Nyerere! Huyu mzee kiboko!

Yule mzee alikuwa kichwa basi tuu alizaliwa kipindi amabacho alizungukwa na misaidizi mijinga na mpuuzi! lakini laiti toka alipoondoka tungeedelea natrend ile ile tukaacha ya le mabaya yake tu, tungefika mbali.....
Siyo hawa wanoulizwa umeifanyia nini Tanzania wanasema "nimeitoa hapa nikaipeleka pale". fuulstop kamaliza kuongea ..
 

Kiranga wala sikatai hayo ktk story ila pia lazima tuwe makini na hizi taarifa, i am not condoning his actions from the story, ila nakubaliana na wewe kuwa ile inaweza ikaleta mtafaruko mkubwa sana sababu amefanya makosa ya kumuanika whistle-blower! i have to admit it was wrong BUT je hivi vitu vilitokeaga!? au ni zile bed time stories tulizozoea!
 
Hivi mnayajuwa ya Nyerere au mnasikiliza porojo zake za kwenye vibaraza vya kuchezea bao?

Hana jema aliloifanyia hii nchi. Lipi moja?

Hajaacha misingi imara ya kuendesha hii nchi kama aliacha ni ipi?

Hata katiba alizokuwa akiandika Ikulu na mawakili wake wabovu leo kila mTanzania hazitaki.

Hebu mmoja tu, anambie kitu kimoja kizuri alichofanya Nyerere zaidi ya kuongea sana na wanafiki kucheka hata pasipo chekesha.

Angekuwa na mawazo na fikra nzuri japo chembe, leo Tanzania na utajiri ilionao ingekuwa kwenye neema ya ajabu.

Tunapomsifia nyerere, tunafanya hivyo kwa kumlinganisha na marais wengine tuliowahi kuwa nao na hata marais wengine wa afrika. Kwa kufanya hvyo utaona mengi mazuri aliyoyafanya, lakini pia utaona kwamba kulikuwa na mapungufu ktk utendaji wake, kama tulivyo binadamu wote. Tatizo wengine tumeaminishwa toka tukiwa wadogo kwamba adui yetu ni nyerere na hatupo tayari kuutafuta ukweli sisi wenyewe bila kuwa influenced na watu wengine, pamoja na elimu nzuri tuliyo nayo.

Huwezi kuwa na mafanikio kama hutambui na kuheshimu mafanikio ya watu wengine. Mpeni sifa zake mzee huyo, anastahili. Jilinganishe uwezo wako wewe na ule aliokuwa nao yeye alipokuwa umri wako! Mlinganishe nyerere na babu yako, halafu jiulize wewe na babu yako mmelifanyia nini taifa hili.
 
Tunapomsifia nyerere, tunafanya hivyo kwa kumlinganisha na marais wengine tuliowahi kuwa nao na hata marais wengine wa afrika. Kwa kufanya hvyo utaona mengi mazuri aliyoyafanya, lakini pia utaona kwamba kulikuwa na mapungufu ktk utendaji wake, kama tulivyo binadamu wote. Tatizo wengine tumeaminishwa toka tukiwa wadogo kwamba adui yetu ni nyerere na hatupo tayari kuutafuta ukweli sisi wenyewe bila kuwa influenced na watu wengine, pamoja na elimu nzuri tuliyo nayo.

Huwezi kuwa na mafanikio kama hutambui na kuheshimu mafanikio ya watu wengine. Mpeni sifa zake mzee huyo, anastahili. Jilinganishe uwezo wako wewe na ule aliokuwa nao yeye alipokuwa umri wako! Mlinganishe nyerere na babu yako, halafu jiulize wewe na babu yako mmelifanyia nini taifa hili.

Nyerere alikuwa philospher na mpenda watu! hakuwa kiongozi!
 
Kusema kweli hata mimi sioni kitu hapa kwangu. Nifanyeje ili nione (Unaweza hata kuni-PM kuhusu cha kufanya)
Natanguliza shukrani.

Wakuu kwani huwaga mna uwezo wa kuona clips a youtube ktk systems zenu? kama jibu ni yes then sielewi vije mshindwe kuona hii! maana ni work of you tube ngoja nitafute link nikuwekee,, hiyo hapi chini

www.youtube.com/watch?v=6cAxan2Vp18&feature=player_embedded#at=11
 
Ahsante sana LTC, ni wazi kabisa hatuna serikali, iliyopo inatumwa na kutumikia wenye mali! RIP baba wa Taifa letu!
 
Ahsante sana LTC, ni wazi kabisa hatuna serikali, iliyopo inatumwa na kutumikia wenye mali! RIP baba wa Taifa letu!

Mwasi tuna matatizo makubwa sana! HATUNA UCHUNGU NA NCHI NA MALI ZA NCHI YETU! Isome signature yangu quoted from GB Shaw! it make senses na ndio yanayotokea leo TZ!
 
Majimshindo uko sahihi, na mimi nakubaliana na wewe. Wewe si mnafiki kama wengine kwasababu unasema unayoyafahamu na kuyaamini. Lakini, si lazima yawe ukweli wote (absolute truth). Haiwezekani kuwafanya watu wote kumtazama Nyerere kama kiongozi mzuri sana au mbaya sana.

Hata kwenye dini ni hivyo. Kuna watu wanasema Yesu ni Mwana wa Mungu, wengine wanasema ni Nabii tu. Wengine wanasema Mtume Mohamme (s.a.w) ni Nabii wa Mwisho wa Mungu, na wengine wanasema ni Nabii wa Uongo... mlolongo ni mrefu. Je ni nani yuko sahihi zaidi?

Kuna mambo mengi magumu, yatamngoja Mwenyezi Mungu kuja kuyatolea hukumu ya haki. Hapo hakutakuwa na ubishi. Sasa hivi tutaumiza vichwa bure tu.

Mimi kama mimi, namtazama Nyerere, kama kiongozi mmoja mwenye hekima ambazo hazimithiliki, na hafanani na viongozi wengi wa duniani na hususani wa-Tz. Siwezi kumlinganisha Mzee AH Mwinyi, Mzee BW Mkapa ama Mzee JM Kikwete na Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere.


Angalia yafuatayo
  1. Aliachia madaraka ya rais wakati watu na katiba vinaruhusu kuendelea kutawala
  2. Alirudi kijijini kwao kulima kwa jembe la mkono na kukokotwa na ng'ombe. Hakuna duniani kiongozi wa namna hiyo labda Uchina ya zamani
  3. Alijitoa kuelimisha watu wake bure ili wapate kujitambua na kujilinda dhidi ya mafisadi na mabeberu kutoka ndani na nje
  4. Aliwapa watu wake huduma ya afya bure, ili waweze kuwa na afya waijenge nchi yao
  5. Aliwakusanya watu wake ktk vijiji ili apate kuwahudumia kwa urahisi zaidi
  6. Alitaifisha shule za mission ili wanchi wake wa dini zingine kama waislam (ambao si dini yake) nao wapate kusoma, kuelimika ili wapate toa mchango wa kuijenga nchi yao
  7. Alilazimisha chama chake kuanzisha vyama vingi ili kusaidia nchi iende na wakati na pia kuweka mfumo wa checks and balance (ambao sasa unafanya kazi kama alivyotegemea)
  8. Alijitolea kusaidia mataifa jirani yaliyokuwa hayapata uhuru yaweze kujikomboa.
  9. Alizuia maliasili zetu ziendelee kubaki salama hadi hapo tutakapopata utambuzi wa kutosha kuzisimamia ili ziweze kunufaisha uchumi na maisha yetu. Hapo alikataa kuwa kama Mobutu Seseko aliyejilimbikizia mali na wananchi wake wakawa masikini
  10. Alikataa kuwa na mahusiano na Israel waliokuwa wakwaonea wananchi Wapalestina
  11. Alipingana hata na Wajerumani, Waingereza waziwazi pale walipokuwa na misimamo ya ubaguzi au uonevu kwa binadamu wengine.
  12. Alikuwa hana unafiki, na alikuwa yupo tayari kukemea hata taifa kubwa la America lilipochukua msimamo wa kukandamiza mataifa madogo na masikini kwa sababu za kimabavu tu.
  13. .... orodha ni ndefu sana
Nyerere, alikuwa binadamu, anayo makosa. Lakini alikuwa akisema tujisahihishe...Alipoondoka madarakani alisema tuyaache mabaya yake lakini mazuri tusiyatupe. Hata alikubali tuache Ujamaa lakini tubaki na Kujitegemea.. Bahati mbaya viongozi wetu wameshindwa kujifunza kutoka kwake. Wanataka kuwasikiliza mafisadi zaidi ya wananchi wao masikini. Hiyo ndio shida iliyopo
Asante sana kwa maelezo haya, hakuna binadamu mkamilifu, sote tuna mapungufu. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
 
Kuna wakati nilipokuwa nikisoma chuo kikuu hapo Dar es slalaam, nilianza kupinga sana siasa zake za Ujamaa na Kujitegemea. Sio kusema zilikuwa si sahihi, bali niliona zilianza kuleta matabaka kati ya wtawala (CCM) na raia, jambo ambalo limedumu mpaka leo. Vile vile niliona kuwa itikadi yake ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa na mapungufu mengi na isingeweza kufanikiwa kama vile ilivyokuwa katika jamii yetu. Nilikuwa nimejazwa kichwani mwangu fikra za Marx na Lenin na ukommunisti. Hata hivyo namheshimu sana kwa misingi ambayo alitujengea na kutuwezesha wengine kusma hadi chuo kikuu na kupata shahada zaidi ya moja, kitu ambacho sikuhizi ingekuwa shida.

Think of how a selfish gene of a human being can do! Wale wale ambao leo hii bila huyu mzee wasingeweza kufika hapo walipo wanataka kuangamiza mfumo ambao unaruhusu fursa sawa kwa wote na kila mwenye utashi na uwezo aweze kulitumikia taifa lake ili wao na vizazi vyao wabakie watawala milele kwa kujenga mifumo yenye kusababisha matabaka ambayo yatawaondoa hao wengine technically. Angalia mifumo ya elimu meaning wanaopata elimu bora ndo watapata nafasi bora, angalia huduma ya afya meaning wenye access living expectancy itaongezeka; nasi za uwongozi kuwa na kiingilio, kama fedha za kuchukua form etc meaning wenye ajira bora na wazazi wenye uwezo ndo wataweza kuongoza. Mmmh hawa hawa ambao bila huyu mzee leo hata watoto wao kupangusa kamasi wangejifunzia kwenye television ya tajiri kijijini....So pity!
 
naomba katika familia/kizazi cha mwalimu jk nyerere apatikane anayemfanana kwa upendo, uzalendo, akili na busara. Itakuwa ni hazina kubwa kwa taifa!!!

wapo tena wapo vizuri tu....ila hawapewi nafasi kutokana na mfumo tuliona
 
Asante sana kwa maelezo haya, hakuna binadamu mkamilifu, sote tuna mapungufu. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!


This statement is password towards compromising good leadership! we dont need leaders then!
 
wapo tena wapo vizuri tu....ila hawapewi nafasi kutokana na mfumo tuliona
Sio rahisi ku break through kama mfumo wenyewe ni kama huu! no matter how talented or educated you are! Mafisadi rules na ni kweli lazima kuna walio na talent kama hii au hata kumzidi mwalimu to be honest! lakini mmhh!
 
Mahesabu na LTC Cometh the hour cometh the man/woman. Msitumie sababu ya current situation kua ni hindarance ya kutoa mtu/watu wenye uwezo,its pathetic reasoning. Sijui hata nianze vp kuwaonyesha fallacy ya reasoning yenu maana it is precisely these situations that are convinient for the 'great' to push through.
 
Mahesabu na LTC Cometh the hour cometh the man/woman. Msitumie sababu ya current situation kua ni hindarance ya kutoa mtu/watu wenye uwezo,its pathetic reasoning. Sijui hata nianze vp kuwaonyesha fallacy ya reasoning yenu maana it is precisely these situations that are convinient for the 'great' to push through.

Mkuu can you break it down to make it easier! maana bado sijaelewa this post! i do apologize!
 
Ila friends nafikiri kuna umuhim wa sisi waAfrika/waTz kuachana na hii mentality ya kukaa kusubiri na kuomba mkombozi atokee. This waiting for a messiah mentality itatuumiza,kwanini mpaka tusubiri atokee mtu halafu ndio eti atuletee ukombozi? Kwani hatuwezi kurise behind a principle instead of a person. Wote tumechoshwa na maisha haya duni na yasio na furaha,sababu zinazochangia hali hii twazijua e.g. ufisadi kwanini basi tunaweka hopes kubwa kua ni mpaka Dr Slaa, Lipumba or who ever aje kuleta mabadiliko badala ya kufanya hii ni movement ya sisi tuliochoka regardles of gender,TRIBE or RELIGION!
 
Back
Top Bottom