Nyomi la CHADEMA Arumeru leo

Ebu tujikumbushe kidogo katika haya ili kuondoa ama kupunguza pressure huko Arumeru hapo 1st April 2012 (Foolish Day)

quote_icon.png
By Dr.W.Slaa (Katibu Mkuu Chadema)

WanaJF,
Niko uzini leo siku ya Tatu. Naomba niwahakikishie wanachadema na wapenzi wenu kuwa tutafanya mpaka kieleweke. Uzini wananchi ni waelewa sana. Wanapenda hoja na si porojo. Wanaopiga porojo kwenye jamvi hili au hawajui kinachoendelea on the ground au wanasukumwa na ushabiki tu kama walivyozoea. Uzini na Zanzibar iko tayari kwa mabadiliko makubwa. Uzini tofauti na watu wanavyofikiri Chadema ina matawi sasa kila Shehia katika Shehia (sawa na vijiji au mitaa bara). Jana nimezindua ofisi, matawi,maskani 7 katika majimbo mbalimbali nje ya Uzini mathalan Mfenesini,Magogoni, Bububu na kadhalika. Kwa hakika moto utakaowaka kutokea Bambi(Uzini) tunakozindulia Kampeni yetu kwa hakika utaunguza Zanzibar yote. Kwa bahati mbaya ndani ya Uzini hakuna network isipokuwa Zantel na hata hivyo hakuna mtandao (internet hadi uende mjinZanzibar. Ndio maana hakuna taarifa. Tunaomba radhi. Lakini kuanzia leo waandishi wa habari watakuwepo ambapo jioni wanaweza kuleta habari wakirejea mjini.
Narudia tena wananchi ni wakarimu sana. Kwa kuwa hakuna guesti kabisa wananchi wamewapokea timu yetu ya Kampein kwenye nyumba zao. Hii ni dalili njema. Tunawashukuru sana.


quote_icon.png
By Ng'wana Sweke (Kamanda)

Habari ndiyo hiyo,CHADEMA inaongoza shehia kibao.Stay tuned nitawamwagia full data muda si mrefu.


quote_icon.png
By Tumaini Makene (Afisa Habari Chadema)
Updates;

Ngoma sasa iko kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Uzini. Matokeo yanaendelea kukusanywa na kufanyiwa majumuisho kwenye kompyuta. Mechanism yetu pia inaendelea kukusanya matokeo yote ya kura zote na taarifa za mchakato mzima wa leo. Uchaguzi umetawaliwa na vitisho na ubabe mwingi. Mpaka sasa zipo taarifa juu ya CCM kuweka ofisi ndogo katika kila kituo cha kupigia kura. Wakiwakamata wapiga kura na kuwashikisha vitambulisho vya kupigia kura. Wakitoka kupiga kura anakuwepo mtu maalum anawapatia pesa.


quote_icon.png
By Tumaini Makene (Afisa Habari Chadema)
Msimamizi kamtangaza Mohamedraza Hassanal Mohamedali wa CCM kuwa mshindi kwa kura 5,377 (91.1%) akifuatiwa na Maalim Ali Mbarouk Mshimba wa CHADEMA, kwa kura 281 (4.8 %), wa CUF anafuatia akiwa na kura 223 (3.8), kisha TADEA kwa kura 14 (0.2%)na AFP kura 8. Jumla ya kura halali zilizopigwa ni 5,903 na zilizoharibika ni 28.
 
Hakuna picha iliyochanganywa hapo labda useme sio Arumeru, uoga haufai kiukweli Cdm wanaonekana kupata watu wengi Arumeru lakini cha msingi hao watu wamejiandikisha?
 
ni nyomi kweli au ni kale kamchezo ka camera zetu za kisasa!!!

You made me laugh!
Kumbe hizo kamera za kisasa ziko CDM tu? Nawashauri CCM nao wakazinunue badala ya kununua shahada za kupigia kura! Na sasa nasikia shahada zimepanda bei kwa 400% kutoka 5000 hadi 20,000 ndani ya serikali iliyoahidi maisha bora kwa kila mtanzani, miaka saba tu tangu kuahidiwa maisha bora, wameru tumeyaletewa mlangoni kwa biashara ya kununua shahada, hali ikiendelea hivi watu watashawishika kujiandikisha mara nyingi ili wawe nazo nyingi wauze uchaguzi utakapotangazwa tena na hivyo kuingia hatiani kwa kosa hilo!

Lakini jambo moja litakumbukwa, ni kwamba kwa miaka saba aliyoongoza Mh. Marehemu Sumari barabara ya akeri haijawahi kuchongwa mpaka alipofariki ndipo ilipochongwa ili kupitishia maiti ya Mhe! Wameru wanajiuliza kama kuna mgombea yeyote mwenye kuonekana ana afya mbovu wampe ili ikitokea bahati nzuri akafariki akiwa mbunge wachongewe barabara tena!

CCM Oyeeeeee!
 
Duh! Mshkaji hili ni changa la macho. Huu ni mkutano wa Dr. Slaa uliofanyika Mbeya ktk viwanja vya Dr. Slaa (Mama John area).
 
........ kiukweli Cdm wanaonekana kupata watu wengi Arumeru lakini cha msingi hao watu wamejiandikisha?

I don't care kwa kuwa inaonekana hujui hesabu! Sikia,

Kama 50% ya wana Arumeru hawajajiandikisha na CDM wakipata watu 1000 ujue wana kura 500, na CCM wakipata watu 50 ujue ni kura 25 hizo, akili kumkichwa ndugu!

Usifikiri kirahisi kuwa CDM ni disadvantaged group always! Leo (hiyo picha) ilikuwa ni katika uwanja wa Akeri ambapo ni mita kama 50 tu kwenda nyumbani kwa mgombea wa CCM, na kama ulishuhudia mazishi ya Mh. Sumari, huo uwanja ndio uliotumika kama parking siku hiyo! Leo asubuhi CCM imefanya mkutano hapohapo watu hawakufika 50 take it from me! masaa machache tu baadae CDM inaleta mamia hapohapo!

For sure CCM imepoteza mvuto kwa wengi, nilikuwa mwanza 2010 wakati wa kampeni haikuwa hivyo, Aruha town nilishuhudia pia kabla ya kwenda Mwanza haikuwa hivyo pia!
 
Back
Top Bottom