USICHOKE KAKA PITA NA HAPA ILI UMJUE VIZURI HUYU UNAYEMSEMA, UKIWA MVIVU WA KUSOMA NAKWAMBIA HUTOMWELEWA MWALIMU! Julius Nyerere: Biography from Answers.com
Tatizo kubwa la threads nyingi humu jamvini kuhusu Nyerere ni pale mapungufu ya wakati wa utawala ule wa awamu ya kwanza yanatumika kujustfy uzembe, wizi, ufisadi na kukosekana uwajibikaji wa serikali zilizofuata. Lakini dimensions na vigezo vinakuwa jumla jumla tu. Mfano mtu anasema JK ameleta zahanati nyingi kuliko raisi mwingine yeyote, lakini ukichallenge kwamba mbona hamna wauguzi wala madawa inaletwa hoja wakati wa Nyerere zilikuwa ngapi???????
....
Mkuu mimi nakuunga mikono na miguu yote kwa huo mtazamo wako, unayoyasema yanaukweli sana, ni kwa mvivu tu wa kutafakari ndiye atakayepingana nawe. Mimi hilo jambo nimekuwa nikilitafakari kwa muda mrefu sana.Humu ndani, kuna watu wakiona Hayati Julius Nyerere, the First Preisdent wa URT anasemwa vibaya basi wanakuja juu!! Kinachonikera mimi, ni wengi wao kuhusisha na imani za dini! Kwamba, mtu akisema ubaya wa Nyerere, na hasa mtu huyo akihisiwa ni Mwislamu, basi hoja ya wapofu wa hoja watachukulia ukosoaji huo ni chuki ya waislamu dhidi ya Nyerere!! Hivi ni lini Waislamu wamepata kuwa na chuki na mwalimu?! Sasa haya mambo kwamba mtu akitaja mabovu ya Mwalimu basi ni chuki za waislamu dhidi ya mwalimu yanatoka wapi?! Binafsi, am muslim, na kama utaniambia nikutajie my favorite president sitasita kumtaja Julius Nyerere. lakini pamoja na yote hayo, kama nitaambiwa nitaje top two poorest presidents ever happaned in our history, basi Nyerere ni mmoja wapo, akiwa sambamba na mwinyi! Binafsi, nikimwangalia Nyerere, ni eneo moja peke yake ambalo linaweza kumweka kama best leader! hakuwa corrupt leader ingawaje serikali yake ilikuwa very corrupt government!! Na wala si kweli kwamba Nyerere alikuwa mkali kwa corrupt leaders, vinginevyo nchi hii Mwinyi asingeikuta alipoikuta! Sana sana ki2 ambacho labda Nyerere aliweza kuzuia ni kutokuwa na State House corrupt leaders...lakini ukitoka hapo, wengi walikuwa corrupts!
Serikali ya Nyerere ilijaa watendaji ambao walikosa kabisa uwajibikaji na ndio maana Mwinyi alikuja na kitu kilichojulikana kama Fagio La Chuma! Kwanini awe na fagi la chuma wakati uwajibikaji ulikuwapo?! Serikali isiyo corrupt, haiwezi kuwa na irresponsible leaders. Ni kweli, Nyerere hakuwa corrupt leader, lakini aliendesha corrupt government na anayebisha aniambie kwanini viwanda vyote vilifia mikononi mwake!!
Ni kweli JK ni goi goi! hata Nyerere alikuwa ni goi goi kupita kiasi!! hakuwa mkali kama tunavyoaminishwa watu ambao hatukuwa na ufahamu wakati wa utawala wake. Nyerer alikuwa mkali kwa wapinzani wake wa kisiasa, and not otherwise!! Kama alikuwa mkali kweli, umasikini tulionao ulitokea wapi?! Aliwafanya nini waliokuwa wanaharibu mali za umma zaidi ya kuwahamisha?! kama sio ugoi goi tuite nini hii?!
Kulikuwa na miradi kadhaa ambayo ilianzishwa wakati wa utawala wake, na vilevile ilikufa hata kabla haijafika kokote....sasa kama sio ubadhirifu huo tuite nini?! Siwezi kumsifia kiongozi aliye msafi yeye pekee na familia yake wakati serikali yake imejaa watu irresponsible!!
Amekaa Ikulu more than 20 years lakini ametoka akiwa ameachwa barabara zimejaa mahandaki kila mahali!! Bahati mbaya sana, sehemu ambazo zilikuwa na corrupt leaders toka kwenye serikali yake ndio sehemu pekee ambazo angalau zilikuwa na barabara nzuri kidogo! Sehemu ambazo walitoka honest leaders kama yeye, ndizo zikabaki balaa tupu!!! Hiyo ndio sababu kuu iliyofanya mikoa ya kusini kuwa hoe hae zaidi kwani viongozi wake wengi walikuwa honest kama yeye...hawa ni pamoja na akina Kawawa na Nnauye! Hivyo, umaskini wa kusini haukusababishwa na Nyerere kama Nyerere, bali ulisababishwa na irresponsible central government ambayo ugawaji wa keki ya taifa haukuwa the same! ilitegemea sana sehemu husika ana power gani serikalini and how corrupt s/he is!!!
Nyerere ameondoka akiwa ameacha vyuo vikuu viwili tu, UDSM na SUA na kuishia tu ktk kujenga vyuo vya kati ambavyo hata hivyo navyo productivity yake ilikuwa chini. Chuo pekee cha kati ambacho kilikuwa kinatoa elimu ya maana labda ni Mzumbe peke yake....na sababu kuu ni kwavile kilikuwa more political! Tena hata nina mashaka kama kweli kilikuwa kinatoa elimu ya maana!! tangu lini katibu wa nini sijui mwenye miaka 45++ akaweza kuhimili mikiki mikiki ya elimu ya juu?! Tunaambiwa enzi zake elimu ilikuwa na ubora kuliko sasa!! na hii ndio tabia ya wazee....kwamba kila ki2 chao kilikuwa bora!!! Huo ubora ulisaidia nini basi katika kutatua matatizo ya uchumi wa nchi hii?! Sana sana hao tunaoambiwa walikuwa wasomi wakati wa elimu bora ndio hao hao waliogeuka kuwa corrupts wasio na haya wakati wa Mwinyi.....bisheni!!! Kama ni kweli wakati huo elimu ilikuwa bora basi vilevile ilisaidia kuzalisha BEST CORRUPT LEADERS!!! Serkali corrupt haiwezi kuwa na jeuri ya kujenga vyuo vikuu vya kutiosha kwavile haina fedha.....kutokuwa na fedha ni dalili ya serikali corrupt!!!
MATATIZO ya umeme tuliyonayo hivi sasa source yake ilikuwa enzi za mwalimu!!! Serikali ya Mwalimu haiku-forecast mahitaji ya umeme over the next 50 years!! Ni kweli, wakati wa Nyerere, haukuwa wa mgao! Sasa mgao ungetoka wapi wakati nyumba zenyewe za umeme zilikuwa chache?! Mgao ungetoka wapi wakati hakukuwa na uzalishaji mkubwa wa kuhitaji matumizi ya umeme?! Mgao ungetoka wapi wakati hata kumiliki radio ilikuwa ni anasa?! Kwahiyo, si kwamba ni uongozi bora wa Nyerere ambao ulifanya nchi isiwe na mgao/upungufu wa umeme, bali hiyo ilikuwa ni matokeo ya serikali mbovu!
Tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Huduma gani za jamii?! hizo za kufuata zahanati kilometa 50 na shule ya msingi kilometa 10?! Dar es salaam yote hii aliacha shule saba tu za sekondari (za serikali, ambazo hata hivyo hakujenga yeye)-Jangwani, Azania, Tambaza, Forodhani, Kisutu na Kibasila!!! Nani atakayethubutu kusema kwamba shule hizo zilikuwa zinakidhi mahitaji ya elimu ya sekondari jijini? Huko mikoani ndo ilikuwa balaa tupu, unaweza kukuta mkoa mzima una shule moja au mbili za serkali.....bado tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Ni serikali gani ingeshindwa kuhudumia shule chache kama hizo?!
Ubovu wa serikali ya Nyerere ni mwingi kuliko uzuri wake, otherwise, wale wanaoona kwamba mgtu akisema basi ana chuki za kidini (styupid thinking) basi anitajie hapa mazuri yaliyofanywa na serikali yake ambayo natarajia yawe mengi kuliko mabovu!
wapo watakaosema kwamba Nyerere amewezesha nchi hii kuwa na amani! Kwani aliichukuwa wakati nchi haina amani?! Sifa kama hizo anatastahili kupewa Kagame aliyechukua nchi baada ya mauaji ya kutisha nchini mwake! Anyway, waliosoma historia wanisaidie kunitajia ni vita gani vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimepata kupiganwa Tanganyika katika karne ya 19! Kama hakuna au zilikuwa si za kutisha sana, basi inawezekana Watanganyika hatuna silika ya kupigana tangu zama hizo!!
Hivyo basi, mtu anavyotaja ubovu wa Nyerere inakuwa ni ujinga uliepitiliza kusema kwamba ni chuki binafsi...Na inakuwa sio ujinga, bali ni upumbavu mtu akisema ni chuki za kidini! Nyerere kama Nyerere alikuwa was a very good person BUT NOT A GOOD LEADER! He was a good person who was a poor leader! Kutokana na hayo, sipati kigumumizi hata chembe kusema wazi kwamba SI KWAMBA NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU, BALI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU! Ukweli wenyewe ndio huo, ukiona mgumu kuumeza, chukua maji ushushie!
Anayekataa, atoe data za mazuri yake kama kiongozi yenyewe manufaa kwa Tanzania!
Yule babu na apumzike kwa amani tu, ila kiukweli hakuwa kiongozi mzuri japokuwa binafsi alikuwa mtu mzuri. Kama aliweza kutumia nguvu nyingi kuwadhibiti wapinzani wake kisiasa, kwa nini asingetumia nguvu hiyohiyo kuwawajibisha wala rushwa na watumia madaraka vibaya? Kuna wakati alikuwa mbishi sana kufuata ushuri wa maana toka kwa watu wa chini yake, huo ni udikteta. Nchi hii mtu akifa basi hata mabaya yake yote hugeuka kuwa mazuri.Haya wa dunia leteni mazuri ya Nyerere maana mimi nikisema hakuna, mtabisha lakini kuonesha zuri lake hamuwezi.
Mimi kwa mtazamo wangu what I can say in brief ni kwamba Nyerere was a greater leader who did
a great mistake.
Mojawapo ya makosa ambayo sitamsamehe kabisa Nyerere ni kuwa pioneer wa uchakachuajia wa kura
Tanzania. Pale alipochakachua ushindi wa Maalim Seif dhid ya Dr. Salmin Amour, Zazinzibar 1995. Hii dhambi ya
"kula nyama ya mtu" aliyo warithisha CCM ndiyo inaendelea kututesa hadi hii leo.
Nyerere set a bad precedence of vote rigging in Tanzania and History will be always there to judge him.
Hakuna kama Nyerere. Kampeni yoyote chafu kuchafua jina lake haitashinda.
Tatizo lililokuwepo chini ya mwalimu la kuwahamisha viongozi wabovu na wala rushwa kama punishment badala ya kuwavua madaraka na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria, kusema kweli limetu cost na bado linaendelea kufanya hivyo...Ni culture mbovu ambayo mizizi yake ni CCM.
Humu ndani, kuna watu wakiona Hayati Julius Nyerere, the First Preisdent wa URT anasemwa vibaya basi wanakuja juu!! Kinachonikera mimi, ni wengi wao kuhusisha na imani za dini! Kwamba, mtu akisema ubaya wa Nyerere, na hasa mtu huyo akihisiwa ni Mwislamu, basi hoja ya wapofu wa hoja watachukulia ukosoaji huo ni chuki ya waislamu dhidi ya Nyerere!! Hivi ni lini Waislamu wamepata kuwa na chuki na mwalimu?! Sasa haya mambo kwamba mtu akitaja mabovu ya Mwalimu basi ni chuki za waislamu dhidi ya mwalimu yanatoka wapi?! Binafsi, am muslim, na kama utaniambia nikutajie my favorite president sitasita kumtaja Julius Nyerere. lakini pamoja na yote hayo, kama nitaambiwa nitaje top two poorest presidents ever happaned in our history, basi Nyerere ni mmoja wapo, akiwa sambamba na mwinyi! Binafsi, nikimwangalia Nyerere, ni eneo moja peke yake ambalo linaweza kumweka kama best leader! hakuwa corrupt leader ingawaje serikali yake ilikuwa very corrupt government!! Na wala si kweli kwamba Nyerere alikuwa mkali kwa corrupt leaders, vinginevyo nchi hii Mwinyi asingeikuta alipoikuta! Sana sana ki2 ambacho labda Nyerere aliweza kuzuia ni kutokuwa na State House corrupt leaders...lakini ukitoka hapo, wengi walikuwa corrupts!
Serikali ya Nyerere ilijaa watendaji ambao walikosa kabisa uwajibikaji na ndio maana Mwinyi alikuja na kitu kilichojulikana kama Fagio La Chuma! Kwanini awe na fagi la chuma wakati uwajibikaji ulikuwapo?! Serikali isiyo corrupt, haiwezi kuwa na irresponsible leaders. Ni kweli, Nyerere hakuwa corrupt leader, lakini aliendesha corrupt government na anayebisha aniambie kwanini viwanda vyote vilifia mikononi mwake!!
Ni kweli JK ni goi goi! hata Nyerere alikuwa ni goi goi kupita kiasi!! hakuwa mkali kama tunavyoaminishwa watu ambao hatukuwa na ufahamu wakati wa utawala wake. Nyerer alikuwa mkali kwa wapinzani wake wa kisiasa, and not otherwise!! Kama alikuwa mkali kweli, umasikini tulionao ulitokea wapi?! Aliwafanya nini waliokuwa wanaharibu mali za umma zaidi ya kuwahamisha?! kama sio ugoi goi tuite nini hii?!
Kulikuwa na miradi kadhaa ambayo ilianzishwa wakati wa utawala wake, na vilevile ilikufa hata kabla haijafika kokote....sasa kama sio ubadhirifu huo tuite nini?! Siwezi kumsifia kiongozi aliye msafi yeye pekee na familia yake wakati serikali yake imejaa watu irresponsible!!
Amekaa Ikulu more than 20 years lakini ametoka akiwa ameachwa barabara zimejaa mahandaki kila mahali!! Bahati mbaya sana, sehemu ambazo zilikuwa na corrupt leaders toka kwenye serikali yake ndio sehemu pekee ambazo angalau zilikuwa na barabara nzuri kidogo! Sehemu ambazo walitoka honest leaders kama yeye, ndizo zikabaki balaa tupu!!! Hiyo ndio sababu kuu iliyofanya mikoa ya kusini kuwa hoe hae zaidi kwani viongozi wake wengi walikuwa honest kama yeye...hawa ni pamoja na akina Kawawa na Nnauye! Hivyo, umaskini wa kusini haukusababishwa na Nyerere kama Nyerere, bali ulisababishwa na irresponsible central government ambayo ugawaji wa keki ya taifa haukuwa the same! ilitegemea sana sehemu husika ana power gani serikalini and how corrupt s/he is!!!
Nyerere ameondoka akiwa ameacha vyuo vikuu viwili tu, UDSM na SUA na kuishia tu ktk kujenga vyuo vya kati ambavyo hata hivyo navyo productivity yake ilikuwa chini. Chuo pekee cha kati ambacho kilikuwa kinatoa elimu ya maana labda ni Mzumbe peke yake....na sababu kuu ni kwavile kilikuwa more political! Tena hata nina mashaka kama kweli kilikuwa kinatoa elimu ya maana!! tangu lini katibu wa nini sijui mwenye miaka 45++ akaweza kuhimili mikiki mikiki ya elimu ya juu?! Tunaambiwa enzi zake elimu ilikuwa na ubora kuliko sasa!! na hii ndio tabia ya wazee....kwamba kila ki2 chao kilikuwa bora!!! Huo ubora ulisaidia nini basi katika kutatua matatizo ya uchumi wa nchi hii?! Sana sana hao tunaoambiwa walikuwa wasomi wakati wa elimu bora ndio hao hao waliogeuka kuwa corrupts wasio na haya wakati wa Mwinyi.....bisheni!!! Kama ni kweli wakati huo elimu ilikuwa bora basi vilevile ilisaidia kuzalisha BEST CORRUPT LEADERS!!! Serkali corrupt haiwezi kuwa na jeuri ya kujenga vyuo vikuu vya kutiosha kwavile haina fedha.....kutokuwa na fedha ni dalili ya serikali corrupt!!!
MATATIZO ya umeme tuliyonayo hivi sasa source yake ilikuwa enzi za mwalimu!!! Serikali ya Mwalimu haiku-forecast mahitaji ya umeme over the next 50 years!! Ni kweli, wakati wa Nyerere, haukuwa wa mgao! Sasa mgao ungetoka wapi wakati nyumba zenyewe za umeme zilikuwa chache?! Mgao ungetoka wapi wakati hakukuwa na uzalishaji mkubwa wa kuhitaji matumizi ya umeme?! Mgao ungetoka wapi wakati hata kumiliki radio ilikuwa ni anasa?! Kwahiyo, si kwamba ni uongozi bora wa Nyerere ambao ulifanya nchi isiwe na mgao/upungufu wa umeme, bali hiyo ilikuwa ni matokeo ya serikali mbovu!
Tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Huduma gani za jamii?! hizo za kufuata zahanati kilometa 50 na shule ya msingi kilometa 10?! Dar es salaam yote hii aliacha shule saba tu za sekondari (za serikali, ambazo hata hivyo hakujenga yeye)-Jangwani, Azania, Tambaza, Forodhani, Kisutu na Kibasila!!! Nani atakayethubutu kusema kwamba shule hizo zilikuwa zinakidhi mahitaji ya elimu ya sekondari jijini? Huko mikoani ndo ilikuwa balaa tupu, unaweza kukuta mkoa mzima una shule moja au mbili za serkali.....bado tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Ni serikali gani ingeshindwa kuhudumia shule chache kama hizo?!
Ubovu wa serikali ya Nyerere ni mwingi kuliko uzuri wake, otherwise, wale wanaoona kwamba mgtu akisema basi ana chuki za kidini (styupid thinking) basi anitajie hapa mazuri yaliyofanywa na serikali yake ambayo natarajia yawe mengi kuliko mabovu!
wapo watakaosema kwamba Nyerere amewezesha nchi hii kuwa na amani! Kwani aliichukuwa wakati nchi haina amani?! Sifa kama hizo anatastahili kupewa Kagame aliyechukua nchi baada ya mauaji ya kutisha nchini mwake! Anyway, waliosoma historia wanisaidie kunitajia ni vita gani vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimepata kupiganwa Tanganyika katika karne ya 19! Kama hakuna au zilikuwa si za kutisha sana, basi inawezekana Watanganyika hatuna silika ya kupigana tangu zama hizo!!
Hivyo basi, mtu anavyotaja ubovu wa Nyerere inakuwa ni ujinga uliepitiliza kusema kwamba ni chuki binafsi...Na inakuwa sio ujinga, bali ni upumbavu mtu akisema ni chuki za kidini! Nyerere kama Nyerere alikuwa was a very good person BUT NOT A GOOD LEADER! He was a good person who was a poor leader! Kutokana na hayo, sipati kigumumizi hata chembe kusema wazi kwamba SI KWAMBA NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU, BALI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU! Ukweli wenyewe ndio huo, ukiona mgumu kuumeza, chukua maji ushushie!
Anayekataa, atoe data za mazuri yake kama kiongozi yenyewe manufaa kwa Tanzania!
Nimesoma kwa makini hii post. Nadhani vichwa vya waafrika vina shida fulani na ninadhani ni matokeo ya kitu kinachoitwa mental slavery, utumwa wa mawazo na umaskini wa mawazo pia ambao Nyerere alisisitiza pia. Pia ukiangalia kwa makini ndicho kilichotokea Libya (kwa kufananisha kwa uchache as a broader concept...).
Umaskini wa mawazo huja kwa hali ya kuwa proud na mawazo finyu ambayo mara nyingi ni zao la kutawaliwa na kukosa elimu sahihi ju ya maswala muhimu. Kwa mfano kutokana na kutwaliwa muda mrefu na wazungu, ilifikia wakati wazungu kutulazimisha kuingia katika vyama vingi na kusema ni demokrasia, kumbe maskini kwa nchi changa na maskini kama zetu ni sumu mbaya ya kuleta malumbano na utengano hivyo kuvunja kabisa nguvu moja ambayo matokeo yake yangekuwa pigo baya kwa wazungu, wazungu wenyewe waliwaza mbali na wao siku zote ni huleta mawazo ambayo kwa nje huonekana mazuri sana lkn kwa muda mrefu huwa ni mafanikio yao, kitaalam na kayika intelligensia ya maendeleo huwa ni matumizi ya doctrine mbili tofauti, moja ikiwa ni initiator na ingine ni sacred. Siku zote huwezi jua lengo la mwisho ni kama unavyoletewa zawadi ya vito na almasi huku wakichukua almasi au barabara na uranium, hii imeendelea kwa muda mrefu.
Sasa basi wanaomlaum Nyerere ni upungufu wa mawazo tu maskini, kumbe watu wengi hawakujua lengo lake kwenye nchi hii, na bahati mbaya watu wamekua wanashabikia kuongea hovyo tu bila hata takwimu. Hawajui wakati Mwinyi amechukua nchi ilikuwa na hali gani na baada ya kuachia kwa Mkapa aliiacha na hali gani, hata hivyo vipimo hawavijui jinsi vinavyotumika, again ni jambo la elimu finyu. Kwa uchache tu hata inflation na GDP ni vipimo ambavyo watanzania wengi hawavijui maskini na uhusiano na maendeleo ya nchi pia hawajui. Ni shida kubwa!!
Kifupi tu- Nyerere aliongoza na kuacha nchi na inflation ya chini ya asilimia 5. Wazungu waliona Tsh ni very strong currency na hivyo walishinikiza kudevalue Tsh kwa vipingamizi kadhaa mara baada ya vita ya Kagera na kwa mshtuko wa uchumi wa dunia baada ya cold war, baada ya Mwinyi kuchukua nchi inflation ilipanda kufikia 30%!Government revenue ikashuka mpk 30 billion per month! Hali ya uchumi iliharibika wakati wa Mwinyi kwa kuwa wazungu kupitia IFM na World bank kushinikiza mambo mengi yaliyolenga total control kwa nchi za afrika. Rushwa ikashamili zaidi maana walilenga pia kanuni za kijinga za utawala bora, free trading etc, zilizoleta upenyo wa mashirika ya umma kufa na kuruhusu sector binafsi.
Wengi hawajui hata New World Order ambayo Nyerere alijua from start, na hata katika kikao cha NEC cha dom alipokuwa anahutubia south south commission report aliongea, lengo la Nyerere lilikuwa ni kupambana na nguvu hizi kwa kutumia umoja wa afrika, hakuwa akingalia karibu kama viongozi wengi wafinyu wa mawazo, tafuteni elimu hii mpate kujua wazungu wanatumia mbinu gani kudidimiza mawazo endelefu, acheni kulaum.
Read more books, history and facts..--