Nyaraka: Ripoti ya Nundu kwa Kamati ya Miundombinu na MoU halisi

Hii ndo Tz ndugu! Waziri wa watu katoa povu jingi kujitetea lkn tukamuona mjinga! Serikali yetu ni ya madili. Kama hutaki kuyacheza hayo madhli ni bora usikubali uteuzi. Maana wewe msafi ndo utafanywa mchafu
 
Kumbe Nundu yuko makini sana kiasi hicho. Serukamba hawezi kuwa na uchungu na nchi hii yeye ni Banyamurenge
 
Kesi ya Nundu ni mtihani mkubwa kwa Kikwete; itabidi aamue kuamini hilo genge la wahuni wakina Serukamba wanaotumiwa na wakina Lowassa kufanikisha mambo yao au kumuamini mzalemdo Nundu anaeweka maslahi ya nchi mbele!!

Nundu akiondolewa kuhoka wizara hiyo utakuwa ni ushindi kwa mafisadi wanaotaka hiyo kampuni y CCCC ipate ili hicho walichoahidiwa wachote kama inavyodhihilishwa na hesabu zao kubadika badilika ili kukidhi hizo 10% walizoahidiwa wao mafisadi!

Kwa vile Nundu anatetea maslahi ya wengi, anatetea maslahi ya Mungu na Mungu hamtupi mja wake. Inshallah Mungu atamlinda.
 
Je, taratibu za manunuzi zilifuatwa?

Kwa kawaida mradi mkubwa kama huu ulitakiwa ufanyiwe upembuzi yakinifu na mtu ambaye ni independent baada ya hapo anachaguliwa consultant ambaye anakuwa kama wakili wa serikali na mwisho inatangazwa zabuni ya wanaotaka kujenga. Baada ya kila kampuni kuleta profile yake inabidi wakaguliwe miradi waliyofanya na kampuni hizo zisiwe hata na chembe ya rushwa.

Hivi Serukamba si ndio alikuwa anamtetea Lowassa kwa nguvu zote wakati sisi wote tunajua ni mchafu? Nundu inabidi apongezwe na bodi ya makandarasi isikae kimya imchunguze Mfutakamba maana wakisubiri ashitakiwe itakuwa aibu kwao maana kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa huko na bado tulishuhudia majengo mengi yakijengwa chini ya viwango pamoja na barabara. Ingawa mara nyingi walikuwa wanalaumu wanasiasa lakini inaonyesha huu mchezo ameanza muda mrefu
 
nundu ni mzalendo sn ila tz tuna siasa za ushabiki na majungu mengi,watu wanaogopa kufanya kazi kuhofia majungu
 
Mie ninaomba RAIS WETU Dr. Slaa akiwa na kundi lake la watu makini na hasa Ndugu (sitaki kumuita Muheshimiwa) Tundu Lissu waje walivalie hili swala njuga na kuweka wazi Pumba na mchele.

Kama swala lina utata namna hii, basi Zitto Kabwe pia atupe ukweli wake maana inaonekana na yeye kadanganywa na Homeboy wake Serukamba.

Nilishangaa sana kumuona Serukamba ghafla kawa MZALENDO mkubwa namna hiyo akitetea maslahi ya Taifa ila alipoona mambo yanakwenda vibaya kiasi kwamba hata Naibu Waziri wa Nundu anakwenda na maji, ghafla mdomo ukapata maji kinywaji na akashindwa kabisa kuweka sahihi kwenye listi ya Zitto. Na niseme wazi kabisa na wengine kama mimi mkumbuke milele kuwa ukimuona Peter Serukamba anamshambulia MTU WA CCM basi ujuwe hapo kazibiwa ulaji. Nafikiri hili inabidi liwe wazi milele. Ukimuona anamshambulia mpinzani, hapo ndiyo unaweza kushindwa kuelewa katangulia Tumbo mbele au CCM mbele. Huyu jamaa Serukamba kama ni kweli, ni mtu mbaya sana na wa kuogopa kama ukoma.

Kama hayo madudu ni kweli basi Nundu ahamie kabisa Chadema maana huko ndiko wapo Wazalendo wa kweli. Tunashukuru sana kuona bado wapo Watanzania wanataka kuokoa hata kidogo kilichobaki maana hii mifisadi ipo tayari kuwauza hata mama zao ili muradi itajirike. Mijitu hatari sana hii, khaaa!!!!!

Tafadhali sana CHADEMA, hili swala mliingilie kati na mlivalie njuga na mchukue msimamo mapema. Nundu lazima abaki kama waziri hapo alipo akama itaonekana kweli ni MZALENDO kama makaratasi yanavyoonyesha.

Serukamba, najua hukumu ya Ubunge wako imehamia Mahakama kuu, naombea Mungu na wewe ushindi wako wautengue. Wengine watasema dua la kuku..... Ila kuna siku Dua la watu laweza kukupata.
 
Inatakiwa Mh. Serukamba aje hapa au atume wawakilishi watuwekee vitu hapa vinginevyo yeye ndiye msariti wa Watanzania.
 
Mkuu kwa taarifa hizi hamna Waziri Mzalendo kama Mh. Nundu, ila kwa Mafarisayo au wala rushwa mapapa Nundu ni adui namba moja? Kwa ukweli huu hivi Serukamba ni mbunge mwenye nia ya dhati kwa maendeleo ya nchi hii au ni mla rushwa bingwa, tena siyo yeye tu hata kamati yake yote ni wala rushwa, wahenga walisema samaki mmoja akioza ni wote wameoza.

Serukamba amekuwa akipigania maslahi ya ngoyai kwa miaka mingi sana. Suala la yeye kutetea wananchi ni kwa vile yeye au ngoyai hawapo kwenye hii dili lakini haaminiki kabisa huyu mwogopeni kama ukoma
 
Zililetwa 'nyaraka' humu kuhusu sakata la ujenzi wa gati ya 13 na 14 bandarini,lakini ukweli ni kuwa waliozileta wamekuwa 'selective', kwa kuchagua zile tu ambazo zitamu-implicate Waziri mzalendo Nundu na kwa mtiririko ambao unaleta picha wanayoitaka iaminike. Kwa sababu hiyo nimepata msukumo wa kuzisaka na kuzipitia nyaraka halisi. Ntaziweka baadhi hapa. Kwa leo nawamegeeni taarifa aliyoisoma waziri kwa kamati ya Miundombinu, chini ya Mh. Serukamba. Kamati iliamua ku-ignore repoti hii na kuwasilisha bungeni namna wanavyotaka wao.

Pia, kwa vile walioleta nyaraka, wameleta '1st draft' ya MoU ambayo inaonekana wazi wazi kuwa HAIJASAINIWA, nimeona pia niwawekeeni MoU halisi, final draft, ILIYOSAINIWA na katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi. Kama alivyotamka waziri, hakuna miaka 45 wala kupewa ardhi wala madudu mengine yaliyomo katika 'draft' iliyowekwa. Mind you, MoU sio hii moja tu, ziko pia with other potential wadau wa maendeleo, lakini bado inabidi washindanishwe ili kumpata the most competent na kupata value for money for the country.

Mkishasoma mtaamua wenyewe.
View attachment 52970View attachment 52969View attachment 52978
View attachment 52968View attachment 52967View attachment 52966
View attachment 52975View attachment 52974View attachment 52973
View attachment 52972View attachment 52971View attachment 52977
View attachment 52976[/QUOTE]

Tusipoteze umakini. Kwanza huo mkataba ukurasa wa 4 umechakachuliwa na kufutwa baadhi ya mambo. Lakini kubwa tatizo la Nundu munalikwepa. tatizo la Nundu ni kwanini anakazania kampuni nyingine wakati kuna mchakato serikalini? je, kwanini sasa ndio ameibuka akijua kesho ndio baraza linavunjwa? katumwa kujitetea ili abaki? Naona watu wanamleta RA hapa kupotosha, ushahidi uko wapi? Acheni PCCB wapitie hizi nyaraka na wakishamhoji yeye na Katibu wake na Naibu wake watajua nani anastahili kushitakiwa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-walikuwa-wapi-hadi-mambo-yanafika-hapa.html

Pia ajibu hoja za yeye kuipeleka kampuni kwao Tanga na kampuni kumsafirisha China na ndio sasa anaimba wimbo wa hiyo kampuni kama mulisoma barua ya Chinese Mecharnt ikilalamikia CCCC, na Nundu ndiye analia. Sasa kama PCCB wataona CCCC wametoa rushwa serikali iisitishe mchakato na kuwashitaki Kawambwa, Mkulo na Chambo na kuanza mchakato wa kampuni mpya bila kulipa fidia kwa kuwa rushwa haina fidia, si anavyofanya Nundu. CCCC walifanya upembuzi na kuttoa bei kubwa ambayo TPA na Bodi walishaamua kampuni mpya ifanye upembuzi huru kuhakiki bei na Bunge nalo baada ya Mnyika kutoa hoja, limeamua hivyo hivyo kufanya uhakiki kama bei ya CCC ni kubwa ama ndogo na kushauri serikali na si Nundu anavyotaka kutafuta mwekezaji mwingine pembeni. Aseme tu ukweli na ukweli ndio kinga si kelele na kuspin
 
Nenda pale wizara ya utumishi staff wanamwita Nundu eti mkoloni,kwao mfutakamba ndo 'mzungu'!!! Baada ya kushindwa kumhonga sasa 'mzalendo' Serukamba kapewa kazi ya kummaliza na kweli kammaliza,wale wenye ma truck walofurahia kufa Tazara sasa kicheko
 
Hivi Serukamba ana taarifa na yanayoendelea kwenye Banadari ya Kigoma iliyoko jimboni kwake?.
 
Kuanzia mwanzo niliposoma maelezo ya Nundu nilijua dhahiri ni nani kati yake na kamati ya Serukamba alikuwa anatetea masilahi ya taifa.
Kwa bahati mbaya bwana mdogo Peter alidhani kuwa bado tuko karne ya 10 na angeweza kutuzuga na fitina za kilafi namna ile.
Naomba sasa wabunge watetezi wa haki wapeleke ombi bungeni ili iundwe kamati teule kuchunguza kadhia hii ya CCCC
 
Nasikia ...kamba ni mke wa watu, usikute anatetea masilahi ya mme wake ambaye inasemekena anatafuta urais kupitia chama cha magamba kwa udi na uvumba.

Musiniquote mie natania tu
 
Omar Nundu hata kwa kumtazama tu unagundua kuwa hana ishara za ufisadi kama walizonazo akina Ngeleja, Maige. Hii nchi inachezewa kwa kuwa maovu yote yanaishia kwenye vyombo vya habari.

Kama hili swala lingeenda mahakamani ingethibitika bila shaka nani ni fisadi na nani ni mzalendo. Kwa serikali hii ya CCM ambayo imegoma kuwafikisha mafisadi mahakamani na imegoma kuwawajibisha TAKOKURU kwa kusinda wanaangalia FACEBOOK badala ya kukamata rushwa.

Mkuu niliwahi kueleza hivyo hivyo kuhusu Mh.Nundu, watu wakanishambulia kweli kweli!
 
Mie ninaomba RAIS WETU Dr. Slaa akiwa na kundi lake la watu makini na hasa Ndugu (sitaki kumuita Muheshimiwa) Tundu Lissu waje walivalie hili swala njuga na kuweka wazi Pumba na mchele.

Kama swala lina utata namna hii, basi Zitto Kabwe pia atupe ukweli wake maana inaonekana na yeye kadanganywa na Homeboy wake Serukamba.

Nilishangaa sana kumuona Serukamba ghafla kawa MZALENDO mkubwa namna hiyo akitetea maslahi ya Taifa ila alipoona mambo yanakwenda vibaya kiasi kwamba hata Naibu Waziri wa Nundu anakwenda na maji, ghafla mdomo ukapata maji kinywaji na akashindwa kabisa kuweka sahihi kwenye listi ya Zitto. Na niseme wazi kabisa na wengine kama mimi mkumbuke milele kuwa ukimuona Peter Serukamba anamshambulia MTU WA CCM basi ujuwe hapo kazibiwa ulaji. Nafikiri hili inabidi liwe wazi milele. Ukimuona anamshambulia mpinzani, hapo ndiyo unaweza kushindwa kuelewa katangulia Tumbo mbele au CCM mbele. Huyu jamaa Serukamba kama ni kweli, ni mtu mbaya sana na wa kuogopa kama ukoma.

Kama hayo madudu ni kweli basi Nundu ahamie kabisa Chadema maana huko ndiko wapo Wazalendo wa kweli. Tunashukuru sana kuona bado wapo Watanzania wanataka kuokoa hata kidogo kilichobaki maana hii mifisadi ipo tayari kuwauza hata mama zao ili muradi itajirike. Mijitu hatari sana hii, khaaa!!!!!

Tafadhali sana CHADEMA, hili swala mliingilie kati na mlivalie njuga na mchukue msimamo mapema. Nundu lazima abaki kama waziri hapo alipo akama itaonekana kweli ni MZALENDO kama makaratasi yanavyoonyesha.

Serukamba, najua hukumu ya Ubunge wako imehamia Mahakama kuu, naombea Mungu na wewe ushindi wako wautengue. Wengine watasema dua la kuku..... Ila kuna siku Dua la watu laweza kukupata.

Mkuu huyu Mh. ni wa kuogopa kuliko hata ukoma, kikubwa ni kuwaatadhalisha wapambanaji wetu kua makini nae. Sijawahi kumuona akitetea masilahi ya taifa, nlishangaa sanaa nilipomuona akiongea kama vile anatetea taifa zima kumbe alikua anamaanisha tofauti na tulivyodhania.
 
Mkuu kwa taarifa hizi hamna Waziri Mzalendo kama Mh. Nundu, ila kwa Mafarisayo au wala rushwa mapapa Nundu ni adui namba moja? Kwa ukweli huu hivi Serukamba ni mbunge mwenye nia ya dhati kwa maendeleo ya nchi hii au ni mla rushwa bingwa, tena siyo yeye tu hata kamati yake yote ni wala rushwa, wahenga walisema samaki mmoja akioza ni wote wameoza.

Simbawene, unapaswa kujua taarifa za mkaguzi mkuu wa Serikali tangu miaka,zimekuwa zikipelekwa Serikalini hukohuko. Kanuni ni "KESI YA NYANI KUMPELEKEA NGEDERE AWE HAKIMU". Kwa hiyo wamekuwa wakifanya kama formality tu na wala hakuna aliyekuwa anazifanyia kazi. Walikuwa wanakaripiana kishikaji, ikizidi, wanabadilishwa tu Wizara na mambo yanakwenda! Tangu utaratibu huu wa kuziwasilisha bungeni uanze ndo tunaona haya. Nundu kakatizia miradi ya Waheshimiwa. Na ninakuhakikishia kwamba hatabaki salama! Wakiendekeza U-NUNDU wataikabili vipi 20015? Huu ndo mfumo wa utendaji kazi wa Serikali ya chama chetu chenye kupendwa na "wadanganyika" wote! Siku si nyoingi utapigia mstari maneno yangu.
 
Back
Top Bottom