats bila ya kujali kama mpangaji ni raia au la - what counts ni hela yako tu.
Kwa hiyo suala hili ya nyumba za Serikali tusilivalie njuga sana, hakuna haja ya kulichukulia kama ni suala la uhaini vile, mimi mpaka sasa nina imani kwamba Serikali ilikuwa na nia safi kuwauzia wapangaji nyumba.