nyimbo za mrisho mpoto

Architect E.M

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,211
1,360
jamani wakuu,, samahanini, pengine ni uelewa wangu mdogo ama sijui ni vipi,, lakini ningelitamani sana kujua maana hasa ya nyimbo za huyu jamaa,,, nimejitahidi mara nyingi kurudia kusikiliza, bado natoka kapa, nikiwauliza ninaoishi nao, bado kapa, sasa pengine ndugu zangu mnaweza kunielewesha maana ya hizi nyimbo. ADELLA na ASANTENI KWA KUJA....
 
Mtazamo wangu: mpoto anazungumzia maisha halisi tz, mfano alisema "mmetupima viatu mwaka jana halafu leo mnatuuliza mlisema mnavaa namba ngapi?" Bila shaka anatafsiri ahadi za uongo au nakosea.
 
usi-comment we huoni amekosea jukwaa,apeleke ktk michezo na burudani ndo atapata wachangiaji weengi.
 
Mkuu kazi zote za fasihi zilizoenda shule kama za mjomba, kwanza hazina tafsiri moja kila mmoja anapata tafsiri yake kwa mazingira yake... pili unahitaji kuchezesha akili yako uweze kupata tafsiri ya ujumbe unaoletwa na tungo au maneno anayotumia!!!!!
 
ADELLA... ni kitu sahihi kwa wakati huu....inawagusa wanafiki ambao wanataka kufaidi wao ttu kuliko wengine.....wanaotafuta umaarufu kwa damu za wengine......na pia inaonya vita ni mbaya......tuwaangalie watoto na akina mama NAPENDA TUNGO ZILIZOENDA NDANI YA JAMII KWANI HAZITACHUJA....(MPOTO IS DR. REMMY WA SASA)
 
Ili kumwelewa Mpoto lazima utulize kichwa na kumbuka fasihi ni yake ni mwangwi ya yale yanayotokea katika jamii yetu, sikiliza tafakari ndipo utaelewa.
 
Ulitupima viatu mwaka jana na mwaka huu unatuuliza hivi mlisema mnavaa saizi gani? Hapa kwangu moja kwa moja aliwalenga viongozi na haswa wabunge wakati wa kampeni wanakuwa majimboni na ahahadi kibao wakijifanya kuzijua shida au matatizo ya wananchi lakini wakishapewa kura wanasahau na wakija tena majimbono wao wanataka wananchi wawasomee risala za matatizo au mahitaji yao kama vile wakati wa kampeni hawakuzigusia wenyewe kwamba wakichaguliwa watazifanyia kazi.
ila nasikitika mpoto mpaka leo hajapata nauli kwenda kwa mjomba wake pale magogoni kumwambib kwamba yale aliyomwambia kwenye tungo za mjomba mengi yametokea na kwamba uongozi umemshinda amebaki kuwa kiongozi wa kupigia picha na kufungua majengo mapya yaani yuko kisherehe zaidi kuna haja ya kuwa na wajomba wawili mmoja wa kupigia picha na mwingine wa kuwajibika kwa mambo magumu ya nchi hii. Huyo mjomba tuliyenaye sasa ni ili na sisi tuseme mama yetu hakuzaliwa mwenyewe lakini hajui wajibu wa mjomba. Safari hii tukikosa nauli mjomba tutakuja hata hata kwa miguu kama misri, si umeona wanavyuo wameshaanza kutembea kwa miguu kuelekea magogoni hizo ni dalili za kukosa nauli. Hiyo ni tafsiri yangu kwa nyimbo kama za mpoto
 
jamani wakuu,, samahanini, pengine ni uelewa wangu mdogo ama sijui ni vipi,, lakini ningelitamani sana kujua maana hasa ya nyimbo za huyu jamaa,,, nimejitahidi mara nyingi kurudia kusikiliza, bado natoka kapa, nikiwauliza ninaoishi nao, bado kapa, sasa pengine ndugu zangu mnaweza kunielewesha maana ya hizi nyimbo. ADELLA na ASANTENI KWA KUJA....


Ili kumwelewa Mpoto lazima utulize kichwa na kumbuka fasihi ni yake ni mwangwi ya yale yanayotokea katika jamii yetu, sikiliza tafakari ndipo utaelewa.

Mfano wimbo huu, ebu usikilize kwa makini



Kumfahamu mrisho mpoto fungua hapa https://www.jamiiforums.com/sports-...anii-mrisho-mpoto-nyimbo-za-mrisho-mpoto.html
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom