Nyerere hakuwahi kupata tunzo ya Nobel

Nazani kunaufitina manake Mwalimu alipigania uhuru wa kila nchi iliyokuwa inatawaliwa Afrika hii alivyoweza. but he has never been given credit for it. I only here Mandela being praise as the best out of african leaders and he was in jail for 27 years na kipindi chote hicho mwalimu alikuwa anapigania uhuru wa Africa he even help South Africa na huyu Mnafiki Mandela hata amtajagi. to me is an impostor.

Any way the winners write the history and give medals to their puppet no wonder Mwalimu does not have any. Mwalimu was no puppet to any one, that's how is gonna go down in history. Dont ever be naive and think Africa leo tunauhuru. We are very far from being free. kuna nguvu ziko kazini, they are well prepared,well infomed, well finance and their goal is nothing but controling us.

ukizani viongozi wetu ndo wanatuongoza fikiria tena. Viongozi wetu wanapewa mkopo $30 million kwa mafano: alafu hizo hela hawapewi leo. wanapewa kwa kipindi lablda miaka 10. hiyo milioni kumi dollars inakuja kwa mfumo wa magari ya laxuri watakayo agiza hao ambao wametoa hizo ela, alafu wataleta watu wao, wanawaita "speshalist" wana ujuzi sawa au zaidi kidogo na jamaa kutoka VETA. alafu hawa jamaa "speshelisti" watalipwa $100,000 kwa mwaka na hiyo ela yetu ya mkopo dola milioni 30. alafu jamaa kutoka bongo hata dola 100 kwa mwezi haambulii kwa project hiyo akiajiriwa. Alafu sijakuambia milioni 30 leo siyo sawa na ukipewa kidogo kidogo in miaka kumi. Manake hela inashuka thamani. Lakini ukinipa milioni 30 leo nikiweka benki ninaweza nikapata faida miaka kumi inaweza kuzaa hata nusu yake.

Then it get craise, we have to pay the loan with interest kiasi ni milioni 30. hata iweje hapa sisi tumeliwa hatuendelei, wewe ukipewa mkopo benki leo si wanakupa kiasi chako chote na unaenda kujipanga mbona hapa masharti ni different kwanini? all this is a set up for us. hela zenyewe zitakuwa zimetumika kuwalipa wadosi wao, kununua magari ya kuwatembeza halafu kidogo kiasi kilichobaki tutapigania ku run our expenses. before we know kamradi hata hakijafika nusu alafu sisi ndio watatulaumu na kusema tunatumia expensive cars kumbe sisi tulikuwa ma dreva tuu na tume be taken for a ride to employ their incompetent watu walioshidwa kupata kazi makwao.

mkuu, Nyerere alipata tuzo mbalimbali zaidi ya 50 ila Nobel haipo. Ni sudi ya Mandela tu kupata tuzo zaidi ya 200 ikiwemo ya Nobel. To me Nyerere is far too revered than Mandela. As far as the prize is subjective, it wont change that fact
 
watoa Nobel are the winners,controlers they write the history and give the medals as long as you fit into their current propaganda agendas. they stand for no honour they either kill you and give you the medal latter or be their puppet and get it alive. they are the same side of the same coin the only thing they stand for is control ya maisha yako ukiwa mjakazi wao na wanafanya, wanachukua kila njia usiweze kufanikiwa.

Huitaji kubarikiwa busara kuona utendaji wao angalia kila kona ya dunia hii kuna watendaji wao wa kazi worl bank,IMF AND UN tekea enzi hizo walivyosema tupo free. Lakini mbona bado wanatufunga na madeni, vita na ukiepuka vita unapata wakimbizi. Yani ni janga moja baada ya jingine wanatuorodheshea kila siku yakifuatana. Usithani tunajitakia wenyewe, mfano malawi 2007 walikuwa na mazao mengi maghalani mwao. Kichaa kikawapanda IMF na world bank wakawashauri wauze kwa vile they had a lot and they will get insentives. Guess what 2008 wakakubwa na drout. world bank and their right wing IMF came from behind to their rescure more madeni with rediculous interest. Walivyo ambiwa they were the course they just rpl they were just advising, hiyo inamaana kweli.
 
Watoa Nobel wanachagua 'mpole' wamtakaye - walimpa Martin Luther King Jr wakamuacha Malcolm X; Walimpa Nelson Mandela wakamuacha Chris Hani; Walimpa Wole Soyinka wakamuacha Chinua Achebe; Walimpa Barack Obama wakamuacha Muammar Gaddafi.

Companero hata mimi napigwa na bumbu wazi kabisa kuhusu huu unafiki wa taasisi hii ya Nobel Peace Prize katika vigezo wanavyotumia kuwa tunukia washindi. Kuna washindi wengine ambao wanafahamika kwa watu wa hiyo kamati ya Nobel pekee ambao waliyoyafanya ndio kwanza unaanza kuyatafuta baada ya kutangazwa. Na kuna wengine kama huyo wa mwaka jana kutoka China anapewa tuzo ili tu kuikera Serikali ya China ambayo imemfunga kwa makosa ya kihaini.
Kwa kweli vigezo ni vya kibinafsi na washindi walio wengi ni wale wanaokubali kuwa vibaraka wao au kwa kutoa tuzo hizo kuna malengo yao yanafikiwa.
Katika bara zima la Afrika kwa muda wa takriban miaka 100 iliyopita simuoni kiongozi yeyote ambaye alijitoa kwa maslahu ya bara la Afrika kama Julius kambarage Nyerere kuanzia waswala ya ukombozi wan nchi mbalimbali. Mwalimu alisema uhuru wan chi moja ya Afrika hauna maana ikiwa sehenmu moja ya bara inakaliwa na wakoloni.
Mwaka 1960 wakati wa Serikali ya Madaraka ya Tanganyika, Mwalimu aliwahi penyeza barua kwa Mwenyekiti wa kikaocha jumuiya ya Madola kilichokuwa kinafanyika pale London. Katika kikao hicho kulikuwa na wajumbe kama Indira Gandhi wa India, Nnamdi Azikiwe wa Nigeria na Kwame Nkrumah wa Ghana wakiwakilisha nchi huru za bara la Afrika kwa wakati ule. Katika waraka huo aliwaambia wajumbe wa Afrika kuwa kama angekuwa miongoni mwao basi asingikaa pamoja na mjumbe wa Afrika Kusini kaburu Verword ambaye ombi lake la kujiunga na Jumuiya hiyo lilikuwa linajadiliwa baada ya Uingereza kuyachia makoloni matano ya Afrika kusini kwa pamoja.
Waraka wa Nyerere vilevile ulinakiliwa kwenye bgazeti la The observer la London na ukachapwa. Matokeo ni kwamba Afrika Kusini ilinyimwa uanachama wa Jumuiya ya Madola kutokana na sera zake za kibaguzi. Pata picha ya mtu ambaye si mwanachama wa kikao lakini ana influence maamuzi ya kikao akiwa nje na wajumbe wanafanya kadri ya maono yake.
Unapomwongelea Mandela lazima ukumbuke kuwa hakuna Mandela bila Nyerere, yaani Nyerere ndiye aliye ongezea umaarufu wa Mandela ambaye anaenziwa sana. Kikubwa utakachokiona kwa Mandela ni kwamba yeye ndiye mfungwa wa kisiasa aliyekaa jela kwa muda mrefu (miaka 27) akiwa amesimama kwenye msimamo wake kwa kile anachokiamini na kwamba alipotoka hakulipa kisasi kwa wale waliomfunga. hilo tu ndilo Mandela analo mzidi Nyerere
Mwalimu vilevile alikuwa ndiyo kiongozi wa kwanza wa nchi ya Afrika kuvunja uhusiano wa kiuchumi na kisiasa mara moja baada ya Ian Smith mlowezi wa Southern Rhodesia (sasa Zimbabwe) kujitangazia Uhuru mnamo mwaka 1966 baada ya Waingereza kuiachia. Na vikwazo hivyo ndivyo vilivyopelekea wapigania Uhuru wa Zimbabwe kujitangazia uhuru mnamo mwaka 1980 na Robert Mugabe akiwa Raisi wao.
Mwalimu alitoa raslimali ya nchi maskini ya Tanzania kwa kuwapa makambi wapigania uhuru wa Namibia (SWAPO), Angola (MPLA na NFLA), Afrika Kusini (PAC na ANC), Zimbabwe (ZAPU na ZANU) na Msumbiji (FRELIMO). Bila ‘sacrifice’ ya Mwalimu na maamuzi mahsusi basi historia ya nchi zote hizo ingeandikwa vinginevyo.

Sasa wanaosema Nyerere kafanya nini katika duru za ki9mataifa sjui wana maanisha nini? Kama unaweza kutoa mchango wa kuikomboa nchi inayogandamizwa kwa ubaguzi wa rangi au ukoloni mkongwe au ukoloni mamboleo je kuna tukio linazidi hilo kimataifa?
 
kuna tofauti ya ukombozi alioufanya Mandela na Nyerere? Wote walipingana na udhalimu wa kikoloni. Na hata kufikia kuundwa tume ya maridhiano SA, tayari damu nyingi ilishamwagika kushinda hata wakati wa Nyerere. Mwisho wa siku utagundua sababu si mapambano ya kijeshi pekee. Itikadi za kisiasa zaweza pia kuchangia

Hoja yako (kuhusu ubaguzi wa Nobel) siikatai; mie mwenyewe nashawishika sana kuamini hawa wakuu wana malengo yao. Ila, kuna sifa moja ya waliopewa tuzo hii inabidi pia tuiangalie. Mandela alikuwa tishio sana kwao alipotangaza na kusimamia mapambano ya silaha dhidi ya makaburu (enzi za Umkhonto we Sizwe). Sadat naye vivyo hivyo, kwa Israel. Lakini wote hawa hatimaye walibadili misimamo yao (iliyotisha) na kukubali kujadiliana na kuwekeana mikataba/maelewano ya amani na mahasimu wao. Mwalimu never compromised. Hata lilipokuja suala la kukubaliana na IMF kwake ilikuwa bora kung'atuka. Na sidhani kama kupata au kukosa tuzo ya Nobel lingekuwa suala la kumsumbua katika kusimamia kile alichoamini. Ndio maana nakubaliana na wale wanaoiona tuzo (ya Nobel) kuwa ya udhanifu (subjective) zaidi na si kipimo hakika (au pekee) cha ukuu wa mtu.
 
Nimewahi kusikia kuwa hawa watoa tuzo wa nobel ukishaenda vitani na nchi nyingine hawakupi sijui kwanini. Vita vya uganda vilimkosesha.naomba kusahihishwa.
 
Ni kweli mkuu stux. Huyu mwenye heri alikuwa na upendo wa mshumaa. Wacha Vatican imtangazie ukuu zaidi ya ule wa Oslo
 
Nimewahi kusikia kuwa hawa watoa tuzo wa nobel ukishaenda vitani na nchi nyingine hawakupi sijui kwanini. Vita vya uganda vilimkosesha.naomba kusahihishwa.

kwani the prize committee haijui kuwa war is peace. Obama karithi vita nyingi tu. Au ndio maana waliwahi kumpa kabla hajaizoea ofisi?
 
Jean Paul Sartre aliwahi kutunukiwa tuzo ya Nobel akaikataa, tujiulize kwa nini!
 
kwanza huyu Sartre alikuwa philosopher. Aliiandikia kamati ya tunzo ya Nobel kuhusu kujitoa kwenye tunzo. Kamati ikampuuzia. Walimtunuku tunzo katika fasihi na akaikataa. Baadae alitoa maelezo katika jarida moja. Hapa namnukuu, "for wishing not to be 'transformed' by the award and take sides in East Vs West cultural struggle by an award from prominent western cultural institutions". Huyu bwana alikuwa ni mfaransa. Kumbe pia sikuwa mbali na ukweli kuwa itikadi za east na west zilikinzana. Nyerere hakutaka kuwa upande wowote wakati wa vita baridi kati ya warsaw pact na nato ndio maana akawa katika Non Allignment Movement. Nadhani pia katika hili, kamati ya tunzo ilisoma alama za nyakati. Kwamba yasijewakuta kwa Nyerere kama yalivyowakuta kwa Sartre
 
Lakini wakuu kwani zaidi ya propaganda zinazofanywa humu ndani ya nchi na baadhi ya watu kumtukuza kwa malengo maalumu amefanya nini cha maana. Maana hata kule kwetu mikoa ya kusini Mwalimu Nyerere hakubaliki kabisa maana alibomoa uchumi wa kusini na pia kusababisha umasikini wa hali ya juu mafanikio makubwa yaliyokuwa yamefikiwa kabla ya uhuru aliyaporomosha kupitia nadharia zake za Vijiji vya ujamaa, Azimio la Arusha, mara sijuwi Ulanguzi. Kwa kweli simkubali kabisa Huyu Marehemu JK Nyerere na nikisikia kiongozi yeyote wa chama chochote kile cha siasa au taasisi yoyote ile akitaja maneno yake tu basi najua ni mbabaishaji.

Kimataifa sifa aliyonayo nadhani ni ya ubishi na kupenda kupigana hii niliisikia huko nchi za asia niliambiwa baada ya kueleza kuwa natokea Tanzania.

Kwa kweli kipengere cha kumpatia hiyo Nobel hakipo maana hakuna WaTz huko kwenye Jopo la majaji.
 
jamani kla kitu huwa kinaanzishwa kwa malengo fulani. walioanzisha hiyo award walikuwa na malengo yao na vigezo vyao kadiri wanavyoona inafaa na labda sisi ndio tunaokosea kuwalaumu kwa kuwa hawakuangalia malengo yetu ama kuzingatia vigezo vyetu.

sisi nao tumezidi mno kutukuza vitu vya kimagharibi, kwani asipopewa heshima na nobel na sisi tunaona kafanya mambo ya maana si tumpe sisi heshima tunayoona anastahli? kwani lazima apewe na wazungu ndiyo iwe heshima?

hapa kwetu tanzania tuna siku mzima ya mapumziko kila mwaka kukumbuka kazi zake, hao akina wangari maathai wanapewa hata dakika mbili huko kwao kukumbuka michango yao? labda ni kichaa peke yake ndiye anayeweza kudhani maathai anaweza kuwa maarufu hapa duniani kumshinda nyerere.

so cool down bros and sistos

tujiamini, God is with us too
 
ukweli kuhusu tunzo hii, Sartres kaweka wazi-kwamba ni ukuu wa Magharibi dhidi ya Mashariki. Kwamba ukipewa tunzo hii basi wewe utafuata tu mtazamo wa kimagharibi, na watakutumia kwa kuwa tayari una ushawishi. Ila wakati mwingine malengo ya jambo fulani hubadilika kutokana na hali na wakati. Lakini siku zote binadamu hupenda kujinasibisha na mwenye nguvu
 
Hivi alichoshare na waziri mkuu wa india na wa sweden kama nina kumbukumbu kweli ilikuwa nini vile, naomba kujibiwa na kukosolewa

Kwanza kabisa Indira Ghandhi alikuwa rafiki mkubwa sana wa Nyerere. Indira gandhi ndiye aliyeanzisha'initiate' suala la kuwa na dunia isiyo na silaha kali kama za nyuklia ili iwe salama. Aliwahi usema usalama wa dunia si suala la kuachiwa White house au Kremlin.
Katika jitihada za 'disarmament' aliwashirikisha viongozi wafuatao:
Nyerere(Tanzania), Olfo Palme(sweden), Andrea Papandreous(greece), Raul Alfonsin(Agentina) na Miguel de la madrid(mexico)
Hii iliitwa six leaders disarmament commission.

Pili, Nobel prize si lazima itolewe kila mwaka, kuna miaka mingi tu haikuwahi kutolewa kama 1948 alipokosekana mtu mwenye sifa.
Siri za kutajwa(nomination) hutunzwa kwa miaka 50. Kwahiyo leo tunaweza jua ni kwanini mwaka 1913 fulani alishinda.
Nobel iliacha kutolewa kwa wafu mwaka 1974 (post humously). Hadi mwaka huo ni watu wawili tu waliowahi kutunukiwa wakiwa marehemu.Hii ina maana kuwa Nyerere hatatunukiwa tena tuzo hiyo.
Mahatma Ghandhi hakuwahi kushinda ingawa alitajwa mara nyingi(nominated) na utata wa 'post humously' ulianzia kwake.

Ama kuhusu mwalim Nyerere mchango wake hauwezi kuangaliwa kwa jambo moja au mawili. Huyu alikuwa ni kiongozi mwenye ushawishi mkubwa sana katika medani za kimatifa. Pamoja na ukombozi akiwa kiongozi wa frontline states, pia alichangia sana katika ukombozi wa makoloni mengi barani Afrika na duniani.
Mwalimu alikuwa Nguzo Muhimu sana katika 'Non alignment movemnt' akiwa na akina Tito wa Yugoslavia, Indira, Toure n.k.
Alikuwa pia ni mwenyekiti wa tume ya south south commission kutoa mapendekezo ni namna gani nchi masikini zinavyoweza kushirikiana.
Wakati OAU ikikaribia kusambaratika mwalimu alikuwa Hotelini Benghazi Libya na mwandishi mmoja wa Reuter alimuuliza' kwanini unaonekana mnyonge sana' yeye akajibu nakumbuka wakati nilipokuwa na wazee wenzangu kama Sellaise, Tolbert, Nasser,Boumediane mambo hayakuwa hovyo namna hii. Inasekana kauli hii ndiyo iliwagusa viongozi wa Afrika na kufanya mkutano Adis Ababa, licha ya kuwa mwalimu alikuwa anang'atuka alipewa uenyekiti kwa mwaka mmoja, utaratibu uliokuwepo ni miaka miwili.
 
Kumbukumbu zangu zinanituma kuamini hivyo. Katika Afrika ni wachache wamewahi kupata tuzo hii yenye hadhi nadhani kushinda zote. Kapata Mandela, Tutu, Wathari, n.k. Nyerere hakuwa na mchango unaostahili hii tunzo? Tunahitaji kufahamu hili toka kwa wajuvi

Kumbuka, kuhamisha makundi kwa makundi ya watu kuwasomba na kuwatupa porini, ukiwaamrisha "anzisheni kijiji cha ujamaa", simba, chui, nyoka, ndio wanawangoja, hakuna matibabu wala usafiri, hakuna nyumba wala tembe. "Imagine scenario" kama hiyo, ni wangapi waliopoteza maisha yao! Halafu apewe Noble prize. Is that "scenario" noble to you? If not, huyo ndio nyerere na hayo yametokea na si ya kuhadithiwa. Nilikuwepo.
 
Kumbuka, kuhamisha makundi kwa makundi ya watu kuwasomba na kuwatupa porini, ukiwaamrisha "anzisheni kijiji cha ujamaa", simba, chui, nyoka, ndio wanawangoja, hakuna matibabu wala usafiri, hakuna nyumba wala tembe. "Imagine scenario" kama hiyo, ni wangapi waliopoteza maisha yao! Halafu apewe Noble prize. Is that "scenario" noble to you? If not, huyo ndio nyerere na hayo yametokea na si ya kuhadithiwa. Nilikuwepo.

hakuna maisha marahisi mkuu. Na hakuna anayetafuta kupendwa na wote na akafanikiwa. Hayo usemayo yalitokea pia China. Walivaa kaki nchi nzima. Walilimishwa na serikali mpaka basi. Walikufa pia lakini China ya leo ambayo ni super power ilianza kama Tanzania. Nyerere wakati huo alikuwa sahihi kuwajenga watanganyika. Wasaidizi wake tu ndo waliharibu. Pengine pia ulaya na marekani walichangia pia. Leo hii ujerumani inasifika kwa miundombinu bora sana. Hii ilijengwa wakati wa Hitler. Leo hii tungekuwa kama Afrika kusini kiuchumi sidhani kama tungemshutumu Nyerere. Ijulikane pia kuwa rasilimali nyingi zilitumika kuyasaidia mataifa mengine kujikomboa. Mwisho wa siku, nobody is perfect
 
Raia Fulani,

Kwa hayo majibu yako ni kiongozi yupi wa China alipata Noble Prize? Kama hakuna ndio jibu langu hapo juu.
 
Raia Fulani,

Kwa hayo majibu yako ni kiongozi yupi wa China alipata Noble Prize? Kama hakuna ndio jibu langu hapo juu.

katika hilo hakuna. Sana sana ni yule mwanaharakati wa kichina ambaye anapingana na serikali yake kimtazamo. Ndio tujue kuwa ile ni tuzo ya kiitikadi zaidi japo ina hadhi yake
 
Nyerere ni zaidi ya Nobel. Wala Hatuihitaji. Ukweli utabaki pale pale katika historia ya dunia hii, Nyerere ni mmoja wa viongozi bora kabisa kupata kutokea. Ni kiongozi aliyekuwa na nia ya dhati kabisa na watu wa nchi hii, na ndio maana katika kila neno alilolitoa lilikuwa na elements za kumtetea mtu mnyonge na kuhimiza usawa katika kila hitaji muhimu la binadamu.Tazama mifano: alitaifisha shule (mfano-Mazengo), vyuo na hospitali za wakristu kuwa za umma ili kila mtu apate elimu; alipenda familia nyingine zaidi ya kwake-tazama watoto wake walivyo masikini,aliendeleza sehemu tofauti za nchi-mfano Dodoma kuliko kwao Butiama; alikomboa nchi nyingi za Afrika kwa fedha zetu.Napenda niseme kipimo cha ubora wa Nyerere ni cha kimungu zaidi na si cha kibinadamu kama ilivyo tuzo ya Nobel.Wazungu watampaje wakati hawaamini usawa wa binadamu ambao ndio ilikuwa sara ya Nyerere. Kwao Mandela amekuwa shujaa kwa kuwa hakulipa kisasi, lakini kwa maoni yangu Nyerere ni zaidi ya Mandela, hili hata Madiba mwenyewe analifahamu.Kudhihilisha ubaguzi wa wazungu.....Mandela aliwahi kusema " walioniita gaidi sasa wananiita shujaa" akirejea maongezi ya Magreth kiongozi wa zamani wa Uingereza. Nguvu ya MUNGU hushinda siku zote...utaona kanisa litakavyowaumbua kwa kumtangaza mwenye heri.
 
kuna tofauti ya ukombozi alioufanya Mandela na Nyerere? Wote walipingana na udhalimu wa kikoloni. Na hata kufikia kuundwa tume ya maridhiano SA, tayari damu nyingi ilishamwagika kushinda hata wakati wa Nyerere. Mwisho wa siku utagundua sababu si mapambano ya kijeshi pekee. Itikadi za kisiasa zaweza pia kuchangia
Naomba kutofautiana na wewe. Ukisoma wasifu wake, yeye anatuhumiwa pia kwa kusababisha hali kuwa tete katika baadhi ya nchi. Yeye ndiye alikuwa anakaa na wafuasi na anawasaidia kuangusha baadhi ya serikali. Hivyo alikuwa ni kama ndumi la kuwili.
 
Back
Top Bottom