Nyambari Nyangwine: Kwa ahadi nilizotekeleza Tarime, CHADEMA hawawezi kuning'oa 2015

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,651
2,627
Mbunge wa Tarime, Nyambari Chacha Nyangwine amesema kuwa ahadi kubwa alizoahidi jimboni Tarime amezitekeleza ikiwemo kusambaza umeme maeneo mbalimbali jimboni humo.

Akizungumza na Jambo press hapa arusha hii leo Nyangwine ameeleza kuwa mbali na umeme amefanikiwa kusimamia malipo ya fidia kwa watu 13 walioathiriwa na maji ya kemikali ktk mgodi wa North Mara hatua itakayowezesha kampuni hiyo kutoa malipo haraka iwezekanavyo siku chache zijazo.

Katika kuhakikisha kuwa mgodi huo unawasaidia wakazi wa Tarime, bw. Nyangwine ameeleza kuwa amefanya mazungumzo yaliyozaa matunda kwa kampuni ya North Mara kukubali kutenga mfuko maalum wa maendeleo na pia kutengwa kwa fedha za fidia za wakazi waliohamishwa kupisha upanuzi.

Aidha kutokana na mafanikio hayo mbunge huyo wa Tarime amedokeza kuwa CHADEMA ina kazi ngumu kumwangusha ktk kiti cha ubunge jimboni humo mwaka 2015.

TARIME NI JIMBO LILILOTAWALIWA NA WABUNGWE WATATU NDANI YA MIAKA MINNE ILIYOPITA.
 
Huyu alisaidiwa na chadema kushinda ashukuru hilo asingekua mbunge kamwe kama sio migawanyiko chadema...mbona hajazuia mgodi kuua watu kila uchao?!! Tarime kuna barrier kila kona ya kamji kadogo kale kuna askari ambao hao kaZi yao ni kuua watu tu na kufanya ujambazi...
 
M4C haijalishi umetekeleza ahadi au la kwan maadam ww ni gamba basi huwezi salimika maana naimani hapo tarime kuna jembe letu Heche litafanya maajabu.

Heche ndo alisababisha jimbo la Tarime likaenda ccm, alikuwa anampiga vita ya chinichini Waitara
 
mwacheni ajambe maputo m4c itamuezua hata kama akiwapa vipande vya dhahabu wanatarime
 
ameshajua kuongea kiswahili vizuri??au bado anaita makampuni MAGAMBUNI??
 
Yawezekana ayasemayo yakawa namna ya kujihami tu, pia hajui kuwa raia bado hajui faida ya madini zaidi ya vifo vya raia wasio na hatia. Pia yeye anafikiri CHADEMA jukumu lao ni kuongoza badala ya kutwa nchi, yeye baada ya kuzungumzia mauji ya raia anaiwaza CHADEMA. Ina maana nyinyiemu wana hofu sana na CHADEMA.
 
Wala asipoteze muda mpaka 2015 aachie ngazi hata Leo hivyo anavyosema amefanya wala havihitaji kufanywa na mbunge hata mjumbe wa nyumba kumi anaweza
 
Hakika namwambia moto huu wa m4c hautomwacha mpaka 2015,m4c inanusa damu ya magamba popote pale yalipo,ukikutana nao bora ukajivua gumba mwenyewe kabla ya kuvuliwa na kuvishwa gwanda
 
Aachane na hizo ndoto za mchana wananchi wake wanauawa kila siku kwakupigwa risasi na polisi wanaowalinda hao wezi wanaoitwa wawekezaji na chama cha magamba afu yeye amekaa Dar es salaam tu hakuna lolote analofanya zaidi yakuwaza ubunge tu!!Huyu ni mmoja ya wabunge wa ovyo kabisa kuwahi kutokea katika hii nchi...akili yake na ya Lusinde hazipishani.
 
Kiazi huyu jamaa!anaongea pumba hakuna mfano,ukikaa nae dk.30 lazima akuchefue na masifa yake!
 
mbunge wa tarime ni ester matiko wa chadema huyo ambaye hana hata nyumba tarime anaishi kwenye nyumba ya kupanga wakati wa uchaguzi na saizi akija tarime anafikia hotel alafu anajiita mbunge wa tarime kachemka sana piia nampa ole sana 2015 asijisumbue
 
Tata Nyangwine, wewe unawajua sana wana Tarime, unakumbuka siku ile kitendawili cha nani atashinda, wewe wajua jinsi unavyopingwa, pole sana ndg yangu, nadhani ukitaka mambo yako yaende tangaza kuhamia CDM, halafu uwaombe wanatarime msamaha, waambie haukujua kwamba moyoni mwako unaipenda CDM, Kweli ndg yangu hebu leo unaweza kufanya mkutano wa hadhara hapa mjini Tarime? unakumbuka Nyamongo mkiwa na m/kiti wa halmashauri? kiukweli ile siyo picha njema kwa kiongozi kama ww, nakuomba ushauri huu utafakari
 
Mbunge wa Tarime Mh Nyambari Chacha Nyangwine amesema kuwa ahadi kubwa alizoahidi jimboni Tarime amezitekeleza ikiwemo kusambaza umeme maeneo mbalimbali jimboni humo. Akizungumza na Jambo press hapa arusha hii leo Nyangwine ameeleza kuwa mbali na umeme amefanikiwa kusimamia malipo ya fidia kwa watu 13 walioathiriwa na maji ya kemikali ktk mgodi wa north mara hatua itakayowezesha kampuni hiyo kutoa malipo haraka iwezekanavyo siku chache zijazo. Katika kuhakikisha kuwa mgodi huo unawasaidia wakazi wa tarime bw nyangwine ameeleza kuwa amefanya mazungumzo yaliyozaa matunda kwa kampuni ya North mara kukubali kutenga mfuko maalum wa maendeleo na pia kutengwa kwa fedha za fidia za wakazi waliohamishwa kupisha upanuzi. Aidha kutokana na mafanikio hayo mbunge huyo wa Tarime amedokeza kuwa Chadema ina kazi ngumu kumwangusha ktk kiti cha ubunge jimboni humo mwaka 2015. TARIME NI JIMBO LILILOTAWALIWA NA WABUNGWE WATATU NDANI YA MIAKA MINNE ILIYOPITA.

Huyu Nyagwine ni Mpuuzi Hajatekeleza Ahadi yeyote, 1. Umeme nguzo zilikuwepo kabla hata ya kuwa mbunge ni mradi REA, 2. Malipo ya mgodi hukasaidia kwa lolote anakimbilia mambo tu. 3 Hakai Tarime 4. Hawaelewani ni mwenyekitui wa CCM Tarime hapiti 5) Wafadhili wake na campaign organisers hawataki tena kwa sababu anatukana watu kama Lusinde. This guy is out of his mind hawezi kuwa mbunge tena
 
Back
Top Bottom