Nyerere alisema binadamu hupenda makuu hasa kujilimbikizia mali

curiosity

Member
Apr 4, 2012
10
1
Baba wa taifa alionya kuwa ipo siku ccm chama hiki hiki kilicho cha wakulima kitakuwa cha matajiri wachache tusipokuwa makini kuwadhibiti. Alisema naona anguko la ccm likisababishwa na matajiri wachache wakihojiwa na maskini walio wengi.

Ninyi mmepata wapi hizi pesa, maskini walio wengu wanakandamizwa na matajiri wachache na kutokana na hilo, uhojaji unaendelea hata nje ya chama..wananchi wanagundua na kulio, wanatambua pia umaskini wao umeletwa na ulafi wa viongozi wao..hapa ndipo anguko la CCM...

CCM inaanguka kwa stahili hii..report ya mafisadi iliposomwa pale mwembe yanga, Raisi angewachunguza na kuwafili kwa hasira ile ile ya baba wa Taifa ya kuchukia wezi wa uchumi "Wahujumu uchumi"

CCM ni chama kizuri kama CCM ila viongozi wake sasa wamelowa pesa hvyo hawana kabisa uzalendo na ndo walio kiua chama na kupoteza mwelekeo..

Nadhani ili watanzania tuweze kuendelea tukipumzishe hiki chama..mapaka pale wazee wote watakapokufa na watoto wao walioridhi ulafi wa baba zao na mali zao zitakapokuwa zimfilisiwa kabisa ndipo wataweza kijifunza nini maana ya kuwa chama cha wakulima...

Pinda mtoto wa mkulima kageuka kuwa pazia la walafi...hajui nini maana ya kauli hyo..ccm imefika mda wa kuoumzika na kuwaoisha watu wenye uzalendo na chi hii
 
Sio Nyerere aliyesema, bali aliayase hayo kwa kurudia tu maneno ambayo yalitabiriwa na Mungu.
 
Tatizo la CCM wanapokutana jioni wanajigamba kwa nani ana mali nyingi zaidi za wizi na sio nani mwadilifu, na utendaji uliotukuka kwao ni majumba mangapi unamiliki, makampuni mangapi unamiliki na ni jinsi gani ulitoa rusha jimboni mwaka, aliye na mali nyingi, aliyeshinda uchaguzi kwa rushwa na mizengwe ndiye anafaa uwaziri
 
Back
Top Bottom