Nyumba aliyoishi Kikwete Singida, funzo kwa wasomi

Kumbe kikwete ni mtoto wa dar

hivi sarakasi za dodoma hukuziona kweli?

Jk ni mtoto wa mjini pure.. ddc kariakoo ameruka sana...

mkwere wa kwanza kusoma special school kibaha na kufika udsm enz hizo hakuna google na kulamba degree yake ya economics... sio sociology au pspa degree za nyumbu.. sio hkl, hgl, hgk au klf combination za nyumbu wavivu.. kasolve sana econometrics tena bila google..

na basketball anacheza don bosco huku anaishi magomeni nyumban kwao..

mzazi wake ni chifu alikuwa na nyumba msoga na magomeni akiwa kwenye biashara zake dar..

Jk ni mhuni pure na mtoto wa mjini anakwambia ccm ina wenyewe na wenyewe ndio sisi.. hapo ameshakata watu wa kutosha tu dom huko..

asingekuwa mtoto wa mjini angefeli siku nyingi
 
Hiyo ndiyo iliyokuwepo kwa wakati ule. I presume that was the best house.... nyumba ya bati? Nyingine pengine zilikuwa zimeezekwa kwa nyasi. Ukitaka kujua kwamba nyumba hiyo ilikuwa nzuri angalia mpka sasa mika 46 bado ni nyumba ambayo anaweza kuishi binadamu, na nahisi kodi yake ilikuwa ya juu kulingalinisha na options nyingine zilizokuwepo
Nakuhakikishia Singida ya Wakati ule hiyo nyumba ilikuwa inakaliwa na Mabilionea wa sasa.
 
Kikwete aliishi miez 2 baadae akahamia hotelini.. Mkwere mnamjua mnamsikia... Kila alhamisi anaanza safari ya dar. Kuwahi weekend
 
Angalia alipozaliwa miaka hiyo nyumba hiyo nyuma ya kaburi hapo akiwa na mama Salma mbele ya sehemu ya nyumba alipozaliwa.Hakuzaliwa kama lofa wewe alikuwa mtoto wa CHifu.Mtoto wa mjini DAR kwenda SINGIDA KUISHI nyumba kama ile ilikuwa uzalendo wa hali juu mno wa kupenda kutumikia watu bila kujali wako mazingira mazuri au mabaya.

View attachment 321436
images
 
Hiyo nyumba yaweza kuwa ndiyo ilokuwa bora zaidi kwa mji wa Singida.

Haina tija na wala haihusiani na wakati kulinganisha maisha ya kijana wa sasa na yule wa 1974.

Too cheap. Tupa huko uozo huu maana sasa hivi graduates wanamaliza elimu yao na wanakaa kwenye chumba kimoja watano (wanabebana kuanzia Chuoni hostel hadi uraiani).
 
Kikwete alipomaliza digrii yake ya uchumi chuo kikuu cha Dar es salaam 1975 hakuwa na nyodo kama ambavyo baadhi ya wasomi wetu wakipata digrii hukataa kwenda kufanya kazi maeneo yenye shida.Kikwete alikwenda bila kinyongo akijua kuwa hata wale wa Singida ni wananchi wanaohitaji pia kuhudumiwa na mtu mwenye digrii.

Pamoja na usomi wake aliamua kukitumikia chama ambacho kilikuwa hakilipi maslahi mazuri kama mashirika ya umma.Uvumilivu wake ulisaidia baadaye zile dua za wanyonge kama hao wa singida kumwezesha kufika mbali

Miaka ile angeweza kataa akapata kazi nzuri tu kwenye makampuni kibao yaliyokuwa Dar es salaaam

Angalia nyumba aliyokuwa akiishi msomi kama yeye wa miaka ile haina maji wala umeme.Kuna kijana yeyote wa UKAWA hata leo hii na kadgrii kake koko aweza kukaa maeneo kama haya? Angepewa nyumba kama hii BAVICHA mwenye kadgrii koko Jamii Forums yote ingejaa matusi ya kutukana serikali hadi basi.

Nimeamini kweli mvumilivu hula mbivu.Vijana jifunzeni kwa Kikwete sio ukipata kadgrii unakuwa limbukeni mwezi wa kwanza tu wa ajira unataka kukaa kwenye ghorofa kama ni mwalimu wa shule ya msingi unajitia siwezi kaa nyumba ya udongo.Hiyo nyumba aliyokaa Kikwete akiwa na digrii ni ya udongo sembuse nyie wengine na vi-certificate?

1.%2BNyumba.jpg
Hivi kikwete naye anahesabiwa kati ya wasomi? Ni kweli alifanikiwa kumaliza udsm, lkn unajua alichokivuna?
 
Hivi kikwete naye anahesabiwa kati ya wasomi? Ni kweli alifanikiwa kumaliza udsm, lkn unajua alichokivuna?

Labda tusaidie kati ya KIKWETE na Mbowe nani msomi zaidi kuliko mwenzie
 
Kwa twarifa yako ufaulu wa JK haungeweza kumpa ajira sehemu yeyote nyeti usitake kudanganya watu hapa. Mahali pekee ni katika siasa ambako alionekana kupamudu kwa kutumia mdomo zaidi.
GPA yake ilikuwa sawa na ile Div 4 ya kidato cha nne jee unaweza mpeleka mchumi wa kiwango hicho kwenye shirika la umma linalotafuta watu mahiri? Kumbuka wakati huo ulikuwa wa Nyerere hakuna kumbeba mtu.
Uzi wako huu ni UPOTOSHAJI NA UONGO ULIOTUKUKA hivyo wadanganye vijana wadogo walioko hapo Lumumba wakati huu.
Wewe na wenzako waliokupa like hamna nidhamu, kwa ubaradhuli na kukosa kwako adabu kwa kiasi hiki hustahili kuwa mwanadamu. Au Mirembe kunakuhusu.

Huna adabu hata kwa wazazi wetu, jaribu kuwa na akili za kibinadamu hata kama humpendi. Heshima kwanza kwa wadogo na wakubwa.
 
Nidhamu huna wewe unaetaka kuishi kwa uongo. Kwani kama hakufaulu vizuri atakuwa peke yake? Nyie ndio mnaopindisha historia, mbona watu huwa wanaweka wazi historia zao za zamani hata kama ni kutopenda kuoga?
 
Weka hapa ya mzazi wako bila kuficha also na mafumanizi yake ili tupime ukomavu wako katika hilo unaloliamini.
 
Kwa twarifa yako ufaulu wa JK haungeweza kumpa ajira sehemu yeyote nyeti usitake kudanganya watu hapa. Mahali pekee ni katika siasa ambako alionekana kupamudu kwa kutumia mdomo zaidi.
GPA yake ilikuwa sawa na ile Div 4 ya kidato cha nne jee unaweza mpeleka mchumi wa kiwango hicho kwenye shirika la umma linalotafuta watu mahiri? Kumbuka wakati huo ulikuwa wa Nyerere hakuna kumbeba mtu.
Uzi wako huu ni UPOTOSHAJI NA UONGO ULIOTUKUKA hivyo wadanganye vijana wadogo walioko hapo Lumumba wakati huu.

Usiseme kitu usichokijua. Nani alikwambia graduates wakati huo walikuwa wanapata kazi kwa kutumia GPA? Kazi wakati ule zilikuwa nje nje za kuchukua tu.
 
Mwaka 1975 kukaa kwenye nyumba kama hiyo nakuhakikishia kwa sasa ni zaidi ya kukaa mbezi, unajua mwaka huo ni watanzania wangapi walikuwa na umeme☺, na kama leo hii anatoka madarakani kama rais na bado watu wanaishi kwenye tembe hapo unasemaje, jaribu kulinganisha na nyumba yake mpya ya bagamoyo, mifupa ya kuku.. Yehodaya
 
Sijui kwanini mara nyingi Mada ikiwa centred kwa kikwete, discussion huishia kuonesha kwamba kikwete au mleta mada ni mpuuzi au wote kwa pamoja wana hiyo sifa..
 
Kwa twarifa yako ufaulu wa JK haungeweza kumpa ajira sehemu yeyote nyeti usitake kudanganya watu hapa. Mahali pekee ni katika siasa ambako alionekana kupamudu kwa kutumia mdomo zaidi.
GPA yake ilikuwa sawa na ile Div 4 ya kidato cha nne jee unaweza mpeleka mchumi wa kiwango hicho kwenye shirika la umma linalotafuta watu mahiri? Kumbuka wakati huo ulikuwa wa Nyerere hakuna kumbeba mtu.
Uzi wako huu ni UPOTOSHAJI NA UONGO ULIOTUKUKA hivyo wadanganye vijana wadogo walioko hapo Lumumba wakati huu.
Umenikumbusha mbali mkuu. Aliulizwa huko ughaibuni alikokuwa anakwenda kuomba omba kuwa kwanini nchi yake ni masikini wakati ina utajiri wa rasmali za asili lukuki akasema hajui kitu naye anashangaa. Halafu mtoa mada asitupotoshe. Miaka ya 70 hizo ndizo zilikuwa nyumba za daraja la kwanza hapa nchini. Mwananchi wa kawaida asingeweza kumiliki nyumba hiyo. Hebu aende ukonga kulikuwa na nyumba 6 ambazo kwa wakati huo ziliitwa majumba 6. Leo ukienda hazionekani tena kama ni majumba na zimefunikwa na majumba ya wakati huu.Aende Kilwa road akaangalie zile nyumba za polisi za wakati huo. Au aende akaangalie zile zilizoitwa nyumba za reli wakati huo ambazo ndizo zilikuwa za kutisha wakati huo. Leo si mali kitu! Mtoa mada ameshindwa kutofautisha mabadiliko ya thamani ya kitu kulingana na wakati.Mshahara mkubwa kwa wakati huo ilikuwa sh 300 na zilikuwa ni hela nyingi sana. Sasa kwa akili atasema wasomi wa sasa na kwa maisha ya wakati huu wakubali hiyo 300 Huyu jamaa kadhihirisha ujinga wake!
 
Weka hapa ya mzazi wako bila kuficha also na mafumanizi yake ili tupime ukomavu wako katika hilo unaloliamini.
Kumbe unataka ya mzazi? Basi wangu toka enzi hizo hakuwahi kuwa mwanasiasa mpaka anastaafu utumishi. Huyo unayetetea Nazi take ya siasa ndio inayotaka awe wazi kwa kila kitu kwani ishi yake ilikuwa inategemea kura
 
Sijui kwanini mara nyingi Mada ikiwa centred kwa kikwete, discussion huishia kuonesha kwamba kikwete au mleta mada ni mpuuzi au wote kwa pamoja wana hiyo sifa..
Hilo nalo neno. Nakumbuka yale maswali ya kuchagua majibu kuwa A na B ni sahihi
 
Back
Top Bottom