Nyerere Day: Maoni yangu

Edwin Mtei

Senior Member
Dec 13, 2008
181
342
Siku ya leo nimeitumia kutazama maadhimisho ya Siku ya Nyerere jinsi yalivyoendelea huko Kigoma. Halaiki ya vijana haikusisimua mpaka Rais Kikwete alipofika, naye kama kawaida hakufika mapema.

Lakini baada ya kumalizika, nimejiuliza hivi kwa nini Serikali yetu imeamua kuadhimisha Tarehe 14 Oktoba kama ndiyo siku ya kumkumbuka Baba wa Taifa? Tarehe 14 Oktoba,1999 ndiyo siku Mwalimu alifariki akipata matibabu katika Hospitali ya St. Thomas, London.

Kwa Mama Maria Nyerere na watoto wake, Makongoro na Madaraka, wajukuu na kwa wote waliompenda na ambao wanajisikia wamepoteza kipenzi chao, leo ingekuwa siku ya kwenda Kanisani kusali, ili Mwenyezi Mungu aipokee roho yake. Leo ndiyo siku ambayo wangekwenda pale kaburini waweke maua ya kumkumbuka.

Lakini, lo leo ndiyo Watanzania baada ya gwaride na halaiki ya kitaifa, wanamiminika katika nyumba za starehe, kunywa, kufurahi na kucheza nyimbo za kizazi kipya!!!!!!.

Ningekuwa mshauri wa Serikali ningependekeza ile siku ambayo familia ya Mwalimu ilikuwa ikiadhimisha kuzaliwa kwake, iwe ndiyo hiyo na sisi Watanzania tunafarahia na kumshukuru Mungu kwamba Baba wa Taifa letu alizaliwa. Tuwaulize familia ya Mwalimu, watuambie ni siku gani.

Mataifa mengi huadhimisha "Founders' Day" kama ni ile ama Mkombozi wao alizaliwa, au siku aliyotiwa mbaroni kutokana na kuongoza harakati za ukombozi na kupinga utawala dhalimu wa nchi yake au utawala wa kikoloni. Sijapata kusikia nchi inaadhimisha siku aliofariki "hero" wao, isipokuwa hii ya kwetu.

Napendekeza Serikali ijayo, itafakari suala hili na kuamua kiustaarabu. Hii haimaanishi kwamba tarehe 14 Oktoba isahaulike. Ikumbukwe ni siku ya huzuni, tulipompoteza Baba wa Taifa. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amina.
 
Mzee Mtei, asante kwa points zako. Ningependa kukujibu kwa nini serikali ya Mkapa iliamua kuadhimisha na kusherehekea siku ya kifo cha Mwalimu lakini naogopa mods hapa watanifungia.

Kwa hakika haiingii akilini watu kusherehekea siku kiongozi wetu alifariki. Tungeweza kumuenzi vizuri zaidi Mwalimu kwa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake na leo iwe siku ya majonzi na kusali kanisani lakini najua waliopanga hivyo walikuwa na sherehe zao moyoni.

Angalia tu jinsi nchi inavyoendeshwa baada ya kifo cha Mwalimu. Jibu lipo hapo.
 
Mzee Mtei, ni kweli kabisa uliyoyasema, maana hapo tunabaki kati kati hatujui hii siku tuiadhimishe vipi kwa furaha kwa kusherehekea au tunatakiwa tusikitike kwa kumpoteza Baba wa Taifa letu! RIP Baba wa Taifa!
 
Mzee Edwin,
Kweli mawazo mazuri lakini sidhani kama huu ni utamaduni wetu kwani Mila zetu baada ya kiongozi au mtu muhimu ndani ya Familia kuondoka basi sisi wananchi au watoto wake huadhimisha siku ya kufa kwake kwa Ibada..Sherehe zote za Birthday huisha siku mtu anapofariki kwa sababu hii ni sherehe ya Uhai wa mtu na ndivyo tulivyolelewa.

Kwa hiyo binafsi sioni tatizo kabisa kumuenzi mwalimu kwa kuadhimisha siku ya kufa kwake, kwani ndivyo wengi tunafanya kuwaenzi wazazi wetu isipokuwa sii kama walivyofanya huko Kigoma. Siku hii inge adhimishwa kwa sala na Ibada kote nchini kisha sherehe kubwa zingefanyika kitaifa Butiama kila mwaka ili kuweza kuweka maua ikiwa ni pamoja na gwaride la heshima kwake. Pengine kinachotakiwa ni hata kubadilisha ile sherehe ya siku ya Mashujaa na kuwa tarehe 14 kumuenzi mwalimu.

Kifupi binafsi sioni sababu kabisa ya kumu enzi mwalimu kwa siku yake ya kuzaliwa kwani hiyo haitakuwa mila yetu.. Hata hivyo tuzudi mumuombea mwalimu, tusipotoshwe na hizi kampeni za kisiasa.
RIP mwalimu...
 
Unajua kwa nini ni siku ya furaha;

Ni rahisi sasa wao kutapanya mali za waTZ, ni rahisi sasa kufanya ufisadi, ni rahisi sasa kuuza mbuga za wanyama, ni rahisi sasa kuuza madini yetu hotelini, ni rahisi sana kutokujali maisha ya maskini na kuendeleza matabaka bila wa kuwahoji; so ni siku ya furaha kwao
 
Shikamoo Mzee Mtei:

Maelezo yako ni muhimu sana. Na nisingepata kurudi ulivyoelezea umuhimu wa siku. Kwa maoni yangu binafsi sikukuu zingine inabidi bunge ndio lipitishe kwa mijadala. Na sio serikali iamue tu kuwa siku fulani ni sikukuu.

Kinachofanyika sasa ni kuwa viongozi wanajilimbikizia mali, na walalahoi wanapewa sikukuu za kupumzika.
 
Mzee Mtei, asante kwa points zako. Ningependa kukujibu kwa nini serikali ya Mkapa iliamua kuadhimisha na kusherehekea siku ya kifo cha Mwalimu lakini naogopa mods hapa watanifungia.

Kwa hakika haiingii akilini watu kusherehekea siku kiongozi wetu alifariki. Tungeweza kumuenzi vizuri zaidi Mwalimu kwa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake na leo iwe siku ya majonzi na kusali kanisani lakini najua waliopanga hivyo walikuwa na sherehe zao moyoni.

Angalia tu jinsi nchi inavyoendeshwa baada ya kifo cha Mwalimu. Jibu lipo hapo.

Jasusi:

Kwani watoto wanaosubiri wazazi wafe hili warithi mali, si wanafurahi vifo vya wazazi wao? Unajua sifichi kuwa na siasa za mwalimu ni mbalimbali. Siupendi ujamaa. Lakini kuna mambo mengi nje na Ujamaa ambayo Mwalimu ni mfano mzuri hata kwa sisi makupe. Alikuwa mwenye ethics za utendaji kazi, mwenye kupenda elimu, mwenye kujali watu n.k

Basi na theme ya sikukuu yake, iwe kujikumbusha mambo yake.

Z10
 
Mzee Edwin,
Kweli mawazo mazuri lakini sidhani kama huu ni utamaduni wetu kwani Mila zetu baada ya kiongozi au mtu muhimu ndani ya Familia kuondoka basi sisi wananchi au watoto wake huadhimisha siku ya kufa kwake kwa Ibada..Sherehe zote za Birthday huisha siku mtu anapofariki kwa sababu hii ni sherehe ya Uhai wa mtu na ndivyo tulivyolelewa.

Kwa hiyo binafsi sioni tatizo kabisa kumuenzi mwalimu kwa kuadhimisha siku ya kufa kwake, kwani ndivyo wengi tunafanya kuwaenzi wazazi wetu isipokuwa sii kama walivyofanya huko Kigoma. Siku hii inge adhimishwa kwa sala na Ibada kote nchini kisha sherehe kubwa zingefanyika kitaifa Butiama kila mwaka ili kuweza kuweka maua ikiwa ni pamoja na gwaride la heshima kwake. Pengine kinachotakiwa ni hata kubadilisha ile sherehe ya siku ya Mashujaa na kuwa tarehe 14 kumuenzi mwalimu.

Kifupi binafsi sioni sababu kabisa ya kumu enzi mwalimu kwa siku yake ya kuzaliwa kwani hiyo haitakuwa mila yetu.. Hata hivyo tuzudi mumuombea mwalimu, tusipotoshwe na hizi kampeni za kisiasa.
RIP mwalimu...

Ivi unaposema ni mila zetu? Mila zipi hizo in such? Maana ninavyojua Tz as much as u wld like to, lakini haina mila moja, au utamaduni mmoja. Na hii mifano ya kuadhimisha siku ya kufa mtu ni nani hao wafanyao ivyo? au hata hizo birthday? Nadhani zote ni mila za kuazimwa, na hivyo i would side with mzee Mtei maana kama zote ni tamaduni za kuazima, basi ni bora kuazima hii ya kukumbuka mtu siku ya birthday yake badala ya siku ya kifo chake.
 
Kitu kingine ni kwamba, kuadhimisha siku ya Mwalimu Nyerere kwa Wafanyakazi wa serikali kutokufanya Kazi ni jambo lisilofaa kwa nchi yetu.

Baada ya hii siku ya Nyerere pia kuna siku ya Karume ambayo serikali ya CCM nayo imeona kuna haja ya Watu kutokufanya Kazi. Karume alifariki wakati Nyerere akiwa madarakani, lakini hajawahi kuadhimisha siku hii kwa kuwataka watu wasifanye Kazi. kwa hiyo ni dhahiri kwamba Nyerere asingeunga mkono watu kutokufanya kazi ili kuadhimishwa siku yake.

Nchi masikini kama yetu jambo hili linaumiza uchumi wetu, ni vyema basi tukaadhimisha siku ya Mwalimu Nyerere na Karume, kwa kufanya Kazi kwa bidii kwa wenye kazi zao, Kwa kujitolea kufanya shughuli za maendeleo kwa wale wenye wasaa kama vile kusafisha mitaa yetu, kupanda miti, kutembelea vituo vya watoto yatima, kutoa elimu ya uraia n.k
 
Mimi naona hata Serikali yenyewe ilishapoteza dira ya hii siku siku zote wanangoja tu ikifika tarehe 14 basi watafanya kumbukumbu kinafiki kwa kuwa kadri siku zinavyokwenda na ndio umuhimu wa kumuenzi Nyerere unavyopungua kwa kuwa wengine ndani ya CCM walifurahi siku alipofariki ili waweze kutimiza mambo yao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom