Nyamongo: "CDM wametujali watasimamia mazishi ya mwanangu" J'tano

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Baadhi ya maneno ya wafiwa
"Chadema ndio ambao wameonyesha huruma ya kutusaidia"
"Chadema watasimamia mazishi ya mwanangu".
"Aprili mwaka jana nilimzika mdogo wangu, Mwita Ngoka, baada ya kupigwa risasi na mwaka huu mdogo wake, Chacha Ngoka, amekufa kwa kupigwa risasi na polisi hao hao"

Soma habari kamili (Mwananchi)

MIILI ya watu wanne kati ya watano waliouawa na polisi katika mgodi wa African Barrick North Mara katika eneo la Nyabirama Nyamongo, wilayani Tarime itazikwa Jumatano wiki Ijayo baada ya kufanyiwa uchunguzi utakaowasaidia wafiwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya serikali.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na ndugu wa marehemu pamoja na uongozi wa Chadema, zinaeleza kuwa baada ya kutokutendewa haki na viongozi wa Serikali ndugu hao wamekubaliana mazishi hayo yagharimiwe na Chadema ambao wameonyesha kuwajali.

Ndugu hao wa marehemu waliiambia Mwananchi Jumapili kuwa wamepanga mazishi hayo kufanyika Jumatano baada ya shughuli za kuaga kufanyika katika Uwanja wa Sabasaba mjini Tarime.Vile vile wamesema wamekataa kuchukua rambirambi za Serikali kwa wakidai kuwa ni sawa na kuuawa kwa makusudi kwa ndugu zao halafu wao wachukue rushwa ya rambirambi.

Mmoja wa ndugu hao wa marehemu, Magige Gati, alisema wafiwa wamekubalia kuipa kazi ya kuratibu mazishi Chadema kwa sababu ndio ambao wameonyesha huruma ya kuwasaidia.Alisema Serikali imeshindwa kuwasaidia zaidi ya kuanza kuwatisha kuwa wazike haraka kabla ya kufanyika kwa uchunguzi wa kisheria.

Naye Samson Chacha Ngoka, mkazi wa Kewanja alisema Aprili mwaka jana alimzika mdogo wake, Mwita Ngoka, baada ya kupigwa risasi na mwaka huu mdogo wake mwingine, Chacha Ngoka, amekufa kwa kupigwa risasi na polisi hao hao, hivyo wananchi wameweka msimamo wa kutokubali kudanganywa na Serikali kukubali kuzika mapema kabla ya uchunguzi kufanyika.

"Mimi sikupenda mwanangu afe, nimehangaika naye halafu leo naambiwa siasa kweli, waue mwanangu kisha waje kunibembeleza kwa fedha haki ikowapi hapa," alisema huku akitokwa na machozi na kuongeza: "Chadema watasimamia mazishi ya mwanangu".

Katika hatua nyingine, viongozi wa juu wa Chadema, akiwamo Mbunge wa Singida Kaskazini, Tundu Lissu na Kada wa chama hicho, Mabere Marando, walitarajiwa kufika jana mjini Tarime kushughulikia taratibu za kisheria. Mkurugenzi wa Sera na utafiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwita Waitara, alisema jana kuwa chama chake kimechukua jukumu la kuratibu mazishi ya watu hao wanne.

Akieleza jinsi Chadema ilivyojipanga katika kuhakikisha inawasaidia wafiwa katika shughuli hiyo, Waitara alisema: "Mazishi ni Mei 24. Tutabeba miili ya marehemu na kuileta Uwanja wa Sabasaba kabla ya kutawanyika kulingana na mipango ya ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko."Alisema Chadema haihofii vitisho vya polisi vya kuongeza vikosi vya askari polisi pamoja na magari ya maji ya kuwasha siku ya tukio hilo.

Alisema kabla ya siku hiyo watahakikisha wanamwona Mkuu wa Wilaya na Kamanda wa Polisi wa Wilaya kuweka wazi msimamo wao dhidi ya mauaji hayo.Kauli hiyo ya Chadema imekuja muda mfupi baada ya wanasheria wawili kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Onesimo Ole Ngurumwa na Pasience Mlowe, kukutana na wafiwa na kuwaahidi kuwa wamekusudia kuwapatia msaada wa kisheria kudai haki baada ya tukio hilo.

Wakati huo huo, polisi wamegonga mwamba katika jutihada za kutaka kuwalazimisha wafiwa kuzika miili ya ndugu zao mapema kabla ya kukamilisha taratibu za kisheria.Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Mwikwabe Makena aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa polisi waligonga mwamba kutokana na msimamo wa familia kuwa hawatazika mpaka haki ipatikane.

Diwani amwaga machozi
Kutokana simanzi iliyojaa eneo hilo diwani Viti Maalumu (Chadema), PhelomenaTontora, huku akitokwa machozi alisema, "Ukimwi, ajali na risasi zinamaliza vijana wetu…"
Mkuu wa wilaya alipoulizwa kuhusiana na tuhuma za wasiwasi wao alijibu; "Suala lao liko mikononi mwa polisi uwaulize wao watakupa taarifa zote.
 
nawapa pole wafiwa wote,MUNGU mkubwa haki itapatikana tu,NDUGU WATANYANIA WENYANGU NATOA RAI HATUNA HAJA ZA KUENDELEA KUIVUMILIA SERIKALI KATILI KAMA HII MIAKA MI4 NI MINGI MNO WANAWEYA TUUWA WOTE TUAMKE WAKATI NI HUU!
 
Nyota ya Chadema kwenye duru za siasa inazidi kung'ara wananchi wameanza kuwaamini hata kabla ya kuingia madarakani Mungu awape nini zaidi.
 
Serikali inawaua RAIA ambao wamewapa ridhaa ya kuongoza.Watanzania tunatakiwa kubadilika.
 
I ever said in this forum that:-
The prompt indicator of persisting POVERTY is following the rule of Law!
 
Chadema bwana wanafiki kweli sijui kwa nini wanachagua misiba mpaka msiba ukiwa na maslahi juzi kafariki Sheikh Yahaya, hakuna ata kiongozi wa Chadema alifika msibani, ata kwenda nyumbani kwa Sheikh Yahaya kutoa pole wakati mtoto wa Marehemu Sheikh Yahaya, Hassana Yahaya Hussein ndio mpambananaji wa Chadema Magomeni, na alikuwa mgombea kiti cha Udiwani kata ya Mikumi Magomeni kupita Chadema, kwenye uchaguzi wa mkuu, hamna lolote wanafiki tu
 
Mtafute Muhadhiri jana alijibiwa vizuri sana haya mambo.
 
Chadema bwana wanafiki kweli sijui kwa nini wanachagua misiba mpaka msiba ukiwa na maslahi juzi kafariki Sheikh Yahaya, hakuna ata kiongozi wa Chadema alifika msibani, ata kwenda nyumbani kwa Sheikh Yahaya kutoa pole wakati mtoto wa Marehemu Sheikh Yahaya, Hassana Yahaya Hussein ndio mpambananaji wa Chadema Magomeni, na alikuwa mgombea kiti cha Udiwani kata ya Mikumi Magomeni kupita Chadema, kwenye uchaguzi wa mkuu, hamna lolote wanafiki tu

Mamia wamzika Sheikh Yahya
• JK, Mbowe, Lipumba, Mahita, Cheyo, Mwinyi waongoza

na Bakari Kimwanga

amka2.gif
MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiongozwa na viongozi wa serikali, dini, vyama vya siasa na makundi ya jamii jana walijitokeza kwenye mazishi ya mnajimu mashuhuri nchini na Afrika Mashariki ya Kati, Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia juzi.
Sheikh Yahya Hussein (87), aliyefariki dunia juzi majira ya saa nne asubuhi, muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mtakatifu Ukombozi, Kinondoni baada ya kuugua ghafla alizikwa katika makaburi ya Tambaza.
Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mufti, Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Shaaban bin Simba, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), la Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo, ni miongoni mwa viongozi waliokuwapo kwenye mazishi hayo yaliyowafanya wakazi wa jiji hilo kuacha shughuli zao kwa muda ili kushiriki.
Baadhi ya viongozi waliokuwapo nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya, Mwembe Chai eneo la Magomeni, walisema kuwa kifo chake ni pigo kubwa kwa Watanzania na hasa Jumuiya ya Waislamu kwa kuwa alikuwa mstari wa mbele kupigania haki za Waislamu.
Mchungaji Lusekelo, alisema kuwa kifo cha Sheikh Yahya ni pigo kubwa kwa Waislamu na hata watu wa dini nyingine kutokana na kuwa msuluhishi mkubwa ilipotokea kuna kutokuelewana kwa viongozi wa dini hizo au makundi mengine ya kijamii.
"Siku tatu nyuma niliota Sheikh Yahya amepandishwa daraja kubwa la uongozi… lakini siku iliyofuata nikasikia taarifa za kifo chake, nilimheshimu na kumpenda kutokana na hekima na busara zake wakati wa uhai wake na hata ulikuwa ukija kwa ajili ya kuomba ushauri hakusita kufanya hivyo kwa wakati.
"Yapo aliyoyafanya na kuwa mchango mkubwa wa nchi yetu, lakini kutokana na aliyoyafanya Mungu amuweke mahali panapostahili, tupo pamoja katika kuomboleza msiba wa Sheikh Yahya na subira ni jambo jema kwa wafiwa," alisema.
Masheikh washindwa kujizuia
Hali ilibadilika katika eneo la msiba mara baada ya mshereheshaji kutambulisha mwanafunzi aliyepewa kofia na Sheikh Yahya, Said Idd kusoma Kuraani huku akitumia sauti ya marehemu Sheikh Yahya na kuwafanya watu kububujikwa machozi mara kwa mara.
Mwanafunzi huyo ambaye pia alivaa mavazi yanayofanana na yale yaliyokuwa yakivaliwa na Sheikh Yahya, alishindwa kuendelea kusoma Kurani hiyo, jambo lililozidisha simanzi kwa waliokuwapo eneo la tukio.
Mawaidha ya Mufti Simba
Mufti, Simba alisema kuwa kifo ni njia ambayo haiepukiki kwa kila binadamu na kila aliye hai anatakiwa kutambua kuwa ni mfu mtarajiwa.
Alisema kutokana na mazingira hayo ni muhimu kila mtu kufanya maandalizi ya kifo kwa kufanya mambo ambayo yatampendeza Mungu mara baada ya kufariki dunia kwa kuwekeza katika mema kama ilivyokuwa kwa marehemu Sheikh Yahya Hussein katika uhai wake.
"Sheikh Yahya, alikuwa mshauri wangu katika mambo mbalimbali na tulifahamiana tukiwa vijana kabisa mkoani Mwanza, alikuwa mwalimu mzuri wa Kuraani, tumeondokewa na tumepata pengo kubwa katika Uislamu nchini," alisema Mufti Simba.
Pamoja na hatua hiyo, viongozi wa vyama vya siasa nchini walipata fursa ya kutoa salamu za vyama vyao katika msiba huo huku Chama Cha Mapinduzi kikiahidi kumuenzi Sheikh Yahya kama mwanachama wao mashuhuri.
Nape Nnauye
Akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika msiba huo, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema utabiri wa Sheikh Yahya ni kigezo tosha cha kumuenzi hasa kwa kuthamini amani na utulivu wa Tanzania.
"Mengi ameyatabiri na alikuwa mwenzetu na katika hili tutaandaa utaratibu wa kumuenzi kada wetu huyo na aliweza kutabiri juu ya maridhiano ya visiwani Zanzibar kati ya CCM na CUF na sasa imekuwa kweli, hakika hiki kilikuwa ni kigezo tosha kwa amani ya nchi yetu," alisema Nape.
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, alitoa pole kwa familia kutokana na msiba huo, alisema umaarufu wa Sheikh Yahya ni fundisho kwa wanasiasa nchini kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kupigania amani ya Watanzania kila mara.
"CHADEMA tumeguswa na msiba huu na hakika umaarufu wa Sheikh wetu ni fundisho kwetu sisi wanasiasa, tumeshtushwa na kifo chake na tunamuombea kwa Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mbowe.
Profesa Lipumba
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema ili kumuenzi Sheikh Yahya ni muhimu kwa wanasiasa kufanya siasa za kutodharauliana na kulinda misingi ya amani ya nchi bila kuwa na ubaguzi.
Alisema alimfahamu Sheikh Yahya mwaka 1971 akiwa mkoani Tabora katika Msikiti wa Manyema ambapo alikuwa akienda kufundisha Kurani.
"Sheikh Yahya alikuwa hapendi kudharauliana na katika hili ni lazima tumuenzi kwa kuepuka kufanya siasa chuki na kudhauriana, alikuwa muasisi wa Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki hadi kufikia kuwa katibu na hakika ni pengo kubwa katika fani ya usomaji wa Kurani nchini…CUF tunawapa pole wafiwa kwa msiba mzito na kikubwa ni kuwa na subira," alisema Profesa Lipumba.
Naye Sheikh na mwanazuoni kutoka taasisi ya Mwinyi Baraka Foundation, Sheikh Khamis Mataka, alisema kuwa katika uhai wake Sheikh Yahya, alikuwa mwanazuoni wa daraja la juu kwani alifikia hatua ya kuwalipa mishahara walimu wanaosomesha Kurani nchini.
Sheikh Mataka, alisema mara baada ya kurudi akitokea nchini India, aliwaita wanafunzi wake wote waliokuwa wakifundisha Kurani katika madrasa mbalimbali na kueleza azima yake hiyo.
"Sheikh alituita wanafunzi wake hasa tuliokuwa tukifundisha Kurani katika Mkoa wa Dar es Salaam, na alipanga utaratibu wa kuanza kulipa mishahara kila mwezi na kima cha juu kilichokuwa kinalipwa ni sh 500,000 na sasa warithi wana kazi ya kuenzi kazi na Kurani katika nyumba yake," alisema.
Mara baada ya kutolewa mawaidha na masheikh na salamu kutoka kwa viongozi wa vyama vya sisa, msafara wa kuelekea makaburini ulianza majira ya saa 8:45 mchana ambapo kulijitokeza kundi kubwa la Waislamu likipinga mwili wa Sheikh Yahya kuingizwa katika magari na badala yake wakataka kutembea kwa miguu hadi Msikiti wa Manyema uliopo Kariakoo kwa ajili ya Swala ya Jeneza.
Hata hivyo hatua hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi hayo ambaye pia ni Sheikh wa Mkoa, Alhad Mussa Salumu, kuwa katika wakati mgumu lakini kutokana na hali hiyo ilimfanya kukubaliana na waumini wake na msafara kuanza, ambapo ulipitia Barabara ya Morogoro, Lumumba hadi Msikiti wa Manyema.
Kutokana na hali hiyo, barabara zilifungwa ili kupisha maelfu ya watu hao waliojitokeza kumsindikiza katika safari yake ya mwisho Sheikh Yahya.
Kuelekea makaburini
Ilipotimu saa 10:30 msafara wa kuelekea makaburini kutoka Msikiti wa Manyema uliingia tafrani baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adamu Malima, kupanda katika gari na ghafla kujikuta akishushwa na watu hao waliokuwa wakisindikiza jeneza la marehemu Sheikh Yahya.
Malima, akiwa makaburini alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa machozi na kumfanya kuwa katika wakatika mgumu kila mara hasa alipokuwa akiuangalia mwili wa mnajimu huyo.
Rais Kikwete ahudhuria mazishi
Katika makaburi ya Tambaza maelfu hayo ya wananchi waliongozwa na Rais Jakaya Kikwete katika msiba huo.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya msiba huo, Sheikh Alhad Mussa Salum, alisema Rais Kikwete amepata fursa ya kuhudhuria msiba kwani alifika nchini muda saa 10:30 akitokea nchini Namibia.
Watu wengine mashuhuri waliohudhuria msiba huo wa Sheikh Yahya ni pamoja na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Omari Mahita, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Husein Mwinyi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima.
 
Chadema bwana wanafiki kweli sijui kwa nini wanachagua misiba mpaka msiba ukiwa na maslahi juzi kafariki Sheikh Yahaya, hakuna ata kiongozi wa Chadema alifika msibani, ata kwenda nyumbani kwa Sheikh Yahaya kutoa pole wakati mtoto wa Marehemu Sheikh Yahaya, Hassana Yahaya Hussein ndio mpambananaji wa Chadema Magomeni, na alikuwa mgombea kiti cha Udiwani kata ya Mikumi Magomeni kupita Chadema, kwenye uchaguzi wa mkuu, hamna lolote wanafiki tu

no ritz,nilimwona mbowe kwenye msiba,halafu hata sheikh mkuu hujui ni mwanachama?
 
Chadema bwana wanafiki kweli sijui kwa nini wanachagua misiba mpaka msiba ukiwa na maslahi juzi kafariki Sheikh Yahaya, hakuna ata kiongozi wa Chadema alifika msibani, ata kwenda nyumbani kwa Sheikh Yahaya kutoa pole wakati mtoto wa Marehemu Sheikh Yahaya, Hassana Yahaya Hussein ndio mpambananaji wa Chadema Magomeni, na alikuwa mgombea kiti cha Udiwani kata ya Mikumi Magomeni kupita Chadema, kwenye uchaguzi wa mkuu, hamna lolote wanafiki tu

Jaribu ku keep updated.
 
chadema bwana wanafiki kweli sijui kwa nini wanachagua misiba mpaka msiba ukiwa na maslahi juzi kafariki sheikh yahaya, hakuna ata kiongozi wa chadema alifika msibani, ata kwenda nyumbani kwa sheikh yahaya kutoa pole wakati mtoto wa marehemu sheikh yahaya, hassana yahaya hussein ndio mpambananaji wa chadema magomeni, na alikuwa mgombea kiti cha udiwani kata ya mikumi magomeni kupita chadema, kwenye uchaguzi wa mkuu, hamna lolote wanafiki tu

avatar yako tu inaonyesha jinsi ulivyo pumba. Soma magazeti ya leo.
 
Chadema bwana wanafiki kweli sijui kwa nini wanachagua misiba mpaka msiba ukiwa na maslahi juzi kafariki Sheikh Yahaya, hakuna ata kiongozi wa Chadema alifika msibani, ata kwenda nyumbani kwa Sheikh Yahaya kutoa pole wakati mtoto wa Marehemu Sheikh Yahaya, Hassana Yahaya Hussein ndio mpambananaji wa Chadema Magomeni, na alikuwa mgombea kiti cha Udiwani kata ya Mikumi Magomeni kupita Chadema, kwenye uchaguzi wa mkuu, hamna lolote wanafiki tu
CCM itawakilishwa na nani kwenye mazishi Nyamongo, Kikwete, Mukama, Nape, au Nyangwine.
 
Nyota ya Chadema kwenye duru za siasa inazidi kung'ara wananchi wameanza kuwaamini hata kabla ya kuingia madarakani Mungu awape nini zaidi.

KWELI NIMEAMINI MISIBA NI MTAJI KWA CHADEMA.....ARUSHA NA SASA NYAMONGO....WAFE WENGINE ,WENGINE IWE NDO NGAZI YAO YA KUKWEA UMAARUFU....shame...shame..shame...!(watu wavamie mgodi wakiwa na silaha,wapambane na polisi leo wanageuka wanasiasa?)
KUFA KUFAANA....!
 
Acha uongo......... Haya yalikuwa maneno ya Mwenyekiti CHADEMA kwenye mazishi
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, alitoa pole kwa familia kutokana na msiba huo, alisema umaarufu wa Sheikh Yahya ni fundisho kwa wanasiasa nchini kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kupigania amani ya Watanzania kila mara.
"CHADEMA tumeguswa na msiba huu na hakika umaarufu wa Sheikh wetu ni fundisho kwetu sisi wanasiasa, tumeshtushwa na kifo chake na tunamuombea kwa Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mbowe.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom