Nyerere, Tanganyika tunatukanwa na tukae kimya?

Status
Not open for further replies.
Zanzibar ni nchi mzee, nenda majuu, TANGANYIKA haipo wala haijulikani. Hivi pakiwepo na ugonvi kati ya yako na jirani yako juu ya mambo ya kimaisha na msuluhishi akasema kila mtu aweke katiba yake mezani ili apate mwongozo wa kupatanisha; hivi wewe isiyekuwa na katiba, jina na hata utambulisho (nembo) si utaonekana *****?. Utapatanishwa utafanywa vipi kati yako usiyekuwa nakatiba na mwenye katiba? Tanganyika isiyokuwepo na Zanzibar ni ipi chi? jibu ni rahisi -Zanzibar huru na bara siyo nchi ni Koloni la Zanzibar.


Samahani kabla sijachangia hivi CAPTAIN MAHFUDHI YUKO WAPI?
 
nyerere mnadhubutu kumuita baba wa taifa anatukanwa kuliko mbwa na bado serikali na majeshi yake inatulia?

Watanganyika (watanzania bara) wanatukanwa na kubaguliwa kuliko mbwa na bado kimya?

Visiwa vyetu tulivyovikomboa kwa jitihada ya mwalimu nyerere ndio leo vinatuita koti linalobana kwa hiyo wanatuvua?

Wamenona kumbe, baada nyerere kumtimua sultani kwa nguvu na jasho letu watanganyika, wananchi (watumwa) walioachwa na sultani tukawalisha mpaka hivi leo wamenona wana maendeleo kuliko bara, wana umeme wetu toka ubungo kwa masaa 23 mpaka 24 wakati watanganyika wengi wakihangaika, vingi wanavyonufaika kutoka kwetu (hebu wakuu jaribuni kuorodhesha wanatutapeli) wao wanaona tunawahonga au kujipendekeza wabaki ndani wakati wao ndio wana deni la kukombolewa, jamani mbona serikali kimya, jeshi kimya?

Na sisi wananchi mbona kimya? Wenzetu wangapi kule zenji wamepigwa, wamebakwa, wamekamatwa, wamechomewa, wamefukuzwa na manyanyaso mengi tu, kwa nini kisehemu cha nchi yetu cha watu laki 6, kwa sababu laki 6 wengine wako bara watuibie na kutunyanya watu milioni 48? Tuwape ushindi makundi ya uamsho wa kiislamu yanayofadhiliwa na iran yanajifanya yanatumia dini ili kuvunja muungano? Au tukabili hili janga lingali bichi?

Dawa ni serikali moja tu, jamhuri ya tanzania (sio ya muungano) muungano ni miaka hiyo, sasa hamna cha kuunga tena wa kugawa, nchi sio koti kama midebwedo inavyodai.

Viva jamhuri ya tanzania!!!

samahani kabla sijachangia naomba mnieleze captain mahfudhi yuko wapi?
 
Mkuu tukuwapa uhuru ndio tutajutia maisha, kwani sasa wanaponzwa na walewale walioipotosha Somalia miaka 22 iliopita na hatimae nchi huyo imefali na inafelisha majirani pia,
Zanzibar kwa asilia 100 itafeli, kwa njaa watahamia baharini kafanya uharamia tu, wataiua Tanganyika kabisa kibiashara.
Samaki mkunje angali mbichi, wasitoke hata kidogo/

samahani kabla sijachangia hivi captain mahfudhi yuko wapi?
 
nyerere amesha fariki. Hakuna kinacho tokea sasa kinacho muathiri. Kina athari walio hai na kizazi kijacho. Kwa hiyo kama tuna bakisha muungano kwa ajili una manufaa kwetu sawa ila tusi tetee muungano kisa tu uliasisiwa na marehemu. Kuna msemo usemao "the only thing that is constant is change". Namheshimu sana nyerere na atabaki kuwa icon wa tanzania ila "life is for the living" and the dead only have dreamless sleep.

subiri kidogo naona zanzibar unaijua vema hebu niambie captain mahafudhi yuko wapi?
 
Ugali hawaupendi kwa kuwa ni mgumu, vitu vigumu gumu hawavipendi! si unajua watu wenye usaudia? wao nakshi nakshi tu, wanapenda khalua, orojo, biriyani, keki, yaani wanapenda laini vitu vya kudondoka bila kusukuma saaaana na pia mafuta ya nazi na manukato ya kiarabu aaakh buheeeri...

subiri kidogo naona zanzibar unaijua vema hebu niambie captain mahafudhi yuko wapi?
 
wazanzibar ndio wenye haki ya nchi yao ndio wataovunja muungano.......nchi nyingi tu duniani wamevunja muungano baada ya kuona hakuna maslahi kwao...kwa nini zanzibar ishindwe?

Senegal and gambia walivunja muungano
ethiopia and eritria walivunja muungano
soviet union ilivunjika yote

why not zanzibar...wewe shogaa nini?

iv unadhan kuvunga muungano ni kama kuvunja kijiti?2mia akili wazanzibar co mature enough kujitawala na kuitwa nchi...wat a such stupid idea kujitenga?
 
WANAJF;
Kwa hali ilivyo sasa kule Zanzibar ni hatari sana kwa ndugu zetu wabara wanaoishi kule, kwani kwasasa ni hatari hata kwao kwenda mtaani hasa maeneo ya Darajani kufanya shopping kwasababu wanafanyiwa dhiaka kubwa sana na hata kudhalilishwa na Wazanzibar. Kauli wanazoambiwa na Wazanzibar ni kwamba waondoke warudi bara kwasababu hawahitaji wabara huko Zanzibar. Hali ni mbaya sana kwa wenzetu na serikali imekaa kimya bila kusema chochote.

Jambo lingine ni ubaguzi hasa wa kidini unaoendelea huko Zanzibar. Ukijaribu kufuatilia ile mikutano yote ya UAMSHO unaofanywa kule, utagundua kwamba viongozi wa nchi wanaochafuliwa ni Nyerere, Pinda na Samuel Sitta. Ukichunguza sana utagundua kwamba hawa wanachukiwa na kudhalilishwa tu kwasababu wana imani nyingine tofauti na Uislamu. Nasema hivyo kwasababu, ni viongozi wengi tu wa CCM ambao ni waislamu tena wamezuia mjadala wa mambo ya Muungano lkn kamwe hutasikia wakitajwa kwenye mikutano yao. Sasa swali la kujiuliza hapa ni kwamba, je Nyerere alitumia nguvu ya dola kumlazimisha Karume kuingia kwenye Muungano? Je, Pinda na Sitta ndiyo wenye sauti ya mwisho kuhusu mambo ya muungano? na kama wapo wakubwa wao, je ni kwanini wao hawaguswi na hawa wanaotaka muungano uvunjike?

Ndugu zangu, kwa hali ilivyo na matatizo wanyokutana nayo wenzetu wanaotoka Bara kule Zanzibar, ni hakika Serikali inabidi ichukue hatua sasa kwasababu watu wetu hawawezi kuwa kifungoni ndani ya nchi yao kisa wanatoka upande muungano wa Muungano. Huu ni unyanyasaji mkubwa sana wa haki za raia halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ni kinyume na haki ya raia kwenye Katiba yetu.

Wazanzibar kama wanataka kujitenga wao wana viongozi wao, ni kwanini wasitumie utaratibu unaokubalika? ni kwanini wawanyayase wenzetu? kwani hao wenzetu walioko huko visiwani ndiyo waliousaini mkataba wa muungano? HAKIKA HUU NI UONEVU MKUBWA SANA UNAOFANYWA NA WAZANZIBAR DHIDI YA WATANZANIA WENZAO WENYE ASILI YA BARA.

Nawasilisha.
TELO.
 
Poleni Watanzania Bara walioko visiwani, huu wote utazidi kuimarisha Muungano
 
Come on great thinkers hapa tujadili udhaifu wa dola jinsi inavyofumbia macho uchochezi wa jumuia ya uamsho na matusi kwa viongozi wa kitaifa,kuweka kejeli na matusi dhidi ya wazenji tunarudia makosa hayo hayo ya upuuzi wa jumuia ya uamsho
 
Poleni Watanzania Bara walioko visiwani, huu wote utazidi kuimarisha Muungano

Mkuu, imani dhahiri kabisa ya moyo wako na akili zako inakubaliana na haya uliyoandika?! Sitaki kuamini kwamba Muungano utadumishwa kwa uonevu na udhalilishaji, na ninaamini ni kina Pharaoh tu wanaoamini kwamba uonevu na udhalilishaji huleta umoja(Muungano)!!
 
sijaona lolote la maana mnalozungumza bali 'porojo' tu. ni kweli waZanzibar tunadai nchi yetu, Zanzibar ilikuwa Dola kabla ya hiyo yenye kuitwa Tanganyika. someni historia jamani! tuna sababu zetu za msingi, tumechoka kunyanyaswa nanyi. tuachieni tupumue jamani, tumekuvumilieni muda mrefu ishafika wakati tunadai haki yetu kwa nguvu moja. "Zanzibar kwanza shengesha baadae". Nyinyi bakieni na hilo jina lenu Tanzania maana yaonesha mwalipenda sana. wengi wenu mliozungumza hapa yaonesha hata hamuijui historia yetu hadi kufikia Muungano huu haramu! najua wengi itawauma lakini ukweli juu ya huu muungano HARAMU uliodumu kinguvunguvu kwa miaka 48, sisi waZanzibari twajinasibu na Uzanzibari wetu kuliko utanzania. LOO! i hate to be called tanzanian!! ipo siku na haipo mbali nitatambulikana duniani kote 'officially' kama ni MZANZIBARI na nakuhakikishieni haipo mbali siku hiyo, wacheni kama tutabaguana, tutatengana, tutapigana, tutaleta ual qaeda nk hiyo si kazi yenu, najua mtanuna lakini habari ndio hiyo! naona mmesahau "when one pipes in Zanzibar, they dance in the lakes" nendeni kaburini kwa huyo baba yenu wa taifa mkamuulize nini Zanzibar! ooo AM proud to be Zanzibari!
 
Poleni Watanzania Bara walioko visiwani, huu wote utazidi kuimarisha Muungano

Ndugu yangu (sijui kama utapenda kukwita hivyo) hamna Mtanganyika anayebughudhiwa kwa maana ya kubughudhiwa hapa Zanzibar. istihzai za hapa na pale zipo sikatai kama zilivyokuwapo huko Tanganyika kwa akina sisi. Sisi ni watu wakarimu na wastaarabu, kama hujatuudhi, nasi hatutakuudhi wacha propaganda zako chafu. Wengi wa waTanganyika walio huku ni wauza karanga/dawa za mbu, wafanyakazi mahotelini ambao wamepanga majumba yetu. Tizama waZanzibari walio huko bara wengi ni wafanya biashara wakubwa, na kwa kiasi kikubwa tumekusaidieni kwenye kila nyanja (kubalini/kataeni) ukweli ndio huo! hapa hamna tena kuimarisha muungano, ustaarabu wetu umetuponza kwa muda wote huo, ni kuuvunja tu baas! kaeni mkao wa kula msikie mziki wetu, mtatujua sisi nani mwaka huu!
 
Come on great thinkers hapa tujadili udhaifu wa dola jinsi inavyofumbia macho uchochezi wa jumuia ya uamsho na matusi kwa viongozi wa kitaifa,kuweka kejeli na matusi dhidi ya wazenji tunarudia makosa hayo hayo ya upuuzi wa jumuia ya uamsho

Kwa taarifa yako, Jumuiya ya Uwamsho (Allah azidi kuibariki) haina uchochezi, nikiwa kama mZanzibari kindakindaki nasema hivyo. Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Taasisi nyengine (adheem) za Kiislam hapa Zanzibar inahubiri kile ambacho waZanzibari tulio wengi tunakitaka tokea 1964, baada ya kupatikana huu wenye kuitwa Muungano (loo!) Tumefikia wakati vyama vya siasa tumeona havitupi haswa kile tukitakacho, imejitokeza Jumuiya hii pamoja na Taasisi nyengine kadha wa kadha kupaisha kilio chetu, na NAAM tumezikubali na tupo pamoja nazo bega kwa bega. Hamna mZanzibari kindaki ndaki kama mimi anayeutaka huu wenye kuitwa Muungano ukiondoa wale wenye maslahi nao. Lakini ndo tusaliti nchi yetu Tukufu, chambilecho chief Anyaoku alokuwa chief sec wa Jumuiya ya Madola "the pearl of Africa" kwa maslahi ya hao wachache?? LAAA time imefika twataka ZANZIBAR yetu imma faimma, imetosha tena imetosha. habari ndo hiyo
 
Nyerere mnadhubutu kumuita Baba wa Taifa anatukanwa kuliko Mbwa na bado Serikali na Majeshi yake inatulia?

"Naam hatumthamini kabisa nyerere kama mnavyomtukuza huko kwenu, ndio hisia zetu samahani kwa hilo, nanyi kama kuna kiongozi wetu aliyekuudhini mnao uhuru wa kumtukana mtakavyo. Ulitaka Serikali na jashi itufanye nini? wakati huo umekwisha itakavyopigwa ndivyo itakavyochezwa, hii ishu ipo kiimaan zaidi kuliko kisiasa. sijui kama umenifahamu?"

Watanganyika (Watanzania bara) wanatukanwa na kubaguliwa kuliko Mbwa na bado kimya?

" sijui tafsiri yako nini kutukanwa/kubaguliwa, (ungesema Watanganyika tu ingetosha, sote twafaham ni akina nani) tuanzeni jamani kuyatumia haya majina yetu ya asili! hajabaguliwa wala kutukanwa mtu kwa maana halisi ya maneno hayo, acha uchochezi wako, mtu mzima haambiwi muongo"

Visiwa vyetu tulivyovikomboa kwa jitihada ya Mwalimu Nyerere ndio leo vinatuita koti linalobana kwa hiyo wanatuvua?

"Ni kweli 'mchonga meno' kashiriki kikamilifu katika mapinduzi/mavamizi yale ya 1964, sasa kwa nini baada ya kufanikiwa kwake asivichukue tu hivi Visiwa, ila amuhadae kiongozi wetu Karume Sr. kwenye huu muungano feki?. Ni kweli ni koti linatubana na ishafika wakati wa kulivua"

Wamenona kumbe, baada Nyerere kumtimua sultani kwa nguvu na jasho letu Watanganyika, wananchi (watumwa) walioachwa na sultani tukawalisha mpaka hivi leo wamenona wana maendeleo kuliko Bara, wana umeme wetu toka Ubungo kwa masaa 23 mpaka 24 wakati Watanganyika wengi wakihangaika, vingi wanavyonufaika kutoka kwetu (hebu wakuu jaribuni kuorodhesha wanatutapeli) wao wanaona tunawahonga au kujipendekeza wabaki ndani wakati wao ndio wana deni la kukombolewa, jamani mbona serikali kimya, jeshi kimya?

"Watumwa umekusudia hao baadhi ya jamaa zako walotoka Bara? maana hakukuwa na Mzanzibari kindakindaki hasa alokuwa mtumwa, watumwa wote wakitoka bara na maziwa makuu, siaktai wengi baadae tumechanganya nao hadi sasa.
Umeme wa ubungo nasi tumechangia kikamilifu kuuvuta toka huko hadi huku (enzi za Rais JUmbe) na ni hiyo serikali yenu ndo imetuwekea vikwazo hadi leo hii kutupa nafasi ya kuwa na chanzo chetu cha umeme (moja katika karaha ya muungano huu feki)... sasa nyinyi mwatuhudumia kila kitu nasi hatuwataki, kwa nini sasa mwatung'ang'aniya tu??!! kichekesho hiki jamaa!, au mwajihisi hamuwezi kuishi bila sisi? Hamjui kukataliwa jamani? Tuwacheni tupumue, penzi halilazimishwi!!"

Na sisi wananchi mbona kimya? Wenzetu wangapi kule Zenji wamepigwa, wamebakwa, wamekamatwa, wamechomewa, wamefukuzwa na manyanyaso mengi tu, kwa nini kisehemu cha nchi yetu cha watu laki 6, kwa sababu laki 6 wengine wako Bara watuibie na kutunyanya watu milioni 48? Tuwape ushindi makundi ya Uamsho wa Kiislamu yanayofadhiliwa na Iran yanajifanya yanatumia dini ili kuvunja Muungano? Au tukabili hili janga lingali bichi?

"Hii ajabu! lini mambo hayo, ama ukinambia waZanzibari ndio walofanyiwa vitendo hivyo wakati ule wa Mkapa na siasa chafu zilizokuwepo nitakukubalia, ila usemavyo ni uwongo wa dhahir! tena uchochezi. Kwani huku kuvunjika huu Muungano feki utaathirika nini wewe? mbona watutukana na kutusimbulia kisha unataka mpaka jeshi likusaidie tusiondokane na udhalimu huu wa Muungano, subhanallah! sijayaonapo haya mambo, wewe ukitaka usitake sisi twadai chetu na hamna wa kutuzuiya, hayo ya Iran sijui nani yako mwenyewe!"

DAWA NI SERIKALI MOJA TU, JAMHURI YA TANZANIA (SIO YA MUUNGANO) MUUNGANO NI MIAKA HIYO, SASA HAMNA CHA KUUNGA TENA WA KUGAWA, NCHI SIO KOTI KAMA MIDEBWEDO INAVYODAI.

" Unaota tena mchana, maana kwa hilo hata hao madalali CCM wa hapa Zanzibar hawalitaki,(CUF wao wakitaka serikali tatu) seuze sisi Wazalendo ambao ndio tupo wengi na tuna nguvu, masikini vyombo vya habari vimejitahid kunyamazia harakati zetu hizi, ila leo twashukuru bila ya wao mambo yapo hadharani tena yashanoga. hapa hamna cha Tanzania wala nini ZANZIBAR kwanza, wewe baki na jina Tanzania sisi hatuna haja nalo, tokea hapo hatujinasib na hilo jina, haijambo hata kwa hili CCM wametusaidia. Tatizo jamaa zetu huko mnafikiri hili jambo limezuka jana na leo tu. ngoja tulikamilishe tukupeni mbinu/mipango tuliotumia, uhakika mshachelewa sisi ni walimu wenu taka usitake"

VIVA JAMHURI YA TANZANIA!!!

"HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHA"
too late!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom