Nyerere Aponda Safari za nje Za Rais

Mimi kwa mawazo yangu raisi anatakiwa kusafiri zaidi ya anavyofanya sasa lakini si kwenye vilio au kuapishwa bali kwenye shughuli za maendeleo. Wizara ya Afya inategemea USA na Bill Gates Foundation, Wizara za elimu zinategemea Norway na Denmark, Barabara USA , Japan na China, IT na dawa India, Msaada kwenye shughuli za serikali EU sasa atawezaje kukaa wakati hatuna hata pesa za kuwalipa madaktari na walimu?.
Mkitaka Raisi akae nyumbani basi mnatakiwa kushinikiza yafuatayo (1) serikali ndogo ambayo haisaini mikataba mibaya, haijiusishi na kampuni kama Tanesco na ATC, yenye wafanyakazi wachache, kujitoa kwenye mikataba ya mashamba n.k (2) Serikali ikomeshe rushwa (3) Serikali ifanye marekebisho ya muhimu kama bank system,
 
Mie hotuba ile nimeisikia pia,.....ila kuna kitu mleta hoja hajakisema.....
Nyerere alisema hivi raisi yeyote anaehangaika kuombaomba na anajisifu kwa kuomba (kumbuka JK alisema anaenda kuhemea) ..huyo ni raisi MJINGA.
Akaongeza haiwezekani kendeleza nchi kwa namna hiyo!
NB: Kwa maoni haya tunayotoa nina shaka kubwa kama leo watarudia hotuba ile.....huenda hata alieiweka akaadhibiwa!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sawa kauli ya mwalimu haipaswi kupuuzwa lakini kila zama na kitabu chake...kuna mambo ya Nyerere ukiyafanya leo wakati wa utandawazi kwa kujifungia ndani ya nchi eti unatuma tu wawakilishi hakika unaowatuma watakudanganya siku moja. Enzi za mwalimu hata viongozi wa chini walikuwa hawasafiri sana hivyo ilikuwa sio rahisi kumdanganya. hivi sasa ni utandawazi ni ama kuchagua kuwapa ruksa wasaidizi wako waende nje na kuja kukushauri Rais ukiwa ndani au kuchagua kupewa majibu ya uongo na wasaidizi katika masuala ya msingi.

Moja katika sifa za utandawazi ni kurahisisha mawasiliano kwa sababu ya maendeleo ya teknolojia; sasa kama ni hivyo mawasiliano yanapunguza kabisa haja ya watu kusafiri safiri kwani kuna njia nyingi na rahisi za watu kuweza kuwasiliana na kufanya maamuzi kwa bei rahisi!! Viongozi hawana ulazima wa kusafiri ili kuongea ana kwa ana kwani kuna teknolojia inayowawezeshs kufanya vivyo kama vile video-conferencing na nyingine. Hakuna sababu ya kiongozi kuwatuma wasaidizi wake kwenda kokote na kuletewa uongo kwani taarifa sahihi zote anaweza kuzipata kiongozi mwenyewe kiurahisi.
 
Nyerere alipata fursa adimu ya kutuongoza Watanganyika na kisha Watanzania kwa takriban miaka 25. Cha kushangaza ni kwamba hayo yoote uliyoyataja na mengine mengi ambayo hukuyataja Nyerere aliyafanya. Likiwamo hilo la safari nyingi za nje kutembeza bakuli (omba omba) na kama ilivyo kawaida ya omba omba, kuna sehemu alipewa na kwingine aliambulia patupu. Kwa hiyo hoja yako dogo haina msingi.
Hata kama Nyerere alipewa 25 uninterrupted years ya uongozi pasi na mafanikio ya kuridhisha, haiondoi validity ya alichokiongea. Hakuna muunganiko.
 
Nikweli ata mie nilisikiliza hiyo hotuba nikafikiri kwanini hotuba km hizo zisiwekwe kwenye vipindi vya habari saa mbili kabla na baada ya habari hii itasaidia kua km miongozo ya uongozi kwetu......mie nadhani aache kusafiri ili tuone km tutakufa na njaa zaidi ya kutufanya tudharaulike kwa kiasi kikubwa.......mie binafsi napinga hii sera ya kuombaomba ajaribu kuona ata rais wa mozambique hua anasafiri mara ngapi kwa mwaka,aje RWANDA,BURUNDI,DRC, KENYA na UGANDA then ahesabu yeye kasafiri mara ngapi na watu aliosafiri nao na gharama zake alizofuja nadhani atasikitika sana kwani alichoomba na kupewa kinaweza kua kidogo kuliko gharama anazofuja za usafiri na posho wanazolipana........(JK) JANGA la KITAIFA
 
Wakati wa uongozi wa baba wa taifa watawala wetu hawa walikuwepo na walikuwa na vyeo mbalimbali tuu.
Wameamua kufumba macho na wanakauli mbiu yao kuwa "kila zama na kitabu chake" lakini wanasahau kuwa mpaka leo hii tuna soma na kufuata misahafu ya dini, tulikuta na tutaiacha.
Mungu yupo atawasikiliza wanyonge siku moja.
 
Kama ilikuwa hujuwi acha nikufahamishe. Safari zao za nje ni kisingizio tu kuomba misaada. Huwa wanakwenda kuwekeza na kukaguwa miradi yao ya nje. I have been there and I know this is true.
 
Ili kuongoza kizazi cha utandawazi ni lazima Rais aujue na kuuelewa utandawazi. kwa kukaa ndani ya nchi ni kupitwa na wakati kwani utandawazi unakimbia kwa kasi ya ajabu
Wamerakani na nchi za magharibi zilizoendelea wanawachukia wachina kwa kuiba teknolojia zao. Hii inatokana na Rais wa china kusafiri mara kwa mara kwenda ktk nchi hizi ili kujua utandawazi unaendelea ndani ya mataifa haya na hatimaye kuuhamishia china.
 
sawa kauli ya mwalimu haipaswi kupuuzwa lakini kila zama na kitabu chake...kuna mambo ya Nyerere ukiyafanya leo wakati wa utandawazi kwa kujifungia ndani ya nchi eti unatuma tu wawakilishi hakika unaowatuma watakudanganya siku moja. Enzi za mwalimu hata viongozi wa chini walikuwa hawasafiri sana hivyo ilikuwa sio rahisi kumdanganya. hivi sasa ni utandawazi ni ama kuchagua kuwapa ruksa wasaidizi wako waende nje na kuja kukushauri Rais ukiwa ndani au kuchagua kupewa majibu ya uongo na wasaidizi katika masuala ya msingi.
Siyl kweli. speech hii ya Nyerere bado ni valid hata kwa wakati wa sasa. Tena ni valid zaidi katika wakati huu ambao unaweza kupata na kufuatilia chochote kinachoebdelea dunian kupitia kiganja cha mkono. Unaweza j
kuhutubia na kutoa speech katika mkutano wa kimataifa ukiwa Ngudu au Matombo. Tukubali tu JK hana jipya na alichukua nafasi ya Uraisi akiwa hana ajenda wa fikra mpya. Ni dhaifu asiyekuwa na mfano. Ni mroho anayependa cheap popularity. Anajisifu eti anapewa msaada badala ya kusikitika.
 
Ili kuongoza kizazi cha utandawazi ni lazima Rais aujue na kuuelewa utandawazi. kwa kukaa ndani ya nchi ni kupitwa na wakati kwani utandawazi unakimbia kwa kasi ya ajabu
have your sit daughter, time for porojo is out! It is time for grownups to discuss great matters. Enjoy a good sleep. We can talk now and let the mama porojo sleep
 
Nyerere ndio aliotufanya mpaka leo tuwe maskini. Aliwaweka watu kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, aliingiza nchi vita vya uganda tukatumia rasilimali zetu zote, aliwafukuza watu wenye akili ili abakie na mazuzu awatawale vizuri, alitumia rasilimali zetu kukomboa nchi zingine ambazo baadae hata shukurani hawana . Hana na nyie endeleeni kuonyesha ubaya wa Nyerere..........................

Kama unaongea kwa ajili ya propaganda za kumchafua mwalimu tu, sawa sikulaumu.
Vita tulipigana watanzia tu hapa duniani? mbona wengine walipigana juzi tu .... na wamepiga hatua kutuzidi!
Ulitaka Nyerere akufanyie nini cha zaidi angetangaza kuwa Kikwete ni BABA MDOGO wataifa?!

Ila kama huo ndiyo mtazamo wako baada ya kufikiri sana...pole kwani wewe una ubongo mdogo kuliko wa Sisismizi!!
 
Nyerere ndio aliotufanya mpaka leo tuwe maskini. Aliwaweka watu kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, aliingiza nchi vita vya uganda tukatumia rasilimali zetu zote, aliwafukuza watu wenye akili ili abakie na mazuzu awatawale vizuri, alitumia rasilimali zetu kukomboa nchi zingine ambazo baadae hata shukurani hawana . Hana na nyie endeleeni kuonyesha ubaya wa Nyerere..........................

Kwa hiyo ndiyo maana bado uko hapo kwa sababu wewe hukufukuzwa, eh?
 
mama polojo vipi,huelewi maana ya utandawazi?yaani kwenda nchi za ngambo ndio utandawazi.hata kama unamlinda raisi sema fact,sio ubabaishaji,lakini yaweza kuwa ndo mwisho wa uelewa wako juu ya utandawazi.busaGARA man
 
mama polojo yaani hujui maana ya utandawazi?hata kama ni kumtetea raisi sema fact,au ndio mwisho wa uelewa wako.
 
Ili kuongoza kizazi cha utandawazi ni lazima Rais aujue na kuuelewa utandawazi. kwa kukaa ndani ya nchi ni kupitwa na wakati kwani utandawazi unakimbia kwa kasi ya ajabu

Ama kweli Mama Porojo! Utandawazi hauhitaji face-to-face contact- angalia tunachofanya hapa! Ni vyema Raisi akajiwekea vipaumbele! Angalia kule Davos- maraisi waliotaka Africa ni Zuma na JK tu! Unakumbuka walipokutana mara ya mwisho, ZUMA alivyoonyesha umahiri wa kuchenza ngoma za utamaduni? Nchi zingine zimetuma Prime Minsiters, kwa nini? Pengine ili kushughulikia mambo mengine nyumbani!

Kweli mgomo wa madaktari upo- usingetegemea Raisi atoe neno- walau awepo na kuagiza kufanyika kitu! Kule anaenda kuomba? Anakwenda kuomba madaktari waje wachukue nafasi za hawa ambao wamegoma? KIPAUMBELE!

Lakini pia ni vizuri tukajivunia utanzania wetu- na hili ni through SELF RELIANCE, TUSIWE KUPE!
 
sawa kauli ya mwalimu haipaswi kupuuzwa lakini kila zama na kitabu chake...kuna mambo ya Nyerere ukiyafanya leo wakati wa utandawazi kwa kujifungia ndani ya nchi eti unatuma tu wawakilishi hakika unaowatuma watakudanganya siku moja. Enzi za mwalimu hata viongozi wa chini walikuwa hawasafiri sana hivyo ilikuwa sio rahisi kumdanganya. hivi sasa ni utandawazi ni ama kuchagua kuwapa ruksa wasaidizi wako waende nje na kuja kukushauri Rais ukiwa ndani au kuchagua kupewa majibu ya uongo na wasaidizi katika masuala ya msingi.
Umepotea "kichakani" na kukosa mantiki iliyoletwa jamvini..Elewa alichosema Nyerere na sio utaratibu wake wa uongozi au wa Kikwete. Pia uelewe kwa sasa teknolojia imetuwezesha kupunguza safari na sio kinyume chake Kama unavosema. Umeshasikia "video conferences,Skype" n.k..?
 
a
Nyerere ndio aliotufanya mpaka leo tuwe maskini. Aliwaweka watu kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, aliingiza nchi vita vya uganda tukatumia rasilimali zetu zote, aliwafukuza watu wenye akili ili abakie na mazuzu awatawale vizuri, alitumia rasilimali zetu kukomboa nchi zingine ambazo baadae hata shukurani hawana . Hana na nyie endeleeni kuonyesha ubaya wa Nyerere..........................

Huyu mzee ameondoka madarakani zaidi ya miaka 25 iliyopita na amekufa zaidi ya miaka kumi iliyopita ni upuuzi na ukosefu wa upeo kumlaumu kwa matatizo ya sasa hivi.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom