NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Apr 23, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,663
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 48
  Conclusion utaipata ukisha-download nyaraka hizi.

  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 8,708
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 48
  HUjaeleweka mkuu

  Unasafishaje mtu kwa barua moja
   
 3. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Soma kwanza uone. Hakuna anayemsafisha, soma uhukumu!!
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Ni msafi maana hajawahi kwenda China, bali aliyeenda ni Naibu wake
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,106
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38
  Hao wachina mbona wanaonekana wanapata habari kuhusu nini kinaendelea kwenye serikali ya Tanzania toka vyanzo vingine? Kwa mfano walijuaje Hazina wameandika barua? Hapa naona Nundu alikuwa na team yake, na naibu waziri wake alikuwa na team yake! Lakini wote kwa pamoja wana interest moja = screw Tanzania kama zile twin towers za BOT!
   
 6. P

  Papizo JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,009
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  Acheni uvivu wakuu,kama mnatumia simu sawa, ila hapo kuna file Invisible ameattach mautamu yote yapo humo, kabla ya kucomment angalie kwanza maana amesema hapo inabidi u download hataki kumwaga mtama kwenye kuku wengi....
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Afadhali Mkuu umetusaidia!! Watu waburudike na mziki!!
   
 8. G

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 8,205
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 48
  Hizi barua hazimsafishi Nundu bali zinaonyesha kuwa alikuwa ana kaurafiki haramu na hii kampuni ya China Merchants Holdings nje ya njia zinazokubalika yaani kiofisi maana hawa wanaonekana hawafuati njia sahihi zinazotakiwa kufuatwa na kampuni bali wanatumia kiongozi mla rushwa/mlafi kama Omar Nundu kuipiga bao kampuni ya China Communications construction Ltd ambayo tayari proposal yake imekubalika na imeshapata fedha toka Exim Bank China! Sasa sijui ni punda gani anaweza kuacha mradi ulioiva namna hiyo wa China Cummunications Construction Ltd akaenda kwa huu wa China Merchants Holdings ambao haujasema ni kiasi gani ita-finance huo mradi na kwa riba kiasi gani! hapa simply hii barua inaonyesha jinsi mawaziri wetu vilaza walivyo tayari ku-take risky decisions na ku-subotage miradi mikubwa ya maendeleo ili mradi tu wamehakikishiwa kushibishwa matumbo yao na miradi fake inayokosa transparency bali kupitia kwa vimemo viinavyoweza kui-cost nchi kama mikataba ya umeme ta Tanesco! Omar Nundu lazma ajiuzulu manina.....!
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 63
  I see!!...
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Hebu tusaidieni hizo nyaraka za Naibu Waziri alivyohusika. Maana kama alihongwa tiketi ya ndege na vijifedha, aliyesema hayo ni Nundu ambaye anataka kutuambia, Naibu alimzidi nguvu, sasa hebu tujiridhishe kabla ya kubeba maneno ya mwizi mtoto anayesema sikuiba peke yangu!!!
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 28,492
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 83
  Sijapenda habari za kutoa bandari rehani kwa miaka 45.
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Mhnnn!!! Haya!!! Kumekucha!!
   
 13. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,403
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Wengine tumeshindwa kuifungua hiyo attached file.
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,207
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 48
  Haya ndiyo yalikuwa yanasemwa bungeni.
  Hapa Invisible una maana gani kuwa Nundu ni msafi?
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 63
  Hivi inawezekana JK kwake habari nzito ni kwenda kuzika a Dead body Bingu wa Mutharika kuliko hii, bado siamini kama JK pamoja na udhaifu wake mwingi bado atakuwa amefanya kosa hili.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,252
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 48
  Mbona juzi Nundu aliliambia bunge kwamba hana kampuni yoyote anayotaka kuipendelea ila anataka tender itangazwe upya ili kampuni nyingi zishindanishwe? Na pia mbona alisema hajui lolote kuhusu CCCC?

  Hapa kweli kazi ipo!!
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 63
  Fuatilia hii thread kwa makini, mambo yote sasa yapo hadharani huitajiki tena kulifunguwa wewe hilo file, hiyo kazi umesharahisishiwa.
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 25,899
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 63
  mimi mwenywe zilinishtua sana aise
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 25,899
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 63
  mods wayaweke yote kwenye post ya kwanza
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,252
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 48

  Unadhani kwa JK hii ni big issue?

  Kama aliacha watu wanakufa wakati wa mgomo wa madaktari, anaweza kustuka kwa issue kama hii??
   
 21. P

  Pasco JF Platinum Member

  #21
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 17,505
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 83
  Endeleeni kumwaga nondo na mimi kesho nakuja na zangu!. Jee nani anajua hao CCCC walipatikanaje?. Jee kuna tenda yoyote ilitangazwa?!. Jee walijuaje TZ tunataka kupanua bandari?. Jee nani aliwapa kibali cha kufanya feasibility study?. Wangapi mnajua kuwa good practice ni feasibility study kufanywa na mwingine, funding kutafutwa kwa mwingine, construction company iwe nyingine na consultants ni wengine for checks and balance!. Jee ni wangapi mnajua feasibility study wanefanya hao CCCC, consultants ni wao wao CCCC wakaja na hiyo figure ya dola milioni 500 plus bila any independent verification na mkopo wakaomba hao hao CCCC kutoka Exim Bank?. Why?. Tangu lini unaomba mkopo alafu banker anakulazimisha usipofanya kazi na CCCC no mkopo!.

  Mbona Mombasa wamejenga kwa 200 why sisi tujenge kwa 600?!.

  Hivi mnajua kiburi na jeuri ya Mfutakamba inatoka wapi?. Mnamjua nani anampa ruhusa kwenda kuhongwa huko nje huku akimby pass boss wake?!. Nnajua aliandika recomendation ya kuifagilia CCCC na kuisubmit wapi bila kumuonyesha waziri?. Amini nawaambieni hao CCCC ni yule yule RA!. Kama Richmond tuu ila this time sio US ni China!. Hivi mnanuamini Serukamba?!. Mnaamini ni yeye ndie aliyeomba kuwa M/Kiti wa Kamati ile?. No amewekwa kama alivyo pewa ubunge!. Yeye ni remote tuu ya RA!.

  Endeleeni kumwaga mboga kesho na sisi tunamwaga ugali wakose wote!. Kusema ukweli napandwa na hasira sana mpaka natamani nchi hii tungekuwa kama China, mafisadi wana kula bullets soonest possible na kusahaulika!.

  Mchukua Nundu na Mfutakamba uwapime nani fisadi na nani sio!. Tatizo la ufisadi ni kubwa kuliko nilivyodhania maana mpaka humu jf vibaraka wao, wametamalaki sana!.

  Mungu Ibariki Tanzania!. Nawahakikishia kama 2015 Watanzania wataamua kufanya kweli, kuna wenzetu humu humu watatafuta pa kutokea maana kwao pia ni kilio na kusaga meno!.
   
 22. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #22
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 924
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 18
  Mkuu taaratibu unaweza sababisha watu kufa kwa Bp!
   
 23. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #23
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 63
  Pasco hapa ndipo unapoweza kumaliza hasira za Boss wako, hakuna kulala mwambie Lowasa akupe details zote anazozifahamu lete mwaga hapa na from there indio utakuwa mwisho wa matumizi ya neno kujivuwa gamba.

  Kuna storm kubwa inakuja ambayo cha kusikitisha mpaka sasa Watanzania wameshindwa kusoma alama za nyakati kwamba Mungu ameamuwa kujidhihirisha upande wa Wananchi lakini cha kushangaza taasisi za kiraia na kidini ziko kimya juu ya swala hili.

  Kwa hakika huu ndio wakati muhafaka wa kuing'oa serikali ya Kikwete madarakani, hatuna sababu ya kusubili mpaka 2015 maana hata JK akisema avunje baraza lake leo atapata Mawaziri kutoka miongoni mwa Wabunge wepi? Lusinde!!??....
   
 24. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #24
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,252
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 48

  Ngoja tuendelee kuangalia wanavyomalizana wenyewe kwa wenyewe. Sikujua kama wamefikia hapo!!
   
 25. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #25
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 658
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Now your talking Pasco. Kuna haja ya kuazima viongozi wa nchi zingine watusaidie kupata solution ya mambo yetu. Napendekeza kazi ya kutafuta mkandarasi wa hizo bandari tuwape Rwanda, Burundi, Zambia na Malawi watutafutie mkandarasi, ajenge then mwishoni watupe gharama, nzima tuwalipe, maana hawa ndugu zetu bandari hii ni muhimu kuliko sisi tunavyofikiri. Maskini Tanzania mafisadi wanagombania kama mpira wa kona
   
 26. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #26
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,207
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 48
  Pasco anatia mkwara tuu huo. Kwanza ile habari ya asubuhi vipi keshaifafanua?
   
 27. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #27
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,403
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Wengine tumeshindwa kuifungua hiyo attached file.
   
 28. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #28
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 63
  JK anapaswa avunje baraza au Pinda aachie ngazi au wale Mawaziri wajiuzuru wenyewe later today, maana zikija kupigwa kura utashangaa kura robo tatu zitasema hatuna imani na Pinda, maana kama watasubiri mpaka kura zipigwe maana yake zitakuwa ni kura za siri na hapo ndipo utakapojuwa kumbe hii move inaungwa mkono zaidi na CCM kuliko hata Upinzani wenyewe.
   
 29. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #29
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 27,733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 63
  Aliamka na hangover akadhani yupo Facebook, kuja kutaamaki ameshapost ule utumbo, basi tumsamehe bure na saa hizi yupo Sinza kwa wajanja!!......
   
 30. G

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #30
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 8,205
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 48
  mi nathani hiyo miaka 45 haitakuwa na shida kama kodi watakayokuwa wanalipa hao wawekezaji itawekwa in such a way ina appreciate! Maana hata tukipewa tuendeshe hizo berths nakuhakikishia hata hiyo miaka 40 haitafika! na isitoshe kuna nyingine 12 ambazo TPA na TICTs wanazimiliki kwahiyo sioni tatizo!
   
Thread Status:
Not open for further replies.

Share This Page