Nyerere Alishindwa - Munishi.

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Nyerere alishindwa mambo mengi Kiafrika Mtu akishakufa siyo
vizuri kuusema ubaya wake
maana mwenyewe hayuko
kujitetea. Lakini anapokuwa
hai, hata kama ni uhai
unaosaidiwa na mitambo, bado watesi wanaruhusiwa
kuusema ubaya wake ili
akipona ajirekebishe.Na
asipopona basi itawabidi
watesi wanyamaze kimya
wawasikilize mashabiki wake wakisema uzuri wa Mwalimu
wa kuwakomboa Watanzania
kutoka katika minyororo ya
ukoloni wa Waingereza na
kuwaigiza kwenye ukoloni
mwingine wa Julius Kambarage Nyerere. Ukoloni
wa kwanza haukuwa mbaya
kuliko huu wa pili,ila tofauti
yake ni kwamba ukoloni wa
pili uliongozwa na Mwafrika
kutoka Butiama, na ule wa kwanza uliongozwa na
mzungu kutoka Uingereza.
Kwa hiyo tofauti ilikuwa ni
viongozi wa ukoloni, na
Watanzania hawakutoka
katika minyororo ya ukoloni, bali walibadilika kutoka
ukoloni huu kungia mwingine
ambao ndio unaowatawala
mpaka leo. Kwa watu wenye
mawazo kama mimi, ni heri
tungebaki kama tulivyokuwa maana msaada wa kweli
ungetoka popote, kuliko
kujidanganya kuwa tulikuwa
salama na kumbe ukweli wa
mambo ni kwamba tulikuwa
pabaya kuliko mwanzo.Ilikuwa kama kukimbia mvua na
kuingia kwenye kibanda cha
nyasi kinachovuja. huwezi
kueleza tofauti maana bado
unanyeshewa. Na mpaka leo
Watanzani kama mimi hatujui tofauti ya kuwa huru na
kutawaliwa.Ikiwa kuwa huru
ni kumruhusu Nyerere
kujaribia mawazo yake ya
siasa ya ujamaa kwenye
maisha yetu na baada a miaka 30 atuambie mawazo yake
yalishindwa kwa sababu
alikosea, na adhabu tuliyompa
ni cheo cha baba wa Taifa, basi
mtanisamehe nikisema kuwa
mwacheni huyo mzee apumzike kwa amani kutoka
katika dunia hii, ili akapate
nafasi ya kukutana na Muumba
wake ambaye akiamua
kumsamehe amsamehe. Na pia
akiamua kumhukumu yote ni sawa, lakini siwezi kumwomba
Mungu amponye Nyerere aje
kufanya nini? Ambacho
hakukifanya kwa miaka yote
77 aliyoishi duniani? alitumia
nusu ya maisha yake kufanya majaribio na Watanzania,na
sasa Mungu atatushangaa
kwamba tunamsumbua
amponye. Mungu wetu ni
Mungu mwenye wivu, na
hawezi kukubali kushiriki utukufu wake na
Nyerere.Amewaona
Watanzania wanamwabudu
Nyerere kuliko yeye na
ameamua kumchukua ili wajue
kuwa wanaweza pasipo Nyerere.Tena Yeye Mungu
pekee ndiye Baba wa vyote.
lakini wanadamu wanamwita
mwanadamu baba wa taifa?
hiyo ni kufuru. Elimu ni nzuri,
lakini ile inayotoka kwa Mungu.Hii ya wanadamu mara
nyingi inakuwa na kasoro
nyingi.na wale waliyo nayo
husahau kumtegemea
Mungu,na kuitegemea elimu
yao ambayo mara nyingi inashindwa kuwatatulia
matatizo. Elimu ya madarasani
na uongozi ni vitu viwili tofauti
lakini wanadamu huvutiwa
sana na viongozi waliosoma
wanasahau kuwa uongozi unatoka kwa Mungu.Na mara
nyingi hawa viongozi
waliosoma hawaongozi vizuri.
Tuna mifano mingi, lakini
Nyerere ni mmoja wa hao
viongozi wasomi ambao hawakuongoza vizuri.Hotuba
nzuri, maneno ya kushawishi
akili na kupendwa na
waandishi wa habari siyo cheti
cha kiongozi mzuri.Na Nyerere
anasifiwa kwa hiyo lakini ukija kwenye matendo ya zile
hotuba nzuri hakuna hata kijiji
kimoja cha maonyesho
kuonyesha kuna msomi mmoja
aliyewahi kufikiri kuhusu vijiji
vya ujamaa na hiki ni kimoja ya vijiji alivyovianzisha, na
watu katika kijiji hiki
wanafurahia mawazo ya
msomi huyo. Lakini Tanzania
nzima hakuna hata kijiji
kimoja cha ujamaa kilichobaki kama maonyesho ya mawazo
ya msomi Nyerere badala yake
Tanzania ni moja kati ya nchi
masikini duniani. Na yote hayo
ni matunda ya msomi mmoja
waliyemwita Mwalimu wa umasikini.Sasa mambo yakiwa
hivyo najiuliza kwa nini
alipoteza muda kwenda
Makerere kupata shahada ya
DR. ambayo haikumsaidia
kuifanya Tanzania mahali pazuri pa kuishi? Bado nasita
katika njia mbili, sijui
nimpeleke mtoto wangu
Makerere apate shahada kama
ya Nyerere ndipo aje agombee
uongozi wa Tanzaia, au tumtegemee Mungu atupe
kiongozi ambaye ataongoza
vizuri hata kama hana karatasi
ya chuo kikuu? Na kama Mungu
anaweza kutupa kiongozi basi
hata mimi niko tayari maana kile ambacho sina ni karatasi
ya chuo kikuu tu.na kama
Nyerere DR. anaweza
kushindwa mambo mengi
hivyo, basi nina hakika siwezi
kushindwa kama yeye.Kwa Watanzania ni vizuri Nyerere
aondoke ili tuwe na mawazo
mapya na mbinu mpya za
kuikomboa kikweli
Tanzania.Hata Musa
alipokufa ,Yoshua alifanya makuu kuliko Musa Na Yoshua
wa Tanzania ni mimi Faustin S.
Munishi
 
Back
Top Bottom