Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,877
- 2,758
Hivi mnadhani uumbaji umekamilika? Kwamba Mungu alimaliza kila kitu ile siku ya saba? Kwamba hakuna tena haja ya kumfanyia binadamu marekebisho madogomadogo? Ukiangalia maendeleo ya ubunifu wa vitu kama magari utaona yamepitia hatua nyingi hadi leo hii, na bado uboreshaji unaendelea. Kwa upande wa binadamu, tangu alipopumbwa hivyo alivyo, ndivyo alivyo na atakavyokuwa hadi dahari. Lakini ingekuwaje kama kutokana na purukushani hizi tunazoziona leo za mtindikio wa uaminifu katika mahusiano na hatimaye visa na mikasa, binadamu akawekewa pass word kwenye nyeti ili kuzuia mwingiliano usio rasmi? Hii pass word ifanye kazi tu pale ambapo mihemko ya kimapenzi inaaza ndipo nyeti zijilock kwa namna itakayokuwa muafaka. Hapo ndipo mwenye 'pini' aidha azitaje kimoyomoyo au kwa njia nyingine ili access ipatikane. Hii pini atakuwa nayo mtu mmoja tu. Kama nyeti ni za mwanamke, basi pini awe nayo mwanaume tu bila ya mwanamke kuitambua, and vice versa. Haya marekebisho yangeokoa ndoa nyingi pamoja na kuleta ahueni duniani. Ni rasimu tu