Nyerere alishiriki Mauaji ya Kassim Hanga?

Status
Not open for further replies.
Junius, kwako kupindua serikali halali ni kitu kizuri? Mapinduzi yanaendana na umwagaji wa damu. Na ndiyo aliyotaka kuyafanya Hanga. Kumbe badala ya kumpa nafasi Hanga amwage damu ya wengi tena wasio na hatia ikabidi yeye apotezwe na mzee Karume.

Hatuwezi kumlaumu Nyerere kwa yale aliyoyafanya Karume kwani kama Rais wa Zanzibar alikuwa na uwezo wa kufanya lolote kwa wale waliokuwa chini yake. Siamini kama Nyerere alijua yale yatakayompata Hanga. Pengine alifikiri atashtakiwa na akipatikana na makosa atafungwa jela. Kumbe ikawa si hivyo! Katika jambo kama hili si rahisi na si vema kumlaumu Nyerere kwa makosa/matendo ya Karume. Kufanya hivyo si kumtendea haki.

Nyerere asingeweza kujua yaliyo moyoni mwa Karume.
 
...

....

Joseph Mihangwa said:
source: Raia Mwema - Muungwana ni Vitendo

KATIKA sehemu ya pili ya makala haya wiki iliyopita, tuliona jinsi kufikia mwaka 1972, Rais Abeid Amani Karume wa Zanzibar alivyoanza kupoteza uvumilivu kwa changamoto za kisiasa kutoka kwa wanasiasa mashuhuri wenzake Visiwani; kiasi cha kuwatungia tuhuma za uongo za kutaka kumpindua; nao wakatiwa kizuizini, kuteswa na wengine kuuawa kikatili .

Na kwa wanasiasa wa Zanzibar waliokuwa Tanzania Bara, chini ya Serikali ya Muungano na wengineo, akiwamo Waziri wa Mipango ya Uchumi na Maendeleo, Abdulrahman Mohammed Babu, Karume alimshinikiza Mwalimu Nyerere awarejeshe Zanzibar "wakahojiwe".

Hata hivyo, Nyerere alikataa. Alikataa kwa kukumbuka jinsi alivyofanya hivyo kwa wengine mwaka 1967, akiwamo Waziri wa Muungano katika Serikali ya Muungano, Abdullah Kassim Hanga, Othman Sharrif na wengine wawili na wakauawa kikatili mwaka 1969; na wengine 19 mbali na Hanga na wenzake walivyopigwa risasi bila ya kushitakiwa.

Mwalimu alilaumiwa sana na jumuiya ya kimataifa kwa hatua yake ya kuwakabidhi Hanga na wenzake kwa Karume. Ilitafsiriwa kwamba, Nyerere, bila ya kujua, aliwahukumu watu hao kufa bila mashitaka.
Alipobanwa baadaye aeleze kwa nini alifanya hivyo, Mwalimu alisema: "Wapate kuhojiwa. Nilitaka nijiridhishe kama yako mashitaka ya kweli yanayowakabili. Ningewezaje kumwambia Karume: Kwa kuwa unadhani watu hawa wanastahili kukabili mashitaka, basi, njoo wewe Tanzania Bara uzungumze nao?".

Lakini pamoja na hayo, utetezi wake ulikuwa dhaifu; kwani ukweli ulibakia kwamba uamuzi wake wa kuwatoa Hanga na Sharrif kwa Karume ulikuwa wa makosa makubwa.

Hanga na wenzake watatu na hawa 19 wengine, waliwakilisha hisia na mtazamo wa kisiasa wa wanaharakati wakuu wa siasa za mrengo wa kushoto (Wakomunisti) ndani ya Chama cha Afro-Shirazi (ASP), na wale wa Chama cha zamani cha Babu cha Umma Party, walioongoza Mapinduzi ya Januari 12, 1964 Visiwani; na ambao kusema kweli walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa jamii ya Kizanzibari, na hivyo kuwa tishio kwa utawala wa Karume.

Ni mazingira haya yaliyozaa kuuawa kwa Karume kutokana na sababu ambazo zimeacha maswali mengi kuliko majibu katika sehemu ya kwanza ya makala haya, kuweza kubaini kama kuuawa kwake kulikuwa na lengo la kulipiza kisasi au kumpindua.

Hayo hayakuwa mambo madogo; bali makubwa na ya kutisha kiasi kwamba lolote lingetarajiwa kutokea kwa Karume na Serikali yake; kwa uhakika na kwa kutabirika. Mwanazuoni mahiri wa Sayansi ya Siasa barani Afrika, Profesa Ali Mazrui anathibitisha hili katika kitabu chake: Africa's International Relations (Uk. 11) anaposema: "Ukizingatia jinsi Sheikh Abeid Karume alivyoitawala Zanzibar kwa ukatili na ubaguzi mkubwa na wa kutisha, lolote baya lilitarajiwa kutokea dhidi yake; ingawa hakuna aliyetarajia kwamba angedumu kwa miaka minane madarakani. Ndiyo maana, hatimaye, wengi hawakushangaa alipouawa mwaka 1972".
 
Ni Nyerere aliyemuhakikishia Sekou Toure kuwa Hanga akirudi Tanzania atahakikisha anakuwa salama, matokeo yake, kama unaona hapo kwenye mkutano amewekwa chini ya ulinzi akidogolewa kwa maneno ya kejeli na baadaye, kwa kujuwa kitakachomfika, Nyerere alimrejesha Zanzibar akauwawa.

Kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano mwenye dhamana na usalama wa raia wake tena kiongozi wake aliemteua yeye kuwa balozi Guinea, asijuwe kilichomtokea mpaka leo? hii haiwi hoja kuwa kwa kuwa alijuwa ndiyo maana kanyamaza mpaka kufa kwake?

Usafi wa Nyerere na ubaki pale pale lakini na damu aliyomwaga is haunting him!

Un authibitisho juu ya mawasiliano kati ya Sekou Toure na Mwalimu? Mawasiliano kati ya Marais siku zote huwa ni siri (Top Secret) sasa wewe mwenzetu uliyapataje maana wakati huo na kwa utaalamu upi uliokuwepo wa kudaka mawasiliano kama hayo?
 
Nyerere alifanya mambo mabaya mengi saana huyu jamaa anayelalamika hajapata kuyasikia tu. Watu kibao wamefia mikononi mwake na familia nyingi sana leoo tanzania zinamlalamikia sana nyerere kwa kuzifanyia visa. Kwa mfano kuna wati wengi Tanzania ambao walikuwa wameenda shule na Nyerere aliwanyanganya vyeti wakaishia kuwa walimu tu na wengine kuishia mtaani na kutofanya vitu vya maana. alikuwa anatoa adhabu ambazo ni kubwa na hazina viwango. Kwa wanaomjua mwalimu babu sasa hivi ni marehemu alinyanganywa vyeti na nyerere kwa kuchelewa kuunganisha mitambo tu na mzee wa watu kafa akiwa anafundisha tution tambaza pale. Hotuba zake ni nzuri lakini zilikuwa siasa sana kueleza vitu visivyotekelezeka.

Huoni kwamba unaeneza propaganda ambazo hazijengi ndugu? Hao "watu wengi" unaowataja ni akina nani na ni wangapi hasa? Na huyo Babu aliyenyang'anywa vyeti "kisha akaendelea kufundisha" aifanya kazi vipi bila vyeti? Na hizo hotuba za Nyerere unadai ni "nzuri" huku pia unadai "hazieleweki!" Mbona unajikanganya? Na vipi hazieleweki kwako pekee au namna gani? Na huo utafiti wa "kutokueleweka" kwa "hotuba nzuri za Nyerere" uliufanya lini? Usivamie kutoa hoja kabla hujajipanga!
 
Nyerere alifanya mambo mabaya mengi saana huyu jamaa anayelalamika hajapata kuyasikia tu. Watu kibao wamefia mikononi mwake na familia nyingi sana leoo tanzania zinamlalamikia sana nyerere kwa kuzifanyia visa. Kwa mfano kuna wati wengi Tanzania ambao walikuwa wameenda shule na Nyerere aliwanyanganya vyeti wakaishia kuwa walimu tu na wengine kuishia mtaani na kutofanya vitu vya maana. alikuwa anatoa adhabu ambazo ni kubwa na hazina viwango. Kwa wanaomjua mwalimu babu sasa hivi ni marehemu alinyanganywa vyeti na nyerere kwa kuchelewa kuunganisha mitambo tu na mzee wa watu kafa akiwa anafundisha tution tambaza pale. Hotuba zake ni nzuri lakini zilikuwa siasa sana kueleza vitu visivyotekelezeka.

This is abusurd really! Tupe orodha ya hao watu wengi walionyanganywa vyeti na Nyerere. Mtu moja kuchukuliwa hatua kutokana na uzembe kazini ndio wamekuwa "watu wengi"? It is unfortunate kwamba huyo mzee aliweza kufikwa na yaliyomfika. Naamini kabisa kama angelijaribu kumfikia Mwalimu kwa njia moja ama nyingine na case yake angelisamehewa. Huyo ndiyo aliyekuwa Mwalimu mwenye huruma ya ajabu kama kiongozi. Kama aliweza kuwaachia huru waliotaka kumpindua alingeshindwaje kumrejesha kazini huyo Mwalimu babu?
 
Mwenda wazimu wewe mwenyewe na hao wazenj wenzako.

Usafi wa Nyerere unabaki pale pale.

usafi upi alio nao nyerere na wewe na mawazo yako ya maji taka hayo..unafuata mkumbo tu hata huelewi unachoandika
 
Hingo Ilogi aliyeongoza maasi ya Tanganyika Rifles hakuuwawa, badala yake alifungwa miaka 15. kuna waliojaribu kumpindua Mwalimu mwaka 1972 nao hawakuuwawa. Kasanga Tumbo na Kasela Bantu waliokosana na Mwalimu nao hawakuuwawa bali walitupwa uhamishoni/kizuizini.

matukio hayo hapo juu yananilazimisha kuamini kwamba Mwalimu hakupendelea kuwatoa uhai wapinzani wake kama ilivyokuwa desturi kwa Karume na wana mapinduzi wenzake.

kwa suala la Kassim Hanga, Mwalimu alifanya makosa kumkabidhi kwa Karume na serikali ya Mapinduzi. kwa bahati mbaya kosa hilo liligharimu maisha ya Kassim Hanga. lakini tangu kifo cha Kassim Hanga, Mwalimu aliwanusuru, Abdulrahmani Babu,na Colonel Ali Mahfudhi, ambao wangeweza kukutwa na hatma ileile iliyomkuta Kassim Hanga, ikiwa angeamua kuwarejesha Zanzibar kwa Karume.
 
Na kwa wanasiasa wa Zanzibar waliokuwa Tanzania Bara, chini ya Serikali ya Muungano na wengineo, akiwamo Waziri wa Mipango ya Uchumi na Maendeleo, Abdulrahman Mohammed Babu, Karume alimshinikiza Mwalimu Nyerere awarejeshe Zanzibar “wakahojiwe”.

Hata hivyo, Nyerere alikataa. Alikataa kwa kukumbuka jinsi alivyofanya hivyo kwa wengine mwaka 1967, akiwamo Waziri wa Muungano katika Serikali ya Muungano, Abdullah Kassim Hanga, Othman Sharrif na wengine wawili na wakauawa kikatili mwaka 1969; na wengine 19 mbali na Hanga na wenzake walivyopigwa risasi bila ya kushitakiwa.

Maelezo haya yanatosheleza kabisa kudhihirisha kwamba Mwalimu alikuwa hana hatia katika mauaji ya akina Hanga. Pia asingeliweza kuota ama kudhani kwamba Karume hatakuwa mkweli; badala ya kuwahoji kama alivyomwambia Mwalimu akaamua kuwaua.

Mwalimu alilaumiwa sana na jumuiya ya kimataifa kwa hatua yake ya kuwakabidhi Hanga na wenzake kwa Karume. Ilitafsiriwa kwamba, Nyerere, bila ya kujua, aliwahukumu watu hao kufa bila mashitaka.
Alipobanwa baadaye aeleze kwa nini alifanya hivyo, Mwalimu alisema: “Wapate kuhojiwa. Nilitaka nijiridhishe kama yako mashitaka ya kweli yanayowakabili. Ningewezaje kumwambia Karume: Kwa kuwa unadhani watu hawa wanastahili kukabili mashitaka, basi, njoo wewe Tanzania Bara uzungumze nao?”.

Lawama za Jumuiya ya Kimataifa haziondoi ukweli kwamba Mwalimu hakuhusika katika mauaji ya hao watu. I just can't imagine Mwalimu "kubanwa" na mtu yeyote for that matter! Nadhani mwandishi Mihangwa alikuwa anaongeza chumvi. Jibu la Mwalimu linadhihirisha zaidi jinsi ambavyo alifanya hivyo kwa nia ya kutaka Karume ambaye ndiye alikuwa akihusika na watu hao akawahoji mwenyewe huko huko Zanzibar.

Pia kama Mwalimu angelikuwa 'muuaji' kama watu wanavyojaribu kum-'brand' iweje mara ya pili Karume alipowataka akina Abdulrahaman Babu Mwalimu akakataa na kuokoa maisha yao wakaishi hadi Mungu alipoamua kuwachukua kwa mapenzi yake? Halikadhalika, kama Mwalimu angelikuwa ni muuaji kwa nini asingeliwaua akina watuhumiwa wa uhaini Tanzania Bara badala yake aliwaachia huru? Tukumbuke jinsi ambavyo Kambona aliweza kuachiwa aondoke nchini bila kuguswa. Mwalimu angeliweza kabisa kumkamata kabla hajavuka mpaka lakini hakufanya hivyo. Accomplices wake nao walitiwa ndani lakini baadaye Mwalimu aliamua kuwaachia huru. Nchi gani barani Afrika ambayo Rais aliye madarakani anaweza kuwaachia huru watuhumiwa wa uhaini? Tumpe Mwalimu credit anayostahili.

Muuaji wenu ni Karume. Mwacheni Mwalimu apumzike kwa amani!
 
Ni Nyerere aliyemuhakikishia Sekou Toure kuwa Hanga akirudi Tanzania atahakikisha anakuwa salama, matokeo yake, kama unaona hapo kwenye mkutano amewekwa chini ya ulinzi akidogolewa kwa maneno ya kejeli na baadaye, kwa kujuwa kitakachomfika, Nyerere alimrejesha Zanzibar akauwawa.

Kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano mwenye dhamana na usalama wa raia wake tena kiongozi wake aliemteua yeye kuwa balozi Guinea, asijuwe kilichomtokea mpaka leo? hii haiwi hoja kuwa kwa kuwa alijuwa ndiyo maana kanyamaza mpaka kufa kwake?

Usafi wa Nyerere na ubaki pale pale lakini na damu aliyomwaga is haunting him!

MuchunguZI said:
Mkuu, Mpe kila mtu 'the benefit of the doubt' Hata mzazi wako. Hiyo doubt ndogo unayompa itakuliwaza siku ukisikia maovu yake.

Sasa wewe na mwingine anayesema Nyerere atabakia kuwa msafi siku zote ni kama kwamba Nyerere ni Muumba, Mungu.

Taarifa za siku hiyo zinasema wengi waliamini siku hiyo Nyerere alikuwa kama mulevi.
Alitukana na kutukana na kutukana! Kwa ujumla maneno yake tu yalitosha kuwaonyesha watu wa usalama kwamba huyo mtu alikuwa hatakiwi tena. Na hicho ndo chanzo cha kumuweka hadharani na baadaye kumpoteza.

Hata kama alipelekwa Z'bar bado chanzo alikuwa ni Nyerere. Mbona hazungumziwi katika siasa na kueleza sababu za kifo chake?

Familia ya Hanga iko wapi?

I am not in the position to know the truth or what exactly transpired hivo nyie endeleeni ma ,jadala wenu. Hizi account zinazotolewa kuvutia kamba kila mtu anawamba ngoma kuelekea upande wake, ila one thing I know for sure ni kwamba kipindi kile kulikuwa na intelligence kali sana na si rahisi mtu kuzushiwa vitu kiholela, and furthermore adhabu ya kupanga mapinduzi kuondoa serikali halali adhabu yake ni kaburi futi 6 ardhini.

Ngoja nimalizie Scotch yangu hapa..Brrr pp...
 
Naomba niwawekee dondoo kutoka kwenye Utafiti uliozaa Kitabu cha Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union:

Karume had an intense hatred for and suspicion of the educated...Within the Revolutionary Council, one after another, Karume eliminated the educated. Sometime in 1969, Kassim Hanga and Othman Shariff, were executed. After a stint of a number of ministerial posts in the Union government, Hanga fell out of Nyerere's grace for his apparent friendship with Kambona, who fled the country following the Arusha Declaration...In April 1965, Zanzibar sentenced [Shariff] to death on a charge of treason which was commuted to 10-years imprisonment by Nyerere. Shariff lived on the mainland but was not given any government post. Sometimes in 1969, Shariff and Hanga were alleged to have got involved in some conspiracy to overthrow the government. At Karume's behest, both Hanga and Shariff were arrested on the mainland and, after some reluctance on the part of Nyerere, were sent to Zanzibar where they were executed. There are gruesome stories of how Hanga was killed, some say by drowning, others say by beheading. Whatever the truth, there can be no little doubt of Karume's tactic of physically eliminating his opponents while terrorising potential ones"
 
Huyo aliuwawa na Mayahudi wakishirikiana na Karume. Nasikia walimlawiti sana jela kabla ya kumchinja. Sasa baada kusema hiyo, subirini sasa mla ngamia Sideeq ai-spy hii mada halafu aje kuwateremshia aya zake. Tuone kama atabaki mtu humu..
 
Inasikitisha sana moyo wa mwanadamu una maovu ya kutisha....ukiingalia hiyo picha unaona body language....watu wana tension ajabu!

Mmmh mimi siwezi kumtetea Nyerere wala kumshutumu kwani sina fact yoyote kuhusiana na tukio hili zaidi ya kusoma magazetini na kila mtu anaandika kwa interest yake anyway but all in all viongozi wa africa wengi walikuwa wamwagaji damu miaka ya 60 na 70...lumumba,tom mboya kwa iyo sitashangaa pia kusikia kuwa damu ya hawa watu ilimwaga na viongozi km karume ila hii inatufundisha nini sasa sisi ? tunajifunza nini katika matukio ya namna hii? je ni story ya kulaumiana tu na kushutumu marehemu hawa nyerere na karume?

Kama waliuwa then! tunapata nini kutokana na matukio haya?

Kama kipo ni kipi? je kuelewa tu history? Je tukipewa facts kuwa nyerere alihusika ama hakuhusika what next? je ni kutambua tu kuwa karume na nyerere walikuwa ama hawakuwa wauaji? au

Eeeh lets think then nini hasa tunakipata kupitia mjadala huu than kuijua historia ? huu ni mjadala mzuri sana

'mix with yours as well'
 
Kwahiyo aliyemuua Hanga ni nani? Nyerere au Karume? Hivi ni kweli kwamba Nyerere ali support mambo ya Karume au ni yale yale ya kupiga mdomo tu ili watu waendelee kucheza bao na kunywa ghahawa?
 
Naomba niwawekee dondoo kutoka kwenye Utafiti uliozaa Kitabu cha Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union:

Karume had an intense hatred for and suspicion of the educated...Within the Revolutionary Council, one after another, Karume eliminated the educated. Sometime in 1969, Kassim Hanga and Othman Shariff, were executed. After a stint of a number of ministerial posts in the Union government, Hanga fell out of Nyerere's grace for his apparent friendship with Kambona, who fled the country following the Arusha Declaration...In April 1965, Zanzibar sentenced [Shariff] to death on a charge of treason which was commuted to 10-years imprisonment by Nyerere. Shariff lived on the mainland but was not given any government post. Sometimes in 1969, Shariff and Hanga were alleged to have got involved in some conspiracy to overthrow the government. At Karume's behest, both Hanga and Shariff were arrested on the mainland and, after some reluctance on the part of Nyerere, were sent to Zanzibar where they were executed. There are gruesome stories of how Hanga was killed, some say by drowning, others say by beheading. Whatever the truth, there can be no little doubt of Karume's tactic of physically eliminating his opponents while terrorising potential ones"
Prof Shivji katika moja ya vitabu vyake aliandika mambo haya. Naamini kama tunataka ukweli hatuna budi kuutafuta na sio kupika story tu bila kuwa na facts. It makes sense kwangu kwamba Nyerere alimuona Hanga bure baada ya kujenga urafiki na Kambona kuliko kusema alishiriki kuumua na Karume.
 
Ni Nyerere aliyemuhakikishia Sekou Toure kuwa Hanga akirudi Tanzania atahakikisha anakuwa salama, matokeo yake, kama unaona hapo kwenye mkutano amewekwa chini ya ulinzi akidogolewa kwa maneno ya kejeli na baadaye, kwa kujuwa kitakachomfika, Nyerere alimrejesha Zanzibar akauwawa.

Kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano mwenye dhamana na usalama wa raia wake tena kiongozi wake aliemteua yeye kuwa balozi Guinea, asijuwe kilichomtokea mpaka leo? hii haiwi hoja kuwa kwa kuwa alijuwa ndiyo maana kanyamaza mpaka kufa kwake?

Usafi wa Nyerere na ubaki pale pale lakini na damu aliyomwaga is haunting him!
hebu kuwa specific kidogo, ikiwa Nyerere ilimkamata kutokana na makosa yake na kumrejesha Zanzibar
vipi kifo kimhusu Nyerere?
kwanini statement yako isiseme kuwa, Serikali ya Mapinduzi ilihusika na kifo cha huyu Bwana Kassim Haga? Au mshaanza kuandaa majungu?
 
usafi upi alio nao nyerere na wewe na mawazo yako ya maji taka hayo..unafuata mkumbo tu hata huelewi unachoandika
hebu tuache uzandiki hakuna mwanadamu mwenye upande mmoja tu wa shilingi
nyerere alikuwa na mzuri na mabaya yake kama mwanadamu wa kawaida na hakuwa Mungu,

hata shetani ana mazuri na mabaya kulingana na utashi wa mtu, unadhani aliyepata fedha
kwa wizi atasema shetani mbaya? wakati kamfanikisha kwenye uharifu wake? hata wewe una mazuri yako na mabaya yako? kwa nini tumhukumu mwalimu JK Nyerere kwa mabaya tu?

Labda kama tumetokana na kizazi kile cha wahujumu uchumi wa zamani hatuwezi kumwona mwalini JK N kama alikuwa na mazuri hasa kwa kuwa wazee wetu wahujumu uchumi nyakati hizo walitaifishwa mali zao
 
Shule ni kitu cha muhimu sana. sijui watu wengine watajali madrassa kuliko shule hadi lini, ndo maana muda wote ni kulalamika tu hata kwa jambo lisilokuwa na maana. Sijui tumsaidie vipi uyu aliyeleta mada, manake anahangaika. Kwani mnataka kumfukua nyerere ili mmpeleke mahakamani? Hata kama atakuwa alifanya hivyo, shida yako nini? Mshukuruni uyu nyerere alitunyang'anya shule ili walau na nyie msome kidogo, la sivyo mngekuwa mnapiga debe barabarani na kupiga soga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom