Nyama za kisabato

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,406
1,103
habari ndugu,
kuna stori nimesikia eti kwamba wasabato hawali nyama,na wanatengeneza nyama zao artificial za unga wa ngano,na flavour iko kama ya nyama,fibre kama nyama,almost kila kitu,je hiii ni ya kweli? pia nasikia wao ni tofauti katika kushiriki chakula cha bwana(ekaristi) kwamba wanakunywa juice na maandazi,je kuna ukweli wowote kuhusu hili au ni stori nyoka tu?natanguliza shukrani zangu
 
Usipende mambo ya kusikia, makanisa ya SDA yamejaa tele nchini, kwa nini usiende mwenyewe ukashuhudie badala ya kusikia ... eti nasikia?

Aliyekwambia kwamba wasabato hawali nyama ni uongo, ila kuna wasabato ambao ni vegetarians kama ilivyo kwa watu wengine wowote hata wasio na dini.

Katika maisha yako hujasikia watu wanaitwa 'Vegetarians", "Vegans", wako vegetarians wengi tu ambao si wasabato, kwa hiyo hakuna swala la usabato hapo bali ni afya. Unaweza kutengeneza nyama isiyotokana na wanyama yaani nyama itokanayo na mimea, sio lazima soya, bali hata maharage ya kawaida, mushrooms etc.

Suala la meza ya bwana, divai isiyo chacha hutengenezwa kutokana na matunda ya mti wa mzabibu (yaani zabibu) na mkate usiochachushwa kwa kuwekewa "yeast" (unleavened bread) hutengenezwa kutokana na unga wa ngano. Hayo mambo ya maandazi umeyatoa wapi.

Siku nyingine fanya homework yako kwanza kabla ya kuleta mada.
 
Siku ingine ukisikia kitu fanya kwanza utafiti wa kina kabla ya kuanika upumbavu wako hadharani. Lengo la thread yako imekaa kukashfu zaidi kuliko kutaka kueleweshwa.
 
nashukuru sana ngereja,nilikua sifahamu,kama nimemkosea yoyote anisamehe bure,hii ni JF bwanaa!!!
 
Ikumbuke siku ya sabato na uitakase. Siku sita fanya kazi lakini siku ya saba ni sabato ya bwana. Siku hiyo usitende kazi yoyote wewe wala mwna wako,wala mjakazi wako wala mnyama yoyote aliyekua ndani ya boma lako. Sabato njema watu wa Mungu
 
Pia nasikia wana anza kuhesabu siku kuanzi jua likitua.
Mfano jua likitua jioni,inakua siku nyingine imeanza.
 
Soma kitabu cha Mwanzo kitakufungulia. Na kama tunasherehekea pasaka ijumaa kuu kama siku yesu alikufa (siku ya sita ya juma) akapumzika siku ya saba (jumamosi) akafufuka siku ya kwanza ya juma (jumapili)
 
Ikumbuke siku ya sabato na uitakase. Siku sita fanya kazi lakini siku ya saba ni sabato ya bwana. Siku hiyo usitende kazi yoyote wewe wala mwna wako,wala mjakazi wako wala mnyama yoyote aliyekua ndani ya boma lako. Sabato njema watu wa Mungu

Any day Monday, Wednesday, Friday can be sabbath for sabbath means resting
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom