Cultural imperialism at its bestNi kupoteza asili yetu au ni kwenda na wakati?
Mkuu umenena, sisi twaona eti kucheza huo muziki ndio ustaarabu. Kumbe ni uzuzu tu.Sio kwenda na wakati bali ujinga wetu!
Mwabaluhi, hiyo sio sababu muziki wa south umechangamka kuliko mdundiko, mdumage na msondo? Sidhani. Mbona steps za sangula ya wapogoro na ling'oma ya wanyakyusa ni murua na zinavutia sana.
mie nilizipiga marufuku kwenye harusi yangu and i didnt miss anything, tuna watoto wanaimba vizuri sana siku hizi
Tunahitaji wengi kama wewe, huu ndio ukombozi, the liberation we need.mie nilizipiga marufuku kwenye harusi yangu and i didnt miss anything, tuna watoto wanaimba vizuri sana siku hizi
......ni ushamba/unyarugusu tu.....!...halafu most of ndugu zangu wachagga wakishamaliza lile li-RINGI lao...........wanaanza kuweka ile mijiziki ya kisauzi.....aargghh
Msinikumbushe wadau, kuna harusi kilipigwa kitu cha Mphauphela Amandla, yaani acha tu. Nadhani kuelekea Afrika moja ni heri hizo kuliko ile mibluzi, nyimbo za zouk, mushroom, afrodance pia zinapendeza harusini.
Asili yetu ishapotea siku nyingi tu. Utamaduni wa kigeni ushaota mizizi. Nadhani kwa kujibu swali lako kwa maoni yangu watu hupenda nyimbo zile maharusini sababu zinachangamsha na zinavutia kucheza pia zina involve easy steps ku-boogie na zile steps zinapokuwa synchronised kwa kundi zima huvutia kwelikweli.