Nyati amuua 'jangili' Hifadhi ya Taifa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
MWANAMUME anayesadikiwa kuwa jangili, ameuawa kwa kukanyagwakanyagwa na nyati mwenye hasira ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kumjeruhi mnyama huyo.

Mauaji hayo yaligundulika juzi mchana ambapo inadaiwa kuwa mtu huyo ambaye jina lake halijajulikana mara moja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 40 na 45, aliingia katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuwinda wanyama isivyo halali.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage mwindaji huyo akiwa kwenye harakati za kufanya ujangili hifadhini humo, alishambuliwa na nyati huyo kwa kukanyagwakanyagwa na kuvunjwa mbavu zote.

“Nyati anayedaiwa mwenye hasira baada ya kujeruhiwa, alimshambulia mwindaji huyo haramu na kufa pale pale baada ya mnyama huyo kumvunja mbavu zote kwa kumkanyagakanyaga mwili mzima,” alisema Kamanda Mantage.

Alisema, mwili wa mwindaji huyo, uligunduliwa na askari wa wanyamapori wa hifadhi hiyo waliokuwa doria maeneo hayo kutokana na alama za nyayo za mnyama huyo walizozikuta pembeni ya mwili wa mtu huyo.

“Pia kando ya mwili wa marehemu, askari hao walikuta silaha moja aina ya gobore na risasi zake, mwili huo umehifadhiwa chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya mjini Mpanda kwa utambuzi,” alisema Kamanda Mantage.
 
ndo dawa yao hao poachers ,nadhani hali kama hii ndo inaelekea kumpata mkwere ,na yeye tutamrukia na kumvunjavunja mbavu hadi aelewe kuwa dhama hizi hatuhitaji poachers c wa wanyama wa mwituni bali pia sisi binadamu ambao ni highest rank in the group of animals,big up to that buffalo and to me that is cdm.
 
Du wajina ana hasira sana yaani kama ni kweli inadhihirisha ile methali ya wahenga kuwa akuanzae mmalize
 
Du wajina ana hasira sana yaani kama ni kweli inadhihirisha ile methali ya wahenga kuwa akuanzae mmalize

Na wewe una hasira kama wajina wako?

Ila tukiangalia vizuri tutaona kuwa hawa wawindaji haramu wanajitakia hatari wenyewe.Alikuwa amejiamini sana kwenda kuwinda mahali ambapo haruhusiwi . Watu waache kabisa kuvunja sheria makusudi tena waziwazi.
 
kwanini hakumchapa risasi nyingine alipoona nyati ana hasira au kwanini asingepanda kwenye mti!

Killy,
timing labda ilikuwa mbaya akapata kigugumizi cha akili - miguu ikashindwa kukimbilia mti ( labda hakujua hata kupanda mti!) na mikono ikakosa orientation ya gobole lake!
 
safi sana!ila natoa pole ya dhat kwa familia iliyompoteza baba RIP mwindaji haramu
 
r.i.p ,ni katika harakati za kujikwamua na shida ambazo zingine zimesababishwa na mfumo mbaya na mbovu wa utawala....
 
ndo dawa yao hao poachers ,nadhani hali kama hii ndo inaelekea kumpata mkwere ,na yeye tutamrukia na kumvunjavunja mbavu hadi aelewe kuwa dhama hizi hatuhitaji poachers c wa wanyama wa mwituni bali pia sisi binadamu ambao ni highest rank in the group of animals,big up to that buffalo and to me that is cdm.

Kweli sasa nimeamini watu hawamhitaji JK maana hapa imeletwa topic ya jangili na nyati lakini na mkwere kaingizwa kidogo na mchangiaji
 
Kweli sasa nimeamini watu hawamhitaji JK maana hapa imeletwa topic ya jangili na nyati lakini na mkwere kaingizwa kidogo na mchangiaji

Mkuu unajua simlaumu huyu poacher bt naweza nikamlaumu mkwere kwa asilimia kubwa,yeye ndo alituahidi nchi ya maziwa na asali,ajira nje nje,maisha bora lakini imekuwa mbaya,we acha ajiulie kama angewin ningempongeza ila amekosea step namwona mjinga flani ,hyo ndo hasira yangu kwa mkwere na hata wanadamu wengne wa tz.
 
hapo sasa kila zigo analibeba yeye kaazi kwelikweli bora muda ukimbie tufanye uchaguzi mwingine maana watu wameshaelewa maana ya upinzani ni nini
Kweli sasa nimeamini watu hawamhitaji JK maana hapa imeletwa topic ya jangili na nyati lakini na mkwere kaingizwa kidogo na mchangiaji
 
Hard life with fake promise from JK, me nafikiri huyo marehemu alikuwa na hamu na kitoweo na hakuwa na jinsi na akiangalia bei ya nyama buchani haikamatiki.

Ikabidi ajitose ndani ya mbuga mpaka mauti yalipomkuta.RIP marehemu poleni ndugu wa marehemu
Source ya haya yote ni JK
 
sasa angewezaje kumbeba nyati mzima peke yake hapo unaweza kukuta alikua na kundi la zaidi ya watu 70 wa kumsaidia kubeba hiyo nyama
Hard life with fake promise from JK, me nafikiri huyo marehemu alikuwa na hamu na kitoweo na hakuwa na jinsi na akiangalia bei ya nyama buchani haikamatiki. Ikabidi ajitose ndani ya mbuga mpaka mauti yalipomkuta.RIP marehemu poleni ndugu wa marehemu
Source ya haya yote ni JK
 
Na wewe una hasira kama wajina wako?

Ila tukiangalia vizuri tutaona kuwa hawa wawindaji haramu wanajitakia hatari wenyewe.Alikuwa amejiamini sana kwenda kuwinda mahali ambapo haruhusiwi . Watu waache kabisa kuvunja sheria makusudi tena waziwazi.

Mkuu unajua Gobore ukishapiga risasi inachukua muda kuweka risasi nyingine na kukoki risasi muda wote huo Nyati hakupi nafasi ya kummaliza.

Pia magobore ya aiana nyingine hayakutengenezwa kwaajili ya kuua mnyama mkubwa kama Nyati sana sana yanamjeruhi tu na kumuongezea hasira.

Mara nyingi wawindaji wa aina ya marehemu wanaingia porini kuwinda wanyama wadogo wadogo kwaajili ya kitowewo unajua tena maisha siku hizi yamepanda haswa nyama ya mbuzi au kuku haishikiki.
 
ni kweli na unaweza kufyatua na likagoma kuwaka likaanza kutoa moshi tu wanasema ukiona hivyo litupe chini na ukimbie maana likifyatuka zinaweza kukurudia wewe mwenyewe!
Mkuu unajua Gobore ukishapiga risasi inachukua muda kuweka risasi nyingine na kukoki risasi muda wote huo Nyati hakupi nafasi ya kummaliza.Pia magobore ya aiana nyingine hayakutengenezwa kwaajili ya kuua mnyama mkubwa kama Nyati sana sana yanamjeruhi tu na kumuongezea hasira.Mara nyingi wawindaji wa aina ya marehemu wanaingia porini kuwinda wanyama wadogo wadogo kwaajili ya kitowewo unajua tena maisha siku hizi yamepanda haswa nyama ya mbuzi au kuku haishikiki.
 
Hawa majangili kuna kitu kinaitwa roda, inawezekana nyati alishanasa kwenye roda kwa hyo marehemu akaona kazi imeisha ila nyati wananguvu sana akikuotea anakufa na wewe, huwa wanamtoboa macho kwa spoko.
 
haisee hapo wanakiuka haki za wanyama kweli uanze kwa kumtoboa macho kwa spoko huo ni uonevu wa hali ya juu sana kweli majangili ni lazima wauawe popote pale
Hawa majangili kuna kitu kinaitwa roda, inawezekana nyati alishanasa kwenye roda kwa hyo marehemu akaona kazi imeisha ila nyati wananguvu sana akikuotea anakufa na wewe, huwa wanamtoboa macho kwa spoko.
 
Chondechonde huyo Nyati apelekwe haraka Ngorongoro akawalinde wale nyati waliobaki wanne wa JK.
 
wewe utambebaje nyati aliechanganyikiwa hicho si kifo man kwanza utaanza anzaje
Chondechonde huyo Nyati apelekwe haraka Ngorongoro akawalinde wale nyati waliobaki wanne wa JK.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom