Nyaraka muhimu kwa Maombi ya Kazi; Barua, CV /Resume na Rejea

Huu ndio ushauri bora.kuna wengine sijue ni mashetani ukiomba ushauri anakujibu kwa matusi mwanzo mwisho,sijui hakuzaliza na mama
 
Nice arangment.....hongera mkuu!!


Najua unatujaribu uzalendo wetu...

1. Personal Details
Jina
Sex
D.O.B and P.O.B
Contacts zote simu, box, email, etc
Unaweza ongeza kama Martial Status, Nationality etc

2. Education Background:
Andika ulikosomea, ukianza na elimu yako ya mwisho kabisa. Mfano umemaliza chuo sasa hivi (2013), Basi anza na hiko chuo, kisha shule kabla hujaingia iko chuo etc hadi shule ya msingi inakua chini kabisa.

pia kila uliposoma ni vema ukiandika mwaka na mwezi ulivyoanza hadi ulivyo maliza (kama utakumbuka na tarehe vema zaidi). Pia andika ulichopata (awards).

Cheki mfano huu:

dateinstitutionawards
october 2010-march 2012SIJUI NINI UniversityBA in Sanaa
january 2008-februaly 2010matoke secondary schoolACSEE
Jan 2004 - october 2007wavulana secondary schoolcsee

Wengi wanapendea kuweka katika table ila ata vingine sawa tu.

4. Work Experience.
Tupia sehemu ulizo wahi kufanya kazi, muda ulio fanya kazi na cheo chako bila kusahau majukumu yako ya kazi. anza na kazi ya hivi karibuni ukirudi nyuma. kama hapo juu kwenye education. hapa sio muhimu/usiweke table.

NB: Ni muhimu sana kuandika duties and responsibilities zako ulipokua unafanya kila kazi.

5. Publications/projects

kama umeshawahi kuandika project na kuirelease mtandaoni au kabidhi some where, andika hapa jina la hiyo project (title), ulipo submit, tarehe, etc


6. Other Skills and Activities.

Andika vitu unavyo jivunia wewe binafsi ambavyo unaweza usiwe na vyeti vyake au unavyo. mfano: udereva, kompyuta, problem solving skills, comunication skills, leadership, kama unajua lugha kibaaaao andika, etc


7. Referees

Andika majina ya watu wa3 ambao itakua rahisi muajiri wako kuwasiliana nao ili kupata taarifa zako. wanaweza kua maboss wako, mwalimu wako, wafanyakazi wenzako etc. pendelea kuandika wale watu ambao mnaingiliana katika mambo ya kazi, sio unaandika mke wako, shemeji yako, baba yako etc ata kama ana hela sana ila usimweke.

Weka hivi:

Jina lake
Cheo
Anuani yake (posta, namba za simu na email)


Kumbuka CV ina badirika badirika kutokana na matakwa ya kazi iliotangazwa, so uwe unai update kila unavyoomba kazi mpya.

Pia kuna format kibao za kuandika CV so wadau wanaweza kuongeza zingine hapa.

mwisho, pendelea kutumia GOOGLE, haijawahi shindwa kitu.


 
Jamani mimi sijui inafananaje, humo kwenye cv unaandika nini na hiyo cv kirefu chake ni nini?
natanguliza shukrani!
 
Curriculum vitae ..... Elimu yako na kazi zako za kitaalam. Utaalam wowote ule, research papers, shule ulizopitia, ,jourals ulizoandika kwenye majarida ya kitaalam etc.. ni sawa na kueleza uwezo wako kitaalam na hutumiwa na watu waliosoma elimu za juu sana kama PhDs wakati wakomba kazi zinazohitaji utaalam mkubwa.

Wengi wetu tunapenda kufananisha hii na "Resume" ambayo ni historia yako kikazi na kielimu, kwa watu ambao wanatafuta kazi wakiwa na utaalam wa kawaida na katika fields ambazo siyo rare professions.

Kwa mfano, karani wa Benki huombwi CV ila resume. Mtafiti wa dawa ya Ebola, huombwa CV, siyo resume.
 
Namna ya kuandika CV bomba/nzuri.


CV yenye kujitosheleza ni njia muafaka ya kumfanya bosi wako mtarajiwa kukufahamu wewe. CV nzuri inakupa nafasi ya kung’aa katika kikundi na kupata fursa ya usahili na baadae kazi.

Pitia matangazo ya kazi

Unapopitia matangazo ya kazi katika magazeti, kuta za matangazo au barua pepe hakikisha unapitia matangazo hayo kwa umakini. Fanya maamuzi ya kipi kati ya ujuzi, sifa ama uzoefu utatumia katika kazi yako mpya.


Orodhesha vitu hivi na tumia maneno yenye kuonyesha vitendo kwa mfano : Mimi ni mtu mwenye mpangilio, ufanisi na mchapa kazi, nimeongoza na kusimamia watu na matukio. Nimesoma na kufikia ubora katika weledi na kumaliza shahada ya kwanza katika…..

Kua sahihi kwa kutoa maelezo mafupi yenye kueleweka
Usizidishe maelezo kwa kutoa maelezo yote kukuhusu wewe, hakuna anayetegemea wala kutaka kuyasikia hayo kwa hiyo usifanye hivyo.


CV inatakiwa kumwelezea mtu lakini si kama kitabu kinachoelezea wasifu wako lakini pia si aya/ibara ama kitabu unachoelezea hadithi ya maisha yako ya weledi! Hakikisha huweki taarifa zako binafsi ambazo hazihusiani na nafasi unayoomba.


Sema ukweli

Kua mkweli. Kwa kufanya hivyo unaonyesha kujiamini na mafanikio yako na hii itakusaidia inapokuja kukaa kwa ajili ya usahili. Huwezi kuzungumza kuhusu uzoefu wako kama mwanasayansi wa nyuklia kama hukufaulu masomo ya sayansi shuleni!


Epuka makosa haya

Vitu vichache vya kuepuka kufanya: Usidanganye, usizidishe chumvi, usiweke ahadi usizoweza kuzitimiza.


Vidokezo katika kujielezea

Orodhesha majumuisho yako.
Elezea CV yako katika lugha chanya.
Inasaidia kama utaandika sentensi fupi na zenye kuonyesha uhai na kuepuka kutumia vivumishi vingi.

Anza na mafanikio yako ambayo yanawiana na mahitaji muhimu ya kazi. Usimweleze mwajiri ni kwa vipi atakusaidia bali mueleze ni kwa vipi wewe utamsaidia.

Tia msisitizo katika uzoefu unaohusiana na biashara ama kazi husika. Kama una uhusiano mzuri wa kazi na wataalamu katika fani yako unaweza kuwaomba kuwatumia kama wadhamini.


Pata ushauri kabla hujatuma CV yako. Tafuta mtu unaemjua katika fani husika ili apitie CV yako. Jiandae kurekebisha vitu ulivyoandika.


Jaribisha CV yako kwa kuomba nafasi mbalimbali katika kiwango chako lakini pia kiwango cha juu kidogo. Hii itakusaidia kujua soko la ajira na thamani yako.


Isiwe sawa kila wakati

CV yako inabidi iwe inaendana na kazi unayoomba. Hivyo basi wakati unaomba kazi tofauti kwa kutumia CV ile ile ni vizuri ukajaribu kuiweka CV ikaendana na nafasi unayoomba.


Usikate tamaa

Tumia CV yako kuitwa kwenye usahili. Huko utapata fursa ya kuelezea mafanikio yako.
Kitu cha muhimu, USIKATE TAMAA! Kwa kila CV 100 unazotuma unaweza kuitwa kwenye usahili mara 10, na katika mara kumi hizi utapata kazi moja tu- kazi yako ipo inakusubiria. Kua makini na mwenye malengo na muda si mrefu utakua mmoja ya watu katika dunia ya kazi.

Chanzo: http://www.mywage.org/tanzania-sw/nyumbani/kazi/kutafuta-kazi/andika-cv-nzuri
 
Habari.

Nimekutengenezea CV. Nime ambatanisha mafaili matatu. Kuna cover letter, Resume na Reference ambayo ni referee.

Hata siku moja usiweke referee kwenye CV yako. na usije ukaandika Curriculum Vitae kwenye Resume yako, ni makosa. utaonekana sio professional.

Natumai nimekupa mwanga. Unaweza uka edit hizo attachments kutokana na ujuzi na kisomo chako.
 

Attachments

  • Dar es Salaam.docx
    12.5 KB · Views: 656
  • Masaki Street.docx
    905.2 KB · Views: 617
  • kwetu.docx
    12.5 KB · Views: 562
CV
Personal particulars
Name
Sex
Marital stastus
Address
Contacts i.e emails
Height
EDucation background
Unaanzia level ya elimu yako then unamalizia na level ya chini kabisa.
WORKING EXPERIENCE
unapangilia kama kwenye education background.
ADMINSTRATIVE EXPERIANCE(LEADERSHIP)
Hapa utaandika uzoefu wako katika uongozi.
OTHER SKILLS
Ujuzi ulionao aina yayote utaandika hapa.
HOBI
Utaandika hobi yako/zako
INTRESTI
.............
SEMINA, SIMPOZIAMU,
PRESENTATION
.. .. .
......

RESEARCH
.. .........
Referees
..andres na contacts zao.

NB:: CV huwa inabadilika na inafanyiwa marekeb
isho kutokana na uhitaji pia na muhuska kuendelea kupata maarifa mbalmbal.
Nilichotoa ni kama mfano wa mpangilio wa cv
 
Back
Top Bottom