Nyama ya Ng'ombe, mbona wamasai haiwadhuru?

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,954
Ni kawaida ukienda kwa Doctor ukiwa na magonjwa fulani,basi Doctor atawaaambia huyu mgonjwa wenu jaribuni kuacha kumpa nyama nyekundu (ng'ombe,mbuzi, kondoo na n.k) na badala yake kama anataka kula nyama basi ale nyama nyeupe (samaki au kuku wa kienyeji)

Sasa mimi najiuliza hili swali sipati jibu,mbona wamasai na yale makabila yote yenye ng'ombe,mbuzi na kondoo wengi hawadhuriki na hayo magonjwa.......... maana wenyewe ndio kitoweo chao cha kila siku.
 
Kwani ushaona masai albino mbado!
Masai na ndevu mmbado
Hawa jamaa wanakula sana mizizi kuna dawa moja kipindi nipo loliondo ilichemshwa pamoja na nyama.inakuwa supu dawa aseee ni shida tumbo linasafishwa kama umemeza washing machine
 
Tatizo tusilolijua wengi ni utayarishaji wa hiyo nyama. Wamasai zaidi wanakula nyama ya kuchoma kuliko ya kupika, sasa wao wanachoma nyama kwa kuining'iniza kwenye miti hivyo mafutamafuta yote yanamwagika chini wakati nyama inaiva, tofauti na sisi mijini nyama zinalazwa kwenye majiko (foel).
 
hata siku moja hawadhuriki tena wanatafuna ikiwa bado mbichi mbichi

Kwa taarifa yako Wamasai wanaugua sana.

Nenda Kibong'oto Hospital uone namba ya Wamasai wanaougua TB ilivyo kubwa; na sababu yake ni pamoja na kunywa maziwa yasiyochemshwa, pamoja na nyama mbichi.

Kuna kitu wanayotumia inaitwa "kiloriti" ambayo inasemekana huwasaidia kutokupata gout ambayo inasababishwa na ulaji nyama nyekundu.
 
Nilijifunza kitu kidogo kuhusu wamasai baada ya kutembelea Simanjiro, hawa jamaa tofauti na tunavyowadhania kuwa wanakula sana nyama kumbe si kweli. Mifugo kwao ni ile sifa ya superiority tu. Hapo Simanjiro town hawana hata bucha ya kuuza nyama ya ng'ombe.
 
Combination mbaya ni nyama ya ng'ombe (red meat) na vyakula vya wanga (carbohydrate). Wamasai wanapiga nyama na consumption yao ya wanga si sana. Kuna diet ya Dr Atkins anashauri ulaji wa red meat na salad tu bila carbohydrate, picha hapo chini:

man-at-restaurant-eating-steak-550px.jpg
 
Wamasai wasingekuwa hawaumwi kusingekuwa na hosp kule endulen, aidom(rekebisha jina) n.k wanaumwa sana tu. Na TB ni moja ya magonjwa yanayowasumbua pia hata sukari n.k nenda huko kijijin usikae hapa mjini ukategemea utawaona kwa wingi. By the way wagonjwa sisi madaktar ndo huwajua lakin wewe unaweza usijue kabila la mtu ikiwa hajavaa kikabila
 
nyama ya ngo'mbe inaweza ikawadhuru ila shida ni kwamba wao wana madawa ya kila aina ko wanatumia kujitibu
 
Back
Top Bottom