Nyara za Serikali - Suali.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Ilivyokuwa ile sehemu ya kuuliza naona siku hizi haipo tena ,imenibidi niweke hili suali hapa.

Nauliza kuhusu neno "Nyara za serikali" hivi jamani haya ni mambo gani,maana kwanza hili neno nyara naona pia linanikoroga kwani juzi nimesoma kwenye gazeti kuwa polizi wamemkamata mtu akiwa na nyara za serikali nilipozidi kusoma nikaona kuwa ni nyama ya Paa ,nikastaajabu sana polisi kumkamata mtu akiwa na nyama ya paa na vilevile alikuwa na nyama ya ngurue mwitu(Ngiri) nikaona au kujiuliza kama mtu angekutwa na nyama ya mapanya yale makubwa au mapanya buku kama yanavyojulikana nae angekamatwa ,hapo ndio nikaona bado sijalifahamu neno Nyara.

Hivyo nahitajia msaada wa kufahamishwa maana na jinsi serikali inavyojihusisha kwa kuwakamata watu wakutwapo na nyara.
 
Kuna maliasili fulani ambazo ni haramu kuwa nazo (pembe za tembo, faru, ngozi za chui etc) au unahitaji kuwa na kibali cha serikali. Hizi maliasili ni moja kati ya nyara za serikali. Hao panya kama hamna haja ya kibali na wala si haramu unawinda unavyotaka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom