Elections 2010 Nyomi ya dr. Kikwete mwembeyanga leo ni mara ishirini ya dr. Slaa-inaashiria nini?

chamajani

JF-Expert Member
Sep 22, 2010
552
31
Kativii kangu ka black n white kamepona so uchaguzi niko nao beneti kwa sasa, Jana Dr. slaa nilimuona Jangwani kapata nyomi hata tiviii ilikuwa ndogo, lakini leo huyu Jeykey kapata manyomi ilibakia kiduchu kativii kangu kapasuke kwa watu waliojaa humo tiviini. Hii inashria nini jamani nyie mtakaojengewa barabara za ndege huko dar?
 
Watu inabidi waende kwenye midahalo yote ili waweze kulinganisha sera. Wingi wa watu sio wingi wa kura ................siunakumbuka methali ndugu yangu............ukubwa wa pua sio wingi wa ............................:smile-big:
 
Tofauti kubwa ni kwamba watu wale wa slaa ni wakazi wa temeke lakini wa kikwete ni kusomba kwa malori kutoka mkoa mzima kwani nililiona lori linapita mitaa ya TEGETA kutafuta watu wa kwenda mwembeyanga.
 
[B said:
chamajani[/B];1183482]Kativii kangu ka black n white kamepona so uchaguzi niko nao beneti kwa sasa, Jana Dr. slaa nilimuona Jangwani kapata nyomi hata tiviii ilikuwa ndogo, lakini leo huyu Jeykey kapata manyomi ilibakia kiduchu kativii kangu kapasuke kwa watu waliojaa humo tiviini. Hii inashria nini jamani nyie mtakaojengewa barabara za ndege huko dar?
nimebold jina lako kwa sabau ulichoongea hapa ni matokeo ya kilevi Cha MAJANI.
 
Watu wa dar wanapenda sana matamasha ya wasanii.Hebu muulize mmoja wao uukupe summary ya hotuba ya kikwete.
 
Slaa hakuwepo Jangwani. Ni mwembe yanga.
Siri ya JK kuwa na watu wengi tunaijua sisi.
Watu hao wa JK ni artificial lakini wa Dr. Slaaa ni Natural!!
kama umeelewa elewa kama hujaelewa sikulazimishi!!!
 
Wamesombwa na mabasi na tuliyaona hayo mabasi. CCM wanajidanganya wachukua watu wale wale kule Kawe, Mwembeyanga na hao hao? je watapiga kura mara zote hizo?

Poor CCM, jiandaeni kisaikolojia "kupokea kushindwa"
 
Watu wa dar wanapenda sana matamasha ya wasanii.Hebu muulize mmoja wao uukupe summary ya hotuba ya kikwete.

HA HA HA nimecheka sana inawezekana watu wanaenda pale kuangalia shoo za wasanii na ukiwauliza summary ya hotuba ya mkwere ni wachache sana wanaoweza kukupa hint
 
Poleni sisiem bado 72hrs muondolewe ulingoni na jk wenu,nguvu ya umaa haoooo waja ikulu
 
Kativii kangu ka black n white kamepona so uchaguzi niko nao beneti kwa sasa, Jana Dr. slaa nilimuona Jangwani kapata nyomi hata tiviii ilikuwa ndogo, lakini leo huyu Jeykey kapata manyomi ilibakia kiduchu kativii kangu kapasuke kwa watu waliojaa humo tiviini. Hii inashria nini jamani nyie mtakaojengewa barabara za ndege huko dar?

Kikwete ni dk wa nini?
 
.
CCm2010.jpg

ccm2010_2-1.jpg

Wananchi wanaenda kwa dokta wa ukweli kwa utashi na dhamira zao...
Vipi kwa "dakitari" wenu wanaletwa na nini..?
 
chama cha watu dhaifu na duni, watu wanaobebwa kwenye maroli maana hawajui hata wanaenda kwenye mikutano ile kufanya nini.........
CCm2010.jpg
 
Back
Top Bottom