Fursa Pesa
JF-Expert Member
- May 30, 2012
- 4,433
- 3,253
Enough with romantization of Mwalimu.
99% ya watawala wetu leo wote walilelewa na mwalimu hivyo ni uzao wake
kwa hiyo its fair to say matatizo yetu yalianza toka enzi zake na sasa wanaendelea kuruthishana kama ambavyo CCM wanawapitisha watoto wao kuchukua na nafasi na CHADEMA akina mtei kuwaandaa akina Mbowe kututawala
Mimi naona Mwalimu ndio cause ya matatizo yetu yote haya
hakutaka accountability wala transparency kwa hiyo wanasiasa wetu wa leo wanaendeleza yale yale ya mwalimu.
Kama hamuamini Tazama Cabinet imejaa akina nani na wametokea wapi? Mtu kama Mathias Chikawe tazama profile yake utaelewa naongelea nini
Yaani wewe kununua simu,gari na nyumba ya vyumba kadhaa tayari unajiona tajiri na kusahau kabisa kazi kubwa
aliyoifanya Hayati.Mwl.J.K Nyerere ambayo ndio hio hio inayokufanya leo kupata aka ka uhuru ka kuzungumza haya.
Hayati.Mwl J.K Nyerere alifanya kazi kwa unyenyekevu,busara na hekima kubwa
1.kuhakikisha nchi inakuwa salama kwa gharama yoyote.
2.Kuunganisha makabila zaidi ya 124 kuzungumza kwa lugha moja.
3.Kuwandoa watanzania katika fikra za kufanyishwa kazi kama manamba na kuwajengea uwezo wa pamoja katika kazi zao
hasa zile za kilimo,mifugo,uvuvi na viwandani.
4.Kuyabaini mapungufu ya kiutawala mapema na kuyasemea bila woga,hofu au upendeleo wa kundi fulani kwa maana ya
rangi,dini,kabila au sehemu litokako.
Utawala wake Mwl.Nyerere uligubikwa na misukosuko mingi hasa ile iliyotoka nje ya nchi na hata majirani zetu hivyo
mpaka anastaafu Urais tayari mfumo wa dunia ulikwisha zorotesha mambo mengi muhimu na bora ambayo aliyaanzisha
kwa nia njema kwa taifa lake.Hivyo kumlaumu kwa maana ya materils si sawa,sote yatupasa kumkumbuka na kumuenzi
mwalimu kwa kuwa ndiye alikuwa muasisi wa amani ya roho(spiritual) hata kama hakuna kitu mifukoni.
Kaa tena ufikiri kwa kina hii post yako kama ni sawa au si sawa kwa mkuu wetu kama yule aliyetutoka na kutuachia
pengo kubwa kwa ushauri na maelekezo muhimu yanayojitokeza hasa wakati huu wa Dunia ya utandawazi.