Nyoni hayuko ofisini, yuko kazini

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Blandina Nyoni aliyetangazwa kusimamishwa kazi na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda bado yuko kazini.Ziara yangu ya 'kiintelijensia' Wizarani hapo asubuhi ya leo imebainisha hayo.Nikijifanya ni mtu mwenye 'appointment' na msimamishwa huyo ili nimletee nyaraka zake toka kwenye Kampuni yetu ya Uwakili,nilielezwa kuwa ingawa Nyoni hapatikani ofisini tangu tarehe ya tamko la Waziri Mkuu,bado anaendelea kufanya kazi zake zinazoambatana na posho na marupurupu stahiki,akiwa nyumbani kwake au mahali popote pengine.

'Hatakiwi kuonekana hapa Ofisini ili vuguvugu la mgomowa Madaktari liishe' alieleza mmoja wa wasaidizi wa Nyoni. Imebainika kuwa hadi leo,si Nyoni wala Mtasiwa(Mganga Mkuu wa Serikali-Deo Mtasiwa) aliyepokea barua rasmi ya kusimamishwa kazi.Madaktari na watanzania kwa ujumla wamefanywa mazuzu? Mwenye masikio na asikie...
 
Natamani tungekuwa na ujasiri kama siria, baadhi ya issue zingekuwa imara
 
Diamod bonds ni NGUMU stable sana, which make Diamond one of the hardest stones on earth...........so is CCM katika kusikiliza mambo ya maana na kyatenda...........Kigmu sana hiki chama.

images
 
Madakitari, kwa zarau hizi,
itakuwa jambo la maana zaidi kuanza kwa
mgomo mpya kuanzia mtoto wa mkulima
na safu yote ya afya wale benchi kwanza.
 
Nashauri madakitari wagome tena
kama huyu mama ataonekana ofisin au mawaziri kutoachishwa kazi mpaka wasimamishwa na
sheria ichukue mkondo wake
 
Inakuhusu nini? Hata kama akiachaia ngazi bado atapatakazi kwenye international org. You should be having better things to do than wasting time looking for majungu.
 
Hivi hakuna Balozi wetu nje ya nchi anayekaribia kustaafu au U-Balozi ambao "upo wazi"?
 
Inakuhusu nini? Hata kama akiachaia ngazi bado atapatakazi kwenye international org. You should be having better things to do than wasting time looking for majungu.

kwa wewe sio muathirika wa utendaji kazi wake M-BOVU?? HAYA SIO MAJUNGU NI UKWELI, NA WALA JF SI PAHALA PA MAJUNGU...

AU NI SHUGAMAMII WAKO!!!!????

WEKA WAZI
 
Tatizo sio Nyoni...

Tatizo ni JK, Pinda na CCM...

Badala ya kuwa gerezani muda huu unaweza kuta yuko hata nje ya nchi anakula maisha kwa kodi zetu. BIG UP MAMA NYONI
 
Jamani hivi bado kweli mnaamini kwamba kuna jambo la maana litaamliwa na hawa jamaa wa ccm.. kama kuna watu bado mnamawazo hayo poleni sana, ... yaani ccm ni full usanii tu .. tuna kazi kubwa ya kufanya. yaani ukisoma tuhuma za huyu mama hutaona ajabu kwa nini huduma za afya na za kijamii kwa ujumla ni mbovu na wala hazina mwelekeo wa leo wala kesho, sasa huyu ni mmoja tu wapo wangapi wa aina yake!

Dr Slaa yuko sahihi huduma bora za jamii tena bure au kwa gharama za chini sana zinawezekana TZ.
 
Nimepoteza imani 100% na pinda..he's such a good liar..mbona ana tudhalilisha watu wenye nyota simba?? sisi ni wakali na wachapa kazi..amuone mwenzake lowassa..anatia kinyaa kwakweli..nasikia mwanasheria ..sijui kama kuna kesi hata moja alishinda,,kutwaaa kudanganya tu aibu hata haoni..
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Blandina Nyoni aliyetangazwa kusimamishwa kazi na Waziri Mkuu,Mizengo Pinda bado yuko kazini.Ziara yangu ya 'kiintelijensia' Wizarani hapo asubuhi ya leo imebainisha hayo.Nikijifanya ni mtu mwenye 'appointment' na msimamishwa huyo ili nimletee nyaraka zake toka kwenye Kampuni yetu ya Uwakili,nilielezwa kuwa ingawa Nyoni hapatikani ofisini tangu tarehe ya tamko la Waziri Mkuu,bado anaendelea kufanya kazi zake zinazoambatana na posho na marupurupu stahiki,akiwa nyumbani kwake au mahali popote pengine.

'Hatakiwi kuonekana hapa Ofisini ili vuguvugu la mgomowa Madaktari liishe' alieleza mmoja wa wasaidizi wa Nyoni. Imebainika kuwa hadi leo,si Nyoni wala Mtasiwa(Mganga Mkuu wa Serikali-Deo Mtasiwa) aliyepokea barua rasmi ya kusimamishwa kazi.Madaktari na watanzania kwa ujumla wamefanywa mazuzu? Mwenye masikio na asikie...

Inawezekana kabisa. Pinda kila siku hutia siasa, alishindwa kwa jairo na kama si Bunge kuingilia kati Jairo leo angekuwa ofisini. Werevu hawaambiwi tazama. Mwerevu ukiona au kusikia kaa kimya.

Kwa taratibu za Serikali, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu ni waajiriwa wa Serikali. Hivyo wanalindwa na Sheria za Utumishi wa Umma. Hata kumsimamisha mpaka vikao husika na halali vikae ndio maamuzi yachukuliwe. Pinda alitakiwa kusema tu kuwa maamuzi ya watuhumiwa yatachukuliwa mara baada ya vikao halali na si kuropoka jukwaani. Sheria ya Utumishi wa Umma hairuhusu hivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom