Nyota Nyekundu Special Thread

Mimi nilikuwa mpenzi wa TKY Stars, huu ni wasifu mfupi wa timu yangu iliyochukua ubingwa mwaka 1986.


Suleiman Mathew
KWANZA kabisa nawashukuru wote
waliopiga simu na kutuma ujumbe mfupi
kuwa, ingekuwa vipi kama MECCO na Tukuyu
zingekutana, ipi ingeibuka kidedea?
Baada ya kuandika hoja hii, wengi walitoa
maoni yao kuhusu ingekuwaje kama
Tukuyu Stars ya mwaka 1986 na Mecco ya
mwaka 1988, zingekutana katika Uwanja
wa Sokoine Mbeya.
Kati ya waliotoa maoni yao, 38 wameipa
nafasi Tukuyu Stars kuwa ingeshinda huku
27 wakiipa nafasi Mecco kuwa, ingeshinda.
Kwa idadi ya maoni yote, Tukuyu Stars
imeizidi Mecco kwa kura 11.
Binafasi nasema asanteni nyote kwani
imeonyesha kweli watu wamekuwa
wakizifuatilia timu hizo mbili na kubwa
zaidi, wakiridhika kuwa zilikuwa ni timu
zilizokuwa zikicheza soka ya uhakika.
Baada ya kusema hayo, naomba leo
niwaletee kwa ufupi wasifu kila mchezaji
wa timu hizi ambao niliwataja kwa timu
zote mbili ili kumfanya msomaji upate
ufahamu kwa kiasi fulani kuwa wachezaji
hawa walikuwaje, nikianza na Tukuyu Stars:
Mbwana Makata: Ni kipa wa aina yake
aliyekuwa anajua kusoma mchezo na kutoa
maelekezo kwa mabeki wake na alikuwa
mkali kwa mabeki wazembe wenye kufanya
makosa ya kijinga.
Langoni, alikuwa na uwezo sana wa
kucheza krosi, licha ya kuwa na kimo cha
kawaida, hivyo msimu wa mwaka 1986,
alikuwa kati ya wachezaji waliochangia kwa
kiasi kikubwa mafanikio ya Tukuyu Stars.
Ally Kimwaga: Huyu alikuwa beki wa kulia,
aliyekuwa na uwezo wa kupanda mbele
mara kwa mara kwa dakika zote 90.
Alikuwa na mbio sana baadhi ya mabao
iliyokuwa akifunga Tukuyu Stars, yalitokana
na beki huyu.
Hakuwa mchezaji mwenye makeke, lakini ni
mwajibikaji, sikumbuki kama aliwahi hata
kupata kadi yoyote uwanjani. Aidha, alikuwa
beki asiyekubali kupitwa au kwa maneno
mengine beki king'ang'anizi.
Daniel Chundu: Beki wa kushoto asiyekubali
kupitwa kirahisi huku akipanda mbele na
burudani ilikuwa pale napo anapokumbana
na mabeki wa upande wa pili, ilikuwa ni
shughuli kubwa ya beki dhidi ya mabeki.
Uchezaji wake ulikuwa ukiwapa wakati
mgumu mawingi wa kulia na kwa vile
hakuwa akitumia mguu wa kushoto,
alikuwa anawasubiri mawingi katikati ya
uwanja na kweli alifanya kazi yake vizuri.
Godwin Aswile: Alikuwa ni beki wa aina
yake asiyetaka masihara hata chembe.
Alikuwa kisiki kwa mipira ya aina yoyote ya
juu na chini na ilikuwa vigumu sana
kumpiga chenga za ovyo huku akiwa tayari
kucheza soka ya kistaarabu hata ya kihuni.
Waulize wachezaji machachari wa Red Stars,
jinsi Aswile ambavyo alimfanyia rafu mbaya
Roster Ndunguru, kisa ni kutokana na
ngebe ya Ndunguru uwanjani. Kwa hakika,
alikuwa ni beki wa aina yake dimbani.
Suleiman Mathew: Akiwa beki wa mwisho,
alikuwa hana makeke mengi zaidi ya
kutumia akili katika kukabiliana na
washambuliaji, alitumia nguvu ilipobidi na
alikuwa anajua jinsi ya kujipanga ili kuzuia
mashambulizi.
Alicheza nafasi ya ulinzi wa kati ilivyostahili
hadi mwaka huo kuchaguliwa timu ya taifa.
Aston Pardon: Huyu alikuwa kiungo wa
nyuma alikuwa mahiri katika kukaba na
kupanda mbele kuongeza mashambulizi.
Alikuwa na uwezo wa kucheza soka ya aina
yoyote alipoona timu inaelemewa yeye ndiye
alikuwa mtulizaji wa timu alikuwa anapenda
sana kila mpira upitie kwake kwa kweli
alikuwa na uwezo wa hali ya juu.
Yusuph Kamba 'Sharif': Kiasili, ni mchezaji
wa kiungo namba 8, lakini Kocha Athumani
Juma ambaye kwa sasa ni marehemu,
alikuwa akimtumia sana kama wingi wa
kulia.
Ni mchezaji aliyekuwa na kipaji cha soka,
akili na alikuwa anajua jinsi ya kutoa pasi za
uhakika Yanga wanamkumbuka kwa jinsi
alivyowasumbua Uwanja wa Taifa, kisha
kutoa krosi iliyomkuta Richard Lumumba
aliyefunga bao la ushindi licha ya yeye kuwa
Yanga damu, kwani kitu alichokuwa amejali
ni wajibu wake.
Katika mechi zote, nakumbuka bao lake la
mita 30 alilowafunga Coastal Union pale
Tanga.
Peter Mwakibibi: Kiungo wa kati, aliyekuwa
na nguvu, mashuti na uwajibikaji uwanjani,
aliimudu vema nafasi yake katika
kusambaza mipira kwa washambuliaji na
alikuwa na uwezo wa kupambana na yeyote
wa kiungo, wengi walimheshimu.
Richard Lumumba: Hakuna ubishi kwa
mshambuliaji huyu alikuwa hatari sana kwa
mipira ya juu na alifunga mabao mengi kwa
kichwa, ingawa alikuwa na uwezo wa
kufunga hata kwa mguu.
Alikuwa kipande cha mtu asiyeogopa
chochote, hivyo kuchangia kwa kiasi
kikubwa ubingwa kwa Tukuyu Stars mwaka
1986.
Alimudu sana nafasi yake akiona mambo ni
magumu alikuwa akicheza kibabe.
Kelvin Haule 'Super': Nyota nyingine ya
ushambuliaji ya Tukuyu Stars, alikuwa na
akili ya ziada na uwezo wa kufunga mabao
kutoka pembe yoyote ya uwanja.
Aidha, kasi yake uwanjani ilikuwa ya ajabu
hata kuwa kivutio uwanjani, alifunga bao
aina yake kule Shinyanga dhidi ya Mwadui,
ambalo litabaki kukumbukwa ambalo
lilitosha kuipa Tukuyu Stars ushindi wa bao
1-0.
Karabi Mrisho 'Nnunduma': Nyota
iliyopotea ghafla katika soka ya Tanzania.
Alikuwa wingi ya kushoto hatari sana.
Aidha, naamini kama angeendelea kucheza
soka, Celestine Sikinde Mbunga na Edibily
Lunyamila, wangekutana na upinzani
mkubwa kwani alikuwa na kasi kubwa.
Alikuwa na uwezo wa kupiga chenga kwa
kumfuata adui na krosi za uhakika. Hata
hivyo, aliumia goti katikati ya ligi
inahuzunisha kwamba hakupata nafasi ya
kuonyesha kipaji chake na hilo jina la
Nnunduma alipewa na wapenzi wa soka wa
Mbeya wakimlinganisha na mshambuliaji wa
Zimbabwe.
Kocha wa Tukuyu Stars alikuwa ni Athumani
Juma Kalomba ambaye kwa sasa ni
marehemu.
Wachezaji wa akiba ni: Seleman Mwankenja
(kipa), Hussein Zitto, John Alex Lwena,
Abdallah Shaibu, Dickson Makwaya, Taisi
Mwaliyoga, Danford Ngessy na Mohamed
Salehe.
Hawa wote walishiriki kikamilifu katika
kuchangia ubingwa wa Tukuyu Stars
mwaka 1986. Walikuwa wachezaji wazuri,
isipokuwa tatizo lilikuwa ni kukosa nafasi
na walipopata walitumia vizuri.
Angalia wachezaji kama John Alex na
Danford Ngessy walivyowika miaka
iliyofuata.
Maelezo haya mafupi ya wasifu wa nyota
waliokuwa wakiunda kikosi cha Mecco cha
mwaka 1988, yataendelea Jumatatu ijayo.
Mathew ni mchezaji wa zamani aliyewahi
kung'ara na klabu mbalimbali, ikiwemo
Yanga na timu ya soka ya Tanzania, Taifa
Stars, ambaye kwa sasa anamiliki kituo cha
michezo cha Tanzania Sports Catalyst
kilichopo Kwembe, Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
 
kwa heshima na taadhima, naienzi hii timu ya kijiweni mtaa wa congo ambayo ilishiriki ligi kuu tanzania bara na kuwa tishio kwa kupiga mpira na buti.
Rosta ndunguru na wenzako, tunawakumbukeni sana kwa kuleta na kucheza soka tamu la ushindani nchini mwetu tanzania

nyota nyekundu walikuwa wanapigia tizi ilipo benjamin mkapa sec school chini ya coach wao (rip) omar mahadhi, dah ilikuwa kila siku kabla ya kwenda shule nipitie kuwacheki kina moh'd nyauba!
 
nyota nyekundu walikuwa wanapigia tizi ilipo benjamin mkapa sec school chini ya coach wao (rip) omar mahadhi, dah ilikuwa kila siku kabla ya kwenda shule nipitie kuwacheki kina moh'd nyauba!

Nasikia Rosta Ndunguru alikuwa na mapengo, kwa hiyo alikuwa anatumia meno ya bandia.
Mpira ukitaka kuanza anayotoa kisha anaingia uwanjani.
 
mechi za Nyota Nyekundu na Yanga zilikuwa kali sana.
Yanga walikuwa wanapata kipindi kigumu mno
 
Mnanikumbusha mbali sana, wapi timu za Sigara, Pilsner etc hizi timu pamoja na Nyota Nyekundu ilikuwa zikikutana na Yanga inakuwa patashika hasa hasa
 
Mnanikumbusha mbali sana, wapi timu za Sigara, Pilsner etc hizi timu pamoja na Nyota Nyekundu ilikuwa zikikutana na Yanga inakuwa patashika hasa hasa
Soka letu leo liko hoi, hii ni hatari, TFF badala ya kukuza soka inakaa kungoja mechi za Simba na Yanga
 
Asanga Aswile, Betwel Africa, Said Mrisho (ZICCO wa Kilosa) Peter Tino, Hamis Fande, Isihaka Majaliwa.... wako wapi hawa jamani?
 
Jamani wanajf hebu tujaribu kufikiria soka
la tanzania wakati ule mapaka sasa, je
unafikiri limepanda kiwango ama
limeshuka? na unadhani nani kahusika ktk
kulishusha ama kulipandisha kiwango?
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na
wachezaji kama akina Husein Masha,
Athuman China, Idd Pazi, Rosta Ndunguru,
Pita Tino, Nteze John nk. Kulikuwa na timu
kali ambapo zilikuwa zinatowa upinzani
sawa, timu hizo kwa kujikumbusha ni
kama:-
1. Nyota nyekundu
2. Sigara
3. Pilsner
4. Simba
5. Yanga
6. Coastal Union
7. African Sports
8. Majimaji
9. RTC Kigoma
10. CDA Dodoma
11. Tukuyu Stars
12. Mecco
13. Pamba
14. Ndovu
15. Bandari Mtwara
16. Lipuri Iringa
17. Ushirika Moshi
Hebu angalia timu hizo wakati huo kisha
linganisha na timu zetu za sasa. Wakati
huo mabasi ya mikoa yalikuwa yanasafiri
usiku tu
 
JOHN ONDOLLO CHACHA:- Mtoto wa mwanamuziki aliyerithi soka.


INAWEZEKANA kabisa nyoka akazaa mjusi?
Sidhani; mara nyingi nyoka huzaa nyoka.
Lakini imetokea kwani nyoka amezaa mjusif
Msemo huo unaweza kwenda sambamba na
aliyekuwa mchezaji mahiri wa zamani, John
Ondolo Chacha ambaye alicheza katika timu
ya Lipuli ya Iringa msimu wa 1991-92
akitokea jijini Dar es Salaam.
Chacha ambaye alipachikwa majina ya Niva,
Pembe ya Ndovu na Thobias Ocholla
kutokana umahiri wake wa kucheza beki
namba nne katika timu alizowahi kucheza,
baba yake alikuwa ni mdau mkubwa wa
sanaa.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii,
anaanza kwa kuelezea tofauti iliyoko kati ya
soka la sasa na la miaka waliyocheza wao.
Anasema, ilikuwa ni kwamba, wao
walijituma katika mazoezi binafsi, kuliko wa
sasa ambao ni wavivu.
Anaongeza kuwa, sababu ya uvivu wa
mazoezi, inasababisha kupozesha mpira
katika mashindano ya kimataifa, ambayo
Watanzania wengi wanajitokeza
kuwashangilia.
Chacha anasema, anashukuru elimu kubwa
aliyoipata kutoka kwa Kocha Abdallah
Kibadeni ‘King Mputa’, ambaye mara nyingi
alimpa mawazo mengi, ambayo yalimsaidia
katika kucheza soka.
Anaeleza, katika safari yake ya soka, alipata
elimu kutoka kwa aliyekuwa Naibu Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Joel Bendera, ambaye aliwafundisha wakiwa
katika timu ya Shekilango huku Bendera
akiishi katika ghorofa za Shekilango.
Pamoja na kupata elimu kutoka kwa
makocha ambao wazoefu, lakini alitatizwa
na suala la uvumilivu wa kukaa katika timu
moja zaidi ya miaka minne.
Ananasema, alianza kusakata soka mwaka
1986-87 alipoajiriwa katika kiwanda cha
Alminium Africa kilichopo Temeke, ambako
alicheza msimu mmoja na kukutana na
kocha Kibadeni katika timu ya Future,
iliyokuwa na maskani yake Urafiki jijini Dar
es Salaam.
Akiwa Alminium, alikutana na wachezaji
wengi ambao baadhi yao walicheza Ligi
daraja la kwanza (sasa hivi Ligi Kuu
Tanzania bara), mmojawapo akiwa ni
kiungo Suleimani Ally aliyewahi kucheza
Yanga miaka ya 1987-88.
Hakudumu sana Alminium, akarejea timu
iliyoko karibu na nyumbani kwao
Shekilango ya Future, iliyokuwa na vijana
wengi ambao walikuja kuwa tishio katika
medani ya soka la Tanzania.
Alipokuwa Future, timu hiyo ilikuwa chini ya
Kibadeni kipindi hicho, ambako alikuwa ni
mfanyakazi wa kiwanda cha nguo cha
Urafiki akiwa ametokea masomoni nchini
Ujerumani kwenye kozi ya ukocha.
Kutokana na umahiri wake uwanjani,
Kibadeni alimpeleka kiwanda cha Urafiki na
kupata kazi kitengo cha ufundi wa magari,
akiwa pia ni mchezaji.
Akiwa Urafiki, alifundishwa pia na Salum
Madadi ambaye ni Ofisa wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), na kukutana na
wachezaji wengine kama Wema Juma,
Kenny Mwabulambo, Habibu Kondo, Muhesa
Kihwelu, Jumanne Ucheche ambaye baadaye
walihamia Lipuli ya Iringa na John Ngunde
ambaye sasa hivi ni mmojawapo ya Maofisa
Watendaji wa Mitaa jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo ilikuwa mojawapo ya timu ngumu
katika ligi ya soka Mkoa wa Dar es Salaam,
lakini iliishia ligi ya Kanda ya Dar es Salaam.
Kutokana na umahiri wa ufundishaji,
Kibadeni alichukuliwa na Chama cha Soka
Tanzania (FAT), sasa TFF kuifundisha timu ya
Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, hapo Chacha
akahamia Nyota Nyekundu yenye maskani
yake Kariakoo Mtaa wa Congo jijini na
kukutana na Faustine Kibingwa, Rosta
Ndunguru, Ayoub Mzee na John Bosco,
ambako aliendelea kupata uzoefu mkubwa,
kwa sababu mara kadhaa timu hiyo ilicheza
mechi za kirafiki na Taifa Stars.
Mara nyingi, Kibadeni alimweleza Chacha
kwamba, kwa jinsi anavyocheza soka,
atafika mbali zaidi ya Tanzania, ila kikubwa
zaidi ni kuzingatia miiko ya mchezo huo na
kuwa na uvumilivu.
Mwaka 1989, alichukuliwa na timu ya
kiwanda cha Twiga Cement kilichopo Wazo
Hill jijini Dar es Salaam, kutokana na umahiri
akiwa uwanjani, akapewa ajira kiwandani
hapo na kukutana na ofisa wa TFF hivi sasa,
Idd Mshangama akiwa kocha.
Mwaka 1991, alihamia Lipuli ya Iringa baada
ya kuonekana katika mashindano ya ligi
daraja la pili ambako alikutana na akina
Peter Lugenzi, Willy Komakoma, David Kika,
Elisha John, Nurdin Gogola na Hassan
Mwajeki.
Kipindi hicho kikosi cha Lipuli kilikuwa chini
ya kocha Mzambia, Donald Phiri ambaye
aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya
Zambia na Pascal Bella, ambako alikutana na
viwango zaidi, kwa sababu alipata nafasi ya
kucheza na timu kama Simba, Yanga, Coastal
Union, African Sports na Milambo ya Tabora.
Pamoja na timu yao kuwa bora katika ligi
daraja la kwanza, lakini anaikumbuka mechi
waliyofungwa mabao 5-0 na Pamba ya
Mwanza, ambayo ilikuwa na wachezaji
mahiri kama Kitwana Seleman, Nteze John
Lungu, Madata Lubigisa na wengineo.
Anasema, cha kushangaza baada ya mchezo
huo uliochezwa jijini Mwanza, tajiri wa
machimbo ya Mgusu aliialika timu hiyo kwa
gharama zake kucheza na timu yake ya
mgodini.
Katika mchezo huo, alikutana na
mshambuliaji mahiri wa timu hiyo, Eliud
Ngessa ambaye alicheza naye utafikiri
wanawania nafasi ya kufuzu kombe la
dunia, hadi mwamuzi wa mchezo aliwatoa
nje kwa kadi nyekundu.
Anaongeza kuwa, cha kushangaza zaidi
baada ya kutolewa wachezaji hao, mpira
ulipooza sana, hali ambayo ilisababisha
mwamuzi huyo kuwaita na kuwaamuru
warejee kwa mara nyingine uwanjani, hali
ambayo hakuelewa refa huyo alitumia
sheria ipi, kwani mchezaji akitolewa nje kwa
kadi nyekundu haruhusiwi kurejea
uwanjani mara nyingine.
Kwa kuwa tamaa yake ilikuwa ni kucheza
nje ya mipaka ya Tanzania, akatoka Lipuli na
kurejea Dar es Salaam msimu wa 1992-95,
ambako baadhi ya viongozi wa timu ya
Konde ya Pemba, wakamtaka akachezee
timu yao katika ligi kuu kisiwani humo.
Akiwa na wachezaji wenzake sita kutoka
Dar es Salaam, Abdul Ramadhani ‘Mashine’,
Mohamed Mwape, Abdallah Mohamed, Omar
Mbweza na Ramadhani Abdallah, baadaye
timu hiyo ilifuzu kucheza ligi ya Muungano
katika mashindano ya kila mwaka.
Wakati akiwa katika hatua za mwisho za
mkataba wake, timu za Jamhuri na Kipanga
ambazo zote ni za Jeshi la Wananchi
zilimuhitaji, alikataa na kurejea Dar es
Salaam, ambako alikutana na Kibadeni kwa
mara nyingine, ambaye alimwelekeza
kwamba, kutokana na umahiri alionao
katika soka, asubiri kidogo atamtafutia timu.
Kwa kuwa hakuwa na uvumilivu, alielekea
Kenya na kufanya majaribio timu za AFC
Leopards, Kenya Breweries na Mumias Sugar
ambako ndipo alipofanikiwa timu hiyo
iliyokuwa ikifundishwa na kocha Dennis
Munyendo na kukutana na nyota kama
akina Mark Serengo na Nika Hammer.
Mwaka 1996-98 akajiunga na Posta ya
Kakamega nchini humo, ambako akiwa
katika timu hiyo, alipata hisia ya kumrejea
Mungu kwa kenda chuoni kupata elimu ya
dini katika chuo cha Mtakatifu Makarios cha
Kenya na kufanikiwa kupata cheti cha
uchungaji.
Anasema, kipaji chake katika soka, alikirithi
kutokea kwa babu yake, aliyekuwa akiitwa
John Alyango, ambaye aliwahi kucheza
Kombe la Gossage.
John Chacha, ni mtoto wa pili kuzaliwa kati
ya 12 wa marehemu Mzee Ondolo John
Chacha, ambaye alikuwa ni mojawapo ya
wadau mahiri wa muziki na sanaa hapa
nchini, ambaye aliweka mikakati ya kukuza
na kuendeleza sekta hiyo kwa kujenga kituo
kikuu nyumbani kwake Shekilango jijini Dar
es Salaam.
John aliyezaliwa miaka 45 iliyopita, hivi sasa
ana mke na watoto wanne na ni mchungaji
wa kanisa la Full Categro lililopo katika kituo
cha Sanaa Shekilango jijini Dar es Salaam.
Anasema, mipangilio iliyopo kwa sasa ni
kukuza na kuendeleza sanaa sambamba na
michezo mignine kama soka na kuwa kituo
cha kusaka vipaji na kuviendeleza kimataifa.
Anatoa wito kwa TFF, kufanya mabadiliko
makubwa ya Kamati ya Ufundi, ambayo
inaonekana kuelemewa na mzigo, kutokana
na kwamba, hivi sasa Tanzania hakuna timu
inayoeleweka ya Taifa.
Anapendekeza, Kamati hiyo inaweza
kuongozwa na Watanzania kama Kibadeni,
Adolf Rishard na Charles Boniface Mkwasa,
ambao wana elimu ya kutosha ya kuifanya
kazi hiyo.
Anatoa wito pia kwa mawakala, kuwaandaa
wachezaji kisaikolojia ili wawe mfano bora
katika timu za nje na kuwataka pia
wachezaji wa sasa, kuacha uvivu na
kumuiga Mohamed Ngulungu ambaye
alicheza timu ya Taifa miaka 10 bila ya
kupoteza uwezo wake.
 
MAKATA, Mbwana: Golikipa mahiri wa zamani wa Tukuyu Stars ya Mbeya. Akiwa Tukuyu alicheza na akina Godwin Aswile, Karabi Mrisho, Kelvin Haule, Yusuph Kamba, Aston Pardon, Danford Ngessy, Peter Mwakibibi, John Alex, Daniel Chundu, Ally Kimwaga na Suleiman Matthew tukuyustars1986.JPG
 
MAKATA, Mbwana: Golikipa mahiri wa zamani wa Tukuyu Stars ya Mbeya. Akiwa Tukuyu alicheza na akina Godwin Aswile, Karabi Mrisho, Kelvin Haule, Yusuph Kamba, Aston Pardon, Danford Ngessy, Peter Mwakibibi, John Alex, Daniel Chundu, Ally Kimwaga na Suleiman MatthewView attachment 55776


Waliochuchumaa wapili toka kusho sie marehemu RICHARD LUMUMBA?
 
Rosta Ndunguru na Salum Kabunda Ninja ni yupi alikuwa mkali wa madaluga?

Naweza kusema Salum Kabunda ndio akapewa jina la NINJA,Rosta Ndunguru alikuwa anacheza nafasi ya kiungo hakuwa na kimo lakini alikuwa matata sana naweza kumfananisha na Joey Barton wa QPR...Utoto wa mjini mwingi uwanjani.
 
red star watoto wa mtaa wa Congo na Aggrey, lile jengo lao kwa sasa ni fremu za maduka na nafikiri lilishauzwa
marehemu Amir Ally "Bamchawi" alikuwa mmoja wa waanzilishi na viongozi wa timu hii ambayo nadhani ilimeguka kutoka Sunderland(Simba) na ndio maana iliposhuka daraja na kuelekea kufa mwaka 1991 Bamchawi alirudi Simba na kuwa mwenyekiti akiifunga Yanga mara kwa mara
Roster Ndunguru na muhiddin cheupe ndio wachezaji maarufu ila Ndunguru nafikiri alizidi kwa rafu
 
Back
Top Bottom