Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

kichuguu said:
(a) Sikusema vitabu hivyo hapo vimejibiwa; ila nilisema niliwahi kuvisoma pamoja na vingine vya aina hiyo.

(b) Nikipata nafasi nitakutafua majina ya wandishi na references zote nilizowahi kusoma kuhusu hii topic. Kwa sasa hivi naishi nje ya nchi na collection yangu ya vitabu haina vitabu vya siasa za Tanzania. Ila nikisearch internet ninaweza kuzipata references hizo; kwa hiyo tulia

(c) je una reference ya nyerere kusema hakuna la kujibu!

(a) OK, samahani kama sikukuelewa mwanzo .. nliona umeimply kuwa kuna waliovijibu.

(b) Natulia, take your time.

(c) Duh .. haikuwa documented, kwa hiyo sina reference. Ila nilifahamishwa na mtu asiye na sababu ya kuzua.. kuwa huyo prof muhusika .. tena muislam, at least by name .. na alikwenda in good faith. Ingekuwa vizuri kuwa muislam ameandika kitabu kumtetea mwalimu katika shutuma za udini dhidi ya waislam. Kama huiamini pia ni sawa.

Kwa kuwa hukugusia tena suala la author muislam kutumia pen name ya kikristo.. bila shaka umekubali sasa kuwa huo haukuwa ukweli.

Haya .. umesema huko nyuma
kichuguu said:
... Kwanza kabisa ni vizuri kuthibitisha credibility ya kila author; hawa wote hawawezi kupasi credibility test kwa vile siyo independent: wote ni waislamu ingawa wengine wametumia pen-names za kikristo. ...

(i) Hiyo ndio credibility test yako ya kutokuwa independent?
(ii) Since we have established kuwa Dr. John C Sivalon was infact a christian... tena a Father, .. na alipata ushirikiano wa kanisa katika kuandikia aliyoyaandika (Hata publishers wake ni Benedictine Publications. Ndanda, Peramiho),... vipi sasa anapasi hiyo credibility test yako?
 
Jasusi said:
DrWHO,
Your comparison of Mwalimu and Mahathir is misplaced. Mwalimu should rightfully be compared to Tunku Abdul Rahman Putra. They both fought colonialism and helped realise independence for their respective countries. They both set out to build an identity for their nations. Mahathir was the third leader of Malaysia. So he should compare with Mwinyi or Mkapa at best. Mwalimu inherited a backward underdeveloped Tanganyika. Our economy was basically agrarian. The majority of our people rural, sick and uneducated. He set out to educate us. There was not a single manufacturing industry in Tanganyika. The British made sure there would be no industries to compete with their industries in Kenya. Tanganyika was the first market for Kenyan made goods. For educating us, and contrinbuting to the liberation struggle Mwalimu was laying a foundation for a Mahathir in Tanzania. But the leaders that followed: Mwinyi and Mkapa, kila mtu aliamua kufanya vitu kivyake vyake tu.


Yes Tanzania at this very moment can develop like this Countries of East Asia known as the Tiger Economies. The first thing South Korea did in the 1960s is increase the nuber of schools and Universities from seven (7) to about forty seven (47) check fugures and numbers. They also opened many vocational training centers to train a skilled workforce. The government then encouraged private businesses and entrepenuership and they sponsored and gave credits to those companies that are doing good. In addition the government targeted and sponsored specific industries that are technology based such as electronics, automobile, aircraft and heavy industries.



At this very moment Tanzania has the capability to be another Japan or Singapore. The key is to develop both our human resource together with the natural resources coupled with GOOD LEADERSHIP. Good leaders with a vision and common sense equals a succesfull country like Japan.


and this is whats been missing in TANZANIA
 
nauliza jee kipindi cha nyerere kuna padree aliyefungwa? au kipindi cha mwinyi?au mkapa au JK.
ila kipindi cha mwl. masheikh wengi sana waliwekwa ndani.

mfano sheikh Hassan BIN Amir,Sharif Badawi, sheikh Adam Ahmed yupo Temeke pale sokota. na wengi tu.
uliza mkasa wa sheikh Takadiri na Nyerere? kisa ni udini aliukuwa anaufanya MWL. na mzee Takadiri hakumficha mbele ya wajumbe wa mkutano wa Tanu akamnyooshea bakora kuwa harufu ya udini inakuja kwenye chama na serikali. matokeo yake nyerere akaanza kulia na kuomba msaada wa sheikh Chaurembo.

jee hamyajui haya? nyerere kawavuruga sana waislam kwa choyo chake na hata JM alimnyima urais ili UKATOLIKI utawale TZ.

kisa malecela alitaka kuupa nguvu Uanglikana na alimualika askofu wa Canterbury.jee hamyajui hayo?
nyerere nuksi hana maana hata moja.
 
nauliza jee kipindi cha nyerere kuna padree aliyefungwa? au kipindi cha mwinyi?au mkapa au JK.
ila kipindi cha mwl. masheikh wengi sana waliwekwa ndani.

mfano sheikh Hassan BIN Amir,Sharif Badawi, sheikh Adam Ahmed yupo Temeke pale sokota. na wengi tu.

uliza mkasa wa sheikh Takadiri na Nyerere? kisa ni udini aliukuwa anaufanya MWL. na mzee Takadiri hakumficha mbele ya wajumbe wa mkutano wa Tanu akamnyooshea bakora kuwa harufu ya udini inakuja kwenye chama na serikali. matokeo yake nyerere akaanza kulia na kuomba msaada wa sheikh Chaurembo.

jee hamyajui haya? nyerere kawavuruga sana waislam kwa choyo chake na hata JM alimnyima urais ili UKATOLIKI utawale TZ.

kisa malecela alitaka kuupa nguvu Uanglikana na alimualika askofu wa Canterbury.jee hamyajui hayo?
nyerere nuksi hana maana hata moja.
 
Kwa maoni yangu Mwalimu alikuwa, half bin half, yaani uzuri wake na ubaya wake mimi ninauweka kwenye nusu kwa nusu,

Na Watanzania tunahitaji kuwa wakweli, kwa kuzungumzia tunaoyaona na yanayotugusa katika maisha ya kila siku, as the results ya uongozi wa Mwalimu,

PLUS,
Binafsi ninaziona plus zake katika sisi wabongo kuheshimiana bila ya kujali cheo wala utajiri wa mbongo mmoja dhidi ya mwingine, kwa kawaida wabongo wote huwa tuko sawa katika kushirikiana na maisha ya kila siku, kusoma elimu ya bure ilikuwa ni a big plus, leo wabongo kibao ni wasomi na wako sehemu mbali mbali za dunia, chanzo chake ilikuwa ni elimu ya bure ya Mwalimu, halafu locations za vijiji vya ujamaa, maana leo bongo ukimtafuta mtu yoyote yule utampata, maana wote tuna anuani na hasa kwa kutumia majina ya kijiji, halafu tamaa ya mali, pamoja na kuwa na wabongo wachache wenye tamaa kubwa za mali, wengi wetu huridhika na vichache tulivyonavyo kama alivyokuwa Mwalimu, ukabila na udini sio very severe kama wenzetu wa nchi zingine,

NEGATIVE
Mapungufu ya Mwalimu yanaanzia kwenye uchumi ambako mpaka leo we are paying a very heavy price, yaani sometimes huwa nina wasi wasi kwamba hiki kipengele ni so bad kwamba may be kinafunika hata uzuri wake wote, maana guys sijui kama wabongo wanaelewa how much troubles we are in as far as uchumi is concerned, manake mimi sielewi ni lini tulikuwa kwenye mstari unaotakiwa, au lini tutakuwa maana kila siku tunaporomoka tuu, halafu kutokubali kwake ushauri sasa limegeuka kuwa tatizo sugu la marais wote baada yake, maana sasa tunajionea Jk hataki ushauri wa mtu kama alivyokuwa Mkapa, Mwalimu alimuweka Mkapa bila ya kutu-consult wabongo, na Mkapa naye akafanya hivyo hivyo, na Jk naye atafanya hivyo hivyo atakapomuweka Migiro,(EL hapewi hiyo, labda afanye ujanja mpya), kwenye udini nina wasi wasi na Mwalimu kuwa something was not right, maana ni kipindi cha Mwinyi ndio nimegundua kuwa kulikuwa na wasomi kibao ambao ni Waisilamu, enzi za Mwalimu mimi nilifikiri ni Malima tu aliyekwenda shule,

lakini nitasikiliza mtu yoyote akinitolea ufafanuzi kuhusu hilo la dini, ila ningependa kujua ni kwa nini Waisilamu wasomi wengi walitokea baada ya Mwalimu kuondoka, watu kama Dr. Mtulia, Dr. Kigoda, Dr. Kapuya, Dr. Msabaha, Dr. Omar Juma, Dr. Bilali, na wengineo wengi ambao hatukuwasikia kabisa enzi za Mwalimu what happened Mzee Jasusi?

Mzunguko wa viongozi wale wale, kama Mwalimu alivyokuwa, kukataa ukweli kwa viongozi suala la ujambazi viongozi wamelikataa wee mpaka juzi tu ndio wamekubali, kumbe tungekubali mwanzoni huenda tungeshalizima hilo,

Hayo mchache ndio maoni yangu as far as what ninachokiona katika maisha yangu huku bongo, ya kila siku ambayo yanakwenda mlangoni kwa Mwalimu!

Lakini yote tisa, kumi Mwalimu was the man yaani kidume!
 
MZEE ES your very right there,
lakini mimi nina jambo moja,
ningependa kurejea nyuma na kuelezea the whole story of ujamaa and the like,lakini kufanya hadithi iwe fupi,
mwalimu alipoacha madaraka mwaka 1985, sababu ilikuwa ni kweli alishindwa kuendelea na siasa za kijamaa na yeye akakubali hilo.
sasa toka mwaka 1985 mpaka leo 2006 ni miaka ishirini, kuna mabadiriko gani?
leo hii kunahatari taifa zima laweza kuwa gizani,
leo hii hatuna maji safi na salama
leo hii idadi ya vijana wasio na ajira imeongezeka,
leo hii watanzania hatuna huduma bora za afya,
leo hii watu wanakufa njaa,
pamoja na kutimiza masharti yote ya benki ya dunia na shirika la fedha hatujaweza hata kujenga hata reli moja au kuongeza hata kiwanja kingine cha ndege au hata kujenga chuo kikuu kama kile cha mlimani.
what is wrong??
ukiangalia utaona kuwa miaka 20 ya nyerere mambo mengi sana yalitokea,
mafano pamoja na mambo mazito yaliyotokea kama vile
kunusurika na jaribio la mapinduzi,vita vya idd amin,vita vya cold war.nk
utaona kuwa pia kuna mambo mengi pia yalitokea kama vile kujengwa kwa reli ya tazara,makampuni kama ya urafiki, makampuni ya usafirishaji(kauta,kaudo..),..yalikuwa yakifanya kazi vizuri tu,
yaani kwakweli wakati ule utaona kuwa kulikuwa na a sense of government in place,
lakini since then Mungu saidia.
 
Mzee Q,

Numekusikia mkuu, lakini kugusa mchache uliyosema:

(1). MWALIMU KUSHINDWA NA UJAMAA;-
Wakati Mwalimu anaondoka madarakani, na mpaka leo sio clear kuwa ni kwa nini aliondoka, Mwalimu angekuwa mkweli wa sababu zinazomfanya aondoke angetusaidia sana tuliobaki, maana nyumba ikiwa na matatizo huwa tunaenda kwenye msingi, na in this case msingi wetu ni Mwalimu, sasa kwa sababu hatujui kilichomtoa ndio matokeo yake imewasaidia kina Kingunge kubadili hadithi kuhusu Mwalimu kila wakati wa uchaguzi unapofika,

Mwalimu angesema ukweli hadharani kuwa ninaacha urais kwa sababu 1,2,3, and 4, leo kiongozi yoyote angerudia tena yaliyomfanya Mwalimu aache urais tungemjia juu mapema kabla hajfika, lakini Mwalimu hakusema wazi sababu za kumfanya aachie ngazi, na kama ni kweli aliachia ngazi kama unavyosema kwa ajili ya ujamaa kushindwa, basi asingekuwa anawatukana kina Mwinyi, kila wakati kwa kufananisha na siasa zake ambazo unasema alikubali baadaye kuwa ni mbovu, maana kila alipowatukana kina Mwinyi alikuwa akilinganisha na wakati wake, kwa mfano alisema Ikulu hakuwa pango la mashetani kama ilivyo kipindi cha Mwinyi, lakini akashindwa kuelewa kuwa siasa za 90s, za open market alizozifuata Mwinyi, na tulizonazo leo zinahitaji matajiri kama kina Rostam, sio tu kushinda Ikulu, bali hata kuwaajiri kina Msekwa, Spika wa bunge kwenye kampuni ya vodacom. Zinahitaji kina Mengi kufanya kazi bega kwa bega na serikali kwa manufaa ya wananchi, kwa hiyo ni lazima waingie Ikulu kwa wakati wao bila bughudha,

Au tuseme alikubali kuwa ujamaa umeshindwa angesema wazi na pia kuwashauri viongozi wapya njia inayofaa baada ya ya kwake kushindwa, angetusaidia wote wabongo, sina uhakika kuwa that was the case na Mwalimu!

(2). Katika miaka 20 iliyopita kumetokea mabadiliko makubwa katika maendleo ya wananchi binafsi, kulinganisha na yale ya serikali unayoyasema, leo bongo kuna middle class ambayo haikuwepo enzi ya Mwalimu, leo uhuru wa wananchi ni mkubwa mno kusema wanayotaka as opposed na enzi zile, na hayo ni maendeleo makubwa sana tena sana, uhuru wa kufanya wanayotaka leo kwenda ulaya sio tatizo tena kama enzi zile, kwa hiyo kuna hatua kubwa sana iliyopigwa in the last 20 years.

Nitakuja kumalizia baadaye!
 
(3). Masharti Ya Benki ya Dunia:
Masharti labda tulitimiza sehemu tu ya masharti hayo ndio maana tukasamehewa baadhi ya madeni, kile kipindi cha Mkapa, that is all sidhani kama inahusiana na Mwalimu!

(4). Vita dhidi ya Amin!;
Interesting, hivi unajua kuwa hii ndio moja ya sababu kubwa muhimu ya sisi kukwama kiuchumi, why ilibidi tupigane na Amin in the first place? WHY? Kumsaidia Obote arudi? Je was it an interest ya wabongo wote Obote kuendelea kuwa rais? Je ulisikia wakati maiti yake iliporudishwa Uganda, wananchi walijipanga njiani kuizomea! Wakati mpaka leo bado tunalipa madeni ya vile vita?

(5). SENSE OF Government:-
Ninakubaliana na wewe kuwa kwa salimia fulani, hiyo haipo tena kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu, lakini at the same token tusi-underestimate the sense iliyoko sasa ambayo inafuatana na time tuliyonayo, kwa sababu kwa mfano 90% ya baraza zima la mawaziri leo, ni washikaji wa JK is that a plus or a negative? inategemea ni nani unayemuuliza, I mean kati ya wananchi, kuna wanaofikiri ni babu kubwa na kuna wanaofikiri kuwa ni upuuzi, lakini anyway you have a point kwenye hili, ile sense ya kuwa kuna serikali inayitujali wananchi, ilikwisha.

Kwa ufupi katika miaka 20, iliyopita wabongo tumefanya maendeleo makubwa ya binafsi, tena nina hakika hata majirani zetu wanatushangaa kwa kuweza ku-catch up nao kwa muda mfupi hivi, na man maendleo ya binafsi tulikuwa tunayahitaji mno, sasa the next step tunahitaji kuondoa kiswahili kwenye shughuli za serikali, na uswahili wote kwa ujumla!
 
Mzee Es,
Nakubali maneno yako lakini kwa mtazamo tofauti, sijui kama utakubaliana nami.

MWALIMU KUSHINDWA UJAMAA.
Jamani hii ngoma nzito sana kwa sababu wengi wenu mmechukulia tu kushindwa kwa Nyerere ktk Ujamaa bila kutazama kwamba hakuna hata nchi MOJA duniani iliyokuwa na siasa ya Kijamaa ilifanikiwa ktk kipindi cha (cold war). Binafsi hii ni sababu kubwa ambayo nashindwa kulaumu Nyerere zaidi ya kusema mfumo wa siasa yetu ndio ulikuwa mbaya. Na kweli mfumo huo aliuchagua Nyerere tukapanda ndege ambayo haikufika mwisho wa safari. Kifupi ni ndege iliyoanguka na hakutoka mtu, sii Mrusi, Mchina wala Maleysia!

Sasa hapa tukiangalia hawa waliokuja chukua madaraka baada ya mfumo huo kuondoka ndipo utaona kushindwa. Wenzetu kibao wanapiga hatua mbele sisi ndio kwanza tunanyoosha vidole kwa JKN. Je, kulikuwa na serikali mbaya kiuchumi kama ya China, Urusi na hata Ethiopia waliokuwa wakifa njaa kama utitiri! mbona wametoka shimoni.
Kushindwa kwa Nyerere ni pale alipotuachia WARITHI BOMU!.

Hayo madai ya Nyerere kutupa mwongozo nadhani asingeweza kufanya kitu baada ya Ujamaa kushindwa. Vitabu vyake vyote vilikuwa sumu na adui mkubwa wa UTANDAWAZI!...Focus kubwa ilikuwa kumzima JKN kabisaa, na kibaya zaidi tulifumbwa macho tusione nje ya Nyerere na Tanzania kuangalia nchi nyinginezo za kijamaa kama ziliweza kufanikiwa.

Kumbuka alikuwa a good dikteta na alipoondoka hakukumbuka yaliyomkuta Julius Caesar!

Je, Umehesabu pia Madaktari wapya waliojitokeza baada ya Nyerere toka dini nyinginezo?
 
Mzee Bob,

Ninakuelewa vizuri na sina noma na mawazo yako, nyongeza yangu ni kwamba Mwalimu angekubali wazi kuwa ujamaaa umeshindwa na sababu zake, angetusaidia kuelewa tulipo na tunakokwenda, leo CCM inasema bado inaendelea na siasa ya ujamaaa na kujitegemea, hapo ndipo tunchangnywa?
 
Swahiba Mkandara,
Hapo umenikuna, well said!
Watanzania wengi na au waafrika wengi tumeshindwa kutofautisha au kulinganisha na kuunganisha Democracy, Our Rights, and responsibility. Watu wanasema Nyerere alikuwa dictator, to which extend? Aliyoyafanya mazuri tumeyaona, ok, wote about our responsilities? Did we fulfil our responsibilities? Nadhani Democracy ndiyo kinyume cha dictatorship. Singapore Lee Kwangye aliendesha nchi yake kwa mising ya ki-dictatorship, hadi leo Singapore ni a country very advanced! Lee alifanya misingi ile ile kama ya Nyerere, kuwasomesha watu wake kwa nguvu zote, na waliosomeshwa wakawa na responsibility to pay back to their country. Singapore haina mineral or oil reseves, hata ardhi haitoshi, lakini leo ina uchumi mkubwa duniani. Na hadi leo hii is a dictatoriaal state.

Twende China, wao wanakwambia democracy and socialism in Chinese Characteristics. Wanasema nchi yao ina democracy na human rights to their citizen ni access to FOOD, SHELTER, AND SECURITY!! Sasa unaona hapo. Ofcourse wanafungua pole pole ingawa access to information bado kidogo.

Lakini Wachina au Wasingapore hawakai kumlalamikia Lee Kwanye au Mao, they are putting their resposnibilities and rights together. Democracy ya West haijazi tumbo. Mie nafikiri Nyerere kwa misingi ile ya wakati ule alikuwa right, but We as CITIZENS and LEADERS below Nyerere were not responsible.

Nyerere kilichofanya ashindwe si kuwa alikuwa hajui uchumi, la hasha, alikuwa ni msomi mzuri sana, alijua stage ya watu wake ni ipi, kama kuwaadhibu, au kuwa funga, angewafunga wengi sana, alijua kuwa kama angefanya hivyo sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine.

Mistake as a leader Nyerere alifanya makosa, kosa mojawapo ni lile la kutohusisha na kutenganisha peasantry farming and Large Scale farmers na settlers farmers. Utaifishaji wa mashamba, yale ya Kilimanjaro, Tanga na Iringa ilkuwa ni makosa makubwa. Kumbuka mwaka 1967 Tanzania ilikuwa inaexport chakula, katani, tumbaku, coffee, pamba etc. Alibidi atenganishe Large Scale farmers na peansatry. Yeye angejishughulisha zaidi na settlement na allocation ya peasants.

Kama alivyosema Mzee Es, Vita ya Kagera na Idd Amin iligeuza kaabisa Economy ya Tanzania, Tanzania ilitumia reserve na mikopo kumtoa amini. Hayo ndiyo matokeo ya foleni, unga wa mhogo, na sukari yenye mchanga.

Kosa jingine ambalo limefichika sana ni lile la ukombozi wa bara la africa. Kuikomboa mozambique, zimbabwe, Angola, Namibia, na Africa Kusini pesa zilizotumika ni nyigi mno!! Kuna zaid ya USD 3billion ambazo huwa hazieleweki zilitumika vipi as donated money kutoka western world, hizi pesa zilienda kwenye ukombozi wa Africa. Fikiria yale makundi ya Waafrika kusini, Zimbabwe, Angola, Mozambique walikuwa na camps Tanzania na nyingi zilikuwa funded na Tanzania.

But otherwise what should we say? Ndiyo ilikuwa siasa ya wakati ule. Kama alivyosema Mkandara, Mwinyi, Mkapa, wamefanya nini kurekebisha haya mambo? JK sasa anafanya nini? It is almost 21 years tangu Nyerere aache madaraka, where are we? Kumbuka 20 years after China imekuwa na maendeleo makubwa, why so?

REmember: Rights GO with responsibility; we demand rights; but are we responsible for our own country, people, families etc etc???
 
Kabla ya kuwa rais Mwinyi aikuwa amewahi kufanya nini cha maana, na hasa kuhusu uchumi? Na Mkapa je aliwahi kufanya nini? Je ni sisi wananchi ndo tuliwachagua hawa?

Je majibu ya maswali haya mawili si ndio ukweli wa kwa nini hatujafanya kitu kama Wachina for the last 20 years yalipo?
 
Mzee ES,
In the absence of Mwinyi and Mkapa, unadhani ni nani kati ya ile safu ya viongozi wanaojulikana angefanya maajabu? Nimekuwa nje ya mada kwa muda sasa, lile swali lako jingine nitakujibu kabla ya mwisho wa wiki hii.
 
IO,
Swahib maneno mazito na sijui lini tutaweza jifunza!..

kwa kuongezea tu binafsi naamini watu hutegemea kuongozwa kufikia malengo fulani. Kiongozi akiwa bomu basi hata sera zake huwa bomu vilevile!

mapinduzi ya kiuchumi China, Maleysia na nchi zote za tiger yalisubiri tu viongozi wenye upeo mkubwa ktk hili swala la Accountability. Singapore na hata Libya ambazo zipo chini ya madikteta ziko mbali sana... mshikaji huwezi kumkuta M-Libya nje ati mkimbizi...Ukizaliwa tu Libya nyumba ni moja ya haki za mzawa! hakuna nchi inayowalipa wananchi wake mshahara mkubwa kama Libya.. yaani mshahara wa chini Libya ndio pato la middleclass US, lakini hapohapo huna sababu ya kutofikia malengo ya uzalishaji unaotegemewa kwa mwaka....Mtoto kutokwenda shule ni criminal offense kwa mzazi!

Nakubaliana na wewe mia kwa mia kwamba mbinu zipo kibao isipokuwa isipokuwa uzembe upo kati yetu na Utawala tuliokuwa nao. Hakuna hata nchi moja duniani iliyokuwa tajiri mwanzo na kipimo cha mafanikio yake kikaanzia hapo isipokuwa nchi zote zilianza somewhere kama hazina kitu.

Kuhusu vita mshikaji nadhani ule ulikuwa wakati mwingine kabisa!.. vigumu kuelewa sababu na umuhimu wa ukombozi wa Afrika hasa baada ya sisi kujiuza kama malaya kwa wazungu na huu Utandawazi. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanamke malaya na yule mwenye staha ya mwili wake na mwenye Self confidence ya kuweza kufanikiwa bila umalaya. Kwa hiyo swahib hapa sii kazi ndogo kuelewa kwa nini tulifunga ndoa na mume wa kwanza asiyekuwa na kitu ikiwa umalaya ndio unaoweka mkate mezani petu.

Nyerere alijaribu kuwa superpower of Africa lakini akasahau kukusanya shukrani zake (PUNGUFU). Ukitazama kwa makini marais wote waliochukua madaraka kusini mwa Afrika baada ya mapigano na matumizi makubwa ya fedha zetu utakuta karibu viongozi wote aliwaweka yeye na walikuwa wakilindwa na makomandoo wetu. Kwa nini hakukusanya kurudisha fedha zetu?...

Kwa hiyo IO mimi nakubali sana tunaposema hili ni KOSA kuliko kutumia neno MAPUNGUFU kwa sababu kama Nyerere aliweza kufanikisha azma yake sidhani kama kulikuwa na mapungufu ktk uongozi wake..tukiacha hilo la kutoweka madai ya fadhila yetu kulipwa. Ukombozi kusini mwa Afrika ulikuwa lazima mshikaji nakumbuka Zimbabwe walipopata uhuru, sisi tulikwenda huko kwa mara ya kwanza mtu mweusi machinga sisi tuliweza kuingia nchi hiyo kama binadamu. Tukahudumiwa na wazungu ingawa iliwauma sanaa!

Ebu fikirieni kitu kimoja - South yote ingeekuwa chini ya apartheid hadi leo hii. Jamani msifanye mchezo na Ubaguzi hasa anapokamata mzungu!

Mzee ES,
Yes, nimekubali mwenyewe kuwa hoja yako nzito kuhusu Nyerere!..

Nimekaa hapa na kujiuliza maswali yako mshikaji sina jibu isipokuwa kweli kama sii Nyerere akina siye tusingelaumu kuhusu Mwinyi wala Mkapa na leo hii JK. Imekuwaje sisi tuyaone mapungufu haya tukiwa watoto wa Nyerere lakini Mzee alishindwa kuona mapungufu ya wanawe!.
 
Mzee Jasusi,

Mwalimu was the man, maana yake sio kwamba kulikuwa na wengine, HAPANA! wote tumejionea kwa macho yetu vipindi vya Mwinyi, Mkapa, na sasa kwamba Mwalimu pamoja na uzuri na ubaya wake, bado hana mpinzani katika siasa yetu ya bongo, I mean no body, viongozi wote wengine should go home! FULL STOP!

Yes!, kwa sababu inawezekana ndio maana hakutaka ushauri wa viongozi wenziwe, hebu niambie ushauri wa nani? Mtei? Mtei huyu aliyeruhusu mtoto wake akala hela zote za Chadema kule DC na wanawake na mapombe kibao ndio mnasema Mwalimu angemsikiliza?

Mwalimu angemsikiliza marehemu Prof. Rweyemamu? another shock, huyo Mzee akaacha mke wa miaka karibu 30 na watoto wake bila msaada wowote na kwenda kuoa kimada na kumuachia mali zake zote huku familia yake ameiacha ikiahangaika, ndio angetusaidia taifa letu huyu?

Angemsikiliza Kambona, a foreigner? Unajua I get so upset kwamba sometimes ninafikiri Mwalimu was right kutosikiliza viongozi hawa uchwara, maana at least chini ya Mwalimu kuna mengi ya kuonyesha, physically, Tanzania tulikuwa tunaongoza Africa nzima kwa literacy, wakati anaacha urais dola moja ilikuwa ni shillingi 16, za bongo as opposed to shillingi 1, 300 leo!

Viongozi walikuwa na adabu, maana kuitwa Ikulu na Mwalimu ilikuwa sio mchezo, muulize Mwabulambo, aliyechaguliwa kwenda Songea kuwa mkurugenzi wa maendeleo, akawa anakwepa na kuwaambia wenziwe eti Songea ni shamba hawezi kwenda huko, Mwalimu akasikia, akamwita, alipoitwa tu alijua kuwa anaitiwa nini, alianza mwenyewe mlangoni wakati wa kuingia kwenye ofisi ya Mwalimu,"..... Mwalimu nimeshasafirisha mizigo ninaondoka kesho........", kabla hajaulizwa, that is leadership, na ndio maana ninasema kina Mwinyi, Mkapa, na hawa uchwara wote please just go home!

Lakini bado ninahitaji maelezo kuhusu wasomi wa Kiisilamu, ambao mimi binafsi sikujua kuwa wapo mpaka Mwalimu alipoachia ngazi, WHY?
 
Mzee Es,
hawa wasomi wote wa Kiislaam, kifupi ni matunda ya Nyerere. Walikuwa shule nchi za nje kwa scholarship za Nyerere...Na kama hujaangalia vizuri leo hii tuna maprofessor kibao TZ wa kila dini na kabila... kumbuka Mzee ES ni miaka 22 imepita toka Nyerere ajiuzuru na hawa ma DR. wengi ndio kwanza wanacheza na 50...kifupi walikuwa vijana wadogo wanaotafuta elimu kama mlivyokuwa mkuwaagiza waislaam watafute elimu.
Na mshikaji ukiangalia watumishi wa serikali siku hizi hao wenye Ma -DR walivyojaa utakaa chini na huwafahamu kabisaaaa! na kwanza gari letu linarudi nyuma...
Wewe sema unataka kijiwe kiingie ngazi nyingine hapa lakini hatutakimbia mara hii tupo na wewe sambamba!
 
Kwenye hiyo point sidhani kama umenielewa, my point ni kwamba siamini kuwa Mwalimu alikuwa mdini kama yote tuliyoyasikia wakati wa Mwinyi, kwamba Mwalimu alikuwa mdini na aliwabana Waisilamu,

As much as sitaki kuamini hiyo charge against Mwalimu, bado ni lazima ni-face ukweli kwamba baada ya Mwalimu kuondoka, ndipo Waisilamu wasomi wakatokeza kwa wingi na kuwekwa kwenye nafasi muhimu za serikali, wakiwemo kina JK, Msabaha, Mtulia, Daraja, Lipumba, na the likes,

Sasa swali langu ni kwamba je Mwalimu alikuwa mdini? Kama hakuwa ilikuwaje Waisilamu wasomi watokeze baaada ya yeye kuondoka? I mean Bob nimekusikia, lakini bado ninashindwa kumhukumu Mwalimu on this, kwa sababu ninaamini kuwa Mwalimu was a good man, lakini ya Waisilamu walikuwa wanasoma, ni sawa lakini not enough, kwa sababu sikujua kuwa watu kama Daudi Mwakawago, Haas Kitine, Mtulia, walikuwa ni Waisilamu, mpaka Mwalimu alipoacha madaraka,

Je ni kwa nini enzi za Mwalimu walikuwa wanajificha dini ku-practice dini yao, kama walivyofanya baada ya Mwinyi kuingia? Enzi za Mwalimu walikuwa wanaogopa nini?

Hilo tu ndilo swali langu ninaona hujanielewa vizuri, na hat lisipojibiwa sio tatizo lakini sina mpango wa kuanzisha issue ya udini, na niliamua kuchangia hii mada tu baada ya kuiona inaogopwa, that is all!
 
Swali lako zuri Mzee ES!

Hiyo kwangu inaonyesha ni jinsi gani wakati huo watu walikuwa wanaweka dini zao nje ya kazi!

Tena Haas(Hassan) kitine ni mwislamu na amewahi kuwa mkuu wa usalama wa taifa kwa muda mrefu katika utawala wa Mwl. Na mambo yalikuwa saafi kabisa!

Tukifanikiwa kutenganisha upendeleo wa kutoa kazi kwa kigezo cha dini tutafi tutaendela kuwa na taifa lenye mshikamano.
 
Kwa Haraka Tu Nawakumbuka Waislam Hawa Waliwahi Kushika Nafasi Mbalimbali Kama Uwaziri Au Ubalozi Wakati Wa Mwalimu Nikikumbuka Nitakuja Na List Kamili
Rashid Kawawa
Chief Abdalah Fundikila
Thabit Kombo
Titi Mohamed
Amir Habib Jamal
Prof Mohamed Babu
Balozi.ally Mchumo
Ibrahim Kaduma
Makame Hasnu
Ali Hassan Mwinyi
Dk.salim Ahmed Salim
Anna Abdalah
Balozi Hassan Diria
 
Mzee ES,
Swali lako zuri. Sidhani kuwa naweza kujibu zaidi ya alivyofanya Mkandara. Lakini eti walijitokeza wengi baada ya Mwalimu kuondoka mamlakani huenda ikahusiana na dhana iliyoenea wakati wa Mwinyi kuwa umefika wakati wa kuwapromote Waislamu. Si unalijua sakata la Harun Mahunda? Alipokutana na Mwinyi wakati anateuliwa kuwa mkuu wa polisi Mwinyi akamshauri kuwa kila inapopatikana nafasi awapromote "waislamu wenzetu." Mahundi akamjibu rais kuwa mimi ni Mkristo. Sasa ungeweza kuimagine Mwalimu amwambie afisa wake ujinga kama huo? Wakati wa Mwalimu dini haikuwa kipaumbele. Lakini kitu alichojaribu kufanya Mwalimu ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania is represented katika appointments muhimu. Kuna jamaa kaulizia mambo ya Takadir. Nikipata fursa nitaongelea ninayoyajua kuhusu hilo. Kwa sasa nakimbia kanisani.
 
Back
Top Bottom