Gagurito
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 5,600
- 803
Mwaka 1968 katika kitabu chake cha Ujamaa Mwl. J. K. Nyerere alipata kuzungumzia juu ya madhara ya utegemezi wa fedha toka nje! Ktk kitabu hicho alipaswa kunena haya, namnukuu...
Tumekua tukishuhudia safari za mara kwa mara za viongozi wakuu wakitaifa nje ya nchi kutafuta wawekezaji pia kuomba msaada, pia tumekuwa tukishudia nchi yetu ikipokea misaada kadhaa kutoka nje kwa malengo ya kuleta maendeleo.
SWALI: Je kwa mwendo huu twaenda vyema? Je tutafikia maendeleo kwa mendo huu?
MY TAKE:Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni masikini. Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe.
Ni ujinga kwa sababu mbili.
1. HATUWEZI KUZIPATA: Nikweli kwamba ziko nchi ambazo zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga viwanda ktk nchi yetu kwa kiasi cha kuiwezesha nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.
2. Misaada na Mikopo vitahatarisha Uhuru wetu. Kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya taifa jingine kwa maendeleo yake.