Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
- Thread starter
- #41
Junius,
Uadilifu wa Nyerere unabaki palepale. Kumbuka kabla ya Hanga kwenda Guinea (kumfuata mkewe) alisetiriwa mainland na Nyerere. Alipofika Guinea akaungana na Kambona katika mipango ya kupindua serikali. Katika mazingira kama hayo Nyerere hakuwa na sababu tena ya kumhifadhi Hanga. Ndio maana nimesema Hanga alijichimbia kaburi lake mwenyewe/
Tuseme kweli kulikuwa na mpango huo kama unavyotaka, kwa nini Nyerere akaamuru aidha kwa kauli au matendo, Hanga auwawe?
Hanga alikutana na Bibi Titi Mohammed wakati harakati hizo za kina Kambona na Maganga, Nyerere alipomkamata Bibi Titi na kumpeleka Zanzibar gereza la kiinua miguu kwa Mandera au "kwa bamkwe", alihakikisha kuwa Bibi Titi anateswa na kukashifiiwa tu lakini asiuwawe, naye kama kama Hanga alikuwa akituhumiwa na madai hayo hayo unayoseama, na Bibi Titi alipotaka kukutana na Nyerere Zanzibar kwa kile alichokieleza "...anieleze kile hasa nilichomfanya mpaka kustahili kuvuliwa nguo na kukashifiwa na watoto wadogo ni nini...", Nyerere alikwenda akaonana naye na kumhakikishia vyombo vyake vya usalama vitafanya kazi yake, kwa nini hii isiwe kwa Hanga na wenzake ambao Nyerere aliwatoa kutoka mikononi mwake?
Nikauliza hata kama kulikuwa na mpango gani, kwa nini asishitakiwe kama Bibi Titi na badala yake akauwawa?