Nyama ya NYANI

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
Kwa miaka mingi wakulima wa Kisarawe tumekuwa tukisumbuliwa sana na wanyama waharibifu hasa nyani na nguruwe, mwaka huu neema ya ajabu imetuzikia, kwani sasa hivi wapo wawindaji wengi sana kutoka jijini Dar es Salaam wakiwinda na kutega mitego kuwakamata wanyama hawa. Ni wiki ya pili sasa niko shamba sijaona nyani wala kishindo cha nguruwe mwitu usiku kama tulivyozoea miaka ya nyuma, tulikuwa tukiweka mtego jioni, asubuhi mtakuta bonge la nguruwe limeshikwa kwenye mtego, jamani leo ni wiki ya pili tukiamka asubuhi mitego zaidi ya mitano haina kitu.

Nyama ya nyani inauzwa Dar kama nyama ya mbuzi, baada ya watu wengi kushidwa kuhimili bei za nyama ya ng'ombe na mbuzi kwenye mabucha. Naomba hali hii ya iendelee hadi msimu wa mwaka huu uishe, utupunguzie gharama za ulinzi wa mashamba.
 
utamaduni wa kula kila kitu sasa unaingia taratibu nchini, si ajabu tukajikuta tunakulana wenyewe kwa wenyewe huko mbeleni kama Asia.
 
Kwa miaka mingi wakulima wa Kisarawe tumekuwa tukisumbuliwa sana na wanyama waharibifu hasa nyani na nguruwe, mwaka huu neema ya ajabu imetuzikia, kwani sasa hivi wapo wawindaji wengi sana kutoka jijini Dar es Salaam wakiwinda na kutega mitego kuwakamata wanyama hawa. Ni wiki ya pili sasa niko shamba sijaona nyani wala kishindo cha nguruwe mwitu usiku kama tulivyozoea miaka ya nyuma, tulikuwa tukiweka mtego jioni, asubuhi mtakuta bonge la nguruwe limeshikwa kwenye mtego, jamani leo ni wiki ya pili tukiamka asubuhi mitego zaidi ya mitano haina kitu.

Nyama ya nyani inauzwa Dar kama nyama ya mbuzi, baada ya watu wengi kushidwa kuhimili bei za nyama ya ng'ombe na mbuzi kwenye mabucha. Naomba hali hii ya iendelee hadi msimu wa mwaka huu uishe, utupunguzie gharama za ulinzi wa mashamba.

Mkuu pole sana kwa kuchelewa kugundua mbinu hii shirikishi.

Nina kashamba kangu fulani mahali fulani huku Pwani, nilipopeleka kuku walisumbuliwa sana na vicheche. Nikatunga uongo, nikawaambia jamaa wa jirani pale kuwa siku wakimkamata kicheche wanipigie simu. Nikafika pale nikawapa 50,000/ na nikaondoka na yule kicheche, mbele ya safari nikamtupa.

Jamaa wale majirani wakaniuliza, yule kicheche ulimfanya nini? Nikawaambia hamjui kuwa nyama ya kicheche inaongeza nguvu za kiume !!! hasa ukipata maini yake. Mpaka leo kuku wangu wanalala nje ya banda kwa raha zao.
 
Ha haa haa! Kweli Malila wewe ni mbunifu. Kwa hiyo unataka kusema umegeuza kicheche kuwa dawa kwa baadhi ya watu huko Pwani, sasa unastahili hata kubadil proffession (hamia JF Doctor). Yaan utakuwa umewandaa kisaikolojia kweli. Nimeipenda hii
 
Kwa miaka mingi wakulima wa Kisarawe tumekuwa tukisumbuliwa sana na wanyama waharibifu hasa nyani na nguruwe, mwaka huu neema ya ajabu imetuzikia, kwani sasa hivi wapo wawindaji wengi sana kutoka jijini Dar es Salaam wakiwinda na kutega mitego kuwakamata wanyama hawa. Ni wiki ya pili sasa niko shamba sijaona nyani wala kishindo cha nguruwe mwitu usiku kama tulivyozoea miaka ya nyuma, tulikuwa tukiweka mtego jioni, asubuhi mtakuta bonge la nguruwe limeshikwa kwenye mtego, jamani leo ni wiki ya pili tukiamka asubuhi mitego zaidi ya mitano haina kitu.

Nyama ya nyani inauzwa Dar kama nyama ya mbuzi, baada ya watu wengi kushidwa kuhimili bei za nyama ya ng'ombe na mbuzi kwenye mabucha. Naomba hali hii ya iendelee hadi msimu wa mwaka huu uishe, utupunguzie gharama za ulinzi wa mashamba.

Sasa itabidi nami nirudi Msanga nikachukue shamba, kwani uwepo wa wanyama hawa ulinikatisha sana tamaa. Nashukuru sana kwa taarifa zilizonifikia kwa wakati muafaka
 
Ha haa haa! Kweli Malila wewe ni mbunifu. Kwa hiyo unataka kusema umeguza kicheche kuwa dawa kwa baadhi ya watu huko Pwani, sasa unastahili hata kubadil proffession (hamia JF Doctor). Yaan utakuwa umewandaa kisaikolojia kweli. Nimeipenda hii

Ukiweza kucheza na mazingira vizuri hupati taabu. Pale Vianzi kwa chini kidogo unapovuka kwenda kwa Wakorea,kuna kijito,zamani kulikuwa na mamba kibao,walisumbua watu sana. Kaja jamaa kawageuza mtaji. Baada ya mavuno ya mamba na shamba kaacha anafanya biashara nyingine kabisa. Ukipata changamoto fulani,usiiangalie upande mmoja tu,huenda ukiigeuza upande wa pili kukawa na dili.
 
Ha haa haa! Kweli Malila wewe ni mbunifu. Kwa hiyo unataka kusema umegeuza kicheche kuwa dawa kwa baadhi ya watu huko Pwani, sasa unastahili hata kubadil proffession (hamia JF Doctor). Yaan utakuwa umewandaa kisaikolojia kweli. Nimeipenda hii

Wao ndio wamepata faida kuliko mimi,nimewaongezea idadi ya vitoweo,kwa sababu zamani kicheche alikuwa haliwi,pili wanapata protein natural kabisa,tatu wanapata kitowea kwa gharama karibu na sifuri. Na mimi kuku wangu wanaongezeka, hii ndio inaitwa win-win !!!!!!!!!
 
Ngoja siku uende ukatembelee mifugo yako halafu wanakijiji wenzio wakukaribishe Ugali. Sijui utafanyaje?
 
Tayari yalishanikuta,

Siku hiyo nikavamia ugali kwa nyama,baadae ndio wakasema,eti kweli mimi mkulima. Nikawauliza kwa nini? Tulidhani wewe huwezi kula nyama pori. Kumbe walipika nungu nungu mkuu, nyama ya nungunungu ni tamu balaa.
 
Tayari yalishanikuta, Siku hiyo nikavamia ugali kwa nyama,baadae ndio wakasema,eti kweli mimi mkulima. Nikawauliza kwa nini? Tulidhani wewe huwezi kula nyama pori. Kumbe walipika nungu nungu mkuu, nyama ya nungunungu ni tamu balaa.
Haa haaa haaaa, kwii kwii kwiii. Huko ndo kusocialize sasa na wanakijiji. Lakin kama hukudhurika, right? Itabidi nami nitaitafute ili niionje kama ni tamu namna hiyo. Mimi kuna nyama niliwahi kula pale zizi la ng'ombe (Iringa) lakini habari iliyotokea sasa! nadhan si busara nikiweka hapa.. (Sijui alikuwa Mbwa yule).
 
Back
Top Bottom