Nyerere alitoa wapi uwezo ule?

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Pamoja na mambo mengi kwenda ndivyo sivyo hapa TZ lakini hakuna Kiongozi yoyote wa zamani mwenye uwezo wa kukemea nchi isiangamie, nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini? Nimepata jibu kwamba japo hakuna mtu mkamilifu kabisa 100% lakini Mwalimu Nyerere alikuwa mtu safi ndio mana hakuogopa kusema pale alipoona ndivyo sivyo.

Ari hiyo hakuna aliyenayo sasa kwani kila mmoja akijaribu anaogopa kuambiwa mbona na wewe......................................................

Wana JF kweli si kweli? kama si kweli nani anaweza kuvaa kofia ya Mwalimu Nyerere?
 
Kweli alikuwa shupavu, kwenda kupindua Zanzibar Jan 11 kuamkia 12 mwaka 1964 we unafikiri mchezo?
 
Mashirika mengi ya umma yalikufa enzi za Nyerere...! Na wale waliyo yauwa wakaamishiwa kwenye mashirika mengine.

Tukaanza panga foleni kwenye maduka ya kaya.

Kweli alikuwa shupavu na alijuwa kuwalinda watu wake.
 
tatizo sio nyerere la bongo tatizo ni kila mtu kwa nafasi yake tumesahau kujenga nchi na wananchi wake kila mtu amekua akiangalia tumbo lake hapa cha muhimu mkuu wa nchi angeanza kwa kuonyesha mfano wa uwajibikaji yeye mwenyewe then baraza lake la mawaziri pamoja na viongozi wote anaowateua rais mimi naona jamaa angekua mkali na muwajibikaji kuanzia ngazi za juu haya yote yasingekua yanatokea leo hii tatizo kubwa kwamba mkuu mwenyewe hawajibiki ndio maana unaona hata hawa wachini hawapo makini yaani ukiritimba kila idara watu wanalia majungu maofisini ndio usiseme!
 
Alikuwa akiona mbali,, ila watu wake hawakumpa ushirikiano wa kutosha,,
ndo maana unaona haya yote yanatokea.
suala ni usafi kuanzia moyoni mwa mtu.

ila binadamu si mkamilifu 100%
 
X-PASTER......!
mashirika mengi yalikufa kipindi au awamu ipi?
UFI,KIUTA,ELIMU SUPPLY,ZZK,URAFIKI,KAMATA,UDA,KAURU,PRINTPAK,KIBUKU,KAUMU,KAUDO,MWATEX,TACOSHILI,TIPER,ATC,TRC,MAHOTELI(kilimanjaro hotel,new africa hotel,mwanza hotel,moshi hotel,seventy seven hotel,mount meru hotel,...) CO-CABS,N.M.C, NDC,NBC,THB,TIB,TIMU ZA MASHIRIKA(ushirika moshi,nbc mbeya,reli morogoro,rtc kigoma,sigara,bandari mtwara,kurugenzi dodoma,ujenzi rukwa,plisner,ndovu ya arusha/now AFC, ),RANCHES,MUTEX,...........PUGU ROAD ILIKUWA INDUSTRIAL AREA KARIBIA VYOTE VILIKUWA VYA SERIKALI
X-PASTER UNASEMAJE?
 
Are you serious mkuu!?
I should ask you if you're serious.

Sasa wewe unataka kumfananisha Nyerere na nani, Mkapa? Mashirika yote aliyoanzisha yalikufa wakati wa Mwinyi. Nchi ikakosa misimamo na mwelekeo wewe uliza nchi zote zilizoendelea zina misimamo, zinajua kusema 'no' pale ambapo maslahi yao yasipotekelezwa. Wakati wa Nyerere nchi ilikuwa inamalengo na wakubwa wa magharibi walikuwa wanajua hilo ndio maana walihakikisha baadhi ya mambo yake hayakufanikiwa.

We angalia tuu idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ilivyoongezeka baada ya yeye kung'atuka. Sasa ni nani unataka kumfananisha na Nyerere katika hao viongozi waliomtangulia? Nyerere alikua binadamu kama mimi na wewe na alikose mengi tuu lakini alikuwa mwadilifu na alitekeleza alichoahidi. Au wewe unafurahi kuona magorofa kariakoo na vijigari vingi ukidhani ndiyo maendeleo, du kweli tuna safari ndefu.
 
Mkuu kweli kabisa mashirika yote yamekufa wakati wa Nyerere, siasa ndio ilikuwa inatumikia uchumi wetu kwenye mashirika hayo kulikuwa na vikundi vya ngoma, kwaya, siasa, mpira, sarakasi, maigizo. vyote vinatumia pesa ya mashirika ya umma
 
Hakuna mwingine wa kumfananisha naye kama jakay kiwete ameweza kuvaa viatu vyake haswaaa kama mnavyoona neema zinavyotuneemesha watz chini ya uongozo wake shupavu
 
We want to push our won problems to other people as if they are concerned! Nyerere was a great man and his actions showed what he meant by being the leader....hawa wapiga story tulionao kila la kheri mtafika muendako
 
I should ask you if you're serious.

Sasa wewe unataka kumfananisha Nyerere na nani, Mkapa? Mashirika yote aliyoanzisha yalikufa wakati wa Mwinyi. Nchi ikakosa misimamo na mwelekeo wewe uliza nchi zote zilizoendelea zina misimamo, zinajua kusema 'no' pale ambapo maslahi yao yasipotekelezwa. Wakati wa Nyerere nchi ilikuwa inamalengo na wakubwa wa magharibi walikuwa wanajua hilo ndio maana walihakikisha baadhi ya mambo yake hayakufanikiwa.

We angalia tuu idadi ya wasiojua kusoma na kuandika ilivyoongezeka baada ya yeye kung'atuka. Sasa ni nani unataka kumfananisha na Nyerere katika hao viongozi waliomtangulia? Nyerere alikua binadamu kama mimi na wewe na alikose mengi tuu lakini alikuwa mwadilifu na alitekeleza alichoahidi. Au wewe unafurahi kuona magorofa kariakoo na vijigari vingi ukidhani ndiyo maendeleo, du kweli tuna safari ndefu.

nakubaliana sana nawewe mkuu. Kwan sasa hakuna kiongozi ambaye yupo teyari kusema hapana. Wote wao ni maslahi yao tu. Kwan nakumbuka kipindi cha Nyerere mambo yalikuwa safi hatakama wengi wakimlaumu kwa kubana sana lkn nazani alikuwa na mtazamo chanya na mawazo ya mbele sana kuliko hawa viongozi waliofatia. wewe unawezaje kusema "soko Huria" hivi unaweza kwenda marekani au UK na kuanzisha kampuni yako wewe mtz? au tunadanganyana tu hapa. Hakuna hata sera ya kumlinda mtz na mazao yake au bidhaa zake. Tume huza benki zetu, makampuni yote tumeua leo mnataka kuchimba uranium kwa faida ya nini? mbona mm siwaelewi. Nitamkumbuka sana Nyerere maisha yangu yote na kumsifu kwa uongozi wake bila kuogopa chochote. Nani hapa tz anaweza simama umoja wa mataifa nakusema kwamba matatizo tuliyo nayo nisababu yawao wazungu nani nasema nani hapo?

Nyerere, Sokoine na wote mashujaa wetu R.I.P
 
Alikuwa anamwogopa Mungu hawa jamaa tulonao ni kama atheists wala hawaogopi chochote!
 
Sera zake mbovu alizo siasisi ndio zimeimaliza nchi hii. Aliposhindwa baada ya kutawala zaidi ya miaka ishirini na kushuhudia kila kitu kikishindwa na maji yapo shingoni, yanakaribia kuingia mdomoni, kiujanja ujanja na kiutu uzima akaamua kutoroka uongozi, ndio akamtupia Mwinyi kwa kusingizia kuwa anan'gatuka mapema...!

Soma Hapa: Natamani Kuishi Tanzania na si Tanganyika
 
Sera zake mbovu alizo siasisi ndio zimeimaliza nchi hii. Aliposhindwa baada ya kutawala zaidi ya miaka ishirini na kushuhudia kila kitu kikishindwa na maji yapo shingoni, yanakaribia kuingia mdomoni, kiujanja ujanja na kiutu uzima akaamua kutoroka uongozi, ndio akamtupia Mwinyi kwa kusingizia kuwa anan’gatuka mapema...!

Soma Hapa: Natamani Kuishi Tanzania na si Tanganyika

Alishasema mwenyewe, viongozi badala ya kuendeleza mema, wao wanaendeleza mabaya,
Alifikiri wangeona mabaya na kuyaepuka...lakini ni kinyume chake
 
Back
Top Bottom