nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Na Sitta Tumma, Mwanza
MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), amezidi kumkaba koo Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, safari hii akitaka kiongozi huyo aondolewe pensheni yake, akidai kuwa anaitumia kwa maslahi ya chama chake cha CCM.
Nyerere aliingia kwenye mabishano na Mkapa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki baada ya Rais huyo kudai kuwa mwanasiasa huyo si mmoja kati ya wanafamilia wa Julius Nyerere.
Hata hivyo, siku moja baada ya Mkapa kutoa kauli hiyo, familia ya Nyerere kupitia kwa mwanaye Madaraka Nyerere, ilijitokeza na kusema Vicent ni mwanafamilia wao kwa vile ni mtoto wa baba mdogo wao, Kiboko Nyerere.
Toka wakati huo, Vicent amekuwa akimwandama Mkapa, akidai kuwa anatumia nafasi yake vibaya kama Rais mstaafu kwani anagharamiwa mafao yake ya uzeeni (pensheni) kutokana na kodi ya Watanzania wote.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mara baada ya kurejea kutoka Arumeru ambako chama chake kilitwaa kiti cha ubunge na yeye akiwa meneja kampeni msaidizi, Nyerere aliwaambia wananchi kuwa mpaka anapaswa kuiga mfano wa marais wenzake wastaafu.
"Mkapa anapaswa kuachana kabisa na ushabiki wa kisiasa Wakati wa chaguzi ndogo ikiwa ni pamoja na kukumbatia chama kimoja, wakati maisha yake anahudumiwa kwa fedha zetu wote, vinginevyo aondolewe pensheni ili abakie ‘mpiga debe' wa CCM," alisema.
Katika mkutano huo uliyohudhuriwa na mamia ya wananchi ukilenga kuzungumzia maendeleo ya jimbo na kujipongeza kwa ushindi wa Arumeru Mashariki, Nyerere alisema kuwa Mkapa kwa nafasi yake hiyo anapaswa awe mshauri wa vyama vyote na si kuipigia debe CCM.
"Akumbuke kwamba maisha yake yanaendeshwa na fedha za walipakodi wa Kitanzania hadi sasa, aache kabisa ubaguzi huo; atajenga chuki kubwa kwa wananchi," aliongeza.
Nyerere alilazimika kuzungumzia sakata lake na Mkapa baada ya wananchi kumwomba aelezee kidogo kauli ya kiongozi huyo ya kudai kuwa yeye si mwana familia wa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
Kuhsu miradi ya maendeleo jimboni kwake humo, Nyerere aliuagiza uongozi wa manispaa ya Musoma mjini kuhakikisha unamfungulia mashtaka mahakamani mmiliki wa kampuni moja ya Ngeja iliyopewa tenda ya kusambaza umeme katika soko la Kamunyonge, iwapo itafika kesho pasipo kuanza kusambaza nishati hiyo sokoni humo.
Alisema tayari manispaa ilimpa hundi ya fedha za malipo ya kazi hiyo na kwamba ameonekana kutaka kutapeli fedha hizo.