Nyerere alishiriki Mauaji ya Kassim Hanga?

Status
Not open for further replies.
Unajua hawa watu hawajui kuwa Nyerere cheo chake alopewa,alipewa na Kanisa huko Roma,cheo hicho kwa kanisa kitabaki pale pale kwa faida aliowafanyia,lkn kwa upande wa znz ukimtaja Nyerere wamempa cheo cha Mkuu wa mauaji kwa raia wa znz. sasa mtajiuliza wenyewe, bado hapo wahindi wa bara wamempa cheo chake baada ya kutaifishwa mali zao, bado hapo waislam waTZ ukiwatajia nyerere he! hicho cheo walompa duh! utapigana baada ya kufanyiwa ukiritimba mwingi ikwemo kurudisha nyuma waislam kielimu,aliwahi kutamka huyu kijitu wakati wa mwanzo mwanzo wa utawala wake, alisema hivi.. KUNA MIKOA MENGINE KIELIMU WAKO MBELE ITABIDI TUWASIMAMISHE KWANZA HAWA ILI MIKOA MENGINE ILOKUWA NYUMA ISOGEE MBELE,ndo moja kwa moja. bado hapo mashekhe tunaowaju tu kibao wametoweka ktk mazingira ya kutatanisha na ushahidi upo wazi kuwa Nyerere ndio alowachukua,tafuta taasisi za kiislam watakupa ushahidi. bado hapo waTZ kwa jumla ukiwatajia wamempa cheo chake baada ya kuwapa watu mikate kwa kupanga foleni na vile vile baada ya kutuletea Fisadi Mkapa na watu wake walotumalizia nchi,hapo napo mbona patamu,duh! yapo mengi hayamaliziki.. bora tuache tu.
 
Marehemu Hanga hakuwa mbaguzi ndiyo maana alioa mke mzungu mwenye asilia ya kiyahudi na kirussia na wakajaliwa mtoto wa kike maarufu ktk media industry huko USA na Russia kwa jina Yelena Khanga (Hanga)'Yelena is the daughter of Abdullah Kassim, a former vice president of Zanzibar, and Lily Golden, a historian and educator. Her American maternal grandmother, of Polish Jewish descent, Yelena Khanga became one of Russia's best known celebrities | Black Women in Europe

Kuhusu Mwalimu Nyerere kutiwa doa na vifo vya kusikitisha vya Kassim Hanga na wengine wengi huko Zanzibar, pia kuna swali la kujiuliza iweje Mwalimu Nyerere pia alinusuru wengi wasikabiliwe na kifo mfano Abdulrahman Babu, Col. Ali Mahfoudh, Ali Sultan Ali na wengineo wengi
'After the revolution, Umma Party radical elements in the government (Babu, Khamis Abdalla Ameir, Ali Sultan Issa, Ali Mahfoudh, Salim Rashid, Badawi Qullatein, etc) were forging links with the ASP leftists (Abdallah Kassim Hanga. Abdulazizi Ali Twala, Hassan Nassor Moyo, etc.), and this might have scared Karume and other moderate elements within the regime ' IntelliBriefs: April 26, 2009

Pengine tutawafanyia haki marehemu wote na wengine walio hai kwa kusoma kitabu ' Race, Revolution and Struggle for Human Rights in Zanzibar- The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharriff Hamad. Memoirs hizi kinatupa habari za kina kuhusu siasa za Zanzibar na changamoto aliyoipata Mwl. Nyerere na Abeid Karume. Mwl. Nyerere akiamini maneno ya kiongozi mwenzie kuwa kina Kassim Hanga watapata haki mbele ya vyombo vya sheria huku wanamapinduzi wa Zanzibar kipindi hicho walivyochukua sheria mikononi mwao bila kufuata sheria.

Mwl Nyerere alijuta wanamapinduzi kumtoa uhai Kassim Hanga na hivyo akaamua kina Abdulrahaman Babu, Col Ali Mahfoudh na wengine wengi kutopelekwa Zanzibar.
 
Marehemu Hanga hakuwa mbaguzi ndiyo maana alioa mke mzungu mwenye asilia ya kiyahudi na kirussia na wakajaliwa mtoto wa kike maarufu ktk media industry huko USA na Russia kwa jina Yelena Khanga (Hanga)'Yelena is the daughter of Abdullah Kassim, a former vice president of Zanzibar, and Lily Golden, a historian and educator. Her American maternal grandmother, of Polish Jewish descent, Yelena Khanga became one of Russia's best known celebrities | Black Women in Europe

Kuhusu Mwalimu Nyerere kutiwa doa na vifo vya kusikitisha vya Kassim Hanga na wengine wengi huko Zanzibar, pia kuna swali la kujiuliza iweje Mwalimu Nyerere pia alinusuru wengi wasikabiliwe na kifo mfano Abdulrahman Babu, Col. Ali Mahfoudh, Ali Sultan Ali na wengineo wengi
'After the revolution, Umma Party radical elements in the government (Babu, Khamis Abdalla Ameir, Ali Sultan Issa, Ali Mahfoudh, Salim Rashid, Badawi Qullatein, etc) were forging links with the ASP leftists (Abdallah Kassim Hanga. Abdulazizi Ali Twala, Hassan Nassor Moyo, etc.), and this might have scared Karume and other moderate elements within the regime ' IntelliBriefs: April 26, 2009

Pengine tutawafanyia haki marehemu wote na wengine walio hai kwa kusoma kitabu ' Race, Revolution and Struggle for Human Rights in Zanzibar- The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharriff Hamad. Memoirs hizi kinatupa habari za kina kuhusu siasa za Zanzibar na changamoto aliyoipata Mwl. Nyerere na Abeid Karume. Mwl. Nyerere akiamini maneno ya kiongozi mwenzie kuwa kina Kassim Hanga watapata haki mbele ya vyombo vya sheria huku wanamapinduzi wa Zanzibar kipindi hicho walivyochukua sheria mikononi mwao bila kufuata sheria.

Mwl Nyerere alijuta wanamapinduzi kumtoa uhai Kassim Hanga na hivyo akaamua kina Abdulrahaman Babu, Col Ali Mahfoudh na wengine wengi kutopelekwa Zanzibar.

Alijuta ama alitaka iwe fundisho kwa wengine?

Maana uasitake kusema kuwa mwalimu hakufahamu kuwa wanamapinduzi wanauwa ila ni mara baada ya kifo cha Hanga!

Ingekuwa hafahamu vitendo vya kina Karume wakati anamkabidhi Hanga,then ningekubaliana na wewe.

Makosa aliyoyafanya huyo Hanga ni sawa na waliyoyafanya hao wengine alio waprotect!

Na kitendo cha ku mrally unawanjani mbele za umma wa wananchi kuwa ni mhaini kabla ya kumkabidhi ni a clear sign kuwa huyo apotezwe!

Kipindi cha mwalimu watu hata kuongea ilikuwa shida, kila mtu spy...Noma!lol

Unless there is something else Hanga did, then i am sticking to my earlier notion when i said something might be missing!
 
Nimefwatilia mjadala huu tangu ulipoanza siku chache zilizopita na nimeona nichangie kidogo hapa.

Wazanzibari na wengine mnao mlaumu Nyerere, soma yafwatayo kutoka kwa Ali Sultan Issa:

"Karume did not like people who were educated; he did not trust them, so most of those from the ASP who were imprisoned were educated, like Othman Shariff.

Shariff and Karume were rivals within the ASP before independence; after the revolution, Shariff was first appointed minister of education and then Tanzania's ambassador to the United States.

It is said that, on a visit to Tanzania, he was seen taking photographs of the State House, and that was enough for the RC to accuse him of being an imperialist stooge and a CIA spy trying to help the Americans take over.

The authorities arrrested him but released him after Nyerere intervened. He was reduced to serving as a veterinary officer in Iringa on the mainland.

Later, some members of the RC were sent to arrest him and bring him back to Zanzibar, but Nyerere intervened again.

They eventually convinced Nyerere to hand Shariff over, and once he arrived in Zanzibar, that was the end of him.

Abdallah Kassim Hanga was Russian-educated and very popular among younger ASP members. After the revolution, he was named vice president but, after the union, was transferred to Dar es Salaam.

Hanga eventually lost favor with Nyerere because he was very close to Kambona, Nyerere's minister of foreign affairs and defense. During the Tanganyikan army mutiny of 1964, it was Kambona who went to talk with the soldiers, while Nyerere remained in hiding.

After Kambona fell out with Nyerere and went into exile, Hanga lost favor, because he was so close to Kambona. After Hanga was removed from the cabinet, he went to live in Conakry, Guinea, because he had married a Guinean woman.

After some time, Nyerere sent a delegation to President Sekou Toure, asking him to convince Hanga to come back to Tanzania, where he would be safe.

Unfortunately, when he returned, he was arrested and publicly humiliated. At a rally at Mnazi Mmoja in Dar es Salaam, Nyerere had Hanga brought there in handcuffs.

Nyerere publicly insulted him and then later agreed to send him to Zanzibar, where Hanga was tortured and killed." - (Ali Sultan Issa, in G. Thomas Burgess, ed., "Race, Revolution and The Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad," Ohio University Press, 2009, p. 206).

Ali Sultan Issa anaendela hapa chini na kusema:

"The first trial was like a purge. a political case. The authorities just wanted to get rid of us, to execute the Umma elite.

They had a problem, however, in that Nyerere had arrested Babu and some Umma army officers in Dar es Salaam and refused to send them over to Zanzibar for what would have been certain execution.

When we discovered in our prison that Babu was sitting in a prison on the mainland and that we were going to be sent to court and not just taken out and slaughtered, we believed in our hearts that we would not be killed.

Aboud Jumbe, a man of some education, and not Karume or Seif Bakari, was now in power, and Babu was still alive. For this, I am actually very grateful to Nyerere.

Maybe he had learned his lesson after what happened with Hanga and Shariff; by refusing to hand over Babu and other prisoners, he saved us all from execution. Had he handed them over, we would have all perished, all of us together. But Jumbe and his government thought, 'How can we kill them all, when the leader of the consipracy is safe on the mainland?'" - (Ali Sultan Issa, ibid., pp. 139 - 140).

Kambona na Hanga hawakuwa marafiki tu. Walikuwa na mpango wa kuwa viongozi wa Tanzania baada ya kupindua serikali - Kambona akiwa raisi wa Muungano na Hanga raisi wa Zanzibar. Walinaswa kabla ya kufanikiwa.

Pia Kambona alipo ondoka Tanzania mwezi wa Julai 1967 (nilikuwepo nyakati hizo lakini sikumbuki tarehe), hakutoroka. Usalama wa Taifa walijua kila kitu na Nyerere angetaka, angewaamuru wamkamate hata kabla ya kufika Moshi. Usalama wa Taifa miaka ile ulikuwa macho saana - amini, usiamini, na Kambona asingeweza hata kidogo kutoroka. Nyerere mwenyewe alipolihutubia taifa, alisema mwache, let him go.

Nilikuwa kortini, High Court, karibu kila siku wakati wa kesi ya uhaini mwaka 1970. Walikuwa na mpango wa kupindua serikali mwezi wa October 1969. Katika mpango huo, walitaka pia kumuua Nyerere, siyo kupindua serikali tu, na kiongozi wao alikuwa ni Kambona. Nakumbuka Senior State Attorney Nathaniel King kutoka Trinidad alipomwambia John Lifa Chipaka, "You wanted to eliminate the president." Chipaka alimjibu na kusema, "Yes, eliminate him, politically, not phyiscally."

Nakumbuka pia Nathaniel King alipocheka baada ya Chipaka kusema hivyo, na akaja na ushadi wake mzito.

Kulikuwa na ushahidi wa kila aina uliotolewa kortini kuonyesha kwamba walikuwa na mpango wa kupindua serikali na kumuua Rais Mwalimu Nyerere.

Hata hivyo, Nyerere aliwasamehe watu waliotaka kumpindua na kummaliza kabisa. Halafu kuna watu wanao mlaumu na kusema kwamba alihusika na mauaji ya Hanga, Shariff na viongozi wengine.

Angejua kwamba Karume atawamaliza baada ya kurudishwa visiwani, asingewarudisha Zanzibar. Hata Ali Sultan Issa alimshukuru Nyerere na kusema wasingekuwa hai bila Mwalimu ku intervene.

Nyerere alikataa kumrudisha Babu na wenzake Zanzibar ingawa walikuwa na mpango wa kumpindua Karume na ingawa Karume aliuawa kutokana na mpango huo.

Ali Sultan Issa amesema mastermind wa kumpindua Karume alikuwa ni Babu pamoja na Ali Mahfoudh. Amesema pia kwamba ni Mahfoudh aliyewachagua watu waliokwenda na silaha makao makuu ya ASP wakati Karume alipokuwa anacheza karata na wenzake.

Amesema Babu na Mahfoudh na wenzao waliotaka kumpindua Karume hawakuwa na nia ya kumuua. Nia yao, kutokana na kauli ya Ali Sultan Issa, ilkuwa ni kumkamata na kumpeleka redioni ambako angelazimishwa kusema kwamba anajiuzulu. Ali Sultan Issa alisema hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana upande wa Babu na Mahfoudh kwa sababu - Karume hakuwa mtu wa aina hiyo. There is no way Karume would have gone on the radio to say something like that, kwamba anajiuzulu, according to Ali Sultan Issa. He just wasn't that type of person.

Lakini mpango wao haukuenda kama walivyotegemea. Mtu aliyempiga risasi Karume, according to Ali Sultan Issa (amemtaja lakini nimesahau jina lake), alifanya hivyo kwa uamuzi wake na siyo kutokana na maagizo ya Mahfoudh na Babu. Amesema aliamua kumuua Karume kwa sababu Karume alimuua baba yake.

Whatever the case, ukweli ni kwamba Babu na Mahfoudh walikuwa ndiyo mastermind wa kumpindua Karume. Lakini hata baada ya Karume kuuawa, na hata baada ya Nyerere kujua kwamba ndiyo hao waliokuwa na mpango wa kumpindua Karume, Nyerere alikataa kuwarudisha Zanzibar where they definitely would have been executed. Ingawa walikuwa ni mastermind, Nyerere alikataa kuwarudisha visiwani.

Huyo ndiyo kiongozi ambaye kuna watu wanasema alihusika na mauji ya Hanga na wengine.

Nyerere ni binadamu, alifanya makosa kama binadamu wengine. Lakini msije kuongopa hapa na kusema Nyerere was a murderer. That's a downright lie. He was NOT a murderer.

Even Kambona would not have stayed alive aliporudi Tanzania if Nyerere was a murderer. Kambona was the mastermind of the October 1969 coup attempt who also wanted to assassinate Nyerere in that coup - yet Nyerere left him alone after he returned to Tanzania.

Kuna viongozi wangapi katika bara letu wenye moyo wa aina hiyo?

Kumbuka, Nyerere still had a lot of power hata baada ya kuondoka madarakani. If he wanted Kambona arrested or dead, nobody could have stopped him from using his influence to achieve his goal.
 
Hivi Obama anaendesha utawala wa serikali kibabe na kutoheshimu haki za watu? Nyerere alishiriki vipi katika mauaji ya Hanga? Je, Rais wa Marekani anapokataa kutoa reprieve kwa mtu aliyehukumiwa kunyongwa na mtu akanyongwa je anakuwa ameshiriki katika mauaji yake?

Binafsi sijaona kitu chochote ambacho kinawezakutafsiriwa kuwa:

a. Kilikuwa ni kinyume cha sheria
b. Nyerere alifanya mafichoni - as a matter of fact tunaoneshwa na picha na polisi wako karibu na hanga na nadhani kuna mtu aliyekaa hapo chini ambaye wengi hawataki kumtaja kwa jina
c. Na hakuna anayetaka kusema ni nani alikuwa na culpability kati ya Karume na Nyerere.

Hakuna mahali popote ambapo mtu anaweza kuonesha kuwa Nyerere alivunja sheria aidha kwa maamuzi yake kuhusu suala la Hanga au vinginevyo. Zaidi ni suala la hisia na vionjo vilivyoumizwa. Tunataka viongozi ambao wako tayari kusimamia na kulinda taifa kwa gharama yoyote ile.
 
Wakuu zangu,
Leo imenibidi niingilie mjadala huu ambao kwa kina unakera. Ni ukosefu wa nidhamu unaotokana na Ujinga (kutosoma) kwani mnaposema Nyerere alihusika na MAUAJI ya Hanga hii ni dhahiri kabisa hamjui mnachozungumza. Mnashindwa kuelewa mzigo wa chuki na unafiki wenu wenyewe kiasi kwamba serikali ya Zanzibar ikamtaka hata Salim A. Salim kesho based on extradition act kisha wakamwondoa itasemekana Kikwete na CCM wamehusika.

Kwanza nakumbuka mahala nimeandika kwamba kuna Historia mbili ambazo serikali yetu kwa makusudi waliacha kuziwekea kumbukumbu kwa sababu maalum ambazo sisi kama raia wa nchi yetu tulihitaji sana kuziwekea maanani. Nazo ni 1. Uhuru wa Tanganyika na 2. Mapinduzi ya Zanzibar. Sasa maadam wengi wenu hapa hamfahamu Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ila kwa kupitia wazushi waliodandia Mapinduzi hayo -ASP au kupitia ZNP ni vigumu sana kuelewa kwa undani usiri ulojificha ambao wahusika wakuu pekee ndio wanaweza kuandika Upya historia hiyo.

Tukirudi nyuma, kihostoria Kassim Hanga (ASP) alikuja kuwa kiongozi wa chama cha Ushirika (African trade Union) ambacho muasisi wake alikuwa Abrahman Babu wa ZNP alipotoka UK masomoni. Kulikuwa na ushirikiano mkubwa sana baina ya Hanga na Babu hadi kufikia Mapinduzi ya mwaka 1964, hivyo kama wewe unapinga Mapinduzi ya Zanzibar hawa ndio watu wa kuwalaumu..Na kama unalaani mauaji ya Mapinduzi, hawa ndio watu wa kuwalumu lakini isije kuwa mzigo wenu (kimba) mnataka kuutua bara.

Maajabu ya Wazanzibar siku zote wameshindwa kuelewa historia yao wenyewe kwamba toka karne na karne wamekuwa nusu kwa nusu kupinga au kuunga Upande mmoja uwe wa Sultan au Wazalendo. Hivyo hata kuondoka kwa Abrahman Babu ZNP na kuanzisha Umma Party ni katika msuguano wa fikra hizi za kibaguzi baina yao. Pia Kassim Hanga kwa upande ASP alikuwa anti Arabs kabisa, na yeye hakuafiki mambo mengi ndani ya uongozi wa ASP kuhusiana na waarabu. Kassim Hanga alikuwa mkomunist kama Babu,hivyo hata baada ya Mapinduzi huyu jamaa alikuwa pamoja na Umma Party bega kwa bega akiwakilisha vyama vya Ushirika.

Mapinduzi yao hayakudumu akaingia Karume ambaye awali alikuwa akijaribu sana ASP kuungana na ZNP kuunda serikali ya mseto na akatolewa nje na Shamte, hivyo Mapinduzi yalipokuja na wasiwasi ya Zanzibar kuwa kisiwa cha Ukomunist ndipo majasusi CIA, akiwatumia Nyerere na Karume walipoingilia kati na kuwaahadaa Umma party for a coalition government na protection ya Mapinduzi yale..Karume akachukua kiti kikubwa, Kassim Hanga from just a Union leader and member of ASP akachukua Makamu wa rais na Abrahman Babu kiongozi wa Umma Party kutupwa Waziri wa Mambo ya nje ktk serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

ASP (Karume) na Nyerere wakacheza karata kubwa kuunda Muungano wa Bara na visiwani, na baada ya Muungano tu wakuu hawa pamoja na viongozi wengine wote wa Umma party walitoswa..Hanga kapelekwa kuwa Balozi huko Guinea na Babu katupwa bara kama Waziri wa mambo ya ndani (Interior minister), kina Okello wakapigwa masaa 24 kupotea.. Huko Zanzibar chuki zaidi dhidi ya Umma party iliongezeka hadi kuwalazimu wengi kukimbilia bara kwa usalama wao..That was the end of Umma party lakini sii kwa wahusika..

Ikumbukwe tu kwamba chuki ya Mapinduzi ya Zanzibar haikuanza jana...Haya ya CUF na CCM ni marudio tu, Maipinduzi yaliwafuata Umma Party popote walipokuwa kwa sababu nusu ya Wazanzibar hasa wenye uwezo walikuwa pro Sultan na Uhuru wa mwaka 63 chini ya ZNP, na nusu nyingine hao walalahoi waliyafurahia Mapinduzi na serikali kurudi mikononi mwa Wananchi. Lakini kutoswa kwa viongozi wa Umma Party,Karume na ASP walikuwa hawalali.. it was a cold revolution hivyo Karume na ASP walikuwa makini sana kutumia coalition na chuki ya watu dhidi ya Mapinduzi to their advantage.

What Karume did siwezi kuyaweka hapa kwa uhakika isipokuwa ijulikane tu kwamba Uhasama baina ya Wazanzibar kiutawala ndio matokeo ya mauaji na unyama mkubwa ulotokea toka enzi hadi Kifo cha Hanga. Nitarudia tena kusema, chuki mpya baina yao ilizaliwa tena upya baada ya ASP kuchukua madaraka na kuwatosa Umma party hivyo haya maswala ya chuki hayakuanzishwa na Nyerere hata kidogo isipokuwa Nyerere mwenyewe alijiingiza katika mtihani mgumu ambao alifikiria itakuwa jambo rahisi sana kama Bara kuunganisha makundi ya watu kuwa kitu kimoja..Jamani eeeh huyo Salim Ahmed Salim hadi leo hapendwi huko Zanzibar na hakika akisimama kugombea Urais Zanzibar wanaweza kumwondoa vile vile ikasemekana JK kamwondoa..

Muungano wa aina yoyote ile ulionekana ni madhambi makubwa hivyo hata makubaliano haya baina ya CCM na CUF sidhani kama yataweza kudumu sana unless viongozi wa leo wamejifunza kutokana na historia lakini najua fika kuna mmoja atamzidi mwenzie akili..Na kibaya zaidi ni kwamba imetudhihirishia wazi kwamba interest za CUF ni Zanzibar sio bara kwani hakuna sheria inayoruhusu chama cha kitaifa kuweka muafaka wa uongozi kwa serikali moja ya Muungano wakati huo huo Kitaifa serikali hiyo haitambuliki kama nchi (maneno ya Pinda)..
 
MWENYEZI MUNGU ATAIHUKUMU DHULUMA HII ILIYOTENDEKA

Na William Shao

WASOMAJI wengi wa gazeti hili wameuliza maswali mengi wakitaka majibu. Miongoni mwa maswali mengi ni kutaka kujua hatima ya Kassim Hanga katika uchambuzi wa historia ninaoufanya.

Nawashukuru wote walionipigia simu na kunitumia ujumbe kuhusu mada hizi. Lakini napenda kuwaambia kuwa ni vigumu—na pengine haiwezekani—kupata majibu ya maswali yote wanayouliza wasomaji.

Tunao wanahistoria wengi makini wanaoweza kueleza mambo haya kinaganaga kuliko tunavyofanya katika makala za magazetini, lakini ama hawajapata jukwaa au hawako tayari kufanya hivyo.

Namuunga mkono Issa bin Nasser kwa aliyosema katika kitabu chake, ‘Zanzibar: Kinyang’anyiro na Utumwa’. Aliandika: “Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote.” Sentensi inayotangulia maneno hayo, ambayo ndiyo imenikopesha maneno ya kichwa cha habari ya mada hii, inatia uchungu hata zaidi inaposomeka hivi: “…Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka…”

Naiandika mada hii kwa ufupi sana kutokana na ufinyu wa nafasi. Kassim Hanga alikuwa rafiki mkubwa wa kisiasa wa Oscar Kambona. Kama Kambona alivyopoteza nyadhifa zake katika siasa, ndivyo Hanga naye alipoteza nyadhifa zake katika Serikali ya Muungano wakati yalipofanyika mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri.

Hanga hakujua mambo mengi kuhusu Tanzania kama Kambona alivyojua. Baada ya kwenda Guinea, Hanga alihakikishiwa na Rais wa nchi hiyo, Ahmed Sekou Toure, na Nyerere wa Tanzania, kwamba angekuwa huru na salama akirejea nchini. Hanga alirejeshwa Tanzania kutoka Guinea.

Hanga hakuuona uhuru alioahidiwa na, badala yake, Desemba 1967 alikamatwa kwa tuhuma za uhaini. Alipohoji sababu ya kukamatwa alijibiwa kuwa alikula njama za kuwarubuni maofisa wa jeshi ili aweze kuiangusha serikali ya Sheikh Abeid Karume.

Katika mahojiano aliyoruhusiwa kufanyiwa akiwa rumande, kwa mujibu wa jarida Africa Confidential, Hanga alikana kuhusika kwa vyovyote katika kula njama na maofisa wa jeshi na akasisitiza kwamba siku zote jitihada zake zilikuwa ni katika kutaka kuwapatanisha Kambona na Nyerere.

Mapema mwaka 1969, Kassim Hanga aliachiwa huru kutoka rumande. Badala ya kurejea Zanzibar, aliondoka na kwenda kuishi katika mojawapo ya nyumba zilizomilikiwa na Kambona mjini Dar es Salaam ambayo ilikuwa bado kutaifishwa.

Lakini matatizo yake na serikali za Tanganyika na Zanzibar hayakuwa yamemalizika. Kuna Watanzania ambao hawakuridhishwa na hali ya kisiasa nchini. Miongoni mwa mengi waliyohoji ni suala la Kassim Hanga na ‘udikteta wa Zanzibar’ wakidai kuwa Karume hakutaka uchaguzi kufanyika Zanzibar.

Baada ya kupinga sana sera za serikali, Oktoba 1968, wabunge kadhaa walitimuliwa Bungeni na baadhi ya watu wengine wakakamatwa na kutiwa kizuizini. Hawa walikuwa ni pamoja na Eli Anangisye, Joseph Kasella-Bantu, Christopher Kassanga Tumbo, Ndugu Choga, Ndugu Bakampenja na Ndugu Kaneno.

Taarifa za watu kutiwa kizuizini zilipochapishwa katika gazeti Daily Nation (Okt. 2, 1968) la Kenya, serikali ya Tanzania iliamuru kukamatwa kwa mwandishi wa Kitanzania aliyevujisha habari hizo, Melek Mzirai Kangero.

Baadaye ikajulikana kuwa Hanga na Othman Sharif walikamatwa mjini Dar es Salaam kutokana na shinikizo la Karume aliyewataka watu hao kwa gharama zozote—hata kama ni kwa kuuvunja Muungano.

Othman Sharif, msomi kutoka Chuo cha Makerere, alikuwa mmoja wa waasisi wa Afro-Shirazi na kiongozi wa chama Bungeni wakati Karume akishikilia Urais wa chama.

Mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kudhani kuwa Othman alikuwa na tamaa ya mamlaka ya kisiasa na uwezekano wake wa kula njama za kuiangusha serikali yake, akisaidiwa na Nyerere, Karume alimwondosha Othman Unguja na kufanywa kuwa Balozi.

Kwanza alikuwa Balozi wa Tanzania mjini London, Uigereza, kisha akapelekwa Washington, Marekani. Wakati mmoja, inadaiwa, Othman Sharif aliporudi Zanzibar kwa matembezi aliponyoka kuingia katika kucha za Abeid Karume.

Karume alianza kumwandama kama simba anavyoandama windo lake. Kuona hivyo, Nyerere aliingilia kati mara hiyo hiyo akidai kwamba Othman Sharif alikuwa Balozi wa Muungano wa Tanzania, na si Balozi wa Zanzibar.

Karume alipotambua kuwa hakuwa na mamlaka kisheria ya kumdhibiti Othman, alibadili mbinu ya kumtafuta. Nyerere alipogundua hilo alijaribu kufanya kila mbinu aliyoweza ili Othman asirudi Zanzibar.

Baada ya kupoteza wadhifa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mwalimu Nyerere alimpatia Othman kazi nyingine kwa kumteua kuwa afisa uganga wa mifugo mkoani Iringa.

Lakini hiyo haikumzuia Karume kumwandama hadi mkoani Iringa na, kwa mujibu wa kitabu ‘Conflict and Harmony in Zanzibar’, Karume aliwashawishi Wazanzibari watatu waliokuwa marafiki wa karibu sana wa Othman ili wamsaliti.

Watu hao walikubali. Wakafikishwa mbele ya Baraza la Mapinduzi, wakatoa ushahidi kwa kiapo na kudai kwamba ni kweli Othman Sharif alikula njama za kutaka kuiangusha serikali ya Karume. Watu hao walipelekwa kwa Nyerere na kurudia madai hayo hayo.

Wakati Nyerere anaelekea kuuamini huo ‘mchezo wa kuigiza’, tayari uhusiano kati yake na Karume ulianza kuingiwa na dosari nyingine. Muungano wa Tanganyika-Zanzibar ulikuwa majaribuni.

Hatimaye Nyerere akasema watu hao watapokea “hukumu ya haki” Zanzibar. Gazeti Ulimwengu (Nov. 19, 1967) katika tahariri yake liliandika kuwa lazima hukumu ya haki itolewe. Kisha likaonyesha kupinga suala la watu kuwekwa kizuizini.

Kama matokeo, mhariri wa gazeti hilo, Otini Kambona, alikamatwa. Hata ndugu yake Otini, aliyeitwa Mathias, naye alikamatwa kwa sababu nyingine tofauti kwa madai ya kushiriki katika njama za kuiangusha Serikali.

Kikundi cha viongozi kutoka mkoani Iringa, ambako Sheikh Sharrif alikuwa akifanya kazi, walimsihi sana Nyerere asiruhusu watu hao wapelekwe Zanzibar kwani walijua hatima yao.

Jawabu la Nyerere lilikuwa hivi: “…Hili si jambo la ubishi kwa sababu halina uzito wa kubishaniwa. Lakini kama kutakuwa salama, ni vizuri tukajua watu hawa watakuwa salama kiasi gani.” Lakini historia ni shahidi. Hakukuwa na usalama wa kiasi chochote. Wanadamu hawa walinyang’anywa haki yao ya kuishi.

Baada ya kuona kuwa mambo yameshindikana, na kwa kuwa Muungano wa Tanzania ndilo lililokuwa suala kuu katika akili yake, Mwalimu ‘alibwaga manyanga’. Septemba 1969 Nyerere akajikuta akiwapa idhini maofisa wake kuwatoa Kassim Hanga na Othman Sharif wakabidhiwe SMZ kama Abeid Karume alivyotaka.

Walipelekwa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Dar es Salaam (DIA), wakipewa maneno ya kuwafariji, na kisha wakasafirishwa kwenda Zanzibar. Hiyo ikawa ndiyo safari yao ya mwisho—angalau safari ya mwisho kutoka Dar es Salaam—tena, inadaiwa, wakiwa na wamefungwa pingu.
Huko ndiko walikokutana na mauti yao, pengine kwa kupigwa risasi—ingawa taarifa nyingine zilisema kuwa waliuawa kwa kuzamishwa katika maji. Lakini, kinasema kitabu ‘Conflict and Harmony in Zanzibar’, hata wale waliomsaliti Othman Sharif nao waliuawa mmoja baada ya mwingine. Machapisho mengine ya kihistoria yanaunga mkono madai hayo.

Katika hotuba aliyoitoa Oktoba 1969, ukiwa ni mwezi mmoja baada ya kufanyika kwa mauaji hayo, Abeid Karume alitangaza kuwa watu wanne waliokuwa wakila njama za kuiangusha serikali yake “…wameuawa kwa kupigwa risasi.” Hili alilikiri mwenyewe.

Vyanzo kadhaa vinasema kuwa Kassim Hanga, na aliyekuwa Waziri wa Elimu na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Sheikh Othman Sharrif, waliuawa Zanzibar na utawala wa Karume.

Hata hivyo mauaji hayo hayakuwa mwisho wa mambo. Inaelekea kuanzia hapo, au kabla ya hapo, kulijengeka utamaduni wa kuwakamata watu, kuwaweka kizuizini na hatimaye wengine kuuawa.

Zaidi ya watu kuwekwa kizuizini bila kufunguliwa mashitaka, kulikuwa na madai ya kuweko kwa zile kambi za mateso. Kwa mfano katika miaka ya 1960 na mwanzoni mwa 1970, inasemwa, Zanzibar kulikuwa na ile kambi iliyoitwa ‘Kwa Bamkwe’ au ‘Kwa Mandera’.

Mkoani Mwanza kaskazini mwa Tanzania kulikuwa na (kambi ya) Kigoto. Hiyo ni moja ya kambi zilizokuwa mbaya. Baada ya kuwakamata watu kwa tuhuma za uchawi mwaka 1977 katika maeneo ya Mwanza na Shinyanga, ikijumlishwa na matendo waliyofanyiwa watu hao, ilitosha kumfanya Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujiuzulu ‘kwa kuwajibika’.

Ingawa wengi walitarajia kuwa kuwajibika huko kungekuwa ndio mwisho wa Mwinyi katika siasa, Nyerere ‘alimpigia debe’ kuwa Rais wa Zanzibar (Jan. 30, 1984—Okt. 24, 1985) na hatimaye Rais wa Tanzania (Nov. 5, 1985—Nov. 23, 1995) kwa kura za NDIYO.

Kwa mujibu wa kitabu ‘Zanzibar: Kinyang’anyiro na Utumwa’, mwanasiasa aliyekuwa Unguja wakati mambo yote hayo yakitokea, Issa bin Nasser Al-Ismaily, anaandika kuwa mwaka 1970 Wazanzibari tisa “walitiwa nguvuni na Serikali ya ASP kwa kisingizio cha kutaka kuipindua serikali hiyo.”

Wazanzibari hao ni Salim Ahmed Busaidi, Abdallah Suleiman Riyami, Othman Soud, Aziz Bualy, Hemed Said, Muhammed Juma, Muhammed Hamza, Musa Ali na Said Hamoud.

Bila ya kufikishwa mahakamani, Karume aliwahukumu kutupwa gerezani na kupewa kazi ya kuchunga ng’ombe katika uwanda wa “Hanyagwa-Mchana”. Baada ya kifo cha Karume Aprili 1972, “wananchi hao waliuawa wakati wa utawala wa mrithi wa Karume, Aboud Jumbe.”

Kitabu hicho kinaomboleza hivi: “…Mwenyezi Mungu mwenyewe anaelewa namna ya kuihukumu dhuluma hii iliyotendeka…; kwani Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote.” Ni kweli kwamba “Mwenyezi Mungu ndiye mjuaji wa yote” kwa sababu hakuna mwanadamu atakayejua yote yaliyotendeka, hasa yale ambayo hayatajulikana kamwe.

********************************************************
William Shao ni mwandishi wa habari na mwandishi wa kitabu MIAKA 2000 YA UKRISTO: HISTORIA ILIYOPOTOSHWA. Anapatikana kwa simu 0754 989 837. E-mail: shao2020@yahoo.co.uk., Blog: willyshao.blogspot.com.
N.B msisitizo ni wangu.

Hapa kuna kitu kingine tunakipata kumbe Nyerere alikuw tayari kuubariki, kunyamazia, kusaidia, kuunga mkono moja kwa moja au kwa namna nyingine yoyote uhuni, ukatili na ushenzi wa Karume, kwa ajili ya kulinda Muungano.
Hapa tunapata picha zaidi kuwa Nyerere alipowaachia kina Babu na wenzake ilikuwa kwa kuwa hakukuwa na tishio la kuvunjwa muungano kama lililokuwapo wakati Karume yu hai na alitishia kufanya hivyo iwapo Nyerere asingetii matakwa yake ya kuitaka roho ya Hanga na Shariff...kwa hili msikatae Nyerere wa not accomplice but a murderer.
 
Shwari said:
Unfortunately, when he returned, he was arrested and publicly humiliated. At a rally at Mnazi Mmoja in Dar es Salaam, Nyerere had Hanga brought there in handcuffs.

Nyerere publicly insulted him and then later agreed to send him to Zanzibar, where Hanga was tortured and killed
." - (Ali Sultan Issa, in G. Thomas Burgess, ed., "Race, Revolution and The Struggle for Human Rights in Zanzibar: The Memoirs of Ali Sultan Issa and Seif Sharif Hamad," Ohio University Press, 2009, p. 206).
Nimekupata mkuu Shwari, shukran.

Ila nini haswa kilimfanya mwalimu akam rally na kumtukana mbele ya umma?Na baada ya hapo kummkabidhi kwa wauwaji?

Ama ni kweli mwalimu hakujua yatakayompata?

Je is it possible kutuwekea muda hapa ili tupambanue kama ni kweli mwalimu "alijuta" kumkabidhi?
 
Hivi kwanini habari yoyote inayohusu historia ya Zanzibar huwa haitolewe maelezo yakutosha? Vyovyote vile lazima siku moja makaburi yatafunuliwa tuweze kupata ukweli!

Ni nani alimuua Hanga and co.?
- Col Bakari?
- Karume?
- Nyerere?

Bakari.
 
Labda hili kanisa la hawa jamaa wa Uganda wanaweza kukusaidia hata mimi nashangaa sana.Bofya hapa

MICHUZI


Ati nasikia wewe ni MOD kule mzalendo bwa ha ha ha..mijadala hainogi kule mpaka muilete huku kwene 'vichwa'

Kama mod anapoor understanding kaa wewe hao wasomaji sijui wapo ktk hali gani..LMFAO
 
Hata Paulo kabla ya kuitwa Paulo aliitwa Saulo. Zinduka kijana!!


Siyo kila aliye Paulo lazima aanze kuwa Saulo. Tatizo hapa ni wale wanaolazimisha kwamba Nyerere hakuwahi kuwa Saulo.

Huyu Nyerere bado naona kama amekufa bila kueleweka tabia yake. Imani yangu ni kwamba kuna sehemu alipokuwa akikosewa hakuwa na huruma.

Hilo la Hanga linaeleweka sana na munaopinga nadhani muna kasoro zisizofahamika. Hakuna mtu aliyekuwa na akili timamu miaka hiyo ya 60 asiyefahamu kwamba sababu ya kifo cha Hanga ni Nyerere kumukamata.

Kama kweli Nyerere wetu alikuwa wa huruma sana, ilikuwaje askari waliotaka kumpindua Moi pale Kenya aliwapeleka wakati akifahamu fika kwamba watauawa? Tena kwa wakati huo hatukuwa na urafiki na Kenya wala mkataba wa kubadilishana wafungwa!

Kwa kuwa aliwataka sana akina Father Tom waliokuwa wametoroka Keko, Nyerere wetu alikuwa tayari kuwatoa sadaka wakimbizi wa Kenya ambao walikwisha ishi Tanzania muda mrefu. Na mara moja walipelekwa na kuuwawa!
 
Mlitaka Hanga asikamatwe? Wamekamatwa kina Khaled Mohammed na kina Carlos cha Jackal isijekuwa Hanga? Hata hivi tunavyozungumza Serikali ya Obama inawasaka watu wote wenye kujitangaza ni maadui wa US na hata haiwapi nafasi za kujitetea bali huwateremshia haki huko waliko kupitia zile drones!

Sielewi mlitaka Nyerere afanye nini au Karume afanye nini kama kuna njama dhidi yake. Si Karume baadaye kweli aliuawa?
 
Mlitaka Hanga asikamatwe? Wamekamatwa kina Khaled Mohammed na kina Carlos cha Jackal isijekuwa Hanga? Hata hivi tunavyozungumza Serikali ya Obama inawasaka watu wote wenye kujitangaza ni maadui wa US na hata haiwapi nafasi za kujitetea bali huwateremshia haki huko waliko kupitia zile drones!

Sielewi mlitaka Nyerere afanye nini au Karume afanye nini kama kuna njama dhidi yake. Si Karume baadaye kweli aliuawa?

MM, nadhani akina Karume unawafahamu kwa njia ya redio na magazeti.

Ni rahisi sana kuleta argument kama hiyo yako kama waathilika siyo nduguzo. Kama hiyo ndo kazi ya wanasiasa, kuuwa wanaompinga, basi iko kazi.

Karume kuuwawa: ulitaka apewe nini kama kila siku alikuwa akikamata akina mama wa kiarabu na kufanya ngono? Unafahamu alioa wanawake wangapi? It was a shame!
 
Mchunguzi, kumjua Karume au kutomjua Karume siyo issue; watu wengine wangeweza kujenga hoja kuwa utawala wa Sultani ulifanya mambo mabaya zaidi kwa watu weusi vile vile na wapo watu wanaoona kuwa ulikuwa ni bora kuliko utawala wa watu weusi! Kumchukia Karume au Nyerere ni lazima kuwe na msingi hatuwezi kumchukia mtu kwa sababu ya hisia tu..
 
Hakuna mahali popote ambapo mtu anaweza kuonesha kuwa Nyerere alivunja sheria aidha kwa maamuzi yake kuhusu suala la Hanga au vinginevyo.
Kama mtu anawekwa kizuizini bila ya kufunguliwa mashitaka, wala hakuna hali ya hatari iliyotangazwa, hapa mkuu wa nchi hajavunja sheria?
Kuna wakati Nyerere alikuja kuhutubia katika maazimisho ya miaka minne ya Mapinduzi Zanzibar,uwanja wa Amaan, alipokuwa anazungumzia suala la Kambona kukimbia nchi alisema bila ya kificho kuwa "...Kambona ni muhuni na mwizi" na kusisitiza kuwa watu wa namna yake hawawezi kuvumiliwa. Kwanini Nyerere amuhukumu Kambona kwa "uhuni na wizi" kabla ya kumshitaki kama huku si kuvunja sheria ni nini?

Mlitaka Hanga asikamatwe? Wamekamatwa kina Khaled Mohammed na kina Carlos cha Jackal isijekuwa Hanga? Hata hivi tunavyozungumza Serikali ya Obama inawasaka watu wote wenye kujitangaza ni maadui wa US na hata haiwapi nafasi za kujitetea bali huwateremshia haki huko waliko kupitia zile drones!
Sielewi mlitaka Nyerere afanye nini au Karume afanye nini kama kuna njama dhidi yake. Si Karume baadaye kweli aliuawa?

Hivi sisi tunaishi dunia gani, kwa kuwa Wamarekani ni wakatili kwa maadui zao ndiyo ina justify ukatili wa Nyerere kwa maadui zake, Hanga na akamatwe kama walivyokamatwa wenzake, tatizo kwa nini adhalilishwe,atukanwe hadharani mbele ya watoto wake na kadamnasi, halafu apelekwe kwa maadui zake auwawe, iwe hivyo ndiyo sawa kwa sababu US wanafanya? come on!
Kwa hiyo huo ndo ulikuwa utawala wa sheria wa Nyerere ukiwatendea watuhumiwa namna hiyo?


MM, nadhani akina Karume unawafahamu kwa njia ya redio na magazeti.

Ni rahisi sana kuleta argument kama hiyo yako kama waathilika siyo nduguzo. Kama hiyo ndo kazi ya wanasiasa, kuuwa wanaompinga, basi iko kazi.

Karume kuuwawa: ulitaka apewe nini kama kila siku alikuwa akikamata akina mama wa kiarabu na kufanya ngono? Unafahamu alioa wanawake wangapi? It was a shame!
Mkuu umenikumbusha kitu, unajuwa ugomvi wa Karume na Saleh Sadallah, mpaka Karume akaamuru akamatwe na kuwawa ni mwanamke tu. Kitu kibaya zaidi ni kuwa Sadallah alimuowa huyo mwanamke ambaye awali Karume akimchukuwa kwa nguvu, kitendo cha Sadallah kumuowa anti yule ndiyo ikawa yeye na Karume kama paka na chui na ndiyo ukawa mwisho wa Sadallaha ambaye naye kama Hanga, kaburi lake halijuulikani lilipo mpka leo.
 
Mlitaka Hanga asikamatwe? Wamekamatwa kina Khaled Mohammed na kina Carlos cha Jackal isijekuwa Hanga? Hata hivi tunavyozungumza Serikali ya Obama inawasaka watu wote wenye kujitangaza ni maadui wa US na hata haiwapi nafasi za kujitetea bali huwateremshia haki huko waliko kupitia zile drones!

Sielewi mlitaka Nyerere afanye nini au Karume afanye nini kama kuna njama dhidi yake. Si Karume baadaye kweli aliuawa?

Irrelevant, unless uwe clear if you're talking about out of the state or inside state enemies...

Marekani inawa treat tofauti maadui wa ndani ukilinganisha na wale wa mataifa mengine ie terrorists from enemy states...

Hanga si alikuwa mtanzania kama Babu na Kambona?

Hata Taliban Americans wanapewa diffrent treatements tofauti na kina Al Zarqawi pamoja na Sheick Mohamed...Usilinganishe kifo na usingizi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom