Nyongeza ya Mishahara na asilimia ya punguzo kwenye kodi

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Naomba kuuliza, hivi kwa ambao tumeshapokea mishahara je tumeliona lile punguzo la kodi? Kama imeonekana imeonekana kwa kiasi gani au imeongezeka sawa na jinsi mishahara ingeongezwa?

Kila Mwaka Kikwete alikuwa anaongeza si chini ya sh. 25,000 kila tunapoanza mwaka wa fedha. Mfano kuna mtumishi ambaye anapokea 177,000 baada ya makato yote ikiwemo mikopo aliyoichukua kutoka taasisi mbali mbali, salio hilo kwenye payrol ni la mwezi wa 3,4,5,6 sasa mshahara ambao ni wa mwezi wa 7 ambao ndio mishahara mipya au niseme ni mwaka wa fedha wa serikali unaonyesha kumeingizwa sh 187,000. Sasa nauliza hili ndio ongezeko baada ya kupunguza kodi kutoka 11% hadi 9%?

Huyu mtumishi mshahara wake ni sh Laki 5, kwa maana nyingine yumo kati ya wale ambao watapunguziwa kodi kwenye mishahara yao. Naomba mnieleweshe maana kuna tangazo kuwa hakutakuwepo na ongezeko la mshahara kwa watumishi kwa mwaka huu.

Je, kuna uwezekano wa ongezeko kuwepo katikati ya mwaka wa fedha? Kuna haja ya kubaki na lile ongezeko la Kikwete la kila mwaka au ongezeko lifanyike kwa mara moja tu kuliko hizo % zilizotajwa.
 
Kuna mtu aliniambia kuwa nyongeza itaanza kuonekana mwezi wa nane,sasa sijui ni kweli.
 
Naomba kuuliza hivi kwa ambao tumeshapokea mishahara je tumeliona lile punguzo la kodi? kama imeonekana imeonekana kwa kiasi gani au imeongezeka sawa na jinsi mishahara ingeongezwa? kila Mwaka Kikwete alikuwa anaongeza si chini ya sh. 25,000 kila tunapoanza mwaka wa fedha. mfano kuna mtumishi ambaye anapokea 177,000 baada ya makato yote ikiwemo mikopo aliyoichukua kutoka taasisi mbali mbali, salio hilo kwenye payrol ni la mwezi wa 3,4,5,6 sasa mshahara ambao ni wa mwezi wa 7 ambao ndio mishahara mipya au niseme ni mwaka wa fedha wa serikali unaonyesha kumeingizwa sh 187,000 sasa nauliza hili ndio ongezeko baada ya kupunguza kodi kutoka 11% hadi 9%? huyu mtumishi mshahara wake ni sh Laki 5... kwa maana nyingine yumo kati ya wale ambao watapunguziwa kodi kwenye mishahara yao. naomba mnieleweshe maana kuna tangazo kuwa hakutakuwepo na ongezeko la mshahara kwa watumishi kwa mwaka huu. Je kuna uwezekano wa ongezeko kuwepo katikati ya mwaka wa fedha? kuna haja ya kubaki na lile ongezeko la Kikwete la kila mwaka au ongezeko lifanyike kwa mara moja tu kuliko hizo % zilizo tajwa.

tatizo ukiongeza unaongeza na wenye vyeti feki na magumashi
 
Back
Top Bottom