Nyerere na Idi Amin Dada. Marafiki-Maadui. Sijui walikuwa wanaongea nini

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
319702_4052546514308_1794316939_n.jpg
 
Hapa walikuwa wapi namwona kwa mbali Mama Maria Nyerere.
319702_4052546514308_1794316939_n.jpg
 
Nadhani hapo walikuwa hawajaanza kuwa maadui. Kumbuka hawakuzaliwa wakiwa maadui, something happened after sometimes ndo wakaanza kuwa maadui
 
Nakumbuka kwamba hapa ilikuwa mjini Mwanza wakati huo Mwalimu alikuwa ziarani mkoani humo, na Idd Amin alikuja bila taarifa tena kwa ndege ya kivita aliyokuwa akiiendesha mwenyewe. Inasemekana kwenye ndege hiyo walikuwa wawili tu yeye na mwanawe kipenzi akiitwa Moses ambaye wakati huo alikuwa mtoto wa miaka kama kumi hivi. Habari hii ilipatikana kwenye redio mbao miaka hiyo na ilikuwa kabla ya vita na Uganda ingawa uhasama ulishapamba moto.
 
Wanaongea kama Kikwete na Joyce banda walivyoongea jana kuhusu mpaka wa Malawi huku wote Joyce na Jakaya wakicheka kwa furaha.
 
Kwa jinsi walivyokaa uadui ulikuwa bado haujaanza. Wote walikuwa viongozi wa Jumuiya ya Africa Mashariki pamoja na Mzee Jomo Kenyatta iliyovunjika 1977 na vita ya Kagera ilianza 1978.
 
we call it love and hateful relationship! lakini kumbuka ingawa tulikuwa maadaui, Tanzania iliungana na mataifa ya kiarabu duniani kuilaani Israel kwa kitendo chake cha kutumia makomandoo kuokoa mateka wake pale entebe mwaka 1976!
 
Huyo mama ni mama Maria Nyerere, kati ni Idi Amin..mwisho ni Nyerere mwenyewe na huyo aliyeonekana kichwa ni Edward Moringe Sokoine..Fullstop!
 
Idd Amini alikuwa bondia, Nyerere mwalimu, wote kabla hawajawa marais.
Leo mabondia wanadhulumiwa na mapromota na waalimu waadhulumiwa na serikali.
They have something in common to share
 
Iddi Amin ni moja ya kigezo cha Nyerere kutaka apewe utakatifu. Islam Vs. Vatican.
 
Kama alivyosema Husseni Njovu , hapo pilikua ni Mwanza kwenye mwaka kama 1973. Kulikua na mkutano wa Umoja wa Mulungushi yaani Zambia , Zaire Na Tanzania na marasi wote walikua Mwanza - Idi Amin aliteremka ghafla kiwanja cha Mwanza na litaka kushiriki kwenye mukutano huo lakini walimwambia kwa njia ya kiungwana kuwa haiwezekani. Labda alikaa masaa mawili tu hapo akaondoka kurudu Uganda.
 
Nakumbuka kwamba hapa ilikuwa mjini Mwanza wakati huo Mwalimu alikuwa ziarani mkoani humo, na Idd Amin alikuja bila taarifa tena kwa ndege ya kivita aliyokuwa akiiendesha mwenyewe. Inasemekana kwenye ndege hiyo walikuwa wawili tu yeye na mwanawe kipenzi akiitwa Moses ambaye wakati huo alikuwa mtoto wa miaka kama kumi hivi. Habari hii ilipatikana kwenye redio mbao miaka hiyo na ilikuwa kabla ya vita na Uganda ingawa uhasama ulishapamba moto.
Smahani mkuu Njovu, wasiwasi wangu ni hapo kwenye nyekundu kwa kuwa ninajua Idd Amin alikuwa ni mwislamu mbona alimpa mwanaye jina la Moses, naomba ufafanuzi please.
 
Hivi kila mwanamke katika position ya juu au hadhi fulani barani Afrika ni lazima avae kama Rais wa Liberia??

Au ni ushamba wa karne ya 21?
Mama Slama lazima ajipige tambara begani na joyce naye hivyo hivyo mitindo imeisha?

Rais wa Liberia aliiga wapi?
IVI ULIFIKIRIA NA HAWA KWANZA! . Je ni Maadui au Marafiki..?
attachment.php
 
Back
Top Bottom