Nyalandu waachie wazanzibari Zanzibar yao

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,968
Kwa mshangao wangu waziri Nyalandu anaitangazia dunia kuwa Zanzibar iko salama hivyo watalii waendelee kuitembelea Zanziba na serikali itawahakikishia usalama. Je utalii ni suala la Muungano? Je wazanzibari hawana msemaji hadi mtu wa Tanganyika aitangazie dunia. Hivi sisiemu mnanufaika nini na muungano hadi mnawabana ndugu zetu wa visiwani kama luba. Nyalandu uwaziri wako wa utalii huku Tanganyika haukupi uhalali wa kuisemea Zanzibar kwa kuwa wanaye waziri wa utalii, kauli yako inawapa kichwa wale WAHUNI wanaofanya vurugu na kuona ZnZ yao ni dili kwa sisi wabara
 
Hapa Nyalandu kapotea. Unless alikuwa ameambatana na waziri wa utalii Zanzibar lakini kama kazuka mwenyewe basi kateleza. But again, wizara ya Afya nayo si ya muungano lakini inaongozwa na mbunge wa Zanzibar. Muungano umejaa kizunguzungu!
 
nyalandu hajakosea hayo mamlaka anayo since yeye ni waziri ambapo anaplay role kotekote since hakuna waziri huku bara ambaye anahucka na bara tu.
 
Hata wewe hukatazwi kuitangaza nchi yako. Sioni hapa amefanya kosa gani.
 
Ndio ugumu wa muungano wetu, suala la utalii sio muungano lakini usalama wa watalii ni muungano.
 
Mwanamke mwenye kiherehere alimnyonyesha mtoto asokuwa wake. Hawa wazanzibar wanatukataa kila siku lakini sie tunalazimisha (tunajigonga), kiherehere cha namna hii?? Utakufa siku si zako
 
Zanzibar sio nchi yangu! Nchi yangu Tanganyika watu wamestaarabika hawachomi makanisa wala kuvamia bar na kunywa bia zote huku wanadai pombe ni ukafiri. Nilipomskia Nyalandu nikajua ndo ule uking'ang'anizi wa CCM kwa nchi ya WATU
 
Ndio ugumu wa muungano wetu, suala la utalii sio muungano lakini usalama wa watalii ni muungano.
Ilitakiwa watanganyika tuwaambie watalii kule Zenji hakuwafai kuna Boko haram njooni huku Bagamoyo na Mafia kuna usalama. Sio kuwatetea hawa jamaa
 
Kwa mshangao wangu waziri Nyalandu anaitangazia dunia kuwa Zanzibar iko salama hivyo watalii waendelee kuitembelea Zanziba na serikali itawahakikishia usalama. Je utalii ni suala la Muungano? Je wazanzibari hawana msemaji hadi mtu wa Tanganyika aitangazie dunia. Hivi sisiemu mnanufaika nini na muungano hadi mnawabana ndugu zetu wa visiwani kama luba. Nyalandu uwaziri wako wa utalii huku Tanganyika haukupi uhalali wa kuisemea Zanzibar kwa kuwa wanaye waziri wa utalii, kauli yako inawapa kichwa wale WAHUNI wanaofanya vurugu na kuona ZnZ yao ni dili kwa sisi wabara
Sikubaliani na wewe hata kidogo, Nyalandu hajakosea hata kidogo! Au kwakuwa zimetokea hizi vurugu za juzi? Mbona kabla hamjawahi kuse,a hivyo!!
 
Sikubaliani na wewe hata kidogo, Nyalandu hajakosea hata kidogo! Au kwakuwa zimetokea hizi vurugu za juzi? Mbona kabla hamjawahi kusema hivyo!!!
 
Ndio ugumu wa muungano wetu, suala la utalii sio muungano lakini usalama wa watalii ni muungano.

Duh sasa napata kizunguzungu. Hivi mambo ya muungano ni yapi? Nyalandu si ni naibu waziri wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania? Hapo neno muungano lina maana gani? Kaaazi kweli kweli.
 
Masuala ya utalii si ya muungano, lakini usalama ni jambo la muungano. Kama ni ahadi ya ulinzi kwa watalii ni jambo la muungano. Complexity, and more complexity.
 
Hapa Nyalandu kapotea. Unless alikuwa ameambatana na waziri wa utalii Zanzibar lakini kama kazuka mwenyewe basi kateleza. But again, wizara ya Afya nayo si ya muungano lakini
inaongozwa na mbunge wa Zanzibar. Muungano umejaa kizunguzungu!
hata ailyemteua hajui mkataba ukoje!
 
Mwanamke mwenye kiherehere alimnyonyesha mtoto asokuwa wake. Hawa wazanzibar wanatukataa kila siku lakini sie tunalazimisha (tunajigonga), kiherehere cha namna hii?? Utakufa siku si zako

Mawaziri kutokuwa na job description ndo kunasababisha mtu anavuka mipaka ya utendaji bila kujua.
Ukifanya kazi kwa hofu lazima uwe kichekesho kisa unaogopa rais asivunje baraza la mawaziri ukaachwa.
 
Hata wewe hukatazwi kuitangaza nchi yako. Sioni hapa amefanya kosa gani.

Mkuu upo sahihi kabisa, wanajamvi inabidi mkumbuke kauli mbiu ya Tanzania katika kujitangaza kwa mataifa ya nje huwa unatumika huu msemo " The land of Kilimanjaro and Zanzibar", na wizara yenye jukumu hilo ndio hiyo ambayo Nyalandu ni naibu wake.
 
Kumbe yule waziri wa utalii wa Zanzibar ni kibaraka eeh, ngoja JUMIKI wakuskie. Kumbe ndio maana wanadai sovereign Znz
 
naona muanzisha uzi amekwenda mbali zaidi na kufikiri kuwa muungano tayari umekwisha vunjika na waziri hana mamlaka ya kuzungumzia zanzibar.
 
Back
Top Bottom