nyimbo za chama shuleni enzi hizo

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,494
7,517
jamani mnakumbuka enzi za chama kimoja wanafunzi walivyobadili nyimbo za chama na kuziimba vingine. mfano ''chai, chapati, maharage, mchuzi vyajenga nchi'' badala ya ''chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi''. wakati naanza shule nilijua ndivyo zinavyoimbwa mpaka baadae sana baada ya maticha kupiga mkwara ndio ziliimbwa kwa usahihi. kweli wanafunzi walikuwa wabunifu. je wewe una mfano wowote?
 
Kwenye 80s wakati wa mbio za Mwenge kulikuwa na hiki kitu:

Mwenge huo Mwenge : MbioMbio

Sisi siku moja tuliimba hivi:
Mwenge huo Mwenge : Kibatari

Kiongozi wa Mbio za Mwenge (Kumchaya) siku hiyo aliamuru tutiwe ndani mpaka mbio zitakapoisha - hata polisi hatukufika!
 
alisema, alisema; alisema Nyeree alisema, vijana wangu wote msherekee sasa tuanze mchaka , chinja, tupa............
ukipigwa fimbo ya mgongo utafanyaje; ukipigwa fimbo ya mgongo utafanyaje........ ( wimbo wa kipindi cha majira cha radio Tanzania)
 
Kwenye 80s wakati wa mbio za Mwenge kulikuwa na hiki kitu:



Sisi siku moja tuliimba hivi:

Kiongozi wa Mbio za Mwenge (Kumchaya) siku hiyo aliamuru tutiwe ndani mpaka mbio zitakapoisha - hata polisi hatukufika!

mwenge tunaukimbiza, mbio mbio, mpaka makao makuu , mbiombio.:D mwenge huo mwenge.........
 
chama chetu cha majambazi chajenga nchi......chama..aaahhhh, nyerere ajenga nchi.....*2

niliisikia hii nikiwa std 2 jamaa walokuwa wakiimba walikuwa la sita nadhani back in 1985....walichezea mbalati kwa saana tu...

leo nnapowasikia akina mtikila wakisema hayo nashangaa walikuwa wapi those days...
 
Back
Top Bottom