Nyie mbu!!!!!

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,289
781
Wakuu, Nasumbuliwa sana na hawa wadudu. naombeni ushauri wenu, nitumie dawa gani kkuwatokomeza? natumia DOOM, RUNGU mwanzo zilisaidia, lakini sasa hawa mbu nadhani wamevumbua ujuzi mwingine, wanafunua mpaka neti!!! Nataka dawa ya kuwaangamiza kwa sababu zifuatazo
1. Mke wangu atajifungua hivi karibuni, hivyo hatutaki mazoea na MBU.
2. Kutokana na kupenda kukaa barazani, neti hazitatusaidia kitu.
3. Tumezungukwa na miti mingi sana, hivyo jeshi la mbu linapiga mazoezi ya kutosha (wamejazia kama NJIWA!)

Natanguliza shukrani zangu
 
Weka mazingira yako safi, ondoa mazalia ya hao mbu....Rungu, Doom, whatever insectiside ni short term solution. Hao jamaa wameanza develop resistance to most of commonly used insecticide ama larvicides....
 
Inaelekea sehemu unayoishi kuna madimbwi sana ya maji, ndio maana huwezi kuwaondoa mbu wote kwa kutumia hizo rungu na doom.
Inabidi kwenye chumba uweke milango miwili, weka mlango wa kawaida kwa ndani, then nje weka mlango wa nyavu ambao mbu hawezi kupita kwa urahisi.
Kwenye madirisha vile vile weka madirisha ya kioo au unaweza kuweka nyavu ambazo mbu hawawezi kupita.
Pole sana maana mbu ni kero mnooo!!
 
Mkuu, mazingira yangu hakuna kidimbwi hata kidogo!!! isipokuwa kuna miti mingi ya maua ambayo nahisi wanajificha humu! sasa kufyeka miti nadhani hakutasaidia kwa sababu wanatoka mbali na kuja tu! Wananikera sana hawa wadudu!!
 
Kwa maelezo hayo hao mbu hawaenezi malaria, zaidi ya kusababisha annoyances wanapouma hao wapo kundi la mbu liitwalo Culex!
 
Inaelekea sehemu unayoishi kuna madimbwi sana ya maji, ndio maana huwezi kuwaondoa mbu wote kwa kutumia hizo rungu na doom.
Inabidi kwenye chumba uweke milango miwili, weka mlango wa kawaida kwa ndani, then nje weka mlango wa nyavu ambao mbu hawezi kupita kwa urahisi.
Kwenye madirisha vile vile weka madirisha ya kioo au unaweza kuweka nyavu ambazo mbu hawawezi kupita.
Pole sana maana mbu ni kero mnooo!!

madimbwi hayapo kabisandugu yangu, ila madirisa ndiyo hivo tena, hayana wavu wa mbu (hz dizaini za sku hz kutoweka nondo wala wavu), nilifikiria kugonga fremu za wavu lakini nikaona kabla sijaharibu ladha ya madirisha yangu niulize wadau kama kuna dawa ya kuwaangamiza kabisa, kwa sababu hata siwezi kuweka wavu mpaka balazani! hawa wanyama sioni kama wana faida yoyote hapa duniani!
 
Kwa maelezo hayo hao mbu hawaenezi malaria, zaidi ya kusababisha annoyances wanapouma hao wapo kundi la mbu liitwalo Culex!
hapo unani fumbua macho mkuu, kwa hiyo mbu wanaombukiza malaria (sjui anofelesi!) wanatokea wapi hasa, je hawana mahusiano na hawa ulowasema? mimi siwaonei tofauti kabisa mkuu
 
Mkuu if possible hama hayo mazingira utafute kwenye mazingira ambayo haya encourage kuzaana kwa mbu. Kama Masanelo alivyo sema dawa ni short term. Siku zote hauwezi kumaliza maji ya ziwa kwa kunywa.Kwa hiyo kama mazingira yana changia wao kuzaliana utaua wana kuja wengine.
 
Asante mkuu, lakini hapa ndiyo kwangu! nikiwakimbia mbu niwaachie nyumba hainipi kabisa mkuu!
 
hapo unani fumbua macho mkuu, kwa hiyo mbu wanaombukiza malaria (sjui anofelesi!) wanatokea wapi hasa, je hawana mahusiano na hawa ulowasema? mimi siwaonei tofauti kabisa mkuu

Mbu anayeeneza malaria ni mbu jike wa kundi la Anophelesi gambiae wapo kama aina tofauti 30 hivi. Lakini huku kwetu Tanzania zaidi ni Anophelesi gambiae complex (sababu kuna makundi mengine 6 kwenye A. gambiae

Hawa anopheles hupenda kujificha kwenye viambaza vya nyumba na kuvizia kuuma watu. Hao wanaokaa kwenye miti nina wasi wasi wanaweza kuwa si hawa anophelesi maana si tabia zao.

Maelezo zaidi

[ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Anopheles[/ame]
 
Back
Top Bottom