Nyie wenyewe mmezubaa:Mnaweza kujipa hela, hamtaki!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,972
1,649
Bado naendelea kufikiria kauli ya huyu kikongwe alipoitoa hii
kauli akitetea kwa nguvu zote ile posho ya
200,000/= kwa siku. Huyu mama anaelekea kupata waimu kabisa.

Haiwezekani ashindwe kuongelea namna ya kuwaondolea
watanzania umasikini na shida zao, lakini anatumia nguvu nyingi
kutetea ule upumbavu.

Nadhani ameweka rekodi ya umajinuni kati ya maspika wote walowahi
kuliongoza bunge la jamhuri ya muungano!

NOTE: Bado siamini kuwa hao nusu ya wabunge waliopeleka
mapendekezo ya kujiuzulu ubunge wapo wa upinzani pia. Bila
shaka ni wa CCM na CUF.
 
Lazima m2 afikirie kabla ya kusema...nilikuwa na msikiliza spika jana kauli zake kwa wapiga kura wake nikaona kwa hilo amekurupuka.
Manake haiwezekani kwa nchi ilipo sasa ambapo uchumi umedorora na mfumuko wa bei, bado anataka wajilipe pesa nyingi...kisa? eti wenyewe ndo wanajipangia, nchi yetu uchumi bado sana...manake ukiangalia nchi zilizoendele wafanyakazi kama walimu,madaktari ndo wanalipwa zaidi, lakini kwetu ni kinyume...
Namalizia kwa kusema na hao wabunge wanaotaka kuacha ubunge kisa maslai, ina maana walichaguliwa kwa ajili ya kuwatumikia/kuwa wakilisha wananchi au walichaguliwa ili wa kapate maslahi?
 
Mi naona bora wajiudhuru ili tujaribu wengine, maana tumeshawaona wapigania matumbo na wababaishaji
 
hivi ni kweli wamepeleka barua za kujiuzul ubunge?nitafurahiaje!!!nitafurahi zaidi kama lusinde,mrema,cheyo,selasini(chadema),shibuda(chadema) na anne kilanga malecela watakuwepo..
 
Ameona ni sahihi kuyasema ya ndani ya Bunge kwa wananchi kitu ambacho ni kinyume na kanuni za Bunge.
Kila wakati tumeshauri kuwachagua watu makini na wanaojenga hoja za msingi katika kuleta maendeleo.
WanaNJombe wanamatatizo ya kukaa na kuyajadili na hatimaye yapelekwe bungeni na mwakilishi wao Yaani huyo bibi kikongwe cha ajabu yeye anajadili Maslahi binafsi badala ya matatizo ya wananchi. Je huo ni Uungwanaaa???
 
Bi Kidude kakomaa na posho si masihara...anaogopa kupigwa chini na wabunge kwa kutokuwa na imani na uongozi wake anaona bora ajikoshe kwao...vita ya panzi furaha ya kunguru...HAKUNA CHA POSHO... TENA NAPENDEKEZA ISHUKE KUTOKA HIYO SABINI HADI ISHIRINI ILI TUPATE WATETEZI WAZALENDO WA KWELI..SIO KWENDA KUSINZIA BUNGENI..
 
Hii ndio tabu ya kukaa miaka mingi madarakani mpaka unaboronga si aanze na hao mafisadi wenzie waone kama tutaandamana
 
Walidai haki zao huko beijing!kauli mbiu ikawa wakiwezeshwa wanaweza ndo kma ivi kibibi kizee cha turini,,,,kinatetea ujinga,ambao auna mbele wala nyuma dawa yao iko jikoni,,,kuanzia kwa FAKE DOCTOR,na Wafuasi wake wote!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom