Nyerere,kanisa katoliki na muendelezo wa mfumo kristo dhidi ya Uislam Tanzania

Status
Not open for further replies.

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
SEHEMU YA KWANZA:

--Utangulizi
Baada ya kifo cha Julus Kambarage Nyerere tarehe 14 Oktoba 1999 mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu msimamo wake na uadilifu kuhusu Uislam Tanzania.
Nia ya kitabu hiki ni kueleza jinsi Mwalimu Nyerere katika kipindi chake cha uongozi- alivyoshughulikia suala la Uislam na Waislam wa Tanzania.
Hii ni historia ya uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Waislam kwa kipindi cha takriban robo karne toka pale aliposhika madaraka ya nchi mwaka 1961 hadi alipoachia madaraka mwaka 1985.
Ni mategemeo ya mwandishi kuwa kitabu hiki kidogo kitaweka wazi yale ambayo hayafahamiki kwa wengi.
Mohamed Said

Sura ya Kwanza
Uislam Katika Tanzania
Siasa za Uislam, Kanisa, Dola na Mwafrika Mkristo
Uislam umekuwepo Afrika ya Mashariki toka karne ya nane. Hata hivyo wana-historia wameghitilafiana kuhusu ni lini hasa Uislam uliingia. A.A. Ahmed akinukuu mswada ambao haujachapishwa wa Muhammad B. Sharif Al-Baidh, Stages in East African History, anasema kuwa, ‘Uislam uliingia wakati wa Khalifa ‘Abd al Malik bin Marwan, katika mwaka wa 702/80H. Al-Baidh anasema Uislam uliletwa Afrika ya Mashariki na kundi la Waomani, miongoni mwao wakiwemo waungwana wawili Sa’id na Sulaiman. Sa’id inasemekana alikuja Lamu na Sulaiman alikwenda Mombasa’. [1] Lakini wanahistoria wengi wazalendo wanaamini kuwa Uislam ulifika Afrika ya Mashariki wakati wa uhai wa Bwana Mtume (SAW), hata kabla haja hajiri kwenda Madina. Pamoja na Uislam ikazuka lugha ya Kiswahili, lugha ianyozungumzwa Afrika ya Mashariki na ya Kati na utamaduni wa Kiswahili ambao unanasibishwa na Uislam. Nembo ya Muislam katika Afrika ya Mashariki na Kati ni kuikubali lugha ya Kiswahili kama lugha yake ya asili.
Theluthi mbili ya Waislam wote wa Afrika ya Mashariki wanaishi Tanzania [2] ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote katika Afrika ya Mashariki, yaani Kenya, Uganda na Tanzania. Hii ni pamoja na Zanzibar- – nchi ya Kiislam yenye Waislam takriban asilimia tisini na tisa na kuna wakati ilikuwa ndiyo kitovu cha maarifa ya Kiislam katika Afrika ya Mashariki na Kati. Kutokana na sensa ya mwaka 1957, kwa kila Waislam watatu walikuwepo Wakristo wawili. Kwa wakati ule hii ilionyesha kuwa Tanganyika ilikuwa na Waislam wengi katika nchi zote Kusini ya Ikweta. Lakini katika sensa ya kwanza mwaka 1967 baada ya uhuru jumla ya Wakristo Tanzania Bara ilikuwa asilimia thelathini na mbili na Waislam asilimia thelathini na Wapagani asilimia thelathini na saba. Sensa hii inaonyesha kuwa Wapagani ndiyo walio wengi Tanzania. Sensa hii ya mwaka 1967 haikueleza kwa nini katika kipindi cha miaka kumi kwa ghafla Waislam wamepungua nchini au kwa nini ghafla Wapagani wameongozeka katika nchi ya waumini.
Hii ndiyo ilikuwa sensa ya mwisho iliyokuwa ikionyesha mgawanyo wa dini. Inaaminika kuwa matokeo ya sensa hii yalifanyiwa mabadiliko kwa ajili ya sababu za kisiasa pale ilipobainika kuwa Waislam Tanzania walikuwa wengi kupita Wakristo. Upo ushahidi kuwa mwaka 1970, ilipobainika kuwa Waislam ni wengi Tanzania serikali iliiamrisha Idara ya Takwimu kuchoma moto matokeo yote ya sensa ya mwaka 1970.[3]-
Bahati mbaya mgao wa madaraka katika siasa Tanzania umewatupa nje Waislam, ingawa inafahamika kuwa usalama na utulivu wa nchi yeyote unategemea mizani hii kuwa sawa. Vyanzo tofauti vya takwimu vinatoa takwimu tofauti zinazopingana kuhusu hesabu ya Waislam na Wakristo katika Tanzania. Hii inatokana na ukweli kuwa somo hili ni nyeti. Katika nchi za Kiafrika ambazo zina wafuasi wengi wa dini hizi mbili, kwa mfano Tanzania na Nigeria,[4] uchunguzi wa kuwa ni dini gani ina wafuasi wengi kupita mwenzake ni chanzo cha mgongano na mzozo. Tatizo hili lipo Tanzania. D.B. Barret [5] anasema kuwa Waislam Tanzania ni wachache wakilinganishwa na Wakristo. Takwimu zake zinaeleza kuwa Waislam ni 26%, Wakristo 45% na Wapagani ni 28%. Takwimu za Tanzania National Demographic Survey za mwaka wa 1973 zinaonyesha kuwa Waislam ni wengi kidogo kupita Wakristo wakiwa 40%, Wakristo 38.9% na Wapagani 21.1%. Lakini takwimu za Africa South of the Sahara,[6] zinaonyesha Waislam ni wengi Tanzania kwa 60%. Takwimu hizi zimebaki hivyo bila ya mabadiliko toka mwaka 1982. Kwa kuwa utafiti wa Waislam wenyewe katika suala hili ni mdogo sana au haupo kabisa, suala la wingi wa Waislam katika Tanzania halijafanyiwa utafiti na Waislam wenyewe.[7]
Mgao wa madaraka na kugawana vyeo haikupashwa kuwa sababu ya migongano na mifarakano katika Afrika. Lakini kwa bahati mbaya sana hii imekuja kuwa sababu ya mifarakano katika serikali za wananchi wenyewe. Jambo hili limekuwa ni suala nyeti kwa sababu ukabila, udini na kujuana ni kitu muhimu katika serikali za Afrika. Mgawanyo wa madaraka na wingi wa wa wafuasi katika dini au kabila havikuwa vitu vilivyokuwa vikiwashughulisha wananchi wakati wa ukoloni kiasi cha kuleta mifarakano katika jamii. Kwa bahati nzuri ukabila hauna nguvu Tanzania lakini dini imekuwa chanzo cha ubaguzi toka zama za ukoloni, tofauti ni kuwa wakati wa ukoloni waliokuwa wakiwabagua Waislam hawakuwa Wakristo weusi bali Wazungu.
Ukristo ni dini mpya Tanzania kwa kuwa uliingizwa katika karne ya kumi na nane na wamisionari. Kanisa na Mwafrika Mkristo ni matokeo ya ukoloni.- Kwa ajili hii basi historia ya Kanisa katika Afrika ni ile ya kuhirikiana na kuwa tiifu kwa serikali ya kikoloni. Chini ya ukoloni, taratibu Kanisa likaweza kujenga uhusiano maalum kati yake na serikali pamoja na Mkristo Mwafrika ambae imemuelimisha katika shule zake. Mwafrika Mkristo akawa ananufaika na mfumo wa kikoloni. Waislam wakawa wanataabika kwa kuwa dini yao ilikuwa inapingana na dini ya mtawala. Mwafrika Mkristo akawa mnyeyekevu kwa serikali wakati wa ukoloni na baada ya kupatikana kwa uhuru akaja kushika madaraka ya serikali.- Waislam wakatengwa na kuteswa katika ukoloni kwa kubaguliwa na kunyimwa elimu hivyo kuwaondolea fursa ya maendeleo. Kuwepo kwa Waislam kama raia na ili kuinusuru dini yao ilibidi Waislam wasimame kuutokomeza ukoloni. Baada ya uhuru Kanisa likabaki na msimamo wake wa enzi ya ukoloni wa kutii na kujipendekeza kwa serikali mpya iliyokuwa madarakani. Ushirika huu kati ya Kanisa na serikali, uliojengwa na tabia ya Kanisa ya kukubaliana na mfumo wowote wa serikali ulililelewa vyema na umeisaidia sana Kanisa. Kanisa likaweza kujijengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake bila ya kipingamizi wala wasiwasi. Kutokana na uhusiano huu maalum Kanisa likajifanyia msingi imara wenye nguvu- kutokana wa Wakristo waliowasomesha katika shule zao. Kanisa likatumia nafasi na uhusiano huu kwanza na serikali ya kikoloni kisha na serikali ya wananchi kujijengea himaya ambayo wafuasi wake wakaja kushika nafasi zote muhimu katika uongozi wa juu wa serikali, bunge na mahakama katika Tanzania. Katika miaka yake mia moja tu Kanisa likaweza kupata safu yake ya viongozi ambao wanadhibiti kila sekta katika jamii ya Watanzania.
Waingereza walipoja kuitawala Tanganyika (kama Tanzania inavyojulikana) baada ya kuondoka- Wajerumni baada ya Vita Kuu ya Kwanza, Wajerumani walikuwa wameshafanya kazi ya kutosha ya kuiweka Tanganyika ndani ya mamlaka mbalimbali za Kikristo. Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika mamlaka mbalimbali za Kikristo kutoka nchi tofauti za Ulaya. Kanisa Katoliki ambalo ndilo lenye nguvu zaidi, lilikuwa tayari limeshajikita Tanganyika. White Fathers walikuwa wapo Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers walikuwa Morogoro na Kilimanjaro; Benedictine Fathers walikwepo Peramiho na Ndanda; Capuchin Fathers walikuwepo Dar es Salaam; Consolata Fathers walikuwepo Iringa na Meru; Passionist Fathers walikuwa Dodoma; Pallotine Fathers walikuwa Mbulu; Maryknoll Fathers walikuwapo Musoma; na Rosmillian Fathers walikuwa Iringa. [8]
Wamisionari [9]hawa walipotia mguu pwani ya Afrika ya Mashariki, nia yao hasa ilikuwa kuufuta Uislam. Wakazi wa pwani hii iliyokuwa ikijulikana kama Zanj waliuona Ukrsto kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1498 Wareno walipofika sehemu hizo. Mwaka 1567 wamishionari wa Augustinian waliingia Afrika ya Mashariki ili kupambana na Uislam ili Ukristo uwe dini ya dunia nzima. Kadinali Lavigirie alianzisha The White Fathers, taasisi ya Kanisa Katoliki kwa kusudi maalum la kuupiga vita Uislam[10] Wakati huo huo Church Missionary Society (CMS) ilikuwa imjitwisha kazi ya kuondoa ulimwengu kutokana na Uislam, ujinga na giza.[11] Hadi hii leo White Fathers wapo Tanzania wapo Tanzania wakiendelea kufanya kazi iliyowaleta Tanganyika zaidi ya miaka mia iliyopita.
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu. Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.[12] Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu. Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini. Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam. Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu ‘washenzi' badala yake wamewakuta watu walistaaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza. Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na shule zake – madras. Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.
Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi. Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika. Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV- cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884. Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam. [13] Kati ya mwaka 1888-1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo katika Afrika ya Mashariki.[14]- Ombwe lililoachwa na elimu ya Kiislam ikajazwa na elimu ya Kanisa chini ya usimamizi wa Waingereza. Kanisa hivi sasa linaeneza uongo na propaganda kuwa lenyewe ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika. Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.[15] Kwa kipindi cha zaidi ya miaka mia moja Kanisa likaelekeza nguvu zake katika katika kuwatayarisha raia ambao wengi wao walikuwa Wakristo, watakaokuwa watiifu kwa Kanisa na serikali. Ni katika mtandao huu ndiyo Wakristo wanaimiliki serikali na Chama Cha Mapinduzi na kuiamrisha ifanye linavyopenda Kanisa, wakati Waislam na Uislam ukifanywa kama vitu visivyokuwa na maana yoyote.

Hadi kufikia mwaka wa 1960 Kanisa likawa taasisi kubwa inayomiliki mamilioni ya dola ya misaada inayopokelewa kutoka wahisani na wafadhili walioko katika ulimwengu wa Kikristo. Kanisa sasa hivi linahodhi mahospitali, misururu ya ndege binafsi, viwanja vya ndege, makampuni ya uchapaji na mitambo ya kupiga chapa, stesheni za radio na magazeti. Kanisa limekuwa na nguvu na udhibiti wa mambo kiasi kwamba wakati mwingine watendaji, hasa Wakristo katika serikali na ndani ya chama tawala CCM hawajui utii wao upo kwa nani, serikalini au katika Kanisa?- Ni katika kuchanganyikiwa huku kwa watendaji wa serikali kuhusu uhusiano wao na Kanisa na serikali ndiko kulikoamsha kutoaminiana kati ya Waislam na serikali mara tu baada ya uhuru kupatikana. Serikali ikaonekana kama moja ya taasisi za Kanisa na Waislam wakiwa ni watazamaji tu. Mara baada ya uhuru Kanisa likaangalia nafasi yake na serikali mpya iliyokuwa madarakani. Wakati wa kudai uhuru Kanisa lilijiweka mbali na siasa na ikaonekana kuwa Kanisa lilikuwa likiheshima ule mpaka kati ya dini na siasa. Wakati ule mgongano kati ya Kanisa na serikali haukupata kusikika hata kidogo. Baada ya uhuru kupatikana tu na serikali ikawa mikononi mwa wananchi, Kanisa likaanza kusikika likisema kuwa lina haki na wajibu kuwa na ushawishi ndani ya serikali, kuikosoa serikali na kuingooza pale inapoona serikali haifanyi mambo sawa kwa matarajio yake. Katika msimamo huu mpya, Kanisa likajipa fursa ya kuwa msemaji wa watu. Huu ulikuwa ni mwelekeo mpya katika mambo ya siasa na utawala.
Katika Uislam siasa na dini ni kitu kimoja. Vitu hivi viwili havitenganishwi. Lakini mwaka wa 1955 wakati wa siku za mwanzo kabisa za TANU, tuliona jinsi Waislam katika TANU walivyoweza kukiogoza chama katika misingi ya kisekula na utaifa ili kulinda umoja wa wananchi.. Kutochanganya dini na siasa ikawa moja ya maadili makuu ya TANU. Kuanzia hapa ndipo sasa tunaweza kuelewa mapambano kati ya Waislam kwa upande mmoja na serikali na Wakristo kwa upande wa pili yalivyokuja kugubika Tanzania mara baada ya uhuru.

*****ITAENDELEA******
 
YAAAAAAAWWN!
Kama huna jambo la maana la kutuwekea humu nenda kalale!
Acha akili ndogo. Haya mambo ya udini sasa ni boring na yamepitwa na wakati!
Ninachokijua mimi ni waafrika ni ndugu. dini za waarabu na hizi zingine za sijui ni wazungu zilizokuja kwa meli hazipaswi kufuta udugu wetu!
Na kanisa katoriki ndo lipi hilo?
 
ILI:

Uislam: Itikadi ya Kupinga Ukoloni
Uislam siku zote umekuwa kikwazo cha utawala wa kikoloni na kipingamizi kwa mamlaka yoyote ambayo imejaribu kuwakandamiza Waislam. Kwa ajili hii basi, hakuna serikali iliyokuwa madarakani, iwe ya wananchi au ya kikoloni ambayo imepata kuwa na uelewano mwema na Uislam, hivyo basi Waislam wamekuwa daima wakipambana kulinda dini yao na kupigania haki zao.
Ukristo ulipingwa na Waislam tokea mwanzo. Katika kila pambano la silaha dhidi ya ukoloni, Waislam walichukua nafasi hiyo kuwashambulia wamishionari na taasisi zao.[16] Waislam waliwaona wamishionari na wakoloni kama washirika wakishirikiana kupiga vita Uislam na kwa hiyo wote ni maadui. Ukakamavu wa Uislam dhidi ya ukoloni na Ukristo una historia ndefu. Ukristo ukawa kama kibaraka ukijikurubisha na kujinasibisha na ukoloni hata Wakristo kupigana vita pamoja na wakoloni dhidi ya majeshi ya wazalendo. [17] Kuelewa hali ya Uislam wakati ule, unahitaji kusoma barua iliyoandikwa na Chifu Songea bin Ruuf wakati alipokuwa akikusanya nguvu za raia wake dhidi ya majeshi ya Wajerumani na huku akijaribu kupata ushirika wa machifu wengine katika sehemu za kusini ya Tanganyika na ng'ambo ya Mto Ruvuma katika Msumbiji. Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
Sultan Songea bin Ruuf anasema: Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga. Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe. Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini. Tupo katika kupigananao hapa. Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano. Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea. Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu. Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa. Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe. Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na da'wa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Isma'il anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf. [18]
Kitu cha kuangalia katika barua hii, nzuri kama ilivyo, ni kuwa inatiliwa shaka na Becker, ambae msimamo wake ni kuwa chanzo cha barua hiyo ni cha
kutatanisha.
 
Kugombana na kulumbana kila siku kwa sababu ya dini/mila tulizoletewa na waarabu/mayahudi/wazungu ni upu.mbavu wa kiwango cha juu sana!!! Sisi miafrika ni mijinga sana!!! hivi hizi dini za kigeni ndo zinafundisha ubinafsi,kujikweza na chuki kiasi hiki??!!! hizi dini za kigeni zililetwa na haya maguruwe ili tuvurugane tutengane halafu yarudi kututafuna vizuri. Ndo maana kina Kiranga huwa wanasema hizi dini zinasababisha ulemavu wa akili wa kiwango cha juu sana!!! Sijawahi kusikia wanaoabudu dini za asili wakilalama wao kuonewa au dini nyingine kupendelewa!!! Ila hizi dini za wakoloni hizi ni tatizo!! malalamiko na kelele haziishi!!! Yaani miafrika ndo tumekuwa "wafia dini" hizi za kikoloni; tuko tayari kuizika historia yetu na undugu wetu kwa ajili ya kupigania dini hizi!!! Tuko tayari kuitana majina ya kibaguzi ya kila aina,kudhibitisha uumini n ufuasi wetu kwa dini hizi. SHAME, SHAME!!!!!!!!!
Yaani mmeigeuza Tanzania kuwa ya wakristu na waislamu tuu??!! kila tukiamka 'waislam hivi, wakristu vile'!!??
Aliyojisemea James Watson kuwa inawezekana kuwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuwa mjinga na kuwa na ngozi nyeusi.
Haya bwana, "wenye dini" endeleeni kulumbana; wacha sie "wapagani" tupite kushoto.
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA TATU:

Mkutano wa Kwanza wa Waislam, 1962
Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Waislam waliamini kuwa hali yao ya baadae katika serikali huru itakuwa nzuri. Mwaka 1962 ukaitishwa mkutano wa Waislam wa nchi nzima kujadili nafasi ya Uislam katika Tanganyika huru. Taasisi zifuatazo zilihudhuria mkutano huo: East African Muslim Welfare Society (EAMWS), Daawat Islamiyya, Jamiatul Islamiya fi Tanganyika, Jamiatul Islamuyya ‘A'[19] na Muslim Education Union. Mkutano ule ulikubaliana pamoja na mambo mengine umuhimu wa kuanzisha idara ya elimu chini ya EAMWS. Waislam hawakusubiri serikali itimize ahadi yake ya kurekebisha upogo uliokuwepo wa elimu kati ya Waislam na Waislam. Waislam walianzisha mipango yao wenyewe ili isaidiane na juhudi ya serikali. Mipango ikatayarishwa ya kujenga shule Tanganyika nzima na mwishowe kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya Mashariki. Mkutano ukamchagua Tewa Said Tewa waziri wa serikali, mwanasiasa wa TAA na mmoja wa wale wazalendo kumi na saba walioanzisha TANU kuwa mwenyekiti wa EAMWS kwa upande wa Tanganyika.
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa uadui kati ya Waislam na serikali ambayo ilikuwa mikononi mwa Wakristo. Uelewano uliodumu wakati wa kudai uhuru ukaanza kutoweka na siasa zikachukua sura mpya ya uhasama, kutoaminiana na kutafutana kati ya jamii hizi mbili. Kisa cha hali hii mpya ikiwa ni sababu ya Waislam kutaka kuondoa hali ya kikoloni iliyowakandamiza kwa miaka mingi. Waislam waliona kuwa hili lilikuwa ni jambo lisilokuwa na pingamizi kufanyika. Uhuru ili uwe na maana ni lazima Waislam wajitoe ndani ya unyonge waliogubikwa na wakoloni. Kwa upande wa Wakristo hali hii ilisababisha hofu kuu nyoyoni mwao.

*****ITAENDELEA*****
 
Jinga lingine hili. Nenda kapigwe rusherere uarabuni. Pambaf. Unafikiria udini karne ya digitali! Looh!
 
Huyu Mungu wa WAISLAM NI YUPI? Kwanini yeye siku zote anatetewa!!!!. Au hajitambui? Mungu wa wakristo anatetea watu wake kwa jambo lolote lililo jema. Mtalalamika mpaka YESU arudi kwa mara ya pili...
Mtaangamia kwa kukosa maarifa.
 
SEHEMU YA KWANZA:

--Utangulizi
Baada ya kifo cha Julus Kambarage Nyerere tarehe 14 Oktoba 1999 mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu msimamo wake na uadilifu kuhusu Uislam Tanzania.
Nia ya kitabu hiki ni kueleza jinsi Mwalimu Nyerere katika kipindi chake cha uongozi- alivyoshughulikia suala la Uislam na Waislam wa Tanzania.
Hii ni historia ya uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Waislam kwa kipindi cha takriban robo karne toka pale aliposhika madaraka ya nchi mwaka 1961 hadi alipoachia madaraka mwaka 1985.
Ni mategemeo ya mwandishi kuwa kitabu hiki kidogo kitaweka wazi yale ambayo hayafahamiki kwa wengi.
Mohamed Said

Sura ya Kwanza
Uislam Katika Tanzania
Siasa za Uislam, Kanisa, Dola na Mwafrika Mkristo
Uislam umekuwepo Afrika ya Mashariki toka karne ya nane. Hata hivyo wana-historia wameghitilafiana kuhusu ni lini hasa Uislam uliingia. A.A. Ahmed akinukuu mswada ambao haujachapishwa wa Muhammad B. Sharif Al-Baidh, Stages in East African History, anasema kuwa, ‘Uislam uliingia wakati wa Khalifa ‘Abd al Malik bin Marwan, katika mwaka wa 702/80H. Al-Baidh anasema Uislam uliletwa Afrika ya Mashariki na kundi la Waomani, miongoni mwao wakiwemo waungwana wawili Sa’id na Sulaiman. Sa’id inasemekana alikuja Lamu na Sulaiman alikwenda Mombasa’. [1] Lakini wanahistoria wengi wazalendo wanaamini kuwa Uislam ulifika Afrika ya Mashariki wakati wa uhai wa Bwana Mtume (SAW), hata kabla haja hajiri kwenda Madina. Pamoja na Uislam ikazuka lugha ya Kiswahili, lugha ianyozungumzwa Afrika ya Mashariki na ya Kati na utamaduni wa Kiswahili ambao unanasibishwa na Uislam. Nembo ya Muislam katika Afrika ya Mashariki na Kati ni kuikubali lugha ya Kiswahili kama lugha yake ya asili.
Theluthi mbili ya Waislam wote wa Afrika ya Mashariki wanaishi Tanzania [2] ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote katika Afrika ya Mashariki, yaani Kenya, Uganda na Tanzania. Hii ni pamoja na Zanzibar- – nchi ya Kiislam yenye Waislam takriban asilimia tisini na tisa na kuna wakati ilikuwa ndiyo kitovu cha maarifa ya Kiislam katika Afrika ya Mashariki na Kati. Kutokana na sensa ya mwaka 1957, kwa kila Waislam watatu walikuwepo Wakristo wawili. Kwa wakati ule hii ilionyesha kuwa Tanganyika ilikuwa na Waislam wengi katika nchi zote Kusini ya Ikweta. Lakini katika sensa ya kwanza mwaka 1967 baada ya uhuru jumla ya Wakristo Tanzania Bara ilikuwa asilimia thelathini na mbili na Waislam asilimia thelathini na Wapagani asilimia thelathini na saba. Sensa hii inaonyesha kuwa Wapagani ndiyo walio wengi Tanzania. Sensa hii ya mwaka 1967 haikueleza kwa nini katika kipindi cha miaka kumi kwa ghafla Waislam wamepungua nchini au kwa nini ghafla Wapagani wameongozeka katika nchi ya waumini.
Hii ndiyo ilikuwa sensa ya mwisho iliyokuwa ikionyesha mgawanyo wa dini. Inaaminika kuwa matokeo ya sensa hii yalifanyiwa mabadiliko kwa ajili ya sababu za kisiasa pale ilipobainika kuwa Waislam Tanzania walikuwa wengi kupita Wakristo. Upo ushahidi kuwa mwaka 1970, ilipobainika kuwa Waislam ni wengi Tanzania serikali iliiamrisha Idara ya Takwimu kuchoma moto matokeo yote ya sensa ya mwaka 1970.[3]-
Bahati mbaya mgao wa madaraka katika siasa Tanzania umewatupa nje Waislam, ingawa inafahamika kuwa usalama na utulivu wa nchi yeyote unategemea mizani hii kuwa sawa. Vyanzo tofauti vya takwimu vinatoa takwimu tofauti zinazopingana kuhusu hesabu ya Waislam na Wakristo katika Tanzania. Hii inatokana na ukweli kuwa somo hili ni nyeti. Katika nchi za Kiafrika ambazo zina wafuasi wengi wa dini hizi mbili, kwa mfano Tanzania na Nigeria,[4] uchunguzi wa kuwa ni dini gani ina wafuasi wengi kupita mwenzake ni chanzo cha mgongano na mzozo. Tatizo hili lipo Tanzania. D.B. Barret [5] anasema kuwa Waislam Tanzania ni wachache wakilinganishwa na Wakristo. Takwimu zake zinaeleza kuwa Waislam ni 26%, Wakristo 45% na Wapagani ni 28%. Takwimu za Tanzania National Demographic Survey za mwaka wa 1973 zinaonyesha kuwa Waislam ni wengi kidogo kupita Wakristo wakiwa 40%, Wakristo 38.9% na Wapagani 21.1%. Lakini takwimu za Africa South of the Sahara,[6] zinaonyesha Waislam ni wengi Tanzania kwa 60%. Takwimu hizi zimebaki hivyo bila ya mabadiliko toka mwaka 1982. Kwa kuwa utafiti wa Waislam wenyewe katika suala hili ni mdogo sana au haupo kabisa, suala la wingi wa Waislam katika Tanzania halijafanyiwa utafiti na Waislam wenyewe.[7]
Mgao wa madaraka na kugawana vyeo haikupashwa kuwa sababu ya migongano na mifarakano katika Afrika. Lakini kwa bahati mbaya sana hii imekuja kuwa sababu ya mifarakano katika serikali za wananchi wenyewe. Jambo hili limekuwa ni suala nyeti kwa sababu ukabila, udini na kujuana ni kitu muhimu katika serikali za Afrika. Mgawanyo wa madaraka na wingi wa wa wafuasi katika dini au kabila havikuwa vitu vilivyokuwa vikiwashughulisha wananchi wakati wa ukoloni kiasi cha kuleta mifarakano katika jamii. Kwa bahati nzuri ukabila hauna nguvu Tanzania lakini dini imekuwa chanzo cha ubaguzi toka zama za ukoloni, tofauti ni kuwa wakati wa ukoloni waliokuwa wakiwabagua Waislam hawakuwa Wakristo weusi bali Wazungu.
Ukristo ni dini mpya Tanzania kwa kuwa uliingizwa katika karne ya kumi na nane na wamisionari. Kanisa na Mwafrika Mkristo ni matokeo ya ukoloni.- Kwa ajili hii basi historia ya Kanisa katika Afrika ni ile ya kuhirikiana na kuwa tiifu kwa serikali ya kikoloni. Chini ya ukoloni, taratibu Kanisa likaweza kujenga uhusiano maalum kati yake na serikali pamoja na Mkristo Mwafrika ambae imemuelimisha katika shule zake. Mwafrika Mkristo akawa ananufaika na mfumo wa kikoloni. Waislam wakawa wanataabika kwa kuwa dini yao ilikuwa inapingana na dini ya mtawala. Mwafrika Mkristo akawa mnyeyekevu kwa serikali wakati wa ukoloni na baada ya kupatikana kwa uhuru akaja kushika madaraka ya serikali.- Waislam wakatengwa na kuteswa katika ukoloni kwa kubaguliwa na kunyimwa elimu hivyo kuwaondolea fursa ya maendeleo. Kuwepo kwa Waislam kama raia na ili kuinusuru dini yao ilibidi Waislam wasimame kuutokomeza ukoloni. Baada ya uhuru Kanisa likabaki na msimamo wake wa enzi ya ukoloni wa kutii na kujipendekeza kwa serikali mpya iliyokuwa madarakani. Ushirika huu kati ya Kanisa na serikali, uliojengwa na tabia ya Kanisa ya kukubaliana na mfumo wowote wa serikali ulililelewa vyema na umeisaidia sana Kanisa. Kanisa likaweza kujijengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake bila ya kipingamizi wala wasiwasi. Kutokana na uhusiano huu maalum Kanisa likajifanyia msingi imara wenye nguvu- kutokana wa Wakristo waliowasomesha katika shule zao. Kanisa likatumia nafasi na uhusiano huu kwanza na serikali ya kikoloni kisha na serikali ya wananchi kujijengea himaya ambayo wafuasi wake wakaja kushika nafasi zote muhimu katika uongozi wa juu wa serikali, bunge na mahakama katika Tanzania. Katika miaka yake mia moja tu Kanisa likaweza kupata safu yake ya viongozi ambao wanadhibiti kila sekta katika jamii ya Watanzania.
Waingereza walipoja kuitawala Tanganyika (kama Tanzania inavyojulikana) baada ya kuondoka- Wajerumni baada ya Vita Kuu ya Kwanza, Wajerumani walikuwa wameshafanya kazi ya kutosha ya kuiweka Tanganyika ndani ya mamlaka mbalimbali za Kikristo. Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika mamlaka mbalimbali za Kikristo kutoka nchi tofauti za Ulaya. Kanisa Katoliki ambalo ndilo lenye nguvu zaidi, lilikuwa tayari limeshajikita Tanganyika. White Fathers walikuwa wapo Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers walikuwa Morogoro na Kilimanjaro; Benedictine Fathers walikwepo Peramiho na Ndanda; Capuchin Fathers walikuwepo Dar es Salaam; Consolata Fathers walikuwepo Iringa na Meru; Passionist Fathers walikuwa Dodoma; Pallotine Fathers walikuwa Mbulu; Maryknoll Fathers walikuwapo Musoma; na Rosmillian Fathers walikuwa Iringa. [8]
Wamisionari [9]hawa walipotia mguu pwani ya Afrika ya Mashariki, nia yao hasa ilikuwa kuufuta Uislam. Wakazi wa pwani hii iliyokuwa ikijulikana kama Zanj waliuona Ukrsto kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 1498 Wareno walipofika sehemu hizo. Mwaka 1567 wamishionari wa Augustinian waliingia Afrika ya Mashariki ili kupambana na Uislam ili Ukristo uwe dini ya dunia nzima. Kadinali Lavigirie alianzisha The White Fathers, taasisi ya Kanisa Katoliki kwa kusudi maalum la kuupiga vita Uislam[10] Wakati huo huo Church Missionary Society (CMS) ilikuwa imjitwisha kazi ya kuondoa ulimwengu kutokana na Uislam, ujinga na giza.[11] Hadi hii leo White Fathers wapo Tanzania wapo Tanzania wakiendelea kufanya kazi iliyowaleta Tanganyika zaidi ya miaka mia iliyopita.
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu. Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.[12] Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu. Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini. Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam. Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu ‘washenzi' badala yake wamewakuta watu walistaaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza. Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na shule zake – madras. Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.
Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi. Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika. Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV- cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884. Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam. [13] Kati ya mwaka 1888-1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo katika Afrika ya Mashariki.[14]- Ombwe lililoachwa na elimu ya Kiislam ikajazwa na elimu ya Kanisa chini ya usimamizi wa Waingereza. Kanisa hivi sasa linaeneza uongo na propaganda kuwa lenyewe ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika. Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.[15] Kwa kipindi cha zaidi ya miaka mia moja Kanisa likaelekeza nguvu zake katika katika kuwatayarisha raia ambao wengi wao walikuwa Wakristo, watakaokuwa watiifu kwa Kanisa na serikali. Ni katika mtandao huu ndiyo Wakristo wanaimiliki serikali na Chama Cha Mapinduzi na kuiamrisha ifanye linavyopenda Kanisa, wakati Waislam na Uislam ukifanywa kama vitu visivyokuwa na maana yoyote.

Hadi kufikia mwaka wa 1960 Kanisa likawa taasisi kubwa inayomiliki mamilioni ya dola ya misaada inayopokelewa kutoka wahisani na wafadhili walioko katika ulimwengu wa Kikristo. Kanisa sasa hivi linahodhi mahospitali, misururu ya ndege binafsi, viwanja vya ndege, makampuni ya uchapaji na mitambo ya kupiga chapa, stesheni za radio na magazeti. Kanisa limekuwa na nguvu na udhibiti wa mambo kiasi kwamba wakati mwingine watendaji, hasa Wakristo katika serikali na ndani ya chama tawala CCM hawajui utii wao upo kwa nani, serikalini au katika Kanisa?- Ni katika kuchanganyikiwa huku kwa watendaji wa serikali kuhusu uhusiano wao na Kanisa na serikali ndiko kulikoamsha kutoaminiana kati ya Waislam na serikali mara tu baada ya uhuru kupatikana. Serikali ikaonekana kama moja ya taasisi za Kanisa na Waislam wakiwa ni watazamaji tu. Mara baada ya uhuru Kanisa likaangalia nafasi yake na serikali mpya iliyokuwa madarakani. Wakati wa kudai uhuru Kanisa lilijiweka mbali na siasa na ikaonekana kuwa Kanisa lilikuwa likiheshima ule mpaka kati ya dini na siasa. Wakati ule mgongano kati ya Kanisa na serikali haukupata kusikika hata kidogo. Baada ya uhuru kupatikana tu na serikali ikawa mikononi mwa wananchi, Kanisa likaanza kusikika likisema kuwa lina haki na wajibu kuwa na ushawishi ndani ya serikali, kuikosoa serikali na kuingooza pale inapoona serikali haifanyi mambo sawa kwa matarajio yake. Katika msimamo huu mpya, Kanisa likajipa fursa ya kuwa msemaji wa watu. Huu ulikuwa ni mwelekeo mpya katika mambo ya siasa na utawala.
Katika Uislam siasa na dini ni kitu kimoja. Vitu hivi viwili havitenganishwi. Lakini mwaka wa 1955 wakati wa siku za mwanzo kabisa za TANU, tuliona jinsi Waislam katika TANU walivyoweza kukiogoza chama katika misingi ya kisekula na utaifa ili kulinda umoja wa wananchi.. Kutochanganya dini na siasa ikawa moja ya maadili makuu ya TANU. Kuanzia hapa ndipo sasa tunaweza kuelewa mapambano kati ya Waislam kwa upande mmoja na serikali na Wakristo kwa upande wa pili yalivyokuja kugubika Tanzania mara baada ya uhuru.

*****ITAENDELEA******

Ni nchi gan watu wake wamesomea madrassa halafu wavumbua kitu
 
Kosa alilofanya Nyerere ni kutaifisha shule za seminari za kikristo na kuzifanya za serikali ili watu wote wasome bila ubaguzi.
Kwa hatua hiyo, alifanikiwa kuwaamsha waliolala na matunda yake tunayaona leo. Wanaopenda kumkashifu hawapendi kulizungumzia hili
Pia wanasahau ule mpango wa kupeleka wanafunzi sekondari kwa kota kila mkoa bila kujali ufaulu ulisaidia mikoa iliyokuwa nyuma kielimu japo baadae ulifutwa
 
Allah wa waislamu ni kiwete,goigoi na anategemea binadamu amtetea au amkomboe.Lakini Mungu wa Ibrahim,Isaka na Israeli ni Mungu mwenye nguvu hategemei binadamu wala hahitaji kutetewa kwa kujitoa mhanga,kuvaa mabomu wa kuua wasiowakristu
 
Yale yale yanayozidi kuturudisha nyuma watanzania,matusi ya nini ndugu yangu wewe jibu hoja zake kwa ustaarabu huyo Allah hafanyiwi mzaha wala kejeli nyie fanyeni discussions zenu kwa lugha safi na kuheshimiana bila ya kutumia lugha chafu. Watz lini tutajifunza ustaarabu na kuvumiliana?.M/Mpamba.
 
nasikitika title yako imemtaja nyerere lakn habar yenyewe inahusu wakoloni hasa wazungu kwa wingi (chuki na propaganda za kijiweni).

umeongelea ubaya wa wakoloni wazungu tu wakt hata waarabu walikuwa na ubaya wao (biasness). umeongelea maendeleo waliyoleta waarabu kwenye elimu ambayo sisi hatukuyaona hata kuyackia. naomba unikumbushe shule hadi chuo kilichojengwa na waarabu tz. hospital nk.

nakumbuka mkapa aliwapa majengo ya chuo cha tanesco kuwa chuo chenu. waarabu wana pesa sana lakn cjawah kuckia wanaendesha harambee kujenga chuo kikuu tz. au hospital kubwa tz. waarabu yao biashara tangu ukoloni.

mm nimekulia sehemu ambayo hakuna waislamu kabisaa, tulikuwa tunaskia wwaislam ni watu wanaokaa mijini na wanavaa kanzu kama mapadre. hadi nilipoenda mijini nikawaona. hoja yenu kuwa mko wengi kwa nn msihamasishane muhesabiane huko misikitini mlinganishe na idadi ya watz mpate %? mmkiona inakuwa ndogo mhamasishane watu waowane kwa wingi kuraise popln.

kila mwanaume ana uwezo wa kuwa na watoto 20 kwa wake wanne @5 (hii iliwah kufanikiwa kati ya lebanon au jordan) haya mambo ya kukaa unatuletea historia yanakusaidia nn? pambana upate maisha mazuri kwako na ndg zako acha kuleta mambo ya kizushi hapa. hao waarabu wako unaowatetea wamejenga reli? barabara? bandari? shule zipi? zaidi ya kufunga babu zetu waha ha wanyamwez minyororo, kuwahasi na kuwauza arabuni. a

lafu unaweza kukuta ww unatoka hayo maeneo still unawatukuza waarabu. I hate white people, i hate Arabs the most!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom